M'bananga chake hana kondo (If you spoil what is your own you have no quarrel)

Na kuhusu Magufuli, na UBABE wake. Akiwa rais alitangaza VITA vya UCHUMI hadharani na akaanza kupambana na Mafisadi wa ndani na Nje (Presidential Decree) unawezaje wewe raia tena wenfine sehemu ya Utawala kuanza kumpinga na hata kuwa mtetezi wa upande wa Mafisadi? Uzalendo wenu mnauweka wapi? Ilinushangaza sana na hizo HAKI zenu za kupinga hata katika swala linalohusu Maslahi ya Taifa lenu. Only in Tanganyika..
No! waliompinga ilikuwa sababu za njia alizotumia kuliko alichodhamiria. Mfano, kununua ndege kwa Cash kulikuwa na harufu mbaya hata kama lengo ni zuri. Kutuaminisha kuna vita ya uchumi wakati anajua vita ni ndani ya CCM. Kuchepusha pesa kama zile Bilion 70 bila maelezo. Kumuondoa CAG kwasababu hakutimiza matakwa yake n.k. Kwa ufupi alikuwa too mechanical than methodical
Maswala ya Utekaji binafsi naamini Magufuli hakuhusika na Polepole kathibitisha kwetu kwamba kuna kundi la WAHUNI walompiga vita sana na kufanya yote yale. Kama unakumbuka pia alieleza njia 4 au 5 za CCM kumshughulikia mtu kama akiwa amenyooka. Sina sababu kabisa ya kumpinga mtu alokuwa ndani chimboni niseme ati Mtekaji
Hapa ndipo hoja ilipo, kwamba kama hakukubaliana na utekaji je alifanya nini kuuzuia?
Unataka kutuambia Magufuli hakujua uchafu wa akina 7ya na mwenzake.

Magufuli alipeleka mswada wa dharura wa usalama wa Taifa , unajua impact yake
Magufuli aliagiza viongozi wa Polisi waseme maiti za viroba zilitoka South Africa, mbona haziji siku hizi

Hata kama hakuhusika, Magufuli alijua kuna UHALIFU dhidi ya ubinadamu na akiwa Rais hakutumia power kuzuia uhalaifu huo kwasababu aliona kama njia rahisi ya kumwezesha kutawala.

JPM alikiuka haki za binadamu, uovu unao upaka rangi! Uovu ni uovu tu hata ukihubiriwa na malaika
Isitoshe Tundu Lissu kupigwa risasi. Naamini wale walikuwa wahuni tu maana kama Magufuli angetoa amri ya kumuua Lissu wasingekuja wa na SMG tena eneo wanapokaa Viongozi wa Bunge.

Halafu watu wenyewe unaona kabisa sio professional. Unawezaje piga risasi mlangi wa gari zaidi kuliko Kioo cha mlango kuhakikisha unapiga risasi za kichwa au Kifua kuhakikisha unamaliza kazi. Halafu pro. Wasingeondoka bila kuhakikisha wamemaliza kazi walotumwa! Wale watu walitumwa kumchafua Magufuli na bahati mbaya Tundu Lissu aliumizwa kupita walivyotegemea.
Kwanini Kamati ya Bunge chini ya Adadi Rajabu ilizuliwa kuendelea na uchunguzi
Kwanini Camera ziliondolewa nyuma za Bunge
Kwanini Walinzi waliondolewa siku TL anapigwa risasi
Kwanini hadi leo Polisi hawajamhoji mhusika au wahusika

Ikiwa Magufuli hakusika basi angekuwa mstari wa mbelea kutafuta ukweli.
Kwamba alikataa kila kilichofanywa kutafuta ukweli, dunia nzima inajua hivyo isipokuwa Mkandara
Njama zooote mlizofanya dhidi ya Magufuli, mkawapa nafasi Mafisadi waungane nanyi mpaka katangulia mbele ya HAKI, sasa acha Mwenyezi Mungu awanyooshe! Mijitu msokuwa na shukran kama Wa - Libya.
Sina tatizo na rekodi ya utendaji wake katika baadhi ya mambo, ni matatizo na rekodi yake ya UBINADAMU na mwelekeo wa Nchi. Kwa ubinadamu kikosi cha mauaji kilikuwa na baraka zake.

Pili, kuvuruga demokrasia kwa kuanzisha ujinga wa kuengua watu, kupiga watu na kuwapoteza.

Mkuu Rekodi ya Magufuli ina utata sana kuna mema aliyofanya na uhalaifu dhidi ya UTU na Ubainadamu na hili linasemwa na litasemwa. Magufuli hakamiliki bila kusema mazuri na uovu aliotuachia

Na usisahau yeye ndiye muasisi wa nepotism! ukanda na ukabila. Nyufa hizo ni zao la Magufuli na tumkumbuke kwa upuuzi huo! kama tunavyomkumbuka kwa mema ya kuhamia Dodoma, Bwawa, SGR, n.k.
 
No! waliompinga ilikuwa sababu za njia alizotumia kuliko alichodhamiria. Mfano, kununua ndege kwa Cash kulikuwa na harufu mbaya hata kama lengo ni zuri. Kutuaminisha kuna vita ya uchumi wakati anajua vita ni ndani ya CCM. Kuchepusha pesa kama zile Bilion 70 bila maelezo. Kumuondoa CAG kwasababu hakutimiza matakwa yake n.k. Kwa ufupi alikuwa too mechanical than methodical

Hapa ndipo hoja ilipo, kwamba kama hakukubaliana na utekaji je alifanya nini kuuzuia?
Unataka kutuambia Magufuli hakujua uchafu wa akina 7ya na mwenzake.

Magufuli alipeleka mswada wa dharura wa usalama wa Taifa , unajua impact yake
Magufuli aliagiza viongozi wa Polisi waseme maiti za viroba zilitoka South Africa, mbona haziji siku hizi

Hata kama hakuhusika, Magufuli alijua kuna UHALIFU dhidi ya ubinadamu na akiwa Rais hakutumia power kuzuia uhalaifu huo kwasababu aliona kama njia rahisi ya kumwezesha kutawala.

JPM alikiuka haki za binadamu, uovu unao upaka rangi! Uovu ni uovu tu hata ukihubiriwa na malaika

Kwanini Kamati ya Bunge chini ya Adadi Rajabu ilizuliwa kuendelea na uchunguzi
Kwanini Camera ziliondolewa nyuma za Bunge
Kwanini Walinzi waliondolewa siku TL anapigwa risasi
Kwanini hadi leo Polisi hawajamhoji mhusika au wahusika

Ikiwa Magufuli hakusika basi angekuwa mstari wa mbelea kutafuta ukweli.
Kwamba alikataa kila kilichofanywa kutafuta ukweli, dunia nzima inajua hivyo isipokuwa Mkandara

Sina tatizo na rekodi ya utendaji wake katika baadhi ya mambo, ni matatizo na rekodi yake ya UBINADAMU na mwelekeo wa Nchi. Kwa ubinadamu kikosi cha mauaji kilikuwa na baraka zake.

Pili, kuvuruga demokrasia kwa kuanzisha ujinga wa kuengua watu, kupiga watu na kuwapoteza.

Mkuu Rekodi ya Magufuli ina utata sana kuna mema aliyofanya na uhalaifu dhidi ya UTU na Ubainadamu na hili linasemwa na litasemwa. Magufuli hakamiliki bila kusema mazuri na uovu aliotuachia

Na usisahau yeye ndiye muasisi wa nepotism! ukanda na ukabila. Nyufa hizo ni zao la Magufuli na tumkumbuke kwa upuuzi huo! kama tunavyomkumbuka kwa mema ya kuhamia Dodoma, Bwawa, SGR, n.k.Kuna tatizo gani kununua ndege kwa fesha mlokuwa na
1. Ok, nambie kulikuwa na tatizo gani kununua ndege kwa cash badala ya Mkopo? Maanake hao hai wanaolalamika wamenunua nyumba zao magari yao kwa cash! Kinachpungua nini?

2. Kwa hiyo wewe huamini kulikuwa na Vita ya Kiuchumi? Damn ndio maana nakubaliana sana na Nyani Ngabu anaposema Miafrika Ndivyo Tulivyo. Yaani yote ya Makinikia, Kuvamia Benki Kuu, Bandari, Mishahara hewa, Kufichua Mafisadi mpaka kurudisha kesi ya Escrow, IPTL, Acacia, Symbion, Tanzanite na Dhahabu ilokuwa ikiuzwa Kenya kwa njia za Panya na Mikataba mingine ikaandikiwa na kupitishwa na Bunge Sheria Mpya ya Madini! Ulitaka Vita ya namna gani bdio Uamini? Mafisadi wote wanaojilikana walikimbilia South Africa au Dubai leo wamerudi wote.

3. Vita ndani ya CCM haikumhusu yeye kabisa, Ilikuwa watu wa Lowassa vs JK Nyie mkachukua Upande wa Mafisadi kwa sababu ya Lowassa.

4. Hoja ya Kuengua Wagonbea haikuanza na Mahufuli ilikuwepo miakanyote na Vyama vyote vikifanya. Dr Slaa si Chadema walimuengua wakamoa nafasi Lowassa? Yule mshikaji Ben Saa Nane sii alienguliwa kule Arumeru akapewa Nasari unadhani hatujui?

