M'bananga chake hana kondo (If you spoil what is your own you have no quarrel)

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
16,161
Reaction score
9,729
Waswahili wana msema usemao ‘Mbananga chake hana kondo’ (If you spoil what is your own you have no quarrel)

Kulingana na maoni ya Wananchi katika rasimu ya Tume ya Warioba , wananchi wengi walichagua Serikali 3 na nadhani kufikia leo idadi itakuwa imeongezeka zaidi ya asilimia 70.

Lakini ngoja niwaeleze kitu kimoja, sijui kama Watanzania wanaelewa kwamba mabadiliko mengi yamekwisha fanyika ndani ya Muungano kiasi kwamba mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za Serikali zetu toka 1995 haupo haulingani kabisa na muundo wa Serikali 2 uloasisiwa na Viongozi wetu Mwalimu Nyerere na Abeid Karume?

Je nikisema leo hii mfumo unaotumika kuendesha Serikali hizi hauna sura sanifu, unafanana na mseto wa Serikali 3 na ule wa Jumuiya

Kumbukeni katika moja ya hotuba nyingi za mwalimu alieleza kwa nini yeye alichagua Serikali 2 badala ya 1 aloitaka Karume, na sababu gani hakutaka kabisa Serikali 3 ambazo Tanganyika ingebeba mzigo mkubwa kugharamia Serikali ya Muungano.

Hali hii ndio iliyopo sasa hivi na inawakera sana Watanganyika, wanaita Tanganyika yao kwa sababu Mbananga chake hana Kondo.

Tujadili bila mihemko
.
 
Mkuu Mbona Tanganyika haipo kwenye nyaraka zozote zaidi ya serikali inayoitwa ya Tanzania bara na Zanzibar?

Na vipi Yale wanayonufaika nayo Zanzibara Mbona huku
 
Waswahili wana msema usemao ‘Mbananga chake hana kondo’ (If you spoil what is your own you have no quarrel)

Kulingana na maoni ya Wananchi katika rasimu ya Tume ya Warioba , wananchi wengi walichagua Serikali 3 na nadhani kufikia leo idadi itakuwa imeongezeka zaidi ya asilimia 70.

Lakini ngoja niwaeleze kitu kimoja, sijui kama Watanzania wanaelewa kwamba mabadiliko mengi yamekwisha fanyika ndani ya Muungano kiasi kwamba mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za Serikali zetu toka 1995 haupo haulingani kabisa na muundo wa Serikali 2 uloasisiwa na Viongozi wetu Mwalimu Nyerere na Abeid Karume?

Je nikisema leo hii mfumo unaotumika kuendesha Serikali hizi hauna sura sanifu, unafanana na mseto wa Serikali 3 na ule wa Jumuiya

Kumbukeni katika moja ya hotuba nyingi za mwalimu alieleza kwa nini yeye alichagua Serikali 2 badala ya 1 aloitaka Karume, na sababu gani hakutaka kabisa Serikali 3 ambazo Tanganyika ingebeba mzigo mkubwa kugharamia Serikali ya Muungano.

Hali hii ndio iliyopo sasa hivi na inawakera sana Watanganyika, lakini wanaita Tanganyika yao kwa sababu Mbananga chake hana Kondo.

Tujadili bila mihemko
.
Hata sasa Bado Tanganyika inagharamia kila kitu kinachohusu Muungano.
 
Kulingana na maoni ya Wananchi katika rasimu ya Tume ya Warioba , wananchi wengi walichagua Serikali 3 na nadhani kufikia leo idadi itakuwa imeongezeka zaidi ya asilimia 70.
Nadhani inafikia 90%. Mzee Wasira aliyejinasibisha kama mtetezi wa Muungano anapohoji, ujue kuna jambo
Siyo siri tena hata CCM wa Bara hawakubaliani na hali ilivyo
sijui kama Watanzania wanaelewa kwamba mabadiliko mengi yamekwisha fanyika ndani ya Muungano kiasi kwamba mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za Serikali zetu toka 1995 haupo haulingani kabisa na muundo wa Serikali 2 uloasisiwa na Mwalimu Nyerere na Abeid Karume?mfumo unaotumika kuendesha Serikali hizi hauna sura sanifu, unafanana na mseto wa Serikali 3 na ule wa Jumuiya
Tangu wakati wa Nyerere muundo ni kama serikali 3 . Mfano, Waziri mkuu wa Tanzania anakuwaje wa upande mmoja? TAMISEMI inakuwa chini yake lakini Waziri na Watendaji wanaweza kuwa Wazanzibar!

Hoja hapa ni mambo yawekwe wazi, Tanganyika isimamie mambo yake kama ilivyo Zanzibar
Muundo wa ''makande'' kwamba mahindi, maharage, nazi n.k. vinachanganywa haufai na ni mfu

Kama haliwezekani watu wapasue jahazi wagawane mbao! sio wa kwanza zipo nchi zilifanya hivyo
Kumbukeni katika moja ya hotuba nyingi za mwalimu alieleza kwa nini yeye alichagua Serikali 2 badala ya 1 aloitaka Karume, na sababu gani hakutaka kabisa Serikali 3 ambazo Tanganyika ingebeba mzigo mkubwa kugharamia Serikali ya Muungano.
Hata sasa hivi Tanganyika inababe mzigo wa Muungano! Kwa mujibu wa Gavana wa BoT marehemu Ndulu Zanzibar iliacha kuchangia Muungano miaka 40 na sasa ni zaidi ya 50. Mzigo wote kaubeba Mtanganyika

Kasome Bajeti ya Zanzibar unionyeshe haya
1. Fungu kutoka Zanzibar linalopelekwa katika shughuli za Muungano
2. Mapato kutoka Zanzibar yanayoletwa Hazina Dar au Dodoma
3. Bajeti ya Wizara ya Ulinzi
4. Bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani
5. Bajeti ya Wizara ya mambo ya nje
6. Bajeti ya Wizara ya Muungano
7. Bajeti ya kuleta Wabunge 80 kulala Dodoma kwa mambo 3%

Kwa uchache tu wa kutaja

Halafu rudi kwenye Bajeti ya SMZ usome kitu kinaitwa General Budget support ambacho ni pesa za Tanganyika zinazotolewa Hazina Tanganyika kwenda kusaidia Bajeti ya SMZ

Usisahau kwamba Zanzibar inapewa 10% ya Makusanyo ya Tanganyika kwa mwezi. Yaani TRA wakikusanya zaidi Zanzibar wanapata zaidi. Wakati huo huo mapato ya TRA Zanzibar hayavuki bahari.

