Mbagala Dar es Salaam ni chafu sana, inanuka

Mbezi beach napo mvua zikinyesha hapafai, kuanzia Makonde hadi Afrikana hayo mafuriko yake ni balaa tena barabarani kabisa
Mbezi beach wakati wa mvua wanafungulia maji ya chemba wanayapeleka nje,nyumba nyingi
Mbezi beach hazina mfumo wa kupeleka maji taka baharini

Ova
 
Sasa uchafu wote unaenda barabarani na kwenye nyumba za jirani na barabara, ustaarabu zero kabisa
 
Mkuu dar yote kwa kifupi ni chafu na inanuka ikinyesha mvua yaani ni uvundo niliwahi kutoingia kwenye soko la Ilala boma kwa damu za kuku na takataka zilizo oza yaani nilirejea nyumbani sikuweza kuingia kufata bidhaa
 
Ukiondoa Kariakoo, Mbagala ni eneo la pili mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na idadi kubwa ya watu/wafanyabiashara, pili hapo Mbagala katikati fremu ya biashara kama huna milioni 3, million 2 na au milion 1 hupati.

Pana mzunguko mkubwa sana wa biashara na Manispaa ya Temeke tunaona inajenga flats za biashara hapo Zakhem ambazo japo sijui kama zitatosha; zitawachukua wafanyabiashara wote walioko barabarani. Hosptali ya Zakhem inapanuliwa kwa kujengwa kwa ghorofa nyingi zaidi.

Tunatarajia pia, kulivunja soko kubwa la Mbagala ili kulijenga kwa mtindo wa ghorofa kama Zakhem ili kuweza kuwachukua wafanyabiashara maelfu walioko katika maeneo yasiyo rasmi.

Mbagala inatarajiwa kujengwa kwa mfumo wa kisasa na bajeti imeanza na Chamanzi ambapo tunataka uwe SATELLITE CITY ya kulisha southern coridal(Ushoroba wa kusini) yaani Mtwara, Lindi, n.k tayari bajeti ipo tayari. Itajengwa hosptali kubwa kabisa hapo eneo la Muhimbili ukiwa unaianza Kata ya Chamazi ukitokea kipande cha Majimatitu.

Kwa yeyote mwenye eneo Mbagala asilichezee kwani masterplan yake inafanyiwa review na patajengeka kwa haraka na kupendeza zaidi.

Ujenzi wa barabara za Mwendokasi unakamilika na kuanza kutumika mwezi wa tatu mwakani nadhani wote tunaona ubora wa Barabara ile na flyover ya Uhasibu pale.

Pia stand kubwa ya mwendokasi mkoani Dar es Salaam ni ile iliyoko Mbagala inaanza kutumika mwakani na ishakamilika tayari wote tunaona.

Barabara ya Mbagala-Mbande-Kisewe-Chanika itapanuliwa na kuwa njia nne pia kuna Barabara nyingine inaitwa CHALINZE EXPRESS inatokea Kibada inakatiza pale Kokoto inapitia ndani katikati ya Kata za Mianzini, Chamazi mpaka Chanika kwenda Chalinze itakuwa ya malori kutokea bandari. Itajengwa kwa njia nne.

Mbagala kwasasa ni mji wenye watu wengi pengine kuliko maeneo yote ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Kwa mfanyabiashara yeyote lazima apatolee jicho kwani fursa ni kubwa sana.

Swala la uchafu ni changamoto ya master plan maana idadi ya watu ni kubwa sana kuliko uwezo wa eneo, Serikali imeliona hili na wataalam wapo kazini kuliweka sawa.

Muda si mrefu inakuwa Wilaya mpya ambapo tunaangalia Makao makuu yake yawe Chamazi UVIKIUTA au Pale eneo la Muhimbili au tukichukue kipande cha Vikindu kiingizwe Mbagala na Makao makuu yawe Mwandege hilo eneo kubwa opposite na shule ya St. Matthew.

Badae patazaliwa Mkoa mpya utakao jumlisha Mbagala, Kigamboni, na Mkuranga ili kurahisha Huduma za jamii kwa wananchi wa eneo hilo.

