BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali ya Afrika Kusini imetumia Tsh. Milioni 175 sawa na (R1.4 milioni) kukodi ndege kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini kuwarejesha wafungwa Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana waliokamatwa Arusha Aprili 7, mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi aliiambia Kamati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo kwamba walilazimika kukodi ndege kuwarudisha Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana kwa sababu kikosi hicho hakina ndege.
Amesema walikodi mabasi madogo na kuendesha kilomita 600 kutoka Dar es Salaam hadi Arusha, na kurudi.
Motsoaledi amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya viongozi wa Tanzania kuagiza kuwa Bester na Magudumana wakabidhiwe kwa maofisa wa uhamiaji.
Thabo Bester ni mhalifu wa makosa ya mauaji na ubakaji kutoka Afrika Kusini aliyekamatwa jijini Arusha baada ya kusakwa kwa muda mrefu.
MWANANCHI