Labda tu nikupe mfano wa AFCON, gharama zote zinabebwa na kodi za Tanganyika si SMZ

Mfano wa pili, viongozi wastaafu wa Zanzibar wanalipwa na kodi za Tanganyika

Kodi za visa zinazotozwa Zanzibar haziingii Wizara ya mambo ya ndani lakini watumishi wa Uhamiaji Zanzibar wanalipwa na Wizara ya mambo ya ndani ambayo inaendeshwa kwa kodi za Mtanganyika.

Leo Zanzibar ina maafisa uhamiaji 800 kutoka 8 wakati wa Mapinduzi. Hao 800 wanafanya kazi Bara na kulipwa na Tanganyika ingawa mapato ya Uhamiaji Zanzibar ni kwa ajili ya Zanzibar.

Mwisho hivi unajua madeni na mikopo ya Zanzibar inakuja kwa jina la Tanzania na mlipaji ni Hazina Tanganyika!
Yaani ukiona miradi kule Zanzibar ni pesa za madini Geita, Gas Mtwara, Mahindi Sumbawanga n.k.

Bado unaamini Zanzibar inachangia muungano leo! yaani kwa dhati kabisa unaamini ni mshirika na siyo mbeleko
 
Mkuu nadhani unachanganya mambo. Nitarydia kusema Wakati wa Mwalimu tulikuwa na nchi moja Serikali 2 (Unitary States) hazikuwa 3 kwa muundo wowote unaofikiria. Ndio maana rais alikuwa Mmoja na Makamu wake ndiye pia rais wa Zanzibar.

Na zaidi hatukutazama viongozi wanatoka wapi kuwa rais wa Jamhuri, hata kama ni Mzanzibar (Mwinyi) alikuwa Mtanzania kwanza sii Mzanzibar kama leo mnavyomtazama Samia.

Na tazama mambo aloyazungumza Mzee wetu Jaji Warioba, yote haya yametokana na madai yasokwisha ya Wazanzibar wakidai Zanzibar huru na ndio maana Warioba amezungumzia walomsaliti Mwalimu.

Mwisho, nashangaa inaponiuliza kama naamini Zanzibar inachangia Muungano, hapo sijakuelewa kuchangia kivipi yani? Zanzibar ni sehemu ya Tanzania (Muungano)mxhango gani zaidi unautaka?

Yes, kuna Wazanzibar wanataka Zanzibar ijitoe katika Muungano huu tuwe na Muungano wa Jumuiya na katika kuwaridhisha kero zao tumewasaliti Mwalimu na Karume.

Na sipendi kumnyooshea mtu au Chama kidole isipokuwa niseme ukweli tu kwamba maadui wetu wa awali Ukabila, Udini na Ukanda wamerudi kwa kasi ya ajabu sana kutokana na mabadiliko haya ya Utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Na msiombee kabisa Serikali 3 mtakuwa mmekula nyama ya mtu kama wenzetu upande wa pili. Kama Mwalimu na Katume wangekuwa hai leo hii, watu kibao wangefungwa jela za nje mpaka kufa kama Jumbe au Yule mzee wa Iringa. Tumefika pabaya sana na niseme ukweli mimi siitaki kabisa hiyo Katiba Mpya hasa kwenye swali la Muungano.

Tazama hata nchi yenye Serikali 3 hakuna Mamlaka (Agency) wa kukusanya kodi zaidi ya mmoja. Wana mkusanyaji kodi mmoja tu NCHI nzima, wanajua kila astate imechangia kiasi gani, isipokuwa kila State ndio unaamua kuongeza tozo ya VAT au laa.

Kodi ni moja nchi nzima, na hakuna kutoza mara mbili ukivuka kwenda upande mwingine. Sisi kuna kodi za Bara na Zanzibar, kuna tozo za Ushuru kila kata sijui mkoa bidhaa ile ile.ndani ya nchi moja! Mwananchi mkazi wa state fulani hapo ndiko kwao, sio kuzaliwa wapi! Mwananchi ana Uhuru wa kwenda popote anapotaka (kuhamia) na Akihama state anatakiwa kubadilisha tu vitambulisho vyake vya makazi sio kazaliwa wapi! Njoo kwetu, utasikia huyu sio Mzanzibar. Yule Mbemba bana asili yake Mrundi kahamia Kigoma mwambie alete vitambulisho vya Baba na babu zake! Hii akili imwtoka wapi? Maana zamani hatukuwa na mambo haya..

Haya yote haya ndio nasema, sasa hivi Nchi yetu sii ya Serikali 2 bali ina viashrira vingi vya Serikali 3 na Jumuiya, tena labda niseme tunaelekea zaidi kuwa na Serikali za Mkataba (Jumuiya) kama ilivyo EAC. Yale matakwa ya Maalim Seif ndiko tunakoelekea. Usaliti mkubwa sana kwa Waasisi wetu.

Maasalaam.
 
Hoja yako inagusa suala muhimu la muundo wa Muungano na uwajibikaji wa Serikali. Ni muhimu kujadili kwa uwazi faida na changamoto za Serikali mbili na tatu, tukizingatia maoni ya wananchi, gharama za uendeshaji na namna kila mfumo unavyoweza kulinda maslahi ya Watanzania wote.
 