Wakazi wasiuze maeneo yao kwani kwa mujibu wa waziri husika, wawekezaji wakija itabidi mtu atoe ardhi na mwekezaji atoe hela hivyo Kuleta manufaa kwa wote na kwa vizazi vijavyo.

Mbunge wa eneo hili ambaye pia nimwenyekiti wa Kamati ya serikali za mitaa Tanzania Mhe. Chaurembo anajitahidi sana kuhakikisha Barbara za ndani zinarekebishwa kwa kiwango cha lami/zege nadhani wakati mmeona barabara za Kirungule, Kiburugwa, Kijichi, Charambe na sasa Mianzini zinavyoboreshwa.

Barabara mpya na ya kisasa kutokea Njia panda ya Nzasa kuelekea kwa MPA..NGE-Bi kibonge itarahisha Huduma ya usafiri maana imebakiza kisehemu kidogo tu pale kwa mp..nge darajani.

Mbagala mpya kwa Maendeleo mapya kwa wakazi na Watanzania kwa ujumla! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Hivi mbagara kizuiani ile barabara kutokea kiburugwa magenge mapya mmeisusa ama oneni aibu ile sehemu ni ya hovyo sijawahi kuona toka nitembee dar na viunga vyake lami mashimo ya ajabu ajabu hata gari zinapita kwa tabu sana
 
Sidhani kama ni kweli, Mbagala CCM hawajawahi kushinda kihalali ...tujaribu kuongelea hoja iliopo..nini kifanyike hawa ni watanzania kama ilivyo watanzania wengine, hata kama hukai Mbagala.
Wapi CCM waliwahi kushinda kihalali?
 
Ukiondoa Kariakoo, Mbagala ni eneo la pili mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na idadi kubwa ya watu/wafanyabiashara, pili hapo Mbagala katikati fremu ya biashara kama huna milioni 3, million 2 na au milion 1 hupati.

Pana mzunguko mkubwa sana wa biashara na Manispaa ya Temeke tunaona inajenga flats za biashara hapo Zakhem ambazo japo sijui kama zitatosha; zitawachukua wafanyabiashara wote walioko barabarani. Hosptali ya Zakhem inapanuliwa kwa kujengwa kwa ghorofa nyingi zaidi.

Tunatarajia pia, kulivunja soko kubwa la Mbagala ili kulijenga kwa mtindo wa ghorofa kama Zakhem ili kuweza kuwachukua wafanyabiashara maelfu walioko katika maeneo yasiyo rasmi.

Mbagala inatarajiwa kujengwa kwa mfumo wa kisasa na bajeti imeanza na Chamanzi ambapo tunataka uwe SATELLITE CITY ya kulisha southern coridal(Ushoroba wa kusini) yaani Mtwara, Lindi, n.k tayari bajeti ipo tayari. Itajengwa hosptali kubwa kabisa hapo eneo la Muhimbili ukiwa unaianza Kata ya Chamazi ukitokea kipande cha Majimatitu.

Kwa yeyote mwenye eneo Mbagala asilichezee kwani masterplan yake inafanyiwa review na patajengeka kwa haraka na kupendeza zaidi.

Ujenzi wa barabara za Mwendokasi unakamilika na kuanza kutumika mwezi wa tatu mwakani nadhani wote tunaona ubora wa Barabara ile na flyover ya Uhasibu pale.

Pia stand kubwa ya mwendokasi mkoani Dar es Salaam ni ile iliyoko Mbagala inaanza kutumika mwakani na ishakamilika tayari wote tunaona.

Barabara ya Mbagala-Mbande-Kisewe-Chanika itapanuliwa na kuwa njia nne pia kuna Barabara nyingine inaitwa CHALINZE EXPRESS inatokea Kibada inakatiza pale Kokoto inapitia ndani katikati ya Kata za Mianzini, Chamazi mpaka Chanika kwenda Chalinze itakuwa ya malori kutokea bandari. Itajengwa kwa njia nne.

