Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,601
- 34,760
Kwanza, kwa miaka 62 Watanganyika walipoteza nchi yao kwa ajili ya Muungano, hawakuwahi kuisema Zanzibar. Hoja ya Tanganyika imeletwa mezani na Wazanzibar kwa kisingizio kwamba Bara wamejificha katika koti la Muungano. Hivyo Utanganyika umeombwa na Wazanzibar. Mkandara hakuona hiyo kama chuki za kipumbavu.Tumefikia hali mbaya sana kuutaka Utanganyika, sijui Uzanzibar yaani chuki za kipumbavu kabisa utadhani familia moja wanagombania Urithi. Nchi hii kubwa mnataka tugawane kuti kisa Fedha sijui Utajiri. Utajiri wenyewe basi mliutafuta, Mliuchuma hapana! "Chako Changu, Changu Changu" mentalty...
Hapa JF kuna mjadala mkandara ukitetea hoja za Wazanzibar kwamba wasikilizwe. Leo unaita upuuzi na upumbavu kwa hoja zile zile ulizotetea wakati upuuzi na upumbavu ukiwa ''in the making'
Pili, Wakati Maalim Seifa na akina Jussa wakitukana Muungano na kumwita Nyerere LAANATULLAH, wakidai mamlaka kamili Mkandara alikuwa kimya hakuona upuuzi na upumbavu, leo anauona
Tatu, wakati Zanzibar inataka mgao wa kila inachotaka Mkandara ulisema '' ni wadogo'' wanastahili kusaidiwa. Mkandara hakuona upuuzi na upumbavu kwamba zilikuwa nyufa za Muungano, hatimaye amefunguka macho
Nne, wakati Wazanzibar wakiusema Muungano ilikuwa ni halali, Mtanganyika akisema muungano ni haramu.
Prof Kabudi akiwa bado 'mzima' alisema '' Watanganyika wana yao moyoni wakiyatoa na kuidai Tanganyika yao itakuwa tatizo'' . Mkandara alikuwa akimya kwasababu Zanzibar ina haki ya kusikilizwa, si Tanganyika
Tano, hoja ya Mkandara ya changu ni changu na chako ni changu haiwahusu Watanganyika. Tanganyika imebeba muungano 100% . Waeleze Z'bar si kuwalaumu waliobeba zigo la misumari mgongoni
Sita, wakati Zanzibar inaanzisha Taasisi mbadala wa zile za JMT Mkandara alikuwa kimya. Leo akilulizwa kwanini kuna Taasisi mbadala hana jibu anawalaumu Watanganyika wanaohoji.
Hizi taasisi zinazoitwa za Muungano kama TCRA ni za Tanganyika, Zanzibar wana zao. Wazanzibar wanazitumia wanapohitaji mafao. Ni kama kuwa na kitambulisho cha NIDA kwa ajili ya kufanya shughuli Tanganyika
Mfano, Makusanyo ya TCRA yatokanyo na mawasiliano, Zanzibar inapewa sehemu yake. Yaani Mkandara akimpigia simu ndugu yake Ukerewe kuna aslilimia inapelekwa Zanzibar.
Halafu Mkandara huyo huyo anasema sisi ni nchi moja Tanzania kwanini kuwe na double taxation! Hajiulizi kwanini simu ya Mtwara-Musoma iwe na asilimia inaypelekwa Zanzibar
Saba, Mkandara anasema hoja ya kudai kuona mchango wa Zanzibar katika Muungano ni ya kipuuzi.
Mkandara huyo huyo anatetea hoja za Wazanzibar kudai wapewe lakini hataki kusikia wakiambiwa wachangie.
Tumefika hapa kwasababu tlifumbia macho upuuzi wakati unajijenga! Hatukuambina ukweli kwa kisingizio cha Muungano ni tunu yetu. Tuliwapa Wazanzibar kama Raia ''special'' wanaopaswa kuhudumiwa na kuamua hatma ya Tanganyika. Ule muda aliosema Prof Kabudi nadhani umewadia.
Mnyonge mnyngeni haki yake mpeni, Prof Kabudi alikuwa mbele ya muda miaka 12 iliyopita