Mimi nilikuwa mfuatiliaji sana wa Siasa za Bongo, sema sikutaka kuandika Mapungufu hayo maana yalikuwepo miaka. Wagombea wa vyama vyote vya Upinzani walikuwa viongozi wa Chama. Toka Mwenyekiti, Katibu, wajumbe wa Kamati kuu na kadhalika kwa kila jimbo. Unataka kunambia hapakuwepo watu wengine walotaka kushika Ubunge?

5. Kupotea kwa Watu, narudia tena siamini kazi ile ilifabywa na Magufuli bali kubdi la Wahuni walompiga vita kupitia njia hizo. Chukulia mfano hai Mmoja wa Mo Dewji! Rais anasimama hadharani kwenye Mkutani akamuuliza OCD kqma sikosei "Kwa nini kesi ile haipo. Mmemkamata dereva, mmemkamata mmiliki wa nyumba alowekwa inakuwaje kesi haipo?" Na mpaka leo hii kesi imekufa! Still kuna watu waliendelea kuamini Dewji katekwa na Magufuli. Kuna meli ilikamatwa ina tani moja ya Heroin unreahinsikia kesi yake?

6. Utasemaje Magufuli ndiye aloleta Ukanda, Ukabila wakati nyie ndio Mlomwita "Sukuma Gang" Wakati viongozi wale wanatoka Kanda ya Ziwa na wa Makabila tofauti! Yaani msukuma hakufaa kuwa kiongozi? It's Mental Slavery inayowatesa maana wenfine hawajali rais au Kiongozi anatoka wapi, dini gani, kabila gani.

Tanzania toka naijua kila mteule atatazamwa Kabila lake, Dini yake, ama anatoka Ukanda gani! Usinambie hujui wakati hii kitu ipo toka Nyerere. Alipingea hata kuea sii Mranzania. Dini yake, amkatoliki, akaitwa Mchonga meno! Nani mwenye tatizo hapo!.

Maasalaam, naomba tuishie hapa maana utanifanya niingie Black Book buree..

Maasalaam
 
1. Ok, nambie kulikuwa na tatizo gani kununua ndege kwa cash badala ya Mkopo? Maanake hao hai wanaolalamika wamenunua nyumba zao magari yao kwa cash! Kinachpungua nini?
Kukiukwa taratibu za manunuzi! Kutengeneza mwanya wa kuchepusha fedha kwasababu hakuna traceability
Kutokana na hilo CAG akasema kuna Trillion haijulikani ilipo, Magufuli akamuondoa
Kama angekuwa na nia njema ange prove na kumwacha CAG
2. Kwa hiyo wewe huamini kulikuwa na Vita ya Kiuchumi? Damn ndio maana nakubaliana sana na Nyani Ngabu anaposema Miafrika Ndivyo Tulivyo. Yaani yote ya Makinikia, Kuvamia Benki Kuu, Bandari, Mishahara hewa, Kufichua Mafisadi mpaka kurudisha kesi ya Escrow, IPTL, Acacia, Symbion, Tanzanite na Dhahabu ilokuwa ikiuzwa Kenya kwa njia za Panya na Mikataba mingine ikaandikiwa na kupitishwa na Bunge Sheria Mpya ya Madini! Ulitaka Vita ya namna gani bdio Uamini? Mafisadi wote wanaojilikana walikimbilia South Africa au Dubai leo wamerudi wote.
Magufuli alisema kuna Vita ya Uchumi na Nchi za Mgharibi, jambo la uongo. Nchi za Magharibi zikitaka vita na Tanzania ni wiki moja tu kwisha. Nchi hizo zinamiliki transactions, Communications etc . Tanzania si Iran

Kilichokuwepo ni vita ya MAFISADI ndani ya CCM ambao Magufuli aliwajua kwasababu Kikwete aliwalea

Magufuli alijua pesa za Escrow na jinsi zilivyogawanywa kwa mawaziri, Maaskofu n.k. na CCM kwa ujumla

Vita ya Mafisadi ambayo nakubaliana naye ilikuwepo lakini si kutufanya wajinga kwamba kuna vita na Nchi za Magharibi. Kama Nchi za magharibi zilikuwa na mkono, Mpini ni wana CCM na mikataba mibovu
Hoja ya Kuengua Wagonbea haikuanza na Mahufuli ilikuwepo miakanyote na Vyama vyote vikifanya. Dr Slaa si Chadema walimuengua wakamoa nafasi Lowassa? Yule mshikaji Ben Saa Nane sii alienguliwa kule Arumeru akapewa Nasari unadhani hatujui?
Mkandara, kuengua tunakoongelea hapa ni uhuni wa Wakurugenzi kukimbia Ofisi, kukataa Fomu na kuzuia mtu kwasababu jina lake limeanza na herufi ndogo, i.e. mkandara badala ya Mkandara

Mzee Warioba aliulizaa sheria gani imetumika katika hayo? Ni mwaka wa 2 hakuna mtu mwenye jibu
Profesa Mkumbo aliulizwa akashindwa kujibu akisema '' ndio taratibu''.

Hatuongelei kuengua watu katika ngazi za chama Mkandara. Hayo ya akina Lowassa, Nassari, Ben Saanane etc ni irrelevant kwasababu sicho tunachoongelea
Kupotea kwa Watu, narudia tena siamini kazi ile ilifabywa na Magufuli bali kubdi la Wahuni walompiga vita kupitia njia hizo.
Magufuli alifanya nini kuwadhibiti Wahuni akiwa kiongozi na zana zote za Ulinzi na usalama? swali lipo hapo
Utasemaje Magufuli ndiye aloleta Ukanda, Ukabila wakati nyie ndio Mlomwita "Sukuma Gang" Wakati viongozi wale wanatoka Kanda ya Ziwa na wa Makabila tofauti! Yaani msukuma hakufaa kuwa kiongozi? It's Mental Slavery inayowatesa maana wenfine hawajali rais au Kiongozi anatoka wapi, dini gani, kabila gani.
Unajua Nepotism maana yake!
Tanzania toka naijua kila mteule atatazamwa Kabila lake, Dini yake, ama anatoka Ukanda gani! Usinambie hujui wakati hii kitu ipo toka Nyerere. Alipingea hata kuea sii Mranzania. Dini yake, amkatoliki, akaitwa Mchonga meno! Nani mwenye tatizo hapo!.
Hivi Nyerere angefanya hayo kuna watu wangefanikiwa nchi hii. Unaweza kumfananisha Nyerere na Magufuli katika moral campus. Tanzania ipo kama ilivyo kwasababu Nyerere hakuendekeza Ukanda, Ukabila.

Mambo yalirasimishwa wakati wa Magufuli! haikuwa siri tena, weka mtoto wa dada pale, mtoto wa shemeji hapa n.k. kwavile ali normalize ujinga huo sasa ni kama modus operandi , tunayaona

Kukiukwa taratibu za manunuzi! Kutengeneza mwanya wa kuchepusha fedha kwasababu hakuna traceability
Kutokana na hilo CAG akasema kuna Trillion haijulikani ilipo, Magufuli akamuondoa
Kama angekuwa na nia njema ange prove na kumwacha CAG

Magufuli alisema kuna Vita ya Uchumi na Nchi za Mgharibi, jambo la uongo. Nchi za Magharibi zikitaka vita na Tanzania ni wiki moja tu kwisha. Nchi hizo zinamiliki transactions, Communications etc . Tanzania si Iran

Kilichokuwepo ni vita ya MAFISADI ndani ya CCM ambao Magufuli aliwajua kwasababu Kikwete aliwalea

Magufuli alijua pesa za Escrow na jinsi zilivyogawanywa kwa mawaziri, Maaskofu n.k. na CCM kwa ujumla

Vita ya Mafisadi ambayo nakubaliana naye ilikuwepo lakini si kutufanya wajinga kwamba kuna vita na Nchi za Magharibi. Kama Nchi za magharibi zilikuwa na mkono, Mpini ni wana CCM na mikataba mibovu

Mkandara, kuengua tunakoongelea hapa ni uhuni wa Wakurugenzi kukimbia Ofisi, kukataa Fomu na kuzuia mtu kwasababu jina lake limeanza na herufi ndogo, i.e. mkandara badala ya Mkandara

Mzee Warioba aliulizaa sheria gani imetumika katika hayo? Ni mwaka wa 2 hakuna mtu mwenye jibu
Profesa Mkumbo aliulizwa akashindwa kujibu akisema '' ndio taratibu''.

Hatuongelei kuengua watu katika ngazi za chama Mkandara. Hayo ya akina Lowassa, Nassari, Ben Saanane etc ni irrelevant kwasababu sicho tunachoongelea

Magufuli alifanya nini kuwadhibiti Wahuni akiwa kiongozi na zana zote za Ulinzi na usalama? swali lipo hapo

Unajua Nepotism maana yake!

Hivi Nyerere angefanya hayo kuna watu wangefanikiwa nchi hii. Unaweza kumfananisha Nyerere na Magufuli katika moral campus. Tanzania ipo kama ilivyo kwasababu Nyerere hakuendekeza Ukanda, Ukabila.

Mambo yalirasimishwa wakati wa Magufuli! haikuwa siri tena, weka mtoto wa dada pale, mtoto wa shemeji hapa n.k. kwavile ali normalize ujinga huo sasa ni kama modus operandi , tunayaona
Hii ndio kawaida yenu mnapenda sana story za mihemko ambayo iliandaliwa na Wahuni. Yaani Magudili akanunue ndege ambazo aliahidi kwenye Ilani yake kufufua ATCL mkasema haiwezekani! Ahadi za Uongo! halafu atie ndani fedha za Umma mtu mwenyewe Magufuli? Ebu tema mate chini.