Nitarydia kusema Wakati wa Mwalimu tulikuwa na nchi moja Serikali 2 (Unitary States) hazikuwa 3 kwa muundo wowote unaofikiria. Ndio maana rais alikuwa Mmoja na Makamu wake ndiye pia rais wa Zanzibar.
Si kweli! Nyerere alianza na Rais, Makamu wa kwanza wa Rais, na Makamu wa pili wa Rais.
Walikuwa Nyerere, Karume na Kawawa. Kazi za Makamu wa pili ilikuwa kusimamia shughuli za Tanganyika.
Maana yake ni kwamba kulikuwa na JMT, SMZ na Tanganyika a.k.a mambo yasiyo ya Muungano
Na zaidi hatukutazama viongozi wanatoka wapi kuwa rais wa Jamhuri, hata kama ni Mzanzibar (Mwinyi) alikuwa Mtanzania kwanza sii Mzanzibar kama leo mnavyomtazama Samia.
Mkuu Mkandara ''mwiba hutoka ulipoingilia'' haya yameanzishwa na wenyewe. Kuna kiongozi alipoingia madarakani alisimama na kumwambia waziri wake wa mambo ya nje '' Jambo likifanyika huku na kule pia''
Unaweza kuona hata teuzi za nafasi. Narudia tena, mwiba hutoka ulipoingilia
Na tazama mambo aloyazungumza Mzee wetu Jaji Warioba, yote haya yametokana na madai yasokwisha ya Wazanzibar wakidai Zanzibar huru na ndio maana Warioba amezungumzia walomsaliti Mwalimu.
Waliomsaliti Mwalimu si hawa wa mamlaka kamili! kutoka Zanzibar. Hadi leo akina OMO wanauzungumzia Muungano kwa indhara na kashfa na hapo ndipo wametibua nyongo za Watanganyika. When you live in a glass house don't throw stones
Mwisho, nashangaa inaponiuliza kama naamini Zanzibar inachangia Muungano, hapo sijakuelewa kuchangia kivipi yani? Zanzibar ni sehemu ya Tanzania (Muungano)mxhango gani zaidi unautaka?
Kama ni sehemu ya Tanzania, 21% ya ajira ni za nini? 10% ya Mapato ya Tanganyika ni ya nini? Kwanini kuna fungu maalumu la HESLB kwa Wazanzibar? Nitajie mkoa mmoja tu wa Tanganyika unaopewa upendeleo kama huo

Kuchangia muungano ni gharama za kuuendesha. Muungano si gugu maji la kujiendesha lenyewe
Kodi za TRA Zanzibar hazivuki bahari, lakini za Tanganyika zinakwenda kwa mabilioni
Gharama za Taasisi zote na Wizara za Muungano Zanzibar haichangii kwa mujibu wa Gavana Ben Ndulu
Yes, kuna Wazanzibar wanataka Zanzibar ijitoe katika Muungano huu tuwe na Muungano wa Jumuiya na katika kuwaridhisha kero zao tumewasaliti Mwalimu na Karume.
Akina OMO hao na tunawaunga mkono. Wajitoe tu tutakutana EAC na SADC. Hatuna sababu za kutumia mudamwingi kuhangaika na eneo lisilo na tija kwa ustawi wa Tanganyika. Kama muungano ukiwepo ni lazima Wazanzibar watambue nafasi yao. Kwamba ni ka eno kadogo kenye watu wachache na uchumi mdogo
Hata sisi Tanzania tuna ji behave mbele ya Wababe wa Dunia. Tunajua nafasi yetu hatuwezi kutunishiana misuli na Russi, China au USA. Hakuna usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar, waambieni ukweli
Na msiombee kabisa Serikali 3 mtakuwa mmekula nyama ya mtu kama wenzetu upande wa pili. Kama Mwalimu na Katume wangekuwa hai leo hii, watu kibao wangefungwa jela za nje mpaka kufa kama Jumbe au Yule mzee wa Iringa. Tumefika pabaya sana na niseme ukweli mimi siitaki kabisa hiyo Katiba Mpya hasa kwenye swali la Muungano.
Of course Muungano ni moja ya blunder za Mwalimu Nyerere. Mwl hakuangalia mbele katika mfumo na matatizo yatakayojitokeza . Mwl alikumbana na misuko suko ya akina Jumbe , Ramadhani Faki, Maalim n.k. hakuchukua hatua akiamini mambo yatakuwa salama. Mwl hakujua akina OMO watakuja kubomoa Muungano na si kuimarisha. Mtu anaulizwa mamlaka kamili ni vipi, hana jibu. Kesho anarudia yale yale asiyokuwa na majibu!
Tazama hata nchi yenye Serikali 3 hakuna Mamlaka (Agency) wa kukusanya kodi zaidi ya mmoja. Wana mkusanyaji kodi mmoja tu NCHI nzima, wanajua kila astate imechangia kiasi gani, isipokuwa kila State ndio unaamua kuongeza tozo ya VAT au laa.
Hapa unamlaumu nani? Zanzibar wana ZRB hawataki TRA na wanailaani. Waambie ukweli huu
Kodi ni moja nchi nzima, na hakuna kutoza mara mbili ukivuka kwenda upande mwingine. Sisi kuna kodi za Bara na Zanzibar, kuna tozo za Ushuru
Yes ni kwasababu ya ''abuse''. Mfano SMZ ina shirika lake la viwango (ZBS) umewahi kujiuliza ni kwanini! Jibu ni kwamba hawataki TBS ili kuweka viwango vyao vya chini bidhaa ziingie Zanzibar kisha kuletwa Bara.
Kule Bandari Zanzibar wanalipa kodi kidogo sana. Kontena moja la milioni 5 Tanganyika ni Milioni 20.

Arguably utasema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, je, kwa mwendo huo Tanganyika itapata wapi mapato?
Kumbuka mapato ya Zanzibar yanabaki huko

Ni wewe unayepaswa kujiuliza kwanini kila Taasisi ina mbadla Zanzibar. Tanganyika wlaikubali kuwa ni JMT, unapokuwa na TBS na kisha ZBS , hii TBS ni ya nani? Unapokuwa na HESLB na kisha ZHESL hii HESLB ni ya nani?

