Mbagala Dar es Salaam ni chafu sana, inanuka

Mbagala Dar es Salaam ni chafu sana, inanuka

Kuna watu wachafu na washamba na wananuka Tanzania hii kuwazidi wasukuma?
Wasukuma ndio wanao ilisha mbagala kwa mchele acha matusi utalala njaa kwa kukosa ubwabwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mwee laki 3, kweli nitafute hela.

Zinafanya kazi gani hizo?
Unajua kinachosumbua Daslam joto siteee ni lile fukuto, fukuto linaletwa na kiwango cha unyevu angani. Sasa hii kitu inaondosha ule mfukuto unakua kawaida kabisa chumbani au sebuleni, hewa haiwi nzito. Unalala kwa amani tele. Au pia waweza nunua zile feni unaweka barafu inakupepea ili ulale kwa amani na uzuri zinakua pia rechargeable, ila imara ni kuanzia laki 250
 
Ukiondoa Kariakoo, Mbagala ni eneo la pili mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na idadi kubwa ya watu/wafanyabiashara, pili hapo Mbagala katikati fremu ya biashara kama huna milioni 3, million 2 na au milion 1 hupati.

Pana mzunguko mkubwa sana wa biashara na Manispaa ya Temeke tunaona inajenga flats za biashara hapo Zakhem ambazo japo sijui kama zitatosha; zitawachukua wafanyabiashara wote walioko barabarani. Hosptali ya Zakhem inapanuliwa kwa kujengwa kwa ghorofa nyingi zaidi.

Tunatarajia pia, kulivunja soko kubwa la Mbagala ili kulijenga kwa mtindo wa ghorofa kama Zakhem ili kuweza kuwachukua wafanyabiashara maelfu walioko katika maeneo yasiyo rasmi.

Mbagala inatarajiwa kujengwa kwa mfumo wa kisasa na bajeti imeanza na Chamanzi ambapo tunataka uwe SATELLITE CITY ya kulisha southern coridal(Ushoroba wa kusini) yaani Mtwara, Lindi, n.k tayari bajeti ipo tayari. Itajengwa hosptali kubwa kabisa hapo eneo la Muhimbili ukiwa unaianza Kata ya Chamazi ukitokea kipande cha Majimatitu.

Kwa yeyote mwenye eneo Mbagala asilichezee kwani masterplan yake inafanyiwa review na patajengeka kwa haraka na kupendeza zaidi.

Ujenzi wa barabara za Mwendokasi unakamilika na kuanza kutumika mwezi wa tatu mwakani nadhani wote tunaona ubora wa Barabara ile na flyover ya Uhasibu pale.

Pia stand kubwa ya mwendokasi mkoani Dar es Salaam ni ile iliyoko Mbagala inaanza kutumika mwakani na ishakamilika tayari wote tunaona.

Barabara ya Mbagala-Mbande-Kisewe-Chanika itapanuliwa na kuwa njia nne pia kuna Barabara nyingine inaitwa CHALINZE EXPRESS inatokea Kibada inakatiza pale Kokoto inapitia ndani katikati ya Kata za Mianzini, Chamazi mpaka Chanika kwenda Chalinze itakuwa ya malori kutokea bandari. Itajengwa kwa njia nne.

Mbagala kwasasa ni mji wenye watu wengi pengine kuliko maeneo yote ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Kwa mfanyabiashara yeyote lazima apatolee jicho kwani fursa ni kubwa sana.

Swala la uchafu ni changamoto ya master plan maana idadi ya watu ni kubwa sana kuliko uwezo wa eneo, Serikali imeliona hili na wataalam wapo kazini kuliweka sawa.

Muda si mrefu inakuwa Wilaya mpya ambapo tunaangalia Makao makuu yake yawe Chamazi UVIKIUTA au Pale eneo la Muhimbili au tukichukue kipande cha Vikindu kiingizwe Mbagala na Makao makuu yawe Mwandege hilo eneo kubwa opposite na shule ya St. Matthew.

Badae patazaliwa Mkoa mpya utakao jumlisha Mbagala, Kigamboni, na Mkuranga ili kurahisha Huduma za jamii kwa wananchi wa eneo hilo.

Wakazi wasiuze maeneo yao kwani kwa mujibu wa waziri husika, wawekezaji wakija itabidi mtu atoe ardhi na mwekezaji atoe hela hivyo Kuleta manufaa kwa wote na kwa vizazi vijavyo.

