"Mungu ni mkubwa jamani! Mungu Anaweza nyiye! Mungu hashindwi na jambo lolote. Sikutegemea kama Watanzania wenzangu watachangia hadi sasa kupata shilingi milioni thelathini (30,000,000)... "Japokuwa niliamini kwa imani kwamba zitafika. Sasa Mungu yeye amefanya kwa vitendo," Ndivyo alivyosema kijana Saidi Abdallah Mikidadi Potea (33), mkazi wa Dar es Salaam.
Saidi anaendelea kusema: "Huu uvimbe unanitesa sana Watanzania wenzangu. Kwa sasa umezidi kukua hadi nashindwa kugeuka na maumivu makali. Usiku natoka jasho jingi sana mpaka nakuwa hoi." Alianza kulia Saidi.
Akaendelea: "Lakini kwa kiasi cha pesa kilichopatikana nawashukuru sana Watanzania wenzangu. Mungu awabariki sana. Naamini hata hicho kiasi kilichobaki cha shilingi milioni saba, Mungu atajalia tu." Alimaliza kusema ingawa kwa tabu.
Saidi anakabiliwa na uvimbe mkubwa shingoni huku daktari wa Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, Dk. Prased Namani akisema upasuaji wake anatakiwa asafiri kwenda kwenye nchi hiyo iliyopo Bara la Asia.
Dokta Namani alitoa suluhu ya uvimbe huo unaokua kila kukicha huku akiiambia familia yake kulipa Shilingi Milioni Arobaini (40,000,000) ikiwa ni gharama za usafiri na matibabu.
Dokta Namani aliongeza kuwa, endapo uvimbe huo hautafanyiwa upasuaji hadi kufika mwisho wa mwezi Machi, 2026 basi utapasuka wenyewe na Saidi atakuwa amepoteza maisha!
Familia ya Saidi ni ya kawaida sana, hivyo ikawa ngumu kupata kiasi hicho cha pesa kwa namna yoyote ile. Ndipo mdogo wake aitwaye Jondani Abdallah Mikidadi Potea alipoanza kuhangaika kwenye vyombo vya habari akiomba msaada kutoka kwa Watanzania watakaoguswa na ugonjwa wa kaka yake.
Mungu ni mkubwa sana, Watanzania wanatoa sana wakiwa nacho. Watu walianza kutoa michango kwa kila mtu kile alichonacho.
Miongoni mwa waliyochangia ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mbunge) ambaye baada ya kuguswa na hali ya Saidi, alitoa Shilingi Laki Tano (500,000) huku Watanzania wengine wakiendelea kuchangia sambamba naye.
Februari 22, 2026, familia ya Saidi kupitia mseamaji wake, Jondani ilitoa taarifa kuwa, michango ilifikia Shilingi 5, 300, 000 hivyo kubakiza Shilingi 34, 700, 000 ili kufikia lengo.
Machi 7, 2026, familia tena kupitia msemaji huyohuyo, Jondani ikatoa taarifa kuwa, michango ilifikia Shilingi 6,000,000. Hivyo ikabaki Shilingi 34,000,000 kufikia lengo.
Machi 9, 2026, familia ikatoa taarifa tena kuwa sasa michango ilifikia Shilingi 10, 000, 000. Kwa hiyo ikabaki Shilingi 30,000,000 kukamilisha lengo.
Leo, Machi 12, 2026 familia imetoa taarifa mpya kwamba, kuna Mtanzania aishiye nchini Uingereza ambaye aliomba jina lake lisitiriwe, amechangia Shilingi 20,000,000 hivyo kubaki Shilingi 10, 000, 000 ili kufikia lengo.
Kwa mujibu wa familia kupitia kwa Jondani, Mtanzania huyo alisema aliguswa sana na taarifa na picha za Saidi mtandaoni. Hivyo akaona na yeye atimize ibada kwa Mungu kwa kutoa kiasi hicho cha pesa.
Jondani, mdogo wa Saidi, anaendelea kuwaomba Watanzania watakaoguswa na ugonjwa wa kaka yake kumchangia ili aweze kukamilisha kiasi cha pesa kilichotajwa na kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu ya upasuaji.
Jondani akaongeza jambo: "Wiki iliyopita tuliitwa tena Muhimbili (Hospitali ya Taifa), madaktari walimkagua tena braza ili waone kama kuna uwezekano wa kufanya chochote ili kuokoa maisha yake hapahapa Tanzania. Lakini hakukuwa na uwezekano huo. Walisisitiza suluhisho ni kwenda India tu."
Kumbukumbu ya ugonjwa wa Saidi ni kwamba; ilikuwa Julai mwaka jana (2025) ndipo uvimbe mdogo ilipoanza kujitokeza upande wa kulia wa shingo yake.
Alianza kwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kitabibu Ilala (Amana). Madaktari baada ya kutobaini tatizo ni nini, walimshauri aende Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Madaktari wa Muhimbili nao walikaa kama jopo na kumfanyia uchunguzi katika vipimo. Lakini hawakuweza kugundua kama ishu ni nini. Walifikiri ni kansa ili aanze tiba ya chemotheraphy 'kemo' lakini haikuwa kansa.
Wapo waliyomshauri aende Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta-Kibaoni. Alikwenda. Madaktari wa kule hawakuona kama ni kansa au jipu wala tezi. Lakini uvimbe ulionesha kukua kila siku na pia kama akipasuliwa angepinda shingo na mdomo katika kupona kwake hali ambayo ingemuondolea ukamili wa ubinadamu.
Ndipo, Januari 2026, akabahatika kuonwa na daktari huyo wa Hospitali ya Apollo, Prased Namani aliyefika kikazi Muhimbili ambaye alimwambia India wanaweza kumpasua na kutoa uvimbe huu ambao umekuwa ukitutumka kila siku.
Aidha, Dokta Namani akampa tahadhari kwamba, endapo uvimbe huo utamaliza miezi mitatu bila kupasuliwa, yaani kufikia mwisho wa mwezi huu wa Machi, utapasuka na hivyo atapoteza maisha.
Kama hivyo, kwa mujibu wa familia, kiasi kilichobaki ni shilingi milioni kumi tu (10,000,000).
Kwa yule ambaye ataguswa na ugonjwa wa Saidi ambao madaktari wamesema siyo Kansa wala Jipu wala Tezi, anaweza kumchangia chochote kwa namba ya simu ya mdogo wake Jundani Abdallah Mikidadi Potea; 0710434416, NMB: 20310131829 Jundani Mikidadi Abdallah. Kumsaidia mgonjwa ni ibada kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu muumba wa vyote.
Ruksa kushea taarifa hii.