Mbakaji Bester na mpenzi wake Dkt. Nandipha walisafirishwa kwa Tsh. Milioni 175

Mbakaji Bester na mpenzi wake Dkt. Nandipha walisafirishwa kwa Tsh. Milioni 175

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali ya Afrika Kusini imetumia Tsh. Milioni 175 sawa na (R1.4 milioni) kukodi ndege kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini kuwarejesha wafungwa Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana waliokamatwa Arusha Aprili 7, mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi aliiambia Kamati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo kwamba walilazimika kukodi ndege kuwarudisha Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana kwa sababu kikosi hicho hakina ndege.

Amesema walikodi mabasi madogo na kuendesha kilomita 600 kutoka Dar es Salaam hadi Arusha, na kurudi.

Motsoaledi amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya viongozi wa Tanzania kuagiza kuwa Bester na Magudumana wakabidhiwe kwa maofisa wa uhamiaji.

Thabo Bester ni mhalifu wa makosa ya mauaji na ubakaji kutoka Afrika Kusini aliyekamatwa jijini Arusha baada ya kusakwa kwa muda mrefu.

MWANANCHI
 
Serikali ya Afrika Kusini imetumia Tsh. Milioni 175 sawa na (R1.4 milioni) kukodi ndege kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini kuwarejesha wafungwa Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana waliokamatwa Arusha Aprili 7, mwaka huu.

MWANANCHI
Asante kwa taarifa. Ila huyu mhalifu anafikirisha sana kwa namna alivyoendesha shughuli zake akiwa mfungwa gerezani
 
Serikali ya ANC na serikali ya CCM haina tofauti ni vifisadi vifasadi
 
Back
Top Bottom