Ulipouliza Zanzibar ina mchango gani ikiwa ni sehemu ya Tanzania, Mkandara hujiulizi kwanini kuna TBS na ZBS. Kuna HELSB na ZHESLB. Kuna TAAA na ZAAA. Kuna TDA na ZFDA, kuna NECTA na Baraza Zanzibar.
Kila Taasisi ina mbadala Zanzibar hadi Uhamiaji na Jeshi Katika nchi moja.

Watanganyika wanasema hivi, Tanganyika yao iirudi ili wajue wanahangaika na nini. Huu muungano wa kutafuta NIDA ili kupata soko la bidhaa, ajira na ardhi sioni udhati wake

Si kweli! Nyerere alianza na Rais, Makamu wa kwanza wa Rais, na Makamu wa pili wa Rais.
Walikuwa Nyerere, Karume na Kawawa. Kazi za Makamu wa pili ilikuwa kusimamia shughuli za Tanganyika.
Maana yake ni kwamba kulikuwa na JMT, SMZ na Tanganyika a.k.a mambo yasiyo ya Muungano

Mkuu Mkandara ''mwiba hutoka ulipoingilia'' haya yameanzishwa na wenyewe. Kuna kiongozi alipoingia madarakani alisimama na kumwambia waziri wake wa mambo ya nje '' Jambo likifanyika huku na kule pia''
Unaweza kuona hata teuzi za nafasi. Narudia tena, mwiba hutoka ulipoingilia

Waliomsaliti Mwalimu si hawa wa mamlaka kamili! kutoka Zanzibar. Hadi leo akina OMO wanauzungumzia Muungano kwa indhara na kashfa na hapo ndipo wametibua nyongo za Watanganyika. When you live in a glass house don't throw stones

Kama ni sehemu ya Tanzania, 21% ya ajira ni za nini? 10% ya Mapato ya Tanganyika ni ya nini? Kwanini kuna fungu maalumu la HESLB kwa Wazanzibar? Nitajie mkoa mmoja tu wa Tanganyika unaopewa upendeleo kama huo

Kuchangia muungano ni gharama za kuuendesha. Muungano si gugu maji la kujiendesha lenyewe
Kodi za TRA Zanzibar hazivuki bahari, lakini za Tanganyika zinakwenda kwa mabilioni
Gharama za Taasisi zote na Wizara za Muungano Zanzibar haichangii kwa mujibu wa Gavana Ben Ndulu

Akina OMO hao na tunawaunga mkono. Wajitoe tu tutakutana EAC na SADC. Hatuna sababu za kutumia mudamwingi kuhangaika na eneo lisilo na tija kwa ustawi wa Tanganyika. Kama muungano ukiwepo ni lazima Wazanzibar watambue nafasi yao. Kwamba ni ka eno kadogo kenye watu wachache na uchumi mdogo
Hata sisi Tanzania tuna ji behave mbele ya Wababe wa Dunia. Tunajua nafasi yetu hatuwezi kutunishiana misuli na Russi, China au USA. Hakuna usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar, waambieni ukweli

Of course Muungano ni moja ya blunder za Mwalimu Nyerere. Mwl hakuangalia mbele katika mfumo na matatizo yatakayojitokeza . Mwl alikumbana na misuko suko ya akina Jumbe , Ramadhani Faki, Maalim n.k. hakuchukua hatua akiamini mambo yatakuwa salama. Mwl hakujua akina OMO watakuja kubomoa Muungano na si kuimarisha. Mtu anaulizwa mamlaka kamili ni vipi, hana jibu. Kesho anarudia yale yale asiyokuwa na majibu!

Hapa unamlaumu nani? Zanzibar wana ZRB hawataki TRA na wanailaani. Waambie ukweli huu

Yes ni kwasababu ya ''abuse''. Mfano SMZ ina shirika lake la viwango (ZBS) umewahi kujiuliza ni kwanini! Jibu ni kwamba hawataki TBS ili kuweka viwango vyao vya chini bidhaa ziingie Zanzibar kisha kuletwa Bara.
Kule Bandari Zanzibar wanalipa kodi kidogo sana. Kontena moja la milioni 5 Tanganyika ni Milioni 20.

Arguably utasema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, je, kwa mwendo huo Tanganyika itapata wapi mapato?
Kumbuka mapato ya Zanzibar yanabaki huko

Ni wewe unayepaswa kujiuliza kwanini kila Taasisi ina mbadla Zanzibar. Tanganyika wlaikubali kuwa ni JMT, unapokuwa na TBS na kisha ZBS , hii TBS ni ya nani? Unapokuwa na HESLB na kisha ZHESL hii HESLB ni ya nani?

Ulipouliza Zanzibar ina mchango gani ikiwa ni sehemu ya Tanzania, Mkandara hujiulizi kwanini kuna TBS na ZBS. Kuna HELSB na ZHESLB. Kuna TAAA na ZAAA. Kuna TDA na ZFDA, kuna NECTA na Baraza Zanzibar.
Kila Taasisi ina mbadala Zanzibar hadi Uhamiaji na Jeshi Katika nchi moja.

Watanganyika wanasema hivi, Tanganyika yao iirudi ili wajue wanahangaika na nini. Huu muungano wa kutafuta NIDA ili kupata soko la bidhaa, ajira na ardhi sioni udhati wake
Ndugu yangu bado unachanganya vitu. NENO Serikali ni chombo kilichoundwa kuongoza shughuli za Serikali hiyo mahala fulani na sii mtu mmoja kusimamia mambo ya Upande Fulani.

Tunaposema Serikali 3 ina maana zimeundwa wizara zake kushughulikia shughuli zote za usimamizi na utekelezaji ilivyo ama ilivyokuwa upande wa Zanzibar.

Kwa hiyo Bara haikuwa na Serikali yake na hata Mawaziri wa Muungano walishughulika na mambo yote ya Muungano pande zote mbili. Hali yale hii ndio kiini cha mimi kusema Mbananga Chake hana Kondo, tusilaumu upande mmoja wakati Bunge la Jamhuri wameridhia mabadiliko hayo.