Mbagala kwasasa ni mji wenye watu wengi pengine kuliko maeneo yote ndani ya mkoa wa Dar es Salaam. Kwa mfanyabiashara yeyote lazima apatolee jicho kwani fursa ni kubwa sana.

Swala la uchafu ni changamoto ya master plan maana idadi ya watu ni kubwa sana kuliko uwezo wa eneo, Serikali imeliona hili na wataalam wapo kazini kuliweka sawa.

Muda si mrefu inakuwa Wilaya mpya ambapo tunaangalia Makao makuu yake yawe Chamazi UVIKIUTA au Pale eneo la Muhimbili au tukichukue kipande cha Vikindu kiingizwe Mbagala na Makao makuu yawe Mwandege hilo eneo kubwa opposite na shule ya St. Matthew.

Badae patazaliwa Mkoa mpya utakao jumlisha Mbagala, Kigamboni, na Mkuranga ili kurahisha Huduma za jamii kwa wananchi wa eneo hilo.

Wakazi wasiuze maeneo yao kwani kwa mujibu wa waziri husika, wawekezaji wakija itabidi mtu atoe ardhi na mwekezaji atoe hela hivyo Kuleta manufaa kwa wote na kwa vizazi vijavyo.

Mbunge wa eneo hili ambaye pia nimwenyekiti wa Kamati ya serikali za mitaa Tanzania Mhe. Chaurembo anajitahidi sana kuhakikisha Barbara za ndani zinarekebishwa kwa kiwango cha lami/zege nadhani wakati mmeona barabara za Kirungule, Kiburugwa, Kijichi, Charambe na sasa Mianzini zinavyoboreshwa.

Barabara mpya na ya kisasa kutokea Njia panda ya Nzasa kuelekea kwa MPA..NGE-Bi kibonge itarahisha Huduma ya usafiri maana imebakiza kisehemu kidogo tu pale kwa mp..nge darajani.

Mbagala mpya kwa Maendeleo mapya kwa wakazi na Watanzania kwa ujumla! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Mipango ya kwenye makaratasi ndio ccm inachokiweza..kuhamishia kwenye uhalisia ni ngumu sana kutekelezeka.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mbagala inasemwa vibaya Sana Sisi ambao mji huu tunaujua tunakushangaa Sana.. vipi tandale Kwa tumbo utasemaje Kwa harufu au tembelea machinjio ya vingunguti utajua mziki wa harufu au nenda mabibo pale kwenye chujio la maji taka.
Hapa DAR kuna sehemu zinanuka vibaya mno kuliko Huko mbagala ebu nenda ferry pale utajua hiki ninachosema sometimes kama mji huu haujafika sehemu zote ni Bora ukae kimya,subiri siku mvua inanyesha kubwa alafu uje kariakoo uone vinyesi vinaelea
 
Ila feri soko la samaki napo kuna harufu kali sana nahisi mpaka jumba jeupe pale wanalipata

Ova
 
Unaweza kuta huyu anayeisema Mbagala rangi tatu namna hii anaishi kwenye kibanda huko uswekeni. Usiku akilala ukuta umeachia nyufa amezuia na mti unamuuliza nikuue au nikuache? Dirishani ameweka pazia khanga za CCM za kampeni za 2010 "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA".

Social media life versus really life.

Halafu mkuu katika nyama za hovyo ulizoziorodhesha hapo, ondoa huyo nguruwe. Mpe heshima yake hata kama wewe hutumii tafadhali.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
😂😂Ni nyama ya ovyo iyo wanakula watu wa ovyo
 
Mswahili ni mtu wa mwambao wa pwani ya afrika mashariki...mimi ngosha.

#MaendeleoHayanaChama
Ni miongoni mwa watu waliostaarabika wa mwambao vipi una waunganisha na uchafu??? Huwezi kuona wanalala na wanyama nyumba moja mfano kuku nguruwe ng'ombe nk kama nduguzao.
 
Uzazi wa mpango ni suluhisho kwa matatizo mengi Sana Afrika. Mengi sana
 
Back
Top Bottom