Ok hizo hela kazipeleka wapi. Tena kuna zile walisema zilienda China sijii wakati wa Kesi za Ufisadi? Zilirudi au? Acheni hadith nyie hamuwezi kumdhalilisha alomuogopa Mungu na tulishuhudia Ujasiri wake kupambana na mabeberu na watu kama nyie. Na laana zitawatesa sana hao wote walomnajisi..

CAG Assad ni kundi lile lile la Wahuni wa Polepole na wote tuliwajua wakati wake. Kama CAG alikuwa mzuri ilikuwaje hakuona Makinikia ya Acacia? Hakuona mishahara hewa! Hakuona vichwa vya treni TRA vimeuzwa India? Benki zilifilisi watu wakakimbilia South! Wahuni walowauzia Jeshi sijui Polisi uniform kwa mabillioni nguo hazionekani.

Ilikuwaje asizungumzie mikataba mibovu ya Symbion, Madini mpaka Mzeeengi akawataja Mafisadi Papa! Where was he? Zile fedha za IPTL wakati CAG Alomtangulia alisema zile fedha ni za Umma? Kuingia yeye akazima. Madaraja yalijengwa chini ya kiwango, choo kinajengwa kwa gharama ya shule nzima! Jamani hivi kweli mmesahau tulivyokuwa 2010? Naweza kesha hapa kuzungumzia ya Assad ambae kelele zooote kazianza baada ya kufukuzwa.

Ebu weka akili yako sawa, Magufuli alikuwa na akili gani ya mahesabu kumzudi CAG kiasi akajua Benki Kuu na Bandari Kuna Ufisadi? Ile JKN Airport tulipigwa mabillioni ya Usd! Yaani madudu yalikuwa mengi kiasi kwamba hata mimi ningemfukuza CAG..

Halafu of all that, nyie mkakazia 1.5 haijulikani ilipo, wakati mnajua fika 2010-2015 Ufisadi ulikuwa hali ya juu kiasi kwamba kila mtu alikuwa analia hasa watu maskini. Mliambiwa ni fungu la Zanzibar hupewa asilimia 4.5 hamkukubali wakati ni Sheria. Labda wewe nambie uliwahi kusikia Zanzibar wakipewa fungu lao kabla ya Magufuli? Uliwahi kujua kiasi gani kimeenda Zanzibar toka tumeungana? Why question Magufuli ikiwa miaka yooote hamkujua wala kuambiwa...

Sasa kama kulikuwa hakuna vita vya Uchumi na nchi za Magharibi kwa nini alinyimwa mikopo mpaka tukaanza.kutumia hela zetu? Kwa nini kesi zote za nje ziliibuka wakati wake mkazipigia Siasa? Akiwaita Mabeberu mkasema hawezi kushindana na Mataifa makubwa!

Na hata alipokataa kufunga nchi wakati wa Covid sii nyie mlopigia kelele? Mkitudia Costa zinazoenda Moshi utadhani wanakufa ni wa Kaskazini tu! nchi nzima walichanga watu mil.3 hiyo Covid imeishia wapi? Kama watu kufa Tanzania wangekuwa wote.. The guy wa s genius!

Hizo habari za weka mtoto wa fulani pale, ni propaganda zenu tu Magu alinkata mpaka mwanae kwenye Ubunge! Vyama vyote vya Siasa Undugunisation kawaida. Kwani Lissu na Heche huwajui? JK na Ridhwan, mkewe, Kina Mkapa wakigombania mke! Wakwe kibao, Mwinyi yaani labda wa kumuondia alikuwa mwalimu pekee lakini sii Zanzibar sii Bara ajira zore ni kufahamiana, leo Samia kawajaza Wazenj mnapuga kelele! Akuweke wewe ukamlishe sumu!

Hizi habari za jikoni mkuu wangu ebu acheni mtavishwa kanga! Siasa zinazungumziwa SERA sio kabila gani wanaongoza nchi. Kama kiongozi mbovu hana vision ni yeye sio Kabila.lake wala dini yake. Mnajishughulisha sana kuchunguza Kabila na Dini badala ya kutazama SERA hizi zitatuletea Sheria hani, zinatusaidia nini Kimaendeleo, nyie mmekazania tu Taarab tuuu, kusutana midume mizima.

Nimerudi JF kutaka kuibadilisha iwe na Mijadala inayojenga Idea, Solution, sio kutwa Kuzungumzia Matukio yalokwisha tokea. Na Watu. After math hailisaidii Taifa wala kuzungumzia WATU. Leteni Idea, tafuteni Solution za matatizo yetu sio mpaka Tundu Lissi au Wazungu waseme.mdakie hoja - WAHUNI TU..
Am Out bro..
 
Nimerudi JF kutaka kuibadilisha iwe na Mijadala inayojenga Idea, Solution. Leteni Idea, tafuteni Solution za matatizo yetu
Am Out bro..
Nikushukuru kwa kurudi JF kuamsha mijadala tunduizi

Mstari niounukuu hapo juu una maana na kukuhusu. Kila tunapojadiliana na hoja kuwa moto, mara nyingi Mkandara hutafuta njia za kuchepusha hoja au ku twist. Matokeo yake hakuna idea wala solution, na sasa turudi huko

1. Nimekuuliza, wapi Tanganyika kupitia Katiba ya JMT imetumika kuwanyanyasa Wazanzibar? Umekwepa !
2. Nimekuuliza, baada ya kuitathmini hali ya kisiasa na kijamii nini pendekezo lako kuhusu Muundo wa Serikali?
3. Tumekuonyesha Serikali ya JMT inaendelea kufanya kazi, mchango wa Zanzibar katika JMT ni upi au kiasi gani
4.Tumeonyesha malalamiko ya Muungano yalipoanzia! hoja ni kwasababu Rais ni Mzanzibar inatoka wapi
5. Tumekuuliza, kwanini kuna Taasisi za mbadala wa JMT kule Zanzibar? Hizi za JMT ni za nani.

Kwa upande wangu nami nawajibika pia kutoa solution. Plan A
1. Muundo wa Muungano wa Serikali (2) umekataliwa na Watanzania wote, ni non starter.
2.Mfumo wa Serikali moja ya JMT ni DOA (Dead on arrival) kwamba ni maiti ikifika inapotakiwa
3. Mfumo wa Serikali Tatu ili kuwa accomodate Wazanzibar ndio feasible option
4. Muungano wa Mkataba ni RUBBISH, tukutane EAC , SADC, AU na UN

Ikiwa 1,2,3 hazitawezekana tuna plan B
1. Kura ya maoni iitishwe kwa Zanzibar ili waamue wanataka Muungano au la! Hii itasaidia kuua misimamo hovyo
2. Tukubaliane kuishi kama majirani wema na tushirikiane pale tu penye manufaa na si kubebeshana mbeleko
3. Ili kuwe na fairness katika maamuzi, Serikali ya Tanganyika irudi kusimamia mambo yake ikiwemo kuamua hatma ikiwa bado inahitaji kuwa na Zanzibar

Ahsante
 
Nikushurukuru kwa kurudi JF kuamsha mijadala tunduizi

Nikwambie hivi ukiona sijibu swala ujue lopo nje ya mjadala huu kwa sababu hakuna sehemu wala pahala nimezungumzia Unyanyasaji baina ya Bara na Visiwani kupitia Katiba. Sijui wewe umelipata wapi.

Nolichosema mimi kwa maudhui ya Mbananga chake kwa tafsiri rahisi yenye maana ya Ukiukaji wa Katiba. Sasa kama watu wanakouka Katiba inakuwaje Unyanyasaji Uwe ni sehemu ya Katiba?

2. Swali la Pendekezo langu la Seeikali ngapi halihusiani pia na mjadala kwa sababu nikisema MOJA utaanza kusema sasa kwa nini unatetea MBILi au Hoja itageuka iwe kuhusu Serikali MOJA.

Najua unakotaka nipeleka. Kifupi hizi hizi MBILI kulingana na maelezo ya Mwalimu akieleza ubaya wa kila muundo afadhali huu, japo ingrkuea Moja toka 1964 ingrkuwa Vizuri zaidi. Kwa sababu Mwalimu na Karume waliweza kuunganiaha sio Vyama pekee bali Wahusika wa pande zote, waliua vyama vya Upinzani wakawavuta wote kina Mtemvu, Fundikira, Marealle, Maalim Seif, Thabit Kondo, Salim A Salim, Abrahman Babu yaani vichwa vyote vilikuwatana CCM. Hivyo kufikia sasa tusingekuwa na Utanganyika wala Uzanzibar. Ni mtazamo wangu..

Serikali 3 huiwa commodate Wazanzibar kwa sababu tayari wanayo Serikali yao, tukiunda ya 3 niya Tanganyika, wao hawatabadilisha chochote, hata Katiba yao wanaweza kataa kwa sababu wenye shida ya Serikali ni sisi. Wao wana rais wao, wana Katiba yao, wana Serikali, Bunge na mahaka zao, sijui unanielewa?

3. Sijui kama unaelewa swali ilouliza? Unaposema Seeikali ya JMT tayari umeshaiweka Zanzibar, sasa huo mchango unaotaka kujua ni upi ikiwa Zanzibar ina Wabunge katika Bunge la JMT, Zanzibar ina watumishi katika Seeikali ya JMT, Zanzibar ina watumishi katika Mahakama zetu..Mchango upi unaotaka kujua?