Leo hii hata Yale mambo 11 ya awali ya Muungano mengi hayapo tena acha yaloongezwa kufikia 22. Na ukitazama tulipofikia Waziri wa JMT katika mambo ya Muungano hana mamlaka Zanzibar. Na maelezo yako mengi yanazungumzia kile nachosema mimi isipokuwa wewe unalaumu upande mmoja wa Muungano wakati hali hii imeridhiwa na Bunge la muungano, laa sivyo tungesikia Wabunge wa Bara wakipinga yanayofanyika upande wa pili.

Tena Tundu Lissu na Chadema walikuwa wakiunga sana mkono juhudi za upande wa Zanzibar wakati ule wa UKAWA. Alifikia kusema Muungano huu ni mpango wa Nyerere na kwamba Zanzibar inatawaliwa na Bara! Akinadi Nyerere alizoea kula vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.. Records zipo, tusipende kuzusha vitu ambavyo Bara waliridhia kila kinachofanyika Zanzibar kuhusiana na Muungano.

Ukitaka tuzungumzie Serikali 3 kwa mazuri na mabaya yake, ntakwambia nipo tayari kabisa na siombri tufikie huko kwa sababu mzigo tunaobeba sasa hivi kinyume cha Katiba kitahalalishwa kabisa. "Don't jump into deep river if you can't swim"

Nakuomba anzisha MADA nyingine kuhusiana na Serikali 3 kwa mtazamo wako, mimi nitakuja na mtazamo wangu. Kisha tutapima faida na hasara, if it real worth kama sii Chuki za watu ndio zinatusukuma kufanya yasowezekana..

KARIBU sana, maasalaam
 
NENO Serikali ni chombo kilichoundwa kuongoza shughuli za Serikali hiyo mahala fulani na sii mtu mmoja kusimamia mambo ya Upande Fulani.
Mkuu awali ya yote nikutake radhi ikiwa nachangia kitu nje ya mada yako. Nilidhani mada ni pana itahusisha mambo yote. Unaponisihi nianzishe uzi wa serikali 3 pengine ni katika kubakiza uzi huu kwa maana iliyokusudiwa. Niruhusu nijibu machache kama ulivyoeleza

Niliposema Makamu wa pili wa Rais wakati wa Nyerere Mh Kawawa alipewa jukumu la kushughulikia mambo ya Tanganyika nilimaanisha '' Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais'' na si mtu binafsi.
Nimetumia jina Kawawa kwa vijana kama ithbati kwamba Ofisi ya Makamu wa pili ilishikwa na Kawawa.
Tunaposema Serikali 3 ina maana zimeundwa wizara zake kushughulikia shughuli zote za usimamizi na utekelezaji ilivyo ama ilivyokuwa upande wa Zanzibar.Kwa hiyo Bara haikuwa na Serikali yake na hata Mawaziri wa Muungano walishughulika na mambo yote ya Muungano pande zote mbili. Hali yale hii ndio kiini cha mimi kusema Mbananga Chake hana Kondo, tusilaumu upande mmoja wakati Bunge la Jamhuri wameridhia mabadiliko hayo.
Mkuu sikweli kwasababu; Mwaziri wa Mifugo, Utalii, Elimu, Ujenzi, Afya, Kilimo, Viwanda, Nishati kwa uchache tu wa kuwataja hawana shughuli zozote Zanzibar na wala hawatambuliwi. Ikiwa ni hivyo, mambo wanayosimamia ni ya Tanganyika ingawa wamebeba nembo ya JMT.

The fact that hawakutajwa kama Mawaziri wa Tanganyika bado haiondoi ukweli kwamba wanashughulikia mambo ya Tanganyika bila kutajwa ni mawaziri wa Tanganyika. Tunajidanganya wenyewe.

Waziri asiye na kazi Zanzibar unamwitaje wa Muungano? Huyu ni Waziri wa Tanganyika. Ni kama mtu akiamua kukuita Mwanaume badala ya Mkandara katika ku conceal kitu fulani

Ni upuuzi ule ule wa kuita serikali ya Tanzania Bara. Ukishakuwa na Tanzania hakuna Bara. Hiyo ya Tanzania Bara haikuwepo wakati wa Uhuru. Zanzibar haikuungana na Tanzania Bara. Katika kukwepa neno Tanganyika, Watu wanajidanganya kwa kusema Tanzania Bara, upuuzi mtupu.

Hebu nieleze Waziri Mkuu ana jukumu gani Zanzibar ukiachilia kualikwa kufungua majengo siku za Jan 12 ili waweze kupata pesa zaidi za Tanganyika. Nipe kazi moja tu ya Waziri mkuu. Nipe kazi moja tu yaWaziri wa Utalii akiwa Zanzibar. Nipe kazi moja tu ya Waziri wa Afya akiwa Zanzibar n.k.

Kama Waziri hana kazi Zanzibar ataitwaje wa Muungano? Na kama si wa Muungano huyo ni wa kitu gani?
People including erudite should stop fooling themselves
Leo hii hata Yale mambo 11 ya awali ya Muungano mengi hayapo tena acha yaloongezwa kufikia 22. Na ukitazama tulipofikia Waziri wa JMT katika mambo ya Muungano hana mamlaka Zanzibar. Na maelezo yako mengi yanazungumzia kile nachosema mimi isipokuwa wewe unalaumu upande mmoja wa Muungano wakati hali hii imeridhiwa na Bunge la muungano, laa sivyo tungesikia Wabunge wa Bara wakipinga yanayofanyika upande wa pili.
Yale mambo 11 yameondolewa na Zanzibar bila kushirikisha Tanganyika ikiwemo gesi na mafuta, Bandari n.k.

Ukiona jambo Zanzibar haijaliondoa ujue wananufaika nalo. Mfano, Elimu ya Juu haikuwa katika 11, iliongezwa katika 22. Hata siku moja hutasikia Wazanzibar wakitaka Elimu ya juu iondolewe kwasababu vijana wa Zanzibar ni wanufaika, kwanza kwa mikopo wasiyorudisha na pili nafasi za upendeleo katika vyuo hata kama wa D 2

Katika yale 22 yanayolalamikiwa hakuna hata moja lenye manufaa kwa Tanganyika, ni kwa manufaa ya Wazanzibar. Kulalamikia Tanganyika ni kutokuwa mkweli.

