Binadamu tumeumbwa kila mooja wetu amepewa akili tunatofautiana matumizi yake tu. Na sidhani kama naweza washawishi lolote juu ya Zanzibar, Serikali 2 wala hili jipya la Tundu Lissu maanake mmesha kuwa mateka wa Story hadith kolea!
Ebu jiulizeni, Tundu Lissu alokoswa koswa kuuawa na Magufuli alikubalije kurudi nchini kugombea Urais tena dhisi ya hasidi wake baada ya kuahidiwa Usalama wake na mtunyule yule alotaka kumuua? Nanjamaa.karudi kweli tena kwa mbwembwe nyingi Sikuamini macho yangu. Magufuli yule.watu waliogopa hata kuisema Serikali yake? (Tulivyoaminishwa)
Hivi ungekuwa wewe ungerudi? Semeni Ukweli? Kwa.ujasiri gami yaani.. Halafu Magufuli akampa kweli Ulinzi akamwacjia atembee mikoa yote kufanya kampeni kali, fedha zilitoka wapi? Katika kampeni zake zote za ONE LOVE kuna kila sherehe!
Halafu baada ya Uchaguzi ati Magufuli yule yule alomrudisha nchinj ndio kataka tena kumuua baada ya Uchaguzi? Jamaa akatimka tena Ubelgiji na kuanza kampeni dhidi ya NCHI yake badala ya CCM au Magufuli.
Hizi kamba jamani mtanisamehe mimi mtoto wa Mjini sifungiki kirahisi hivyo! Nimesema toka mwanzo walomtwanga risasi Tundu Lissu walikuwa WAHUNI tu, sio Usalama wala Jeshi la Polisi, na ubaya ni kwamba wakati ule vyama hivi vya Siasa vyote vilikuwa vikimiliki majeshi yao. That was very dangerous kwa Usalama wa Taifa. Mpaka Majambazi walikuwa na SMG.
Kuhusu Area D pale nimesema ni Eneo la Mhimili wa Bunge wanakaa Viongozi wa Bunge, Mawaziri (Wabunge) na Wabunge wengine. Ulinzi unafanywa na Polisi kwa viongozi wa Wateule.na upande wa Wabunge wana Private Security Guards, inategemea kutoka kampuni gani. Hapakuwa na Walinzi wa aina moja ama kituo kimoja.
Kuna mtu kasema Bunge linalindwa na Askari Polisi, ndio kwa sababu Bunge ni sehemu ya Serikali kisha hata wewe unalindwa na Polisi. Kina.msemo usemao Serikali ni WATU, Serikali ni SISI.. Sijui mtaitafsirije kauli hii.
Kama mnakumbuka hata mipango yote ya kuntoa Lissu pale na kumpeleka Hospital ilifanywa na Bunge sio Serikali (Executive) mimi nazungumzia protocal nyis mnatumia hisia zenu ama matango mlolishwa. I know how the System works..
Halafu
Nguruvi3 Anasema Tundu Lissu alikuwa akifuatiwa toka kanisani. Mimi nakumbua Tundu Lissu aliwahi kusema anafuatiliwa toka Dar wakati ule wa scandal ya Makinikia na Acacia! Sijui Alisomamisha gari akawauliza wanataka nini? At time Tundu Lissu alikuwa anawasaidia Barricks (Acacia) kujua kinachoendelea Serikalini - Akitekeleza kazi ya Wahuni.
Haya, Baadae wakiwa Dodoma mkasema Makonda kaonekana Dodoma sijui ndiye alofanya mpango wa.kumpiga risasi Tundu Lissu. Makonda akatoka akarhibitisha alikuwa Dar siku walizosema. Yaani maneno mengi yakasemwa Magu akaendelea kushughulika na Acacia, akaita viongozi wa vyama vyote wakutane nar Ikulu, Chadema pekee ndio Mbiwe hakwenda kuonana nae.
Ok, Najiuliza ilikuwaje Samia akenda Nairobi kumtazama Tundu Lissu asionekane YUDA msaliti wa Magufuli? Asiishie hapo tu akalimpa mafao yake ya Ubunge, akamfadhili akiwa Belgium, kutudi akamoa na gari la Kutembelea.. Ghafla Tundu Lissu adui yake ati ni Mbowe Mwenyekiti wake ati Kalamba Asali? Daaah! Ghafla hivyo!