4. Nilikujibu kuhusu Wazanzibar kutaka Serikali 3 pengine hukulipenda jibu langu. Ulimtaja Jumbe, nikasema Jumbe ni Mtanganyika kwa asili kazaliwa tu Zanzjbar kama Hao wengineo.

Na sababu kubwa ni Uroho wa madaraka wawe marais wa NCHI zao kama walivyofanya kina Kenyatta, Obote na Banda. Kwa nini hawakukubali Seeikali 3 wakaamua wajikate! Slave Mentality! Kaona kisha kajivua minyororo. Kwa hiyo Bara nao wanaitaka Tanganyika kwa sababubhizo hizo wajitenge na Zanzibar nothing else, kisa hatiwahitaji.

5. Kwa nini Zanzibar wana Taasisi zao kama ZRA na kadhalika. That's a wake up call kwetu kwamba Zanzibar hawakati Muungano wa Seeikali 1,2 wala 3. Wanataka kujitenga kabisa kwa sababu Mambo yote ya Muungano wa Serikali 3 wanayavunja mbele ya macho yetu na yanapitishwa. Sasa usitake kunambia wamefanya hayo yooote bila ridhaa ya Viongozi na Bunge la JMT. Wewe unaona tunagawana kuti halafu unakuja na Serikali 3, kweli hii ndio Solution ya maana?

Marekani ina States 50, mkusanyaji wa kodi mmoja tu IRS, Canada ina Province 10 na Territory 3 jumla 13 lakini wana Mamlaka ya kukusanya kodi moja tu CRA. Kwa ninj Zanzibar ina yake tofauti na ile ya JMT? Changanya na zako brother!

Hilo nimezungumzia.sana huko nyuma lakini yaonyesha huwa hunisomi vizuri. Yote kwa pamoja Bara na Visiwani " Mbanga Chake hana Kondo"

Je, Umewahi sikia Bungeni wakibishana juu ya Ukiukaji wa Katiba? Lakini tumesikia mara ngapi baadhi yao wakisema wanataka Katiba Mpya!
 
Kifupi hizi hizi MBILI kulingana na maelezo ya Mwalimu akieleza ubaya wa kila muundo afadhali huu, japo ingekuea Moja toka 1964 ingekuwa Vizuri zaidi. Kwa sababu Mwalimu na Karume waliweza kuunganiaha sio Vyama pekee bali Wahusika wa pande zote, waliua vyama vya Upinzani wakawavuta wote kina Mtemvu, Fundikira, Marealle, Maalim Seif, Thabit Kondo, Salim A Salim, Abrahman Babu yaani vichwa vyote vilikuwatana CCM. Hivyo kufikia sasa tusingekuwa na Utanganyika wala Uzanzibar. Ni mtazamo wangu..
OK fair enough! kwa kujificha nyuma ya kauli za Nyerere unapendekeza Muundo wa Serikali 2 uendelee.
Kumeundwa kamati zaidi ya 10 na zote hazikubaliana na muundo uliopo, tunaweza ku sustain hali iliyopo?

Tume ya Waioba ya mwisho ilihitimisha hivyo ukizingatia akina Salim A Salim, Warioba na Butiku ni watoto watiifu wa Mwalimu lakini bado walikuja na pendekezo tofauti. Tunawezaje kwenda mbele na Serikali 2!

Kwa Watanganyika kuingiwa na fatigue ya kuhudumia muungano na kiu ya kutaka kuamua mambo yao kwavile yameanishwa kikatiba bila Muundo (serikali) utawashauri vipi kwamba muundo wa S2 ni chaguo
Serikali 3 huiwa commodate Wazanzibar kwa sababu tayari wanayo Serikali yao, tukiunda ya 3 niya Tanganyika, wao hawatabadilisha chochote, hata Katiba yao wanaweza kataa kwa sababu wenye shida ya Serikali ni sisi. Wao wana rais wao, wana Katiba yao, wana Serikali, Bunge na mahaka zao, sijui unanielewa?
Ni kweli lakini hukuelewa nilichokusudia. Ku accomodate ni kuwaweka karibu na Tanganyika! kwasababu Tanganyika haihitaji Zanzibar. In other words ndio better option, probably not but that's what is available
Unaposema Seeikali ya JMT tayari umeshaiweka Zanzibar, sasa huo mchango unaotaka kujua ni upi ikiwa Zanzibar ina Wabunge katika Bunge la JMT, Zanzibar ina watumishi katika Seeikali ya JMT, Zanzibar ina watumishi katika Mahakama zetu..Mchango upi unaotaka kujua?
Wabunge wa Zanzibar wanakuja kwa yasiyozidi 3%. Wabunge hao wanakuja kukamilisha Katiba kwa 2/3 ya Zanzibar, ndio maana hatuna kura inayowapa Wabunge wa Kigoma, Mtwara au Ruvuma % yoyote

Watumishi wa Umma kutoka Zanzibar wanalipwa mishahara kutoka Bajeti ya Tanganyika.

Nilikuuliza uonyeshe bajeti ya SMZ na mafungu yake hukuweza kutetea hata category moja.

Wizara zote zinahudumiwa na kodi za Watanganyika. Wazanzibar wanapewa 21% lakini mishahara, marupu rupu na hata ustaafu ni pesa za Tanganyika. Mchango wao ni kupewa 21% ya ajira za vijana wa Tanganyika

Jambo jingine pengine hulijui. SMZ inapewa pesa kutoka kodi za Watumishi wa Zanzibar walioko Tanganyika. Yaani Tanganyika inatoa ajira kwa upendeleo kisha inawalipa SMZ kwa kuwasaidia tatizo la ajira.

Turejee tena bandiko la nyuma, tuonyeshe kutoka Bajeti ya SMZ mafungu yanayochangia uendeshaji wa JMT , kuanzia Wizara, Taasisi hadi ving'ora vya OMO!
Nilikujibu kuhusu Wazanzibar kutaka Serikali 3 pengine hukulipenda jibu langu. Ulimtaja Jumbe, nikasema Jumbe ni Mtanganyika kwa asili kazaliwa tu Zanzjbar kama Hao wengineo.
Aha! kwavile kazaliwa Zanzibar ndio maana alitaka serikali 3? Halafu unasema HIZBU ndio wako nyuma ya Serikali 3. Jumbe si Hizbu ! ni Mbara kwa mujibu wako. Unaona jinsi unavyojichanganya, huna consistency.

Tukimuacha Jumbe, Maalim alitaka Serikali 3 akaenda mbali na upuuzi wa Mkataba.
Wazanzibar na Tume ya Warioba walitaka serikali 3, OMO na akina Jussa ndio wapiga debe wa serikali 3

Hoja ya Serikali 3 ni ya Wazanzibar, Watanganyika wanaichukua kwasababu wamechoshwa.
Mzigo wa kuhudumia JMT ni wao, kuhudumia SMZ ni wao kisha wanatukanwa.

Kubwa zaidi ni Wazanzibar kuwa ''special'' kwamba kila jambo wapewe kwasababu ya Uzanzibar! Watanganyika wanajiuliza ni kwa faida gani .
5. Kwa nini Zanzibar wana Taasisi zao kama ZRA na kadhalika. That's a wake up call kwetu kwamba Zanzibar hawakati Muungano wa Seeikali 1,2 wala 3.
Absolutely! ndio maana Taasisi nyingine zinaendelea kujengwa. Kuna Chuo cha Polisi kinajengwa mbadala wa CCP Moshi. Kuna Chuo cha Uhamiaji kinajengwa, mbadala wa chuo cha Tanga.

Kwa uchumi wa Zanzibar hivi vyuo ni vya nini? Kuna mipaka mingapi inayohitaji chuo cha Uhamiaji?
Hata chuo cha Wanyama Pori Mwika kimeambiwa kijengwe Zanzibar, kwa wanyama gani.
Kuna MOI inajengwa Zanzibar n.k. Zote hizo ni gharama anazobeba Mtanganyika kwa jina la JMT

Katika hali hiyo Watanganyika wanakosa gani wakisema wakihitaji Muundo washughulikie mambo yao.

Nakubaliana nawe kabisa, kwamba Muungano uliopo ni wa Vitambulisho vya NIDA kwa ajili ya ajira na rasilimali kama ardhi kwa Wazanzibar. Hili tupo pamoja.

Swali, kwanini tupoteze muda tusiwaache waende zao !
Wanataka kujitenga kabisa kwa sababu Mambo yote ya Muungano wa Serikali 3 wanayavunja mbele ya macho yetu na yanapitishwa. Sasa usitake kunambia wamefanya hayo yooote bila ridhaa ya Viongozi na Bunge la JMT. Wewe unaona tunagawana kuti halafu unakuja na Serikali 3, kweli hii ndio Solution ya maana?
Ni kweli ndio maana nilishauri kwamba ni muda muafaka tuwe majirani ! kama serikali 3 haziwezekani basi tugawane mbao za jahazi. Tanganyika haina cha kupoteza!