Nakupa challenge, katika 22 tafuta moja tu utueleze hapa Tanganyika iliongeza ili kunufaika nayo kivipi.

Kwavile Wazanzibar ni watu wa kusikiliza hadithi zaidi ya kutafiti kuna mtu aliwadanganya kuhusu mambo 22.
Akina OMO ndio kazi yao na wanapoulizwa hawana majibu. Juzi si aliulizwa mamlaka kamili ni yapi.

Jibu la OMO likawa mchezo kwamba Zanzibar hairuhusiwi kujiunga na mashirikisho ya soka ya duniani.
OMO haelewi mambo mawili, kwanza, waliyoondoa Ligi kuu ni Wazanzibar wakiongozwa na Ali Salehe na Alberto. Pili, OMO haelewi kwamba sheria za kimataifa zinaangali bendera! na iliyopo ni ya JMT.

Ili kuondoa mzozo ondoa yote 22 kama Mzee Warioba alivyoshauri ! Ondoa hata kesho tuone nani ataumia!
Mkandara waelezieni Wazanzibar kwamba Tanganyika has nothing to lose! absolutely nothing!
Muungano ni pride tu ya Pan Africanism na legacy ya Nyerere, short of that hatuihitaji Zanzibar

Kuhusu mawaziri, hili umesema vema lakini wanaohusika na ujinga ni Wazanzibar. Hivi Katiba yao inawezaje kuwa na ukuu kuliko ya JMT? Ikiwa sheria za Bunge Dodoma lazima zipitishwe BLW tena licha ya Wazanzibar kuwepo Dodoma hawa watu wanawezaje kumheshimu Waziri wa Muungano!
Tena Tundu Lissu na Chadema walikuwa wakiunga sana mkono juhudi za upande wa Zanzibar wakati ule wa UKAWA. Alifikia kusema Muungano huu ni mpango wa Nyerere na kwamba Zanzibar inatawaliwa na Bara! Akinadi Nyerere alizoea kula vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.. Records zipo, tusipende kuzusha vitu ambavyo Bara waliridhia kila kinachofanyika Zanzibar kuhusiana na Muungano.
Nadhani ulimuona TL na T-shirt ya Tanganyika kabla ya kwenda mahabusu. Nilimwelewa baada ya kutomwelewa siku nyingi sana. Nikupe mfano wa kutafakari. Kabla ya vita ya Iran vs Marekani/Israel kulikuwa na maandamano Tehran tunayojua yaliratibiwa na CIA/MOSAD, Unadhani Trump anayeita Iran terrorists anawapenda Wairan! kama utanielewa
 
Tangu awali pande mbili za muungano zilikuwa na malengo tofauti, na malengo yao yakafunikwa na ulaghai.

Mwalimu alitaka serikali moja, mbili ilikuwa ni kianzio tu. Angalia jitihada za makusudi alizofanya kuongeza mambo ya muungano na kudhoofisha Zanzibar.

Upande wa Pili, Karume alitaka kuutumia muungano kama kinga ya utawala wake katika kipindi kigumu baada ya mapinduzi. Isingekuwa vyombo vya ulinzi vya Tanganyika (kwa kofia ya Tanzania) serikali ya mapinduzi chini ya Karume isingedumu. Na ndio maana alisema muungano ni kama koti, likibana unalivua.

Kutoka 1964 mpaka 1985, mambo yalikuwa yanakwenda upande wa Nyerere. Kutoka 1985 mpaka leo mambo yamekwenda opposite to the extreme.

Kwa sasa tuna nchi moja yenye ma amiri jeshi wakuu wawili. Kila mmoja kwa mujibu wa katiba zao anaweza kuanzisha majeshi yake kulingana na mahitaji.

Mwarobani wa hili ni ukweli na uwazi. Watu waseme, kama wanataka muungano basi uwe serikali moja, tuachane na huu uhuni. Kama sivyo basi kila mtu ashike zake. Siyo dhambi kutengana. Tulikuwa nchi nbili tofauti.
 
Tulikua nchi 2 zilizo ungana ila sasahivi tuna nchi mbili zilizo ungana lakini moja (zanzibar) ina mamlaka kamili na haitakiwi kabisa kuingiliwa kwy mambo yako ilhali hii nchi nyingine (Tanganyika) haitakiwi kabisa ijulikane kama ipo bali ilikufa baada ya muungano na ukiitaja hata kwa kuiulizia tu unaonekana mbaguzi isipokuwa zanzibar ni haki kuizungumzia. Documents zinaonyesha zanzibar kumezwa ila kiutendaji Tanganyika sio tu imemezwa bali imekufa na haitakiwi kufufuka ni Uhaini.
 
Mkuu awali ya yote nikutake radhi ikiwa nachangia kitu nje ya mada yako. Nilidhani mada ni pana itahusisha mambo yote. Unaponisihi nianzishe uzi wa serikali 3 pengine ni katika kubakiza uzi huu kwa maana iliyokusudiwa. Niruhusu nijibu machache kama ulivyoeleza

Niliposema Makamu wa pili wa Rais wakati wa Nyerere Mh Kawawa alipewa jukumu la kushughulikia mambo ya Tanganyika nilimaanisha '' Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais'' na si mtu binafsi.
Nimetumia jina Kawawa kwa vijana kama ithbati kwamba Ofisi ya Makamu wa pili ilishikwa na Kawawa.

Mkuu sikweli kwasababu; Mwaziri wa Mifugo, Utalii, Elimu, Ujenzi, Afya, Kilimo, Viwanda, Nishati kwa uchache tu wa kuwataja hawana shughuli zozote Zanzibar na wala hawatambuliwi. Ikiwa ni hivyo, mambo wanayosimamia ni ya Tanganyika ingawa wamebeba nembo ya JMT.