Na nyie mkaamini kabisa kwamba Mbowe kalambishwa Asali na Samia wakati Mbowe huyo huyo kafilisiwa mali zake zote na Magufuli, Mbowe mkapa huyo mpaka kesho hajarudishiwa hata Kijuko lakini Tundu Lissu alofadhiliwa kapewa na gari la kutembelea na Samia na hata kukutana na Abdul ndio MSAFI. Oooh alipelekwa na Wenje, yaani sijui Huyu Jamaa Mchawi?
Kikubwa kilicho nishangaza mimi zaidi ni Uchaguzi wa 2025, Chadema pamoja na jitihada zote za kufanya Reforms bado.wataingia Uchaguzi Mkuu na nilijua kama Tundu Lissu atasimama hata bila reforms zote, atashinda Uchaguzi a land slide asilimia 80-90.
Sikuona kabisa Samia akimshinda Tundu Lissu 2025, hata kama wataiba kura ingekuwa sii rahisi kabisa kupindua matokeo. Pia kina January, Nape, Bashe wajuzi wa kampeni na Bao la Mkono wametupwa nje, Yaani ilikuwa mteremko tu. October 2025, CCM kulisha vurugika, walowania kugombea wamepigwa chini, Kwenye Ubunge majina yamekatwa! Wwru roho juu. Chadema wakaachia kamba! Khaaaa?
Ukishangaa ya Firauni Utaona ya Mussa! Hee, ghafla namuona akiwambia watia Nia hawataenda Uchaguzi! Wale watu walikwenda kwa nia ya Kugombea Uchaguzi Mkuu, Mwenyekiti anawataarifu ghafla hakuna Uchaguzi., halafu anadai ilikuwa toka mwanzo - No reform No Election hawatashiriki Uchaguzi...What a Play!
Upande wangu nikajua hii michezo tu, Samia atapita bila mshindani na kukamilisha yote wakamweka ndani mchezo umeisha, Mpina nae akajitutumua wakamweka kando! Njia nyeupeeee.. To me all that was well planned.
Mtanisamhe Wana Chadema lakini huyo Tundu Lissu wenu simuamini kabisaa, kwangu ni.MHUNI na Kesi atashinda, wakati Muafaka Ukifika anarudi Mtaani Rastaman Bob Manley - ONE LOVE. Muwe na siku njema.
Jumaa Mubarak - Maasalaam
Umeongea mambo mengi lakini nitayajibu kwa kifupi ili nisikuchoshe.
1.ULINZI AREA D.
Ni eneo lililokuwa makazi ya Naibu Spika, Waziri wa Madini na Nishati, Makatibu wakuu, na Wabunge.
Mahali popote wanapoishi viongozi ni lazima pawe na ulinzi. Naibu Spika, Waziri. lazima makazi yao yawe na ulinzi 24/7.
2.RISASI ZILITOKA WAPI [ mguu wa kulia vs kushoto ].
Hii ni hoja ya kipuuzi sana. Madai kwamba risasi zilitoka upande wa kushoto hivyo Lissu alipaswa kuumia zaidi mguu wa kushoto hayana mashiko.
Kulinganisha shambulizi lile kwa kutumia nadharia ya practice targets za wakati wa mafunzo ya JKT pia sio sawasawa.
Lissu hakuwa amening'inizwa mfano wa practice target wakati wauwaji walipotumwa kumshambulia.
Lakini ili kuwaridhisha wanaoshadidia nadharia hiyo, mkono wa kushoto wa Tundu Lissu ulijeruhiwa kuliko wa kulia.
3.MAMA KUMTEMBELEA NAIROBI.
Mama alikwenda Nairobi kumuwakilisha Magufuli ktk uapisho wa Rais wa Kenya kama sijakosea.
Kama Mama angeondoka Nairobi bila kumtembelea Lissu hospitali ingeleta picha mbaya kwa serikali ya Tanzania.
Kwa hiyo Magufuli alikacha kwenda Nairobi ili kukwepa fedheha ya kumtembelea Lissu.
Mama alikuwa hana namna.
4.KUMPA JINA BAYA LISSU ILI KUHALALISHA SHAMBULIZI.
Mara kwa mara kumekuwa na madai kwamba Lissu alikuwa akiwasaidia Accacia.
Watu wanasahau kwamba kati ya Watanzania waliopambana na makampuni ya madini kwa muda mrefu ni Lissu.
Kwenye sakata la madini Lissu alipinga zile ripoti kwamba sio za kweli na zitaliumiza taifa ikiwa tutashitakiwa ktk mahakama za kimataifa.
