Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji

Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji

Kwa maeneo Lori lilipopata hiyo ajali, nilijua tu lazima cement ziibiwe haziwezi kuachwa,ni tabia mbaya Sana lakini inachagizwa na Mambo mengi ,wengi hapo ni wale wa tabaka la tatu na wanajua Sana tu kuwa wanachofanya ni ujinga,tabia ya wizi ina mizizi mirefu tu kwani walishazoeshwa kwahiyo inaonekana sawa tu...
 
Hawajifunzi matukio yariyopita wa2 wamepoteza maisha kwa upumbavu wa kama huu (wizi),,,refer kirichotokea morogoro gali la mafuta walikufa na sasa wako kaburini washakuwa skeleton.
 
Halafu limeangukia maeneo mabaya sana yale, hapo ni kati ya stesheni hadi Mtoni Mtongani.

Maeneo mengine naweza nika guarantee mzigo ukawa salama ila sio hayo maeneo coz hata spare za gari zinaweza zikawa zinafunguliwa na kuondoka nazo.
Wanahangaika kulitoa jioni hii hapa ni katikati ya misheni na msikitini kwenye ile kona kali jamaa akachochora
 
Hii ndio Taarifa inayozunguka mitandaoni kwa sasa, ambapo baada ya lori hilo kubwa kupata ajali wananchi wa eneo hilo badala ya kuokoa majeruhi wamejisombea mifuko ya cement, huku wengine wakirejea tena na tena bila kipingamizi chochote.

Chanzo : Millard Ayo TV

MYTAKE : Hivi ndio vitu ambavyo Polisi wanapaswa kuvishughulikia badala ya kupambana kuzuia Jogging za BAWACHA
Siyo polisi tuu bali system nzima yapaswa kubadilika. Ipokazi kubwa kuweza kuwabadili watu kuja kwenye imani na kuoneana huruma ikiwa serkali yenyewe haina imani na huruma kwa watu wake
 
Tofautisha wizi na kuokota
acha kuhalalisha wizi,kuokota unajua maana yake?kuokota ni kuona kitu pahalii ambacho unajua wazi mwenyewe hayupo na ima amekisahau au kimemdondoka na hicho huruhusiwi kukichukua bali kukitangaza then umpelekee,leo mtu kapata majanga baada ya kumsaidia unamuibia halafu unasema kuokota?una akili?
 
Umeshatangaza vingapi ulivyookota mheshimiwa
 
Back
Top Bottom