The fact that hawakutajwa kama Mawaziri wa Tanganyika bado haiondoi ukweli kwamba wanashughulikia mambo ya Tanganyika bila kutajwa ni mawaziri wa Tanganyika. Tunajidanganya wenyewe.

Waziri asiye na kazi Zanzibar unamwitaje wa Muungano? Huyu ni Waziri wa Tanganyika. Ni kama mtu akiamua kukuita Mwanaume badala ya Mkandara katika ku conceal kitu fulani

Ni upuuzi ule ule wa kuita serikali ya Tanzania Bara. Ukishakuwa na Tanzania hakuna Bara. Hiyo ya Tanzania Bara haikuwepo wakati wa Uhuru. Zanzibar haikuungana na Tanzania Bara. Katika kukwepa neno Tanganyika, Watu wanajidanganya kwa kusema Tanzania Bara, upuuzi mtupu.

Hebu nieleze Waziri Mkuu ana jukumu gani Zanzibar ukiachilia kualikwa kufungua majengo siku za Jan 12 ili waweze kupata pesa zaidi za Tanganyika. Nipe kazi moja tu ya Waziri mkuu. Nipe kazi moja tu yaWaziri wa Utalii akiwa Zanzibar. Nipe kazi moja tu ya Waziri wa Afya akiwa Zanzibar n.k.

Kama Waziri hana kazi Zanzibar ataitwaje wa Muungano? Na kama si wa Muungano huyo ni wa kitu gani?
People including erudite should stop fooling themselves

Yale mambo 11 yameondolewa na Zanzibar bila kushirikisha Tanganyika ikiwemo gesi na mafuta, Bandari n.k.

Ukiona jambo Zanzibar haijaliondoa ujue wananufaika nalo. Mfano, Elimu ya Juu haikuwa katika 11, iliongezwa katika 22. Hata siku moja hutasikia Wazanzibar wakitaka Elimu ya juu iondolewe kwasababu vijana wa Zanzibar ni wanufaika, kwanza kwa mikopo wasiyorudisha na pili nafasi za upendeleo katika vyuo hata kama wa D 2

Katika yale 22 yanayolalamikiwa hakuna hata moja lenye manufaa kwa Tanganyika, ni kwa manufaa ya Wazanzibar. Kulalamikia Tanganyika ni kutokuwa mkweli.

Nakupa challenge, katika 22 tafuta moja tu utueleze hapa Tanganyika iliongeza ili kunufaika nayo kivipi.

Kwavile Wazanzibar ni watu wa kusikiliza hadithi zaidi ya kutafiti kuna mtu aliwadanganya kuhusu mambo 22.
Akina OMO ndio kazi yao na wanapoulizwa hawana majibu. Juzi si aliulizwa mamlaka kamili ni yapi.

Jibu la OMO likawa mchezo kwamba Zanzibar hairuhusiwi kujiunga na mashirikisho ya soka ya duniani.
OMO haelewi mambo mawili, kwanza, waliyoondoa Ligi kuu ni Wazanzibar wakiongozwa na Ali Salehe na Alberto. Pili, OMO haelewi kwamba sheria za kimataifa zinaangali bendera! na iliyopo ni ya JMT.

Ili kuondoa mzozo ondoa yote 22 kama Mzee Warioba alivyoshauri ! Ondoa hata kesho tuone nani ataumia!
Mkandara waelezieni Wazanzibar kwamba Tanganyika has nothing to lose! absolutely nothing!
Muungano ni pride tu ya Pan Africanism na legacy ya Nyerere, short of that hatuihitaji Zanzibar

Kuhusu mawaziri, hili umesema vema lakini wanaohusika na ujinga ni Wazanzibar. Hivi Katiba yao inawezaje kuwa na ukuu kuliko ya JMT? Ikiwa sheria za Bunge Dodoma lazima zipitishwe BLW tena licha ya Wazanzibar kuwepo Dodoma hawa watu wanawezaje kumheshimu Waziri wa Muungano!

Nadhani ulimuona TL na T-shirt ya Tanganyika kabla ya kwenda mahabusu. Nilimwelewa baada ya kutomwelewa siku nyingi sana. Nikupe mfano wa kutafakari. Kabla ya vita ya Iran vs Marekani/Israel kulikuwa na maandamano Tehran tunayojua yaliratibiwa na CIA/MOSAD, Unadhani Trump anayeita Iran terrorists anawapenda Wairan! kama utanielewa
Narudia tena kusema na kusisitiza kwamba hayo unayozungumza ndio hali iliyopo sasa haikuwa hivyo wakati wa Mwalimu.

Halafu unatakiwa kuelewa kwamba Serikali kwa maana ya Government sio Wizara peke yake. Serikali kwa maana ya Dola katika muundo wake huwa na mihimili mitatu. Yaani Serikali, Bunge na Mahakama. Na kwa maana hiyo hatujawahi kuwa ya Serikali 3. Kuwa na Makamu wa rais ambaye hakuunda Serikali yake ni sawa na Waziri tu maana ameteuliwa na rais. Ni jina la cheo tu ambacho hakibadilishi muundo wa Serikali.

isipokuwa kama nilivyosema awali, kuna Utekelezaji fulani unaotoa mamlaka kana kwamba tuna Serikali 3 ama tuna Muungano wa Jumuiya ndio maana nikaita MSETO. Chukua pia kama alivyosema Mzee Warioba. Wakati ule wa Mwalimu Bunge la Jamhuri lilikuwa na mamlaka kamili, Mahakama ilikuwa na Mamlaka kamili. Leo hii sivyo na hata Marais tunao wawili wanaopigiwa kura na Wananchi na wana Mamlaka hamili ya kuunda Serikali

Na kuhusu Muungano. Nadhani huijui Historia ya nchi yetu kwa sababu Zanzibar haikuwahi kuwa NCHI. Zanzibar ni MJI, hili jina la nchi lilitokana na utawala wa Sultan Sayyid alipohamishia makao makuu pale Zanzibar (Mji - Sultanate) kama alivyokuwa Sultan wa Kishiraz wa Kilwa. Mipaka ya Kilwa Sultanate haikuishia Kilwa kisiwani bali lilikuwa jina la Utambulisho wa Ufalme kutokana na makao ya Sultan mwenyewe kuwa Kilwa.

