Mbagala Dar es Salaam ni chafu sana, inanuka

Mbagala Dar es Salaam ni chafu sana, inanuka

Kama wewe umezoea kuoga baada ya kushauriwa utakuwa na tatizo, ni ajabu haujui wajibu wa kiajira kwa hao niliowataja.
Dhumuni kuu la JamiiForums ni kujadili mambo Critical na Intelligent subjects kama hizi na kuja na productive conclusions ili kutatua changamoto. Sasa wewe badala ya kuja na ushauri na solution unaanza kuleta mipasho. Maana yake hujui unachokitaka na kama mwananchi hujui unachokitaka na unakaa kimya unategemea nini kutoka kwa viongozi wa caliber ya Tanzania? Wakikaa kimya utawalaumu iwapo wewe haujui unachokitaka?

Nini dhumuni la hii mada yako?
 
Hivi mbagara kizuiani ile barabara kutokea kiburugwa magenge mapya mmeisusa ama oneni aibu ile sehemu ni ya hovyo sijawahi kuona toka nitembee dar na viunga vyake lami mashimo ya ajabu ajabu hata gari zinapita kwa tabu sana
Mgh pale mbona amna barabara ya hivyo? Au unasemea Zakhem Darlive kupitia viwandani? Au unazungumzia ile ya kupitia TRA?

Maana kabla ya kizuiani kuna Barbara pale roundabout inaelekea mahakama ya mwanzo, tushaweka lami pale
 
Yeah, hapana mimi ni mtendaji na mwanasiasa pia, siasa kama zilivyo nidhamu(Disciplines) nyingine zinao watu weka na wabaya, hivyo waongo tulionao katika tasnia hii isiwe kigezo cha kuisemea siasa kuwa ni uongo!

Siasa ni tasnia njema sana mkuu. Hili neno tunalifanyia mchakato kuliondoa katika matumizi Ndugu maana limepata athari kimaana, asante sana!
 
Madiwani wao wanafanya kazi gani, nina uhakika wakiwaambia watu wao kwa kujitolea waje na mafagio na matoroli washirikiane na kusaidiana kusafisha watakuja tuu at least mara moja kwa mwezi, hata kama ni maskini nina uhakika hawapendi uchafu, na wawabane viongozi wa soko wanaokusanya pesa wafanye usafi najua sheria inawapa uwezo huo, lakini ukiwa na uongozi wa ovyo ndio hivyo tena
 
Dhumuni kuu la JamiiForums ni kujadili mambo Critical na Intelligent subjects kama hizi na kuja na productive conclusions ili kutatua changamoto. Sasa wewe badala ya kuja na ushauri na solution unaanza kuleta mipasho. Maana yake hujui unachokitaka na kama mwananchi hujui unachokitaka na unakaa kimya unategemea nini kutoka kwa viongozi wa caliber ya Tanzania? Wakikaa kimya utawalaumu iwapo wewe haujui unachokitaka?

Nini dhumuni la hii mada yako?
Kwa ujinga wako unataka niwaambie nini matumizi ya kodi ya maendeleo! JF of GT's, hivi nawe ni sehemu yao?
 
Kwa ujinga wako unataka niwaambie nini matumizi ya kodi ya maendeleo! JF of GT's, hivi nawe ni sehemu yao?
Acha matusi na let have intelligent debate kama watu wenye akili, busara na wanaojitambua ili kufikia productive conclusion.

Nini dhumuni la mada yako?
 
Acha matusi na let have intelligent debate kama watu wenye akili, busara na wanaojitambua ili kufikia productive conclusion.

Nini dhumuni la mada yako?
Ujinga siyo tusi na halijawahi kuwa tusi na halitakuwa tusi, mjinga ukimuelewesha na akajua ujinga humtoka ndiyo sababu tunajenga shule ili tuufute ujinga.
Dhumuni la mada hii ni burudani.
 
Madiwani wao wanafanya kazi gani, nina uhakika wakiwaambia watu wao kwa kujitolea waje na mafagio na matoroli washirikiane na kusaidiana kusafisha watakuja tuu at least mara moja kwa mwezi, hata kama ni maskini nina uhakika hawapendi uchafu, na wawabane viongozi wa soko wanaokusanya pesa wafanye usafi najua sheria inawapa uwezo huo, lakini ukiwa na uongozi wa ovyo ndio hivyo tena
Hilo la watu kujitolea kufanya usafi hufanyika, tatizo wachafuaji wakubwa ambao ni wamachinga huwa hawashiriki kutokana na jeuri waliyojengewa na viongizi wa CCM ambayo huwafanya wawadharau! Usafi unaofanyika huwa haudumu hata dakika moja kwani kuna idadi kubwa sana ya wamachinga wanaofanya biashara barabarani kuashiria zoezi la kuwaondoa limeshindikana, kwa kifupi wakuu wote wa wilaya wamekwisha shiriki zoezi hilo na kushindikana.
 
Mgh pale mbona amna barabara ya hivyo? Au unasemea Zakhem Darlive kupitia viwandani? Au unazungumzia ile ya kupitia TRA?

Maana kabla ya kizuiani kuna Barbara pale roundabout inaelekea mahakama ya mwanzo, tushaweka lami pale
Mkuu nimekwambia kizuiani kwenda kiburugwa magenge mapya
 
Hata vyakula vya ovyo unaweza kulishwa huko sijui nyama ya chura, kenge, panya, nguruwe yaani Pako ovyo kinoma, nyumba hazina ustaarabu, kukabwa nje nje Tena hata saa Saba.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Rangi tatu pananuka shombo la samaki wa ferry. Ardhi yake ni nyeusi, yani ni tope iliyokauka. Mvua ikinyesha ndio unaweza kuelewa namaanisha nini
 
Unaweza kuta huyu anayeisema Mbagala rangi tatu namna hii anaishi kwenye kibanda huko uswekeni. Usiku akilala ukuta umeachia nyufa amezuia na mti unamuuliza nikuue au nikuache? Dirishani ameweka pazia khanga za CCM za kampeni za 2010 "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA".

Social media life versus really life.

Halafu mkuu katika nyama za hovyo ulizoziorodhesha hapo, ondoa huyo nguruwe. Mpe heshima yake hata kama wewe hutumii tafadhali.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Nyama ya nguruwe huwa wanauza huku zakhem.
 
Back
Top Bottom