Kama unafuatilia sakata la Bexit lilizua balaa. England ilitaka serikali yake kwamba maamuzi ya Great Britain yali iumiza, hawakuta Brexit. Maana yangu ni kwamba behind the scene kuna fukuto la kuidai England
Wazanzibar wanasema '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''. Wapo sahihi kabisa kwasababu Tanzania inatokana na Nchi mbili. Ukiondoa Zanzibar kama walivyojiondoa huna Tanzania, unabaki na Tanganyika. Kumbuka Nchi zilizoungani ni ''The Republic of Tanganyika and Zanzibar''
Je, Zanzibar wamejiondoa katika Muungano! Jibu ni ndio kwasababu kila Taasisi ya Muungano wana mbadala. Sasa hivi wanajenga Chuo cha Uhamiaji na Polisi baada ya kuwa na Jeshi lao kama JWTZ wakiliita vikosi maalum.
Wazanzibar watautumia Utanzania kwa masilahi. Mfano, wataingiza bidhaa na kuchukua kodi halafu wanavusha bara kwa kisingizio cha Nchi moja. Kodi wanazochukua hazivuki bahari na hazimsaidii Mtanganyika.
Pili, wanapotafuta nafasi za Masomo wanatumia Utanzania . Tatu Wazanzibar wakitaka ajira za Tanganyika wanatumia Utanzania kama wanavyotumia katika ardhi. Nje ya hapo wao ni Wazanzibar hawana habari na Utanz
Kuendelea kutumia jina Tanzania kunatoa Uhalali ule ule ndani ya Uharamu. Hutaweza kumwambia Mzanzibar hupaswi kuwa na abcd kwasababu ni Mtanzania na ana haki kwa jina, lakini hana haki
Wazanzibar wanajiita hivyo ili kuwabagua Watanganyika. Ili kuondoa mzizi wa Fitna tunataka Tanganyika ya 1961. Tanganyika itakayoshughulika na mambo yake bila kuyafanya ya Muungano
Kuna swali unalikwepa sana! kama unaamini katika Unitary state kwanini kuna Taasisi mbadala Zanzibar?
Yes itatupunguzia mzigo sana. Kwasasa tunagharama za Muungano , gharama za Tanganyika na za Zanzibar
Mkandara unaangalia idadi ya viongozi kama kigezo cha gharama na ku ignore mambo makubwa zaidi.
-Kwamba Zanzibar itawajibika katika Muungano kama mshirika na si kucheza msewe juu ya Mbleko
Mfano, mbona hufikirii gharama za Wabunge wa Zanzibar wanaotetea Zanzibar kulipwa na kodi za Mtanganyika
- Gharama za viongozi wa Zanzibar kuhudumiwa na pia Taasisi za Muungano kwa kodi za Watanganyika
- Gharama za watumishi wa Muungano na mafao ya kustaafu kugharamiwa na Watanganyika peke yao
- Gharama za 10% ya kodi na rasilimali za Watanganyika kupelekwa Zanzibar! unajua ni kiasi gani?
-Gharama za kufidia Bajeti ya Zanzibar kwa kitu kinachoitwa GBS
-Gharama za Elimu ya juu kwa kodi za Watanganyika
- Kwasasa hata simu ukipiga Mtwara-Ukerewe kuna per cent inapelekwa Zanzibar eti tuna shea 255! upuuzi tu
- Gharama za Taasisi kama IMO wakati kodi za Meli zinakusanywa Zanzibar peke yake
- Zanzibar itawajibika kuchangia Taasisi , kwa mfano, vyuo vya Uhamiaji na Polisi watavigharamiwa wenyewe
- Hapo sijakuwekea gharama za Wizara kubwa 4
Hoja yako ya ongezeko la viongozi haina mashiko kabisa ! soma gharama hizo hapo juu.
Tueleze jamvini, kama unajali gharama ni vipi Wabunge wa Zanzibar wanokuja kujadili mambo 3% wakae Dodoma miezi 3 hadi 6 wakijadili; 1. Mambo yasiyowashusu ? 2, Wabunge wanakuja kwa ajili ya Zanzibar kwanini wasilipwe na kodi za Wazanzibar? Kwanini mtu wa Kigoma au alimlipie mtu asiyemhusu? Hizi gharama kwanini huzioni
Bado unatushawishi sisi ni Unitary state! Bado unatushawishi hakuna ubaguzi! Tofauti wanayoitaka ni ya nini kama sisi ni Nchi moja! Bado unatushawishi hawa ni wenzetu halafu unashabikia wao kuonyesha utofauti
Makamu wa Rais Tanzania kama akina Mpango walifanya kampeni Tanganyika na Zanzibar
Wakati wa Karume, alikuwa kiongozi wa Wazanzibar tu!
Ni kama Mwinyi leo awe Makamu! na ndio msingi wa Rais wa Zanzibar kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri
Kwani kwa Zanzibar ipoje sasa hivi. We're not trying to reinvent the wheel dude! the blue print is there already
Kwa maono yako kwasasa Wazanzibar ku practice ubaguzi dhidi ya Watanganyika linatuunganisha! Dude!
Muulize Saada Mkuya atakueleza Mzanzibar ni nani na Mtanganyika ni nani. Hivi ulisikia akimkemewa!
Saada Mkuya anajua ametumwa aseme nini ! UBAGUZI wa Saada ulitakiwa ulaaniwe, kinyume chake kalaaniwa Mbowe aliyetoa tahadhari! Hata Mkandara hakuwahi kumlaani Saada leo anatushawishi hakuna Ubaguzi! phew!