Mbali na kuwa na washirika wengi wanaomuunga mkono Russia, kwa USA, Russia ni kama yuko peke yake!

Nasikia ule ubalozi wa Russia pale bongo bado upo paleoale, mkiwapatia huu ushauri mtakuwa mmewasaidia sana.
 
Wanajitegemea kama taifa au hawajitegemei!?
Wananchi wanapata mahitaji ya msingi, elimu, afya, ajira!?
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huduma za kijamii zinazotolewa na serikali ya Russia haziachani sana na zile zinazotolewa na serikali nyingi katika nchi za dunia ya tatu kwani rasilimali nyingi za serikali ya Russia zinaelekezwa kwenye wizara ya ulinzi.
 
Huduma gani za kijamii ambazo zinatolewa kwenye nchi unazoziita za dunia ya kwanza lakini hazitolewi kwa wananchi wa Russia?
 
Huo ukomunisti mbona haujawazuia China tena hao China bado wanakumbatia fikra za kikomunisti komunisti mpaka leo.

Umeamua kujiongelea chochote kilicho kichwani.
Ukomunisti wao umebaki zaidi kwenye makaratasi sawa tu na ujamaa wa kitanzania.
 
Russia mikwala alisemaga atakayesaidia Ukraine atakutana na moto....tumeona misaada mbalimbali na Russia yupo
 
Ukweli mchungu,ni kwamba Urusi peke yake anapigana na Mataifa 40 na yameshindwa kumtingisha.
 
Huo ukomunisti mbona haujawazuia China tena hao China bado wanakumbatia fikra za kikomunisti komunisti mpaka leo.

Umeamua kujiongelea chochote kilicho kichwani.
Wachina walianza kuachana na Ukomunisti mapema miaka ya 1980 chini ya utawala wa Deng Xiaoping wakati Urusi ikiendelea kupuyanga na Ukomunisti wake, pia Warusi walipohamia katika mfumo wa soko huria walihamishia uchumi kwa watu wachache wanaoitwa "Oligarchs" ambao walikuwa ni wezi tu wa mali za umma na wote waliojikita kwenye biashara za rasilimali na malighafi tofauti na China ambayo ilifanya mabadiliko ya maana ya soko huria.
 
Russia anayo nafasi ya kuwa na economic dominance viwango cya akina us sasa sijuwi anakwama wapi.
Kuna mambo mengi sana
1.Russia ili mtu afanikiwe sana anahitaji connection na kujuana zaidi kuliko uwezo wake au kipaji chake binafsi. US kuna ile hali ya kwamba ni land of equal opportunity, kwamba kila mtu anakuwa na fursa sawa na mwingine bila kujali sana background yake, msimamo wa siasa, kujuana au connections.

2. Sera nzuri za uchumi zinazotoa uhuru kwa watu na kuheshimu property rights.

3.Mfumo bora wa kisiasa na kisheria unaoheshimu due process kupitia mahakama huru.

4. Utulivu wa kisiasa

5. Kuruhusu mchanganyiko wa watu mbalimbali kutoka sehemu zote duniani. Utashangaa kuna Warusi na Wachina wengi sana wamehamia US tangu miaka ya 1850 kutafuta maisha.
 
L
LGBTQ
 
Huduma gani za kijamii ambazo zinatolewa kwenye nchi unazoziita za dunia ya kwanza lakini hazitolewi kwa wananchi wa Russia?
Huduma zinapatikana lakini ubora katika maeneo mengine ya Russia huwezi kabisa ukalinganisha na zilivyo katika nchi zingine zilizoendelea.
 
Huduma zinapatikana lakini ubora katika maeneo mengine ya Russia huwezi kabisa ukalinganisha na zilivyo katika nchi zingine zilizoendelea.
Ebu ngoja kwanza mkongwe, kwani Russia ni nchi ya ngapi kwa ukubwa wa kiuchumi duniani!?
 
Russia hamna makampuni makubwa yanayoweza kuajiri.nimesoma hapa nikajua wewe hujui kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…