Ni kweli kabisa kwamba kuna viongozi wanachagiza haya tena wakifanya maandalizi haswa!
Kwanini tusiwe majirani wema? Wewe ndiye unashikilisa serikali 2 wakati unajua wanajitenga taratibu
Marekani ina States 50, mkusanyaji wa kodi mmoja tu IRS, Canada ina Province 10 na Territory 3 jumla 13 lakini wana Mamlaka ya kukusanya kodi moja tu CRA. Kwa ninj Zanzibar ina yake tofauti na ile ya JMT? Changanya na zako brother!
Thank you! unatoa ushahidi muhimu kwamba hawana mchango, na Tanganyika imebeba mzigo.
Nakubaliana nawe 100% kwa hili, ndio maana narudia tena ikiwa ni hivyo kwanini kila mmoja asikusanye kodi zake! na kama haiwezekani basi tuwe majirani wema tunaopendana. Unaona kwanini Watanganyika wanaitaka nchi yao! halafu unawaita wapumbavu
Je, Umewahi sikia Bungeni wakibishana juu ya Ukiukaji wa Katiba? Lakini tumesikia mara ngapi baadhi yao wakisema wanataka Katiba Mpya!
Hapana kwasababu ni Taboo kuongelea uhuni wa Zanzibar! Yaani Wazanzibar wanaweza kusema chochote ikawa poa akisema Mtanganyika ni tatizo. Mfano, Mbowe aliposema ilikuwa kama nchi inawaka moto, majuzi hapa wale wabunge wanaokuja Dodoma kulala wakasema ''wanataka passport'' wengine Yuda, na kila aina ya upuuzi kwasababu hawana cha kusema, na hakuna aliyekemewa. Kwanini hawakukemewe , wana Uzanzibar Raia bora ndani ya JMT. Wanapewa kila kitu kwa upendeleo kwa gharama za Wananchi wetu!
 
Kama #jamiiforums inahifadhi Mada za zamani ningeomba wahusika watuwekee hapa iile thread tulikuwa tukijadili Lowassa kwenda Chadema.. Ukweli utajulikana.

Na kuhusu Magufuli, na UBABE wake. Akiwa rais alitangaza VITA vya UCHUMI hadharani na akaanza kupambana na Mafisadi wa ndani na Nje (Presidential Decree) unawezaje wewe raia tena wenfine sehemu ya Utawala kuanza kumpinga na hata kuwa mtetezi wa upande wa Mafisadi? Uzalendo wenu mnauweka wapi? Ilinushangaza sana na hizo HAKI zenu za kupinga hata katika swala linalohusu Maslahi ya Taifa lenu. Only in Tanganyika..

Kiongozi anatetea National Interest, halafu mijitu inakuja kupingana na Rais bila sababu kabisa ili mradi waonekane Upinzani? Yaani hata iwe kwa nchi kama Marekani Utaposhughulikiwa kisawasawa!

Maswala ya Utekaji binafsi naamini Magufuli hakuhusika na Polepole kathibitisha kwetu kwamba kuna kundi la WAHUNI walompiga vita sana na kufanya yote yale. Kama unakumbuka pia alieleza njia 4 au 5 za CCM kumshughulikia mtu kama akiwa amenyooka. Sina sababu kabisa ya kumpinga mtu alokuwa ndani chimboni niseme ati Mtekaji alikuwa Magufuli.

Isitoshe Tundu Lissu kupigwa risasi. Naamini wale walikuwa wahuni tu maana kama Magufuli angetoa amri ya kumuua Lissu wasingekuja wa na SMG tena eneo wanapokaa Viongozi wa Bunge.

Halafu watu wenyewe unaona kabisa sio professional. Unawezaje piga risasi mlangi wa gari zaidi kuliko Kioo cha mlango kuhakikisha unapiga risasi za kichwa au Kifua kuhakikisha unamaliza kazi. Halafu pro. Wasingeondoka bila kuhakikisha wamemaliza kazi walotumwa! Wale watu walitumwa kumchafua Magufuli na bahati mbaya Tundu Lissu aliumizwa kupita walivyotegemea.

Mimi nahitimisha kuwa wale walikuwa WAHUNI tu na Tundu Lissu anajua, ndio.maana alirudi kugombea Urais dhidi ya Magufuli 2020 na Ulinzi akapewa. Siamini kabisa kama Tundu Lissu angejua ni Magufuli, halafu anapewa nafasi ya kurudi Tanzania kugombea Uras against Muuaji yuleyule alomkosa kosa? Mtu yeyote asingekubali kurudi nchini unless Magufuli angekuwa sio Rais kama alivyofanya mara ya pili baada ya Samia kuwa rais. It doesn't add up!

Njama zooote mlizofanya dhidi ya Magufuli, mkawapa nafasi Mafisadi waungane nanyi mpaka katangulia mbele ya HAKI, sasa acha Mwenyezi Mungu awanyooshe! Mijitu msokuwa na shukran kama Wa - Libya.

Inaniuma sana, Rurudi kwenye Mada yetu, hapo juu nilikuwa namkumbusha tu Mag3

..kama ni wahuni ndio walimshambulia Tundu Lissu kwanini Magufuli hakuwakamata?

..yaani Magufuli akubali kuchafuka kwa jambo baya la kusingiziwa kumuua mpinzani wake bila kuchukua hatua?

..Na ni nani mwenye uwezo wa kuondoa ulinzi wa serikali, ktk eneo aliposhambuliwa Lissu, wanapoishi Naibu Spika,na Waziri wa Madini na Nishati, tena ktk kipindi ambapo Magufuli alikuwa ametangaza kuwa nchi iko vitani?

..Kuhusu risasi, zilipigwa na kwenye kioo kama unavyodhani ilikuwa sahihi, na nyingine zilipigwa mlangoni.

..Kama zimepigwa na mhuni au professional ukweli ni kwamba 17 zilimpata. Na Lissu alikaa hospitali mwaka na nusu. Na kufanyiwa upasuaji mara 20. Na sasa ni mlemavu.

..Nimeshangaa jinsi ulivyolizungumzia suala hili kana kwamba aliyeumizwa sio BINADAMU mwenzetu. Watanganyika, na Wazanzibari, hatupaswi kufika huko.
 
Hapa ndipo simwelewi Mkandara . Eti anasema ni Wahuni! Magufuli alikuwa Rais wa Tanzania , aliapa kulinda watu na mali za Watanzania na baada ya kiapo akapewa ''instrument of power'' zote za nchi hii. Wana nguvu gani kuliko mtu anayeweza kuamua maisha ya mtu kwa dakika moja.

Bunge liliunda kamati ya kuchunguza tukio la Lissu chini ya Adad Rajab. Matokeo hayajawahi kutolewa wala hata kujadiliwa. Laiti Magufuli angekuwa hahusiki si angeacha ukweli utamalaki ili Wahuni wajulikane.

Hao Wahuni anaosema wanaua watu na kuwafunga katika viroba , tunaambiwa na IGP wameuawa South Africa, Rais wa nchi yupo kimya. Kama hakuhusika kwanini hakutoka kukemea uouvu huo! alikubaliana na IGP?

Rudi nyuma kuna bandiko Mkandara anasema hivi ''......Huwezi kuungana na mafisadi dhidi ya rasilimali za nchi na serikali ikakuacha...'' ni kwamba anajua nini kilitokea lakini anajitoa ufahamu ! so sad
..Kuhusu risasi, zilipigwa na kwenye kioo kama unavyodhani ilikuwa sahihi, na nyingine zilipigwa mlangoni.
..Kama zimepigwa na mhuni au professional ukweli ni kwamba 17 zilimpata. Na Lissu alikaa hospitali mwaka na nusu. Na kufanyiwa upasuaji mara 20. Na sasa ni mlemavu.
Wahuni anaosema Mkandara wana uwezo wa ku command security ya eneo la Bunge! Mkandara anaona hilo ni kawaida kabisa na linakubalika! Rais wa Nchi yupo na anakubali wahuni wamchafue hivyo! real
..Nimeshangaa jinsi ulivyolizungumzia suala hili kana kwamba aliyeumizwa sio BINADAMU mwenzetu. Watanganyika, na Wazanzibari, hatupaswi kufika huko.
Mkandara ana chuki sana na TL kwahiyo uovu dhidi ya TL atautetea hata kwa dhalili juu yake.

Unaweza kutofautiana na TL na ninatofautiana naye sana lakini si katika UBINADAMU.
Yule jamaa wa CCM aliyepigwa na wahuni akachanika makalio bado nalaani kitendo kile kwasababu si UBINADAMU.

Siwezi kutafuta sababu zozote ku justify uovu dhidi ya ubinadamu, kiwango hicho sina!
 
Serikali ya mapinduz, siyo serikali ya muungano
Zanzibar inachangia % ngapi kwenye bajeti ya muungano?

Kuna mdau kasema mapato yote yanayokusanywa zanzibar yanaingia kwenye mfuko wa serikali ya mapinduzi, na serikali ya muungano inawaongezea tena asilimia fulani ya mapato yake.
 
..kama ni wahuni ndio walimshambulia Tundu Lissu kwanini Magufuli hakuwakamata?

..yaani Magufuli akubali kuchafuka kwa jambo baya la kusingiziwa kumuua mpinzani wake bila kuchukua hatua?

..Na ni nani mwenye uwezo wa kuondoa ulinzi wa serikali, ktk eneo aliposhambuliwa Lissu, wanapoishi Naibu Spika,na Waziri wa Madini na Nishati, tena ktk kipindi ambapo Magufuli alikuwa ametangaza kuwa nchi iko vitani?

..Kuhusu risasi, zilipigwa na kwenye kioo kama unavyodhani ilikuwa sahihi, na nyingine zilipigwa mlangoni.

..Kama zimepigwa na mhuni au professional ukweli ni kwamba 17 zilimpata. Na Lissu alikaa hospitali mwaka na nusu. Na kufanyiwa upasuaji mara 20. Na sasa ni mlemavu.

