Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji

Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji

Mida hii mtaa ya mbagala watu wanaiba sementi baada ya gari lililokuwa limebeba mzigo huo kuacha njia na kugonga watu na nyumba.

Bado haijafahamika idadi ya watu waliofikwa na mauti au majeruhi zoezi limetatizwa na idadi ya vijana waliojazana badala ya kuokoa wanaiba sementi.

Mida hii ndio polisi wa doria wanafika

Hii tabia ya wizi kwenye ajari na bado hatujakoma tu, nImekumbuka siku gari lililosheheni vileo lilipoanguka na wanakijiji wakaanza kula ulabu polisi waliofika wakakuta mtaa mzima watu wamelewa.

USSR
Hii ndio faida ya kuchagua ccm
 
Baada ya kutokea ajali ya gari la mizigo barabara ya Kilwa. Watu badala ya kumuokoa dereva na utingo wake wamekimbilia kuzoa sementi.

Hii ni dalili tosha kuwa watanzania kwa sasa wana hali ngumu ya maisha. Wakati tunajisifia kukuza uchumi wakati mifukoni tupo pyeeeeeee.
Mkuu sio hali ngumu ila Wabongo tumeendekeza sana tamaa.
 
Mkuu sio hali ngumu ila Wabongo tumeendekeza sana tamaa.
Kwahiyo unataka kutwambia kuwa wabongo tuna maisha bora kabisa kwa maana ya kuwa na kipato cha uhakika?
 
Wabongo ni wezi wezi Sana hii Tabia chafu inaendekezwa Sana siku Moja litokee tukio Kama Hilo halafu zitembezwe risasi za makalio za moto iwe funzo watu waache kuchukua Mali wasioitolea jasho!
 
Malori yote hutumia diesel,diesel hailipuki kama petrol,acha watu wajiokotee cement
Nami aliyekudanganya? Katika high temperature diesel inawaka sana. Una umri gani? Kuna ajali za mabasi makubwa na malorry, yote yanatumia diesel lakini yamewahi kuwaka moto.
 
Afrika nzima hakuna sehemu roli likaanguka ns bidhaa watu wasiokote ,so kwa mila zetu huo sio wizi
Huo ni wizi usitafute sababu yakuhalalisha dhuluma ingekuwa ni mali au mzigo wako umeanguka na watu wakaushambulia hivyo wewe ungejisikia namna gani
 
Halafu limeangukia maeneo mabaya sana yale, hapo ni kati ya stesheni hadi Mtoni Mtongani.

Maeneo mengine naweza nika guarantee mzigo ukawa salama ila sio hayo maeneo coz hata spare za gari zinaweza zikawa zinafunguliwa na kuondoka nazo.
 
Back
Top Bottom