Tuna Viongozi ambao kwao Siasa ni njia kuu ya ajira inayolipa vizuri sana katika kuondokana na Umaskini, ili mtu yeyote agombee Kiti cha Uongozi wa Kisiasa ni lazima awe amesoma Chuo cha Siasa ili kwanza aihifadhi kichwani Katiba ya Jamhuri. Yapi Maslahi yq Taifa (National Interests).
Mkuu sikubaliana na la kusoma chuo cha siasa! Baada ya Uhuru Baraza kuu la TANU liliundwa na Wazee kwa asilimia 100, hawakusoma popote na wengine walikuwa madereva tu. Nyerere alianza na wasomi wachache akina Msekwa (miaka 28) alikuwa Katibu Mtendaji wa TANU kama sikukosea. Wote walifanya siasa kwa Imani na si shule
Mafunzo ya siasa Kivukoni yalianzishwa ili kukata makali ya Wasomi, ya JKT yalilenga kuwaanda vijana kwa kuondoa tofauti na matabaka.
Leo kuna watu wanaweza kufanya siasa kwa uadilifu wakawa Wabunge kwa Baiskeli. Kwa bahati mbaya siasa imeingiliwa na pesa. Kwamba unanua uongozi ili utengeneze utajiri
Kuondokana na hali hiyo, Wabunge waondolewe kufuru ya pesa. Mshahara wa Mbunge uwe sawa na Katibu Mkuu wa Wizara. Waondolewe shughuli za kamati za kuzunguka bila sababu kupata allowance au kwenda Dubai ili hali si wataalamu, wasilipwe allowance za kukaa kwenye viti, wapewe per diem kama Katibu Mkuu wa Wizara.
Tatu, Wananchi wapewe nguvu za kuwadhibiti Wabunge kama alivyopendekeza Warioba kuhusu ''recalll''.
Nne, Mbunge hataruhusiwa kurudi serikali kwa miaka 5 baada ya siku ya mwisho wa Ubunge.
Hii itadhibiti hongo za vyeo kutoka serikalini na kuwafanya wawe independent na kuwajibika kwa Umma
Tano, kuiweka Mahakama Huru kwa Bajeti na muundo wa kujiendesha ikiwa kama kupata viongozi bila serikali Kuweka ukomo wa Watumishi wa Majaji kwamba wakistaafu hawatateuliwa katika Taasisi za Umma na Ubunge kwa miaka 10
KATIBA MPYA - Turudishe mfumo wa zamani wa Rais mmoja wa JMT na Makamu wake ndiye atakuwa kiongozi wa upande wa pili kwa mambo yasokuwa ya Muungano. Ibakie kuwa MAKAMU wa rais badala ya kuwa na Marais wawili ili kujenga Imani za watu kuwa tuna NCHI moja yenye Historia kubwa hata kabla ya Wakoloni.
Utaratibu uliondolewa kwasababu ya matatizo. Kwa mfano, Makamu wa Pili wa Rais alipotoka Zanzibar, Rais akisafiri alishika nafasi. Swali likazuka, alichaguliwa na nani?
Hoja ya pili, unawezaje kuwa na makamu wa pili ukiwa na SMZ bila Watanganyika kuhoji ipo wapi ya kwao!
Hakuna haja ya kupunguza madaraka ya rais katika kuunda Serikali yake isipokuwa tuondoe KINGA ya VIONGOZI wote Wakiwa madarakani. Separation of Power ya MIHIMILI ya Serikali (Dola) muhimu hakuna kuingiliana katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kuna haja ya kupunguza madaraka ya Rais! Hivi RC, DC, RAS, DED wanafanya kazi gani?
Kumbuka wanamwakilisha. Kinachotakiwa ni Mkoa kuchagua RC wao atakaye manage mambo yote.
Pili, Rais asiteue viongozi wa mashirika! Taasisi zitengeneze taratibu. Kilichoharibu mashirika wakati wa Nyerere ni Siasa kutangulia Utaalam. Kama ni shirika litafute utaratibu wa kupata CEO na Bodi yake!