..Nimeshangaa jinsi ulivyolizungumzia suala hili kana kwamba aliyeumizwa sio BINADAMU mwenzetu. Watanganyika, na Wazanzibari, hatupaswi kufika huko

..kama ni wahuni ndio walimshambulia Tundu Lissu kwanini Magufuli hakuwakamata?

..yaani Magufuli akubali kuchafuka kwa jambo baya la kusingiziwa kumuua mpinzani wake bila kuchukua hatua?

..Na ni nani mwenye uwezo wa kuondoa ulinzi wa serikali, ktk eneo aliposhambuliwa Lissu, wanapoishi Naibu Spika,na Waziri wa Madini na Nishati, tena ktk kipindi ambapo Magufuli alikuwa ametangaza kuwa nchi iko vitani?

..Kuhusu risasi, zilipigwa na kwenye kioo kama unavyodhani ilikuwa sahihi, na nyingine zilipigwa mlangoni.

..Kama zimepigwa na mhuni au professional ukweli ni kwamba 17 zilimpata. Na Lissu alikaa hospitali mwaka na nusu. Na kufanyiwa upasuaji mara 20. Na sasa ni mlemavu.

..Nimeshangaa jinsi ulivyolizungumzia suala hili kana kwamba aliyeumizwa sio BINADAMU mwenzetu. Watanganyika, na Wazanzibari, hatupaswi kufika huko.
Swali zuri sana na ndio maana mimi nilimkubali sana Magufuli kwa sababu hakuingilia kazi za vyombo vingine vya Sheria kama sii mahala pake. Hakuwahi kabisa kuingilia vyombo vya Dola zaidi ya kusema ama kutoa maoni yake akilalamika, yeye huku kwenye Serikali (Executive) alikula nao sahani moja bila msalie.

Chukulia kina Mange Kimambi na Dadatu sijui ndi Shangazi Maria Sarungi. Wote hawa walikuwa wakimshambulia sana Magufuli, lakini hata siku moja hukumsikia akisema lolote juu yao. Na nilipomsikia Polepole nikaweza kuunganisha picha nzima, kulikuwa na Kamoeni Magufuli have to go!

Kuna wakati alikuwa akihoji hata Kesi za Mafisadi akisema "Mtu amekamatwa na ngozi inakuwaje mnaswma Ushahidi bado haujakamilika?" Huyu huyu ndio Mwizi lakini upande wa mashtaka hakuna alotiwa hatiani, kiasi kwamba ikafika wakati akapitisha Sheria ya Plea Bargain ili basi hata zile fedha zirudi maana ilijua nunkiasi gani tumepigwa bora basi hata nusu irudi.

Oooh, watu wakamsakama ati katunga Sheria ambayo haipo wakati nchi nyingi duniani inatumika. Walivyoona hageuki wakaanza kusema fedha za Plea hazijulikani zilipo tena baada ya kumuondoa, mara sijui zimepelekwa China! Sasa Magu na China wapi na wapi?

Isitoshe, Kiongozi fisadi hajifichi hata siku moja. Hata Nyerere kuna watu walisema alikuwa na account Swiss Bank! Haya ziko wapi? Mlizipata zikarudishwa? Yaani TZ ni NCHI ya Tamthilia kuna Series na Episode zisokwisha! Huhitaji kuwa na Phd kuelewa yanayofanyika.

Kuhusu Eneo aloshambiliwa Tundu Lissu, upande ule ni sehemu ya Mhimili wa Bunge kama sikosei sio wa Serikali ndio maana Tundu Lissu alikaa nyumba aloachiwa Mwenyekiti Mbowe.

Kwa hiyo kama tunataka ku question nanii mwenye Mamlaka ya Ulinzi pale nitasema Bunge! Ila kiuhalisia sijui. Ila naelewa kama Magu angektaka kumuua Tundu Lissu asingechukua njia hiyo tena saa Saba Mchana tena eneo la Bunge.

Tundu Lissu kakamatwa mara kibao, na kesi zote kashinda anaachiwa. Magu hakuingiza neni hata moja., angetaka kummaliza, asingeshinda kesi, tena wakati ule hakuwa hata Mwenyekiti.

Na kuna taarifa za kutatanisha ya kwamba walinzi walisha ondolewa siku nyingi kabla na Viongozi wengi walikuwa na Walinzi wao Binafsi. Iwe kweli au sii kweli, nachoweza kusema kulingana Na Shambulio, a pro Assassin asinge piga risasi mlango wa gari, angelenga Kichwa au Kifua sii miguuni.

Nimeenda JKT hata target practice tuliwekewa Kichwa na Kifua sio mwli mzima! Kwangu miye ule ulikuwa nchezo wa kumchafua Magufuli.lakini ukaenda Kombo na Lissu anajua Magufuli hakuhusika ndio maana alipotaka kutudi kugombea Urais aliomba ahakikishiwe Ulinzi.

Najiuliza utawezaje muomba Hasidi wako akuhakikishie Ulinzi ili urudi Tanzania kugombea Urais dhidi yake? Halafu, muda wote anakutana na Samia, kahifadhiwa na Samia akiwa Ubrlgiji, kapewa nauli kurudi na gari la kutembelea haya yote anafanyiwa baada ya Magufuli kufariki wakisema yeye bdio alotaka kumuua Tundu Lissu! Hizi Hisani zote za nini?

Mwisho.kumbuka hata Magufuli.mwenyewe aliwahi kuwekewa Sumu na sii wa kwanza! Mwakyembe, Mzee Makamba na sijui kina nani lakinipaka.leo hakuna Ushahidi wala kesi hata moja unayohusu Nani alowapa SUMU viongozi wa Serikali..

Katika hili, bana naamini kuna MAFIA moja kali sana nchini ambazo haya vypmbo vya Usalama hawawezi kuwagusa.. Ni kina nani hao? Siwajii na wala sitaki kuwajua maana hata kuwajua tu unaweza ondoka!!!

Nguruvi3 nipe muda kidogo nipumzike maana ndio kwanza Narudi, nahitaji pumzi😂😂😂
 
..eneo aliposhambuliwa Lissu ni nyumba za viongozi wa bunge na serikali. Baadhi ya majirani zake walikuwa Naibu Spika Tulia Ackson, na Waziri wa Madini na Nishati Medard Kalemani. Maeneo ya aina hiyo ni gated na hulindwa na serikali.

..Kitendo cha ulinzi kutokuwepo siku aliyoshambuliwa Lissu kunaonyesha ni mpango uliohusisha watu wa serikali ya Magufuli. Haiwezekani ulinzi usiwepo eneo sensitive namna ile bila maelekezo toka kwenye vyombo vyenyewe au serikalini.

..Na kama Magufuli angekuwa ameguswa na tukio lile, au hakuhusika nalo, lazima kungefanyika juhudi kubwa kuwakamata wahusika. Muda wote wa sakata lile serikali haikuonyesha nia ya kuwakamata wahusika. Badala yake juhudi zilielekezwa kumkandamiza Tundu Lissu.

..Kuhusu waliotumwa kumshambulia Lissu mimi naona walikuwa wanaijua kazi waliyotumwa. Kama waliweza kumpiga risasi 17 unawezaje kusema hawajui kulenga shabaha.

..Na kulinganisha target practicing za JKT, na hit and run operation / mission to kill dhidi ya Lissu, nadhani ni kuwa naive, au labda umelenga kupotosha.

..kuhusu Magufuli kuwekewa sumu, hivi unaamini alipopata Uraisi haku-deal na wabaya wake? Ni ama aliwashughulikia kimya kimya, au hakuna aliyeshughulikiwa maana madai ya kulishwa sumu yalikuwa ya uongo.

..Suala la Lissu kuonana na Samia Suluhu liko wazi. Lissu alieleza mambo yote aliyozungumza na Rais. Kuna mpaka waliomlaumu Tundu Lissu kuwa alikuwa muwazi kupita kiasi.

..Serikali ya Magufuli pia ilikataa ombi la familia ya Tundu Lissu kuita wachunguzi toka nje waje kusaidia kuwanasa waliohusika.
 
OK fair enough! kwa kujificha nyuma ya kauli za Nyerere unapendekeza Muundo wa Serikali 2 uendelee.
Kumeundwa kamati zaidi ya 10 na zote hazikubaliana na muundo uliopo, tunaweza ku sustain hali iliyopo?

Tume ya Waioba ya mwisho ilihitimisha hivyo ukizingatia akina Salim A Salim, Warioba na Butiku ni watoto watiifu wa Mwalimu lakini bado walikuja na pendekezo tofauti. Tunawezaje kwenda mbele na Serikali 2!

Kwa Watanganyika kuingiwa na fatigue ya kuhudumia muungano na kiu ya kutaka kuamua mambo yao kwavile yameanishwa kikatiba bila Muundo (serikali) utawashauri vipi kwamba muundo wa S2 ni chaguo

Ni kweli lakini hukuelewa nilichokusudia. Ku accomodate ni kuwaweka karibu na Tanganyika! kwasababu Tanganyika haihitaji Zanzibar. In other words ndio better option, probably not but that's what is available

Wabunge wa Zanzibar wanakuja kwa yasiyozidi 3%. Wabunge hao wanakuja kukamilisha Katiba kwa 2/3 ya Zanzibar, ndio maana hatuna kura inayowapa Wabunge wa Kigoma, Mtwara au Ruvuma % yoyote

Watumishi wa Umma kutoka Zanzibar wanalipwa mishahara kutoka Bajeti ya Tanganyika.

