Mbali na kujipendekeza kwa kiwango cha juu kabisa, bado hatutakiwi! Tufanyeje?

Mbali na kujipendekeza kwa kiwango cha juu kabisa, bado hatutakiwi! Tufanyeje?

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Makazi na mashamba tunatoa umilki kwake, ila kwake sisI hatutakiwi kugusa!

Umeme unashusha bei mpaka kiwango cha maumivu kwa watoto wetu' lakini aah wapi!

Tukasema hiyo isiwe noma! Basi tukafanya hivii, tukienda kukopa, tutagawana naye pasu ingawa nyumbani kwetu inawatoto wengi, hatukujali, lakini aah wapi!

Basi tukafanya tena tukio lingine ili tueleweke zaidi, basi mali zote zilizoko huku, zitakuwa za pamoja kama aridhi n.k, ila zako ni zako, lakini aah wapi.

Tukasema ngoja tuongeze na hili' tumuweke basi mjengoni na tutamupa baadhi ya vitengo aziongoze ila kwake afanye yeye tuu watoto wetu watajitafutia hukuhuku, lakini wapi!

TUkasema isiwe tabu, ngoja sasa watoto wako huko tutakuwa tunawapa ajira na kuwalipa ila wahuku wawe usijali kuwahusu wa huku, Napo wapi!

Kiwango hiki cha kujipendekeza chamhitaji mtu jasiri kwelikweli aisee! Bila ya hivyo ndoa inavunjika mchana kweupe!
 
Aliyezoa kunyonga kuchinja hawezi, subiri mabadiliko ya hali ya hewa duniani yaendelee kina cha bahari kiongezeke baada ya miaka 50 hv kisiwa kimezwe ndio tutaheshimiana hata yule wa serikali tatu tutamuuliza ya tatu na ya pili wapi? HV hamuoni swala la mazingira Dk akiliongelea anasimamia video.
 
Wa kumlaumu hapa ni Nyerere, Tundu Lissu alivyomchana wazi wazi kuhusu huu muungano usioeleweka akaambiwa amekufuru
 
Muungano wa kishenzi kabisa,toa serikali mbili tuwe na serkali moja tu,lasivyo kupe waondoke zao.
 
Back
Top Bottom