Hili litamwezesha Rais na serikali yake kuwawajibisha wanaohusika na uzembe na ufujaji
In other words Rais awe ''watch dog'' si participants katika uendeshaji wa mashirika na Taasisi
Tume Huru mimi nadhani Iwe Chini ya Mahakama na Majaji watasaili majina ya Wagombea na kupitisha mmoja kuwa Mwenyekiti wa Tume Huru na atashirikiana na Mahakama nchini kuunda Watumishi na wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ni kuepusha michepuko ya Kisiasa kutofuata Sheria.
Sikubaliani na hili ! tunataka Mahakama na Majaji wawe huru wakisubiri mashtaka na miongozo ya kisheria..
Huwezi kushiriki kuunda Tume halafu ukasimamia kesi kati ya mtu na Tume. Kuna conflict of interest.
Tume iwe kama ya Ghana au Kenya, kwamba, ni independent na Gov au Mahakama.
Naurudia tena Majaji wasishiriki tena katika shughuli za Umma ili kuondoa ile dhana ya ''kuteuliwa''.
Sasa hivi Mahakama zetu ni politics tu kwasababu kuna Majaji wenye mategemeo ya aina mbili
1. Atumikie serikali akistaafu apewe Taasisi au shirika la Umma au Bodi n.k.
2. Wapo walio katika Kanzi data ''data base'' wakivizia teuzi na hivyo maamuzi yao yanalenga kuwafurahisha watawala. Na wengine wanasubiri promotion katika vitengo nao wanafanya kazi ya kufurahisha viongozi
Ni kwamba mtu akiteuliwa kuwa Jaji, baada ya kustaafu anapewa marupu rupu na pensheni zake.
Ataruhusiwa Siasa miaka 10 baada ya kustaafu ikimaanisha hata watawala hawatamhitaji wala hatawahitaji.
Mwisho tuwe na Vyama Vitatu au Vinne tu vya Kisiasa vyenye mrengo wa Itikadi tofauti na hakuna kufukuza Chama chenye Mamlaka ya Kumfukuza Mwanachama kwa sababu Itikadi ni IMANI ya Kisiasa. Wanachama ni wasaidizi (Volunteers) na sii mtaji wa kura wa Chama.
Utitiri wa vyama ni Siasa za CCM. Msajili alipaswa kuhakiki vyama hivyo kama vina Wanachama na Ofisi zinazofanya kazi. Kudhibiti hilo ni kufuata masharti tu.
Leo kuna mtu ana brief case eti naye anaalikwa mkutano wa TCD na Msajili ili kujaza idadi.
Hapa tatizo ni msajili kutozngatia masharti na sheria ya vyama bali kufurahisha CCM
Wananchi hawalazimiki kuwa Wanachama wa chama chochote cha Siasa
Hakuna mwananchi anayelazimika au kukosa haki kwasababu ya kutokuwa mwanachama
Mwananchi awe Huru kuchagua Kiongozi badala ya kufungwa katika hadaa ya Uanachama.
Wariona aslisema kuwepo na mgombea huru
Haingii akili Kama mimi naamini katika UJAMAA, nifukuzwe Uanachama kwa sababu simkubali au sikubaliani na Kiongozi. Hii husabanisha makundi, hasada na chuki ndani ya Chama na zaidi baadhi kujifanya Chama kina wenyewe.
Chama kiruhusiwe kujiendesha kinavyoona inafaa. Kama Mwanachama haridhiki na Sera za Chama X aondoke kwenda Chama Z. Kama harihidhiki na kote apewe fursa ya Kuwa HURU au mgombe Huru
Mengineyo watajaza wengine lakini kwa mtazamo wangu tuna fail sehemu moja kubwa - UONGOzi BORA.
Hapo ndipo tatizo lilipo! Umasikini wetu ni failure ya Viongozi, hatuna viongozi wanaojua Management!