Nilikuuliza uonyeshe bajeti ya SMZ na mafungu yake hukuweza kutetea hata category moja.

Wizara zote zinahudumiwa na kodi za Watanganyika. Wazanzibar wanapewa 21% lakini mishahara, marupu rupu na hata ustaafu ni pesa za Tanganyika. Mchango wao ni kupewa 21% ya ajira za vijana wa Tanganyika

Jambo jingine pengine hulijui. SMZ inapewa pesa kutoka kodi za Watumishi wa Zanzibar walioko Tanganyika. Yaani Tanganyika inatoa ajira kwa upendeleo kisha inawalipa SMZ kwa kuwasaidia tatizo la ajira.

Turejee tena bandiko la nyuma, tuonyeshe kutoka Bajeti ya SMZ mafungu yanayochangia uendeshaji wa JMT , kuanzia Wizara, Taasisi hadi ving'ora vya OMO!

Aha! kwavile kazaliwa Zanzibar ndio maana alitaka serikali 3? Halafu unasema HIZBU ndio wako nyuma ya Serikali 3. Jumbe si Hizbu ! ni Mbara kwa mujibu wako. Unaona jinsi unavyojichanganya, huna consistency.

Tukimuacha Jumbe, Maalim alitaka Serikali 3 akaenda mbali na upuuzi wa Mkataba.
Wazanzibar na Tume ya Warioba walitaka serikali 3, OMO na akina Jussa ndio wapiga debe wa serikali 3

Hoja ya Serikali 3 ni ya Wazanzibar, Watanganyika wanaichukua kwasababu wamechoshwa.
Mzigo wa kuhudumia JMT ni wao, kuhudumia SMZ ni wao kisha wanatukanwa.

Kubwa zaidi ni Wazanzibar kuwa ''special'' kwamba kila jambo wapewe kwasababu ya Uzanzibar! Watanganyika wanajiuliza ni kwa faida gani .

Absolutely! ndio maana Taasisi nyingine zinaendelea kujengwa. Kuna Chuo cha Polisi kinajengwa mbadala wa CCP Moshi. Kuna Chuo cha Uhamiaji kinajengwa, mbadala wa chuo cha Tanga.

Kwa uchumi wa Zanzibar hivi vyuo ni vya nini? Kuna mipaka mingapi inayohitaji chuo cha Uhamiaji?
Hata chuo cha Wanyama Pori Mwika kimeambiwa kijengwe Zanzibar, kwa wanyama gani.
Kuna MOI inajengwa Zanzibar n.k. Zote hizo ni gharama anazobeba Mtanganyika kwa jina la JMT

Katika hali hiyo Watanganyika wanakosa gani wakisema wakihitaji Muundo washughulikie mambo yao.

Nakubaliana nawe kabisa, kwamba Muungano uliopo ni wa Vitambulisho vya NIDA kwa ajili ya ajira na rasilimali kama ardhi kwa Wazanzibar. Hili tupo pamoja.

Swali, kwanini tupoteze muda tusiwaache waende zao !

Ni kweli ndio maana nilishauri kwamba ni muda muafaka tuwe majirani ! kama serikali 3 haziwezekani basi tugawane mbao za jahazi. Tanganyika haina cha kupoteza!

Ni kweli kabisa kwamba kuna viongozi wanachagiza haya tena wakifanya maandalizi haswa!
Kwanini tusiwe majirani wema? Wewe ndiye unashikilisa serikali 2 wakati unajua wanajitenga taratibu

Thank you! unatoa ushahidi muhimu kwamba hawana mchango, na Tanganyika imebeba mzigo.
Nakubaliana nawe 100% kwa hili, ndio maana narudia tena ikiwa ni hivyo kwanini kila mmoja asikusanye kodi zake! na kama haiwezekani basi tuwe majirani wema tunaopendana. Unaona kwanini Watanganyika wanaitaka nchi yao! halafu unawaita wapumbavu

Hapana kwasababu ni Taboo kuongelea uhuni wa Zanzibar! Yaani Wazanzibar wanaweza kusema chochote ikawa poa akisema Mtanganyika ni tatizo. Mfano, Mbowe aliposema ilikuwa kama nchi inawaka moto, majuzi hapa wale wabunge wanaokuja Dodoma kulala wakasema ''wanataka passport'' wengine Yuda, na kila aina ya upuuzi kwasababu hawana cha kusema, na hakuna aliyekemewa. Kwanini hawakukemewe , wana Uzanzibar Raia bora ndani ya JMT. Wanapewa kila kitu kwa upendeleo kwa gharama za Wananchi wetu!
Kuhusu Muundo wa Serikali umesema kamati 10 zote zilipinga Serikali 2 na tume ya Warioba walikuja hitimisha. Bado haya ni MAONI ya Wananchi ambayo hata mimi nina wajibu wa kutoa maoni yangu hata kama hayakubaliki na wengi otherwise msingejua sababu gani zinanifanya naamini Serikali 2 bado ni bora kuliko Serikali 3.

Nikitazama upande wa Serikali 3 majibu yao ni reactions za Watanganyika baada ya kuona Viongozi upande wa Zanzibar wanakiuka KATIBA ya JMT.

Yale yale alosema Kabudi kuhusu Watanganyika. Sasa hatuwezi kuwa na Muungano wa kutoshana na Kuogopana, kukomeshana sijui hatuwahitaji! Halafu unataka bado kuunda Serikali na hao usowataka.

Mke kama humtaki au hakutaki mpe talaka yaishe, laa mnataka kuwa pamoja itafute njia bora kwa wote pale mlipo, na sii ya kisasi au kukomoana. Ndoa itakufa, na Uadui utazidi zaidi baina yenu...

Mkuu, Hata vyama vingi vilipingwa kwa Asilimia 80 ya Wananchi lakini Mwalimu akalazimisha kinyume cha Matakwa ya Wananchi na Viongozi kina Mzee Ally Mwinyi na baadhi viongozi wengi walikuwa against Vyama vingi. Je, ilikuwa sahihi au ndio maana leo tumefikia hali hii mbaya ya Kisiasa?

Ni hivi mkuu wangu Mimi sijui kutenganisha Wazanzibar na Watanganyika ila naweza tenganusha Viongozi wa pande mbili kutokana na ITIKADI zao. Wanasiasa ndio wametufikisha hapa haswa baada ya kuwa na Vyama vingi.

Na bahati mbaya sana nchi nyingi duniani zimevunjikankutokana na Siasa za Vyama vingi ambavyo vimekuwa vikijikita katika kutetea maslahi ya MAJIMBO fulani within the Country. Siasa zetu zimegeuka sana sii ITIKADI tena bali ASILI zao.

Kwa hiyo, Wananchi wa pande zetu mbili, hawa Waathirika ni VICTIMS wa Siasa zetu zilochukua mrengo wa KIBAGUZI na yawezekana ndio dunia inapoelekea kutokana na UMASKINI ulotamalaki katika jamii zetu, kiasi kwamba imekuwa rahisi kuhadaika na fedha. Mashoga wanazidi kuongezeka na Hata mabinti siku hizi wanasema kama huna Hela usimsalimie

Wanishangaza sana unapohubiri Serikali 3 kwa mifano yako wakati huonhuo unasema kwa nini tusiachane nao, Hatuwahitaji! Kwa nini usisike moja kwamba TUVUNJE MUUNGANO Hatuwahitaji? Bada ya kuwa huku haupo kule haupo wamkula huu!

Na sijui kama unataka tena nirudie Historia yetu kwa nini Hatuwezi kuvunjanMuungano kwa sababubya Mihemko ya Wanasiasa wachache wanaotafuta UONGOZi kwa Udi na Uvumba! Na nimeeleza sana huko nyuma sipendi kutudia tudia viti vile vile nilivyokwisha vitolea maelezonmenfi na kwa kina.

Kila wakati unanipeleka mbele kisha unarudi nyuma yaani sielewi unataka kuelewa kitu gani zaidi. Serikali 3 kwa muundo wowote ulopendekezwa na Warioba ama viongozi wengine ni haufai kabisa utatuongiza shimo la Chewa!

Solution moja tu, Tuandike KATIBA MPYA kwa kuweka kwanza Maslahi ya TAIFA kama kweli pande mbili zinahitaji bado Muungano. Walivunja Katiba zao kupitia Sheria zao, Utekelezaji wao, Utendaji wao, na sehemu zote zinazokinzana na Katiba Hii zirekebishwe na hakuna Upande utaruhusiwa kwenda Kinyume cha Katika. Tufute hizo Taasisi zote ziloanzishwa Zanzibar na kuweka Mwongozo ambao hakuna Chama wala mtu ataruhusiwa kuuvunja.

Inakuwaje Kiongozi anaapishwa kashika Biblia au Kuruani na kusema Atailinda Katiba ya Jamhuri halafu kesho yake akiwa madarakani ndiye wa kwanza kuivunja halafu hakuna hatua zozote zinachukuliwa. Tena wanaisema Katiba kwa dharau kubwa halafu kumkamata mtu mwingine anaitumia Katiba hiyo hiyo alosema Katiba Mbovu!

Hapana mkuu, Sheria kali ziweke, Ukikiukaji wa Katiba ni UHAINI, Hakuna KINGA kwa Kiongozi yeyote. UCHOCHEZI wa Kitaifa pia ni UHAINI isije fika yakatukuta yale ya Rwanda maana sii lazima awe Mchungaji, Padre au Sheikh atakae tugawa kwa Ukabila, Udini au Ukanda.

