Mzee Kijana
JF-Expert Member
- Nov 25, 2011
- 1,442
- 1,140
Kipindi cha nyuma nilikua nampenda na namkubali JPM kwa utendaji wake kazi lakini kwa sasa naona kama vile nikisikia hata jina lake napata kichefuchefu sasa maana imekua too much
katika hali isiyo ya kawaida mimi nashangaa na ninasikitika sana, nimejiuliza sana Hayati JPM alikua na kipawa cha namna gani hiki? sasaivi baadhi mambo hayaendi kwasababu yake, hata marais wengine wastaafu sasahivi hawaheshimiki kabisa kisa JPM
Rais wa sasa anapata wakati mgumu sana kueleweka kwa watanzania, kila anachokifanya watu wanabeza wanataka afanye kama alivyokua anafanya JPM,
Nashangaa sana Rais akitengua uteuzi wowote aliokuwa ameteua JPM watu wanaongea sana, wanafadhaika sana hawataki yani Rais Samia atoe mtu yyte aliyeachwa na JPM,
Jana baada ya utenguzi wa mawaziri wa JPM watu wanalalamika sana, koment nyingi za wananchi wa kawaida mitandaoni wanamlilia JPM, yaani watu wanaona yoyote yule aliyeachwa na JPM hastahili kutenguliwa,
Imefika hatua hadi watu wanamchukia Samia kisa tu ameenda tofauti na baadhi ya mambo ya JPM
Huu sio ustaarabu kwanza mimi ningekua ni Rais Samia, natengua baraza lote navunja hata na bunge tunaanza upya uchaguzi na mambo yangu ninayoyajua mimi , maana nimeona kuwa mstaarabu kwa watu ambao hawajastaarabika ni kama kupaka rangi upepo,
nakushauri Rais bora ufanye mambo yako kivyako kwa mujibu wa katiba asiyekubaliana na wewe afanye mapinduzi akupindue na dunia nzima ijue,
JPM tulimpenda kama Rais wetu lakini sasa tumechoka na huu upuuzi kila kitu JPM kila Kitu JPM Laiti kama mimi ndio ningekua ni Rais wa sasa kwa moyo wangu jinsi ulivyo ningevunja baraza la mawaziri nikaanza upya kabisa na mambo yangu mapya,
Sasa hivi Tuko na Rais mwingine hatuwezi kuongozwa na aliyeishazikwa, Tuwe wastaarabu watu wapuuzi dizaini ya polepole na askofu kibwetere hawafai hata kukanyaga kwenye ardhi ya bunge la nchii hii ndio wanapandikiza chuki dhidi ya serikali ya sasa,
Yaani bado tu hujatambua kuwa nchi hii Rais akiwa Muislamu ni shida?! Niambie Rais gani Muislam hakusemwa vibaya? Mzee Mwinyi kawatoa watu wanavaa viraka na mlo mmoja kwa siku akaweka miundombinu ya utafutaji na kufufua uchumi na watu maisha yakaboreka lakini alisemwa vibaya hadi kuchorwa vikatuni. Anasifiwa Nyerere aliyeua uchumi. Mzee wetu wa Msoga licha ya kuikuza sekta binafsi na kutoa ajira huku akipandisha mshahara kila mwaka alisemwa vibaya. JPM alikuwa na mapungufu kibao na mifano ipo mingi lakini anasifiwa hadi leo. Mama anafanya kazi nzuri lakini utendaji wake unakwamishwa na uharibifu mkubwa uliofanywa na Mwendazake na kundi lake.