Kwa hiyo, hii Zanzibar ni sawa na Tanganyika, nchi zote hizi mbili hazikuwepo kabla ya wakoloni na pengine kabla ya Muingereza kwa sababu hazikujulikana kama NCHI bali HIMAYA za Kifalme.

Upande wa Tanganyika kulikuwa na Machief wa Makabila na Zanzibar kuwa nchi ni baada ya Sultan kuwauzia Wajarumani na Waingereza pwani za Afrika Mashariki akabakia na visiwa viwili, ndio wakaiita NCHI.

Wakati Mjarumaini anatawala, eneo la Utawala wake lilikuwa mpaka Zanzibar, hutasikia wakisema hilo ila utasikia Muingereza.na Sultan tu.

Hii mipaka imewekwa na Wakoloni mpaka majina wametunga wao. Kwa nini sisi tusiwe na jina letu wenyewe? nchi yetu wenyewe?.na kwa mipaka yetu wenyewe? Halafu wanakuja Wanasiasa uchwarw kutaka kuturudisha kwenye Ukoloni mambo leo?

Narudia kusema hivi, nguvu kubwa ya matukio ya Zanzibar yamekuja baada ya Mwalimu kututoka! Wasingethubutu kuleta uhuni huu Na huu utitiri wa Vyama vya Siasa umewapa nafasi Hizbu kurudi na Siasa zake za kuutukuza Usultan. Kumbuka hata Hitler alipenyeza wakati walipokuwa na utitiri wa vyama vya Siasa.

Leo Tanzania tuna vyama 19, it's very dangerous kwa mustakabali wa Taifa hili. Juzi nawasoma baadhi wasomi wanasema tuongeze Vyama vya Siasa sijui kwa vijana! Binafsi ningeshauri vyama vitatu au vinne tu vya Siasa tena SHARTI viwe na Itikadi zinazo tofautiana ili Sheria utunzi wa Sheria utokane na matakwa ya Wananchi.

Na kwa bahati mbaya sana Wazanzibar wengi wanajinasibisha wao na Uarabu kuliko Uafrika. That's mental slavery hatuwezi kuendekeza akili za Kitumwa karne hii HAPANA and we can't give in kwa sababu tu ati Hizbu wana nguvu kubwa Zanzibar na ndio maana nasema Viongozi hawa wamemsaliti Mwalimu na hata wale wa ASP nashangaa sana kuona wamekubali yaishe.

Kuhusu Tundu Lissu, kwangu mie jamaa ni MSANII sana, anajua kucheza na akili za watu hana msimamo kabisa. Aliyasema yale wakati wa UKAWA. Leo anajiita Mandela kama kwamba Tanganyika inapigania Uhuru.

Ndiye alowafukuza kina Zitto na Kitila, Akaja mgeuka Dr. Slaa wakati wa Lowassa na alisema mengi mabaya, vna alihalkikisha Lowassa harudi tena kugombea akaingia yeye. Vijana wengi walikihama Chama wakati yeye mgombea Urais. Muda wote alikuwa anapiga hesabu za yeye kuwa rais wa nchi, yeyote alikuwa njiani alimkanyaga, lawama akabebeshea Mbowe kwa sababu Mbowe alimuamini sana Tundu Lissu.

Na Mbowe kapigwa vile chini vile vile Tundu Lissu anaamka Shujaa wa Taifa. So the guy ni kama yule rais wa Ukraine, play victim for the world to sympathise with you! Na anafanikiwa sana maana dunia hii unashadadia sana Ujinga.

Anyway, niishie hapa kwa leo, maana tumefikia hali mbaya sana kuutaka Utanganyika, sijui Uzanzibar yaani chuki za kipumbavu kabisa utadhani familia moja wanagombania Urithi. Nchi hii kubwa mnataka tugawane kuti kisa Fedha sijui Utajiri. Utajiri wenyewe basi mliutafuta, Mliuchuma hapana! "Chako Changu, Changu Changu" mentalty...

Maasalam...
 
Muungano ukivunjika sina hakika kama serikali ya mapinduzi itamudu hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Wamedekezwa sana.
Hilo sio tatizo hata kidogo kuna visiwa kibao Uchumi wake wanategemea Utalii na Zanzibar inaweza kabisa tena kwa mafanikio makubwa. Leo hii Zanzibar inapokea ndege nyingi za Kimataifa Kuliko Uwanja wa Nyerere. Bado kuna Uvuvi wa Bahari.

Tatizo likitokana na uchangiaji wa mfuko wa Taifa, kesho tutaanza kuisema Mikoa ambayo haichangii, Kanda ya Ziwa na dhahabu zao watadai NCHI yao. Kule Mtwara na gas nao watadai NCHI yao. Hujagusia Kilimanjaro na Arusha. Kumbuka kabla ya Uhuru hizi zilikuwa himaya za Machief na hawakupendana kabisa. Ukabila utarudi kwa vizazi vijavyo. Mnataka tuwaachie wajukuu zetu zahma hizo?

Tukianza Upuuzi huu wa kuigawa nchi elewa hata amani itatoweka. Tazama Sudan, Ethiopia, Somalia, Libya yaani nchi zilotengana kwa sababu za Kisiasa, vita baina yao haitakoma. Mipaka ni ujanja wa Ukoloni Mambo leo na mwanzo wa UADUI.
 
Muungano ukivunjika sina hakika kama serikali ya mapinduzi itamudu hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Wamedekezwa sana.

..Zanzibar ina uwezo wa kujitegemea ikiwa wataamua kuwa kisiwa cha utalii, maraha, na mambo mengine ya kidunia.

..Na watakaoweza kumuda mazingira hayo ni Wazanzibari matajiri.

..Wazanzibari masikini watalazimika kuhamia Tanganyika ambako kuna nafasi ya ku accomodate watu masikini.
 
Back
Top Bottom