Na madai hayo ya Lissu yalikuja kuthibitika pale Mwenyekiti wa Tume za uchunguzi Prof.Mruma aliposhindwa kuzitetea alipokabiliana na mawakili wa kimataifa.
Hakuna mtu amerudi na kumshukuru Lissu kwa kusema ukweli kuhusu umadhubuti wa findings za Tume za uchunguzi.
Tundu Lissu alisimamia UKWELI wakati wote wa sakata la madini.
5.PROF.MRUMA KUTOA MACHOZI SIKU AKIWASILISHA RIPOTI.
Hapa kuna maswali ya kujiuliza.
Je, Prof.Mruma alitoa machozi kwasababu ya uchungu wa wizi wa rasilimali uliofanywa na makampuni ya madini?
Au, Prof.Mruma, alitoa machozi kwasababu alilazimishwa ku present ripoti ya uongo yenye mambo yasiyoweza kutetewa mbele ya wanataaluma, na wabobezi wa sheria?
Na kwanini Ripoti za Prof.Mruma, na Prof.Ossoro, hazijawekwa wazi kama ripoti nyingine za uchunguzi za Dr.Kipokola, Lau Masha, na Mark Bomani?
Ripoti zile zingekuwa za kweli Tanzania ingekwenda mahakama ya kimataifa na Accacia wangetulipa fidia.
6.USALITI KTK RASILIMALI ZA WATANZANIA.
Hii ni dhambi mbaya sana ambayo Magufuli alijaribu kumpachika Lissu.
Magufuli alitaka Tundu Lissu aende kaburini kama msaliti wa taifa hili.
MUNGU amekataa hilo na uwezekano mkubwa ni jina la Tundu Lissu kupambwa ktk historia ya Tanzania.
Magufuli hakugusa mtu hata mmoja aliyehusika ktk kuidhinisha mikataba yote mibovu ya madini na nishati.
Magufuli mwenyewe kabla ya kuwa Rais hakuwahi kupinga mikataba ya madini pamoja na kwamba nyumbani kwao Geita kuna mgodi wa madini.
Lakini kitu cha ajabu kupita vyote ni Magufuli kumpa ubunge wa CCM, Deo Mwanyika, aliyekuwa Ceo wa Barrick, na Accacia, tawi la Tanzania.
Na ukiacha hayo kuna kiongozi mkubwa wa Tanzania alitembelea Canada wakati tuko ktk vita vya uchumi. Je, serikali ya Magufuli ilikuwa na "ndimi mbili" wakati wa vita hiyo?
7.LISSU KURUDI WAKATI WA UCHAGUZI
Ni kweli kabisa hakuna aliyetarajia Tundu Lissu atarudi Tanzania wakati wowote.
Lakini Tundu Lissu kurudi kipindi cha uchaguzi ni kwasababu ya hakikisho la ULINZI kwa wagombea Uraisi.
Na uchaguzi ulipoisha na ulinzi kuondolewa Tundu Lissu akatoroka chini ya kinga ya balozi wa Ujerumani.
Je, kungekuwa hakuna sheria ya wagombea Uraisi kupewa ulinzi Tundu Lissu angerudi Tanzania?
Je, Magufuli asingekufa Lissu angerudi?
8.VIONGOZI WA BUNGE KUMSUSIA.
Viongozi wa Bunge walijiweka mbali na Tundu Lissu wakati akijiuguza. Mtu wa kawaida lazima ajiulize kulikoni.
Kulifanyika jitihada za mazungumzo kati ya familia, na viongozi wa bunge, kurekebisha sintofahamu zilizokuwepo, lakini hazikuzaa matokeo mazuri.
Je, Bunge lilikuwa likishinikizwa lisimsaidie Tundu Lissu wakati akijiuguza? Nani alikuwa akitoa mashinikizo hayo?
9.LISSU NA MAMA SAMIA
Mama Samia alipoingia madarakani alijaribu kujenga taswira ya upatanishi.
Ni kipindi hicho ndipo Tundu Lissu alikutana naye.
Kwa tuliyoyashuhudia tunaweza kusema Mama Samia alikuwa na nia ya dhati ya kurejesha HAKI na usawa ktk siasa?
Kuna taarifa kwamba Mama alimkirimu Tundu Lissu na kumfadhili kurudi Tanzania.
Je, kuna ubaya gani kufanya hivyo? Mimi nilitarajia mambo hayo yafanyike kupitia utaratibu rasmi.
Kuna ubaya gani kwa serikali kuwapa kifuta machozi wote walioumizwa kwasababu ya misimamo yao ya kisiasa?