Mbunge wa eneo hili ambaye pia nimwenyekiti wa Kamati ya serikali za mitaa Tanzania Mhe. Chaurembo anajitahidi sana kuhakikisha Barbara za ndani zinarekebishwa kwa kiwango cha lami/zege nadhani wakati mmeona barabara za Kirungule, Kiburugwa, Kijichi, Charambe na sasa Mianzini zinavyoboreshwa.

Barabara mpya na ya kisasa kutokea Njia panda ya Nzasa kuelekea kwa MPA..NGE-Bi kibonge itarahisha Huduma ya usafiri maana imebakiza kisehemu kidogo tu pale kwa mp..nge darajani.

Mbagala mpya kwa Maendeleo mapya kwa wakazi na Watanzania kwa ujumla! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Ukisikiliza maneno ya wanasiasa utaseme unasikini uleee tumeuaga. Hawa jamaa haya maneno matamu sijui wanayatoaga wapi asee. Wanasiasa hamuendi mbinguni.

Alafu mkuu kila ukuandika kwa MPARANGE mbona unakata/unamute baadhi maneno? Km Hilo jina Lina ukakasi mlibadishe tu kuliko kuona aibu kulitaja.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Unajua kinachosumbua Daslam joto siteee ni lile fukuto, fukuto linaletwa na kiwango cha unyevu angani. Sasa hii kitu inaondosha ule mfukuto unakua kawaida kabisa chumbani au sebuleni, hewa haiwi nzito. Unalala kwa amani tele. Au pia waweza nunua zile feni unaweka barafu inakupepea ili ulale kwa amani na uzuri zinakua pia rechargeable, ila imara ni kuanzia laki 250
Hii ni kweli, mfano hapa nimewasha feni ila upepo nasikia kwa mbali maana kuna fukuto la hatari ukifungua mlango atleast ndio unaiskia hewa nyepesi.
Hiyo kitu nzuri sana basi
 
Nimesema Rangitatu na nikatoa tahadhari usiende mvua ikinyesha sasa Rangitatu nyingine ya Mbagala iko wapi! Kila mara zingatia simama, soma, tafakari kisha chukua hatua.
Umewahi kwenda posta wakati mvua ikinyesha?
Umeenda kariakoo na kuona chemba za mavi zinavyotiririsha maji mchana kweupe? Je umewahi kwenda kariakoo kipindi mvua inanyesha?
Umewahi kwenda kawe kupitia mikocheni wakati mvua ikinyesha?
Nafikiri wewe ni mgeni hapa dar es salaam.
 
Nikilala na feni kabla hata usiku haujafika nusu chafya na mafua kama yote, Asubuhi namka mgonjwa wa mafua.

Ni mateso kwakweli, mvua tu zije
Tumia karafuu kuanzia leo maisha yako yote utakuja nishukuru. Nilikua mhanga wa mafua toka utoto wangu hadi ukubwani, the day nimeanza kula karafuu, sijaumwa mafua nina miaka 3. Kula kila siku asbh na jioni tafuna tembe 4 kila asbh na jioni. Hutaumwa mafua, hutaumwa meno, na kama una vidonda vya tumbo inafunga. Nimepona vidonda kwa hii kitu pia, nilipokuja kutafiti ndio nikajua kumbe alaa inafunga na vidonda vya tumbo. Nimeteseka sana na vidonda licha ya kula sana dawa za kienyeji za kila aina. Mimi natembea nazo hata nikisafiri natafuna tu hata katikati ya siku. Akili ishazoea
 
That place is nasty
Mvua ikinyesha pale ukitoka unaoshwa miguu.

Soko la chakula kuwa katika hali ile ni mbaya sana. Na ndizi Asilimia 90 zinatokea pale kwenda masoko mengine

Lile soko halitakiwi kuwa pale ila siasa
 
Umewahi kwenda posta wakati mvua ikinyesha?
Umeenda kariakoo na kuona chemba za mavi zinavyotiririsha maji mchana kweupe? Je umewahi kwenda kariakoo kipindi mvua inanyesha?
Umewahi kwenda kawe kupitia mikocheni wakati mvua ikinyesha?
Nafikiri wewe ni mgeni hapa dar es salaam.
Mbezi beach napo mvua zikinyesha hapafai, kuanzia Makonde hadi Afrikana hayo mafuriko yake ni balaa tena barabarani kabisa
 
Kama umesikia harufu ya mbagara rangi tatu, ila hujasikia harufu Shekilango, Manzese Bhaheresa, mbezi Stand ya Daladala, Utakua una pua za aina yake.
 
Back
Top Bottom