Mijadala yote inayohusu Pande mbili zitajadiliwa Bunge la JMT sio kwenye mihadhara. Naishia hapa kwa leo, nimechoka mwili unakataa..

Maasalaam
 
..eneo aliposhambuliwa Lissu ni nyumba za viongozi wa bunge na serikali. Baadhi ya majirani zake walikuwa Naibu Spika Tulia Ackson, na Waziri wa Madini na Nishati Medard Kalemani. Maeneo ya aina hiyo ni gated na hulindwa na serikali.

..Kitendo cha ulinzi kutokuwepo siku aliyoshambuliwa Lissu kunaonyesha ni mpango uliohusisha watu wa serikali ya Magufuli. Haiwezekani ulinzi usiwepo eneo sensitive namna ile bila maelekezo toka kwenye vyombo vyenyewe au serikalini.

..Na kama Magufuli angekuwa ameguswa na tukio lile, au hakuhusika nalo, lazima kungefanyika juhudi kubwa kuwakamata wahusika. Muda wote wa sakata lile serikali haikuonyesha nia ya kuwakamata wahusika. Badala yake juhudi zilielekezwa kumkandamiza Tundu Lissu.

..Kuhusu waliotumwa kumshambulia Lissu mimi naona walikuwa wanaijua kazi waliyotumwa. Kama waliweza kumpiga risasi 17 unawezaje kusema hawajui kulenga shabaha.

..Na kulinganisha target practicing za JKT, na hit and run operation / mission to kill dhidi ya Lissu, nadhani ni kuwa naive, au labda umelenga kupotosha.

..kuhusu Magufuli kuwekewa sumu, hivi unaamini alipopata Uraisi haku-deal na wabaya wake? Ni ama aliwashughulikia kimya kimya, au hakuna aliyeshughulikiwa maana madai ya kulishwa sumu yalikuwa ya uongo.

..Suala la Lissu kuonana na Samia Suluhu liko wazi. Lissu alieleza mambo yote aliyozungumza na Rais. Kuna mpaka waliomlaumu Tundu Lissu kuwa alikuwa muwazi kupita kiasi.

..Serikali ya Magufuli pia ilikataa ombi la familia ya Tundu Lissu kuita wachunguzi toka nje waje kusaidia kuwanasa waliohusika.
Nimesema ni Eneo la Bunge, Viongozi wa Serikali waliopo pale ni kwa sababu wao pia ni Wabunge, laa kama tungekuwa na Mawaziri ambao sio Wabunge wasingekaa nyumba hizo pamoja na Wabunge wa vyama vya Upinzani.

Mkuu niacheni nipumzike. Nachoka miye Mkandara kueleza watu wasiotaka kuelewa ila wanacho elewa.
 
Wasichokiona Wasomi, Wenye Busara na Wazee
Kuhusu Muundo wa Serikali umesema kamati 10 zote zilipinga Serikali 2 na tume ya Warioba walikuna hitimisha, ni MAONI ya Wananchi, mimi nina wajibu wa maoni yangu hata kama hayakubaliki na wengi otherwise msingejua sababu gani zinanifanya naamini Serikali 2 bado ni bora kuliko Serikali 3.
Mkuu takwimu zinakataa! kuna kitu kinaitwa margin of error, unapokuwa na mfano 10:0 hakuna margin hapo
Kumbuka, hayo ni maoni ya Wananchi ambao ndio msingi wa muungano si maoni ya Wanasiasa, yaheshimiwe
Upande wa Serikali 3 majibu yao ni reactions za Watanganyika ya kuona Viongozi wa Zanzibar wanakiuka KATIBA ya JMT
Na wamebaini Zanzibar hawana mtu wa kuwakemea na tacitly wanaungwa mkono na viongozi.

Watanganyika wamechoshwa na identity ya Zanzibar katika Muungano, kwamba ukiwa Mzanzibar una hadhi fulani! mfano, utapata ajira si kwa sifa bali Uzanzibar n.k.

Tanganyika imechoka kuwa 'cash cow'' kutoa rasilimali, Zanzibar ikiondoa zake ''changu changu, chako chetu''
Mkuu, Hata vyama vingi vilipingwa nanasilimia 80 ya Wananchi, Mwalimu akalazimisha kinyume cha Matakwa ya Wananchi na viongozi wengi walikuwa against Vyama vingi.
No! mazingira ni tofauti. Kulikuwa na wimbi linapita duniani, Mwalimu akaona ni bora kuliwahi kuliko kusubiri.
Hayo ni maneno yake akisema msisubiri kufanya mageuzi kwa shinikizo! Mwalimu hakuwa na muda hasa akimkumbuka Nicolae Ceausescu wa Romania aliyesubiri wanaompinga wakawa wengi.

Please rejea hotuba yake. Hii ni tofauti na mazingira tuliyo nayo
Wanishangaza sana unapohubiri Serikali 3 kwa mifano yako wakati huonhuo unasema kwa nini tusiachane nao, Hatuwahitaji! Kwa nini usisike moja kwamba TUVUNJE MUUNGANO Hatuwahitaji? Bada ya kuwa huku haupo kule haupo wamkula huu!
Mkuu rejea bandiko langu nililotoa solution yangu. Nilisema hivi
Serikali 1 ni Dead on arrival (DOA)
Serikali 2 ni impossible
Serikali 3 zinawezekana ili kuwa accommodate Wazanzibar kwasababu Tanganyika haihitaji Zanzibar

Nikisema ikiwa 1,2,3 haziwezekani , tuishi kama majirani wema, tuvunje jahazi tugawane mbao kama zipo.
Sijui kitu gani kigumu hapo kuelewa
Hatuwezi kuvunjanMuungano kwa sababubya Mihemko ya Wanasiasa wachache wanaotafuta UONGOZi kwa Udi na Uvumba!
Wewe una mawazo butu sawa na Wazee wa CCM kwamba muungano ulindwe kwa nguvu zote.
Wananchi hawatakiwi kuongelea tatizo la Muungano eti ni taboo na kwamba ni jambo self regulated
Kwamba kuendelea kuwadekeza Wazanzibar na kuwapa kila wanachotaka ni kuimarisha Muungano

Imefika mahali kuna wanaolaani mijadala kama hii wakisema ni kugusa tunu za Taifa!

Wao na wewe humuoni hatari ya kuvunjika muungano usiku mmoja kama ilivyokuwa mwaka 1977 EAC ilipovunjwa na Kenyatta kwa Ushauri wa mpuuzi mmoja , Charles Njonjo.

Wewe na hao wazee tulieni niwape somo na kama mtazuia viburi vya kuelewa, mtanielewa

Rais Trump amekuwa kiongozi USA kwa ku ''tap grievances' kwa kuongelea maduku duku ya Wamarekani kiasi cha wao kusahau tabia zake.

1. Alijua kuna kundi la wabaguzi halimtaki Obama, Rais Trump akawaahidi '' turudishe nchi yetu''
2. Akajua kuna Wayahudi lenye pesa , Trump akawambia nitahamisha mji mkuu na kuvunja mkataba na Iran
3. Akajua kuna makampuni ya Insurance hayataki Obamacare, akaahidi kufuta Obama Care
4. Akajua kuna kundi lina umasikini, akwaahidi hakuna vita na pesa zitatumika kwa Waamerika ''America first''
5. Akajua bei za vyakula zipo juu, akaahidi kushusha bei siku ya kwanza Ofisini
Orodha inaendelea

Trump hakuwa na sera ya ndani au ya nje, alitumia madukuduku ya Wananchi kama sera, akafanikiwa.
Katika aliyoahidi mengi hakufanya , ni utapeli.

Kwa Tanzania, ipo siku ataibuka mtu au Chama na ku 'tap grievances'' au manung'uniko yao, iwe Tanganyika au Zanzibar. Mgombea ataahidi kurejesha Tanganyika. Kule Zanzibar ataibuka na kusema atavunja Muungano

Wananchi wanaweza kufanya maamuzi bila kujali madhara yake kama walivyofanya Wamarekani.
Akachaguliwa wa kuirejesha Tanganyika huku , na kule wa kuvunja muungano. Siku moja muungano unavunjika

Narudia tena masuala ya kijamii hayahitaji nguvu bali akili zaidi. Tumeshajifunza kwamba nguvu zina limitations, beyond the yield point! the results is unthinkable! kama hatujifunzi na kuamka muda utatuamsha

Tukiendelea na sera za kutojadili tatizo la wazi, hatari zake na ukweli mchungu ! tutakuwa tunaenzi sera zinazoitwa ''OSTRICH POLICY'' yaani sera za Mbuni kuficha kichwa mchangani akidhani ame solve tatizo

Nimesema ni Eneo la Bunge, Viongozi wa Serikali waliopo pale ni kwa sababu wao pia ni Wabunge, laa kama tungekuwa na Mawaziri ambao sio Wabunge wasingekaa nyumba hizo pamoja na Wabunge wa vyama vya Upinzani.

Mkuu niacheni nipumzike. Nachoka miye Mkandara kueleza watu wasiotaka kuelewa ila wanacho elewa.

..Ni eneo la SERIKALI.

..wanaishi Wabunge, Mawaziri, Makatibu wakuu.

..Siku ya tukio walinzi waliondolewa.

..Magufuli angekuwa hahusiki, na ana nia njema, angewakamata wahusika.
 
Back
Top Bottom