M'bananga chake hana kondo (If you spoil what is your own you have no quarrel)

Mkuu awali ya yote nikutake radhi ikiwa nachangia kitu nje ya mada yako. Nilidhani mada ni pana itahusisha mambo yote. Unaponisihi nianzishe uzi wa serikali 3 pengine ni katika kubakiza uzi huu kwa maana iliyokusudiwa. Niruhusu nijibu machache kama ulivyoeleza

Niliposema Makamu wa pili wa Rais wakati wa Nyerere Mh Kawawa alipewa jukumu la kushughulikia mambo ya Tanganyika nilimaanisha '' Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais'' na si mtu binafsi.
Nimetumia jina Kawawa kwa vijana kama ithbati kwamba Ofisi ya Makamu wa pili ilishikwa na Kawawa.

Mkuu sikweli kwasababu; Mwaziri wa Mifugo, Utalii, Elimu, Ujenzi, Afya, Kilimo, Viwanda, Nishati kwa uchache tu wa kuwataja hawana shughuli zozote Zanzibar na wala hawatambuliwi. Ikiwa ni hivyo, mambo wanayosimamia ni ya Tanganyika ingawa wamebeba nembo ya JMT.

The fact that hawakutajwa kama Mawaziri wa Tanganyika bado haiondoi ukweli kwamba wanashughulikia mambo ya Tanganyika bila kutajwa ni mawaziri wa Tanganyika. Tunajidanganya wenyewe.

Waziri asiye na kazi Zanzibar unamwitaje wa Muungano? Huyu ni Waziri wa Tanganyika. Ni kama mtu akiamua kukuita Mwanaume badala ya Mkandara katika ku conceal kitu fulani

Ni upuuzi ule ule wa kuita serikali ya Tanzania Bara. Ukishakuwa na Tanzania hakuna Bara. Hiyo ya Tanzania Bara haikuwepo wakati wa Uhuru. Zanzibar haikuungana na Tanzania Bara. Katika kukwepa neno Tanganyika, Watu wanajidanganya kwa kusema Tanzania Bara, upuuzi mtupu.

Hebu nieleze Waziri Mkuu ana jukumu gani Zanzibar ukiachilia kualikwa kufungua majengo siku za Jan 12 ili waweze kupata pesa zaidi za Tanganyika. Nipe kazi moja tu ya Waziri mkuu. Nipe kazi moja tu yaWaziri wa Utalii akiwa Zanzibar. Nipe kazi moja tu ya Waziri wa Afya akiwa Zanzibar n.k.

Kama Waziri hana kazi Zanzibar ataitwaje wa Muungano? Na kama si wa Muungano huyo ni wa kitu gani?
People including erudite should stop fooling themselves

Yale mambo 11 yameondolewa na Zanzibar bila kushirikisha Tanganyika ikiwemo gesi na mafuta, Bandari n.k.

Ukiona jambo Zanzibar haijaliondoa ujue wananufaika nalo. Mfano, Elimu ya Juu haikuwa katika 11, iliongezwa katika 22. Hata siku moja hutasikia Wazanzibar wakitaka Elimu ya juu iondolewe kwasababu vijana wa Zanzibar ni wanufaika, kwanza kwa mikopo wasiyorudisha na pili nafasi za upendeleo katika vyuo hata kama wa D 2

Katika yale 22 yanayolalamikiwa hakuna hata moja lenye manufaa kwa Tanganyika, ni kwa manufaa ya Wazanzibar. Kulalamikia Tanganyika ni kutokuwa mkweli.

Nakupa challenge, katika 22 tafuta moja tu utueleze hapa Tanganyika iliongeza ili kunufaika nayo kivipi.

Kwavile Wazanzibar ni watu wa kusikiliza hadithi zaidi ya kutafiti kuna mtu aliwadanganya kuhusu mambo 22.
Akina OMO ndio kazi yao na wanapoulizwa hawana majibu. Juzi si aliulizwa mamlaka kamili ni yapi.

Jibu la OMO likawa mchezo kwamba Zanzibar hairuhusiwi kujiunga na mashirikisho ya soka ya duniani.
OMO haelewi mambo mawili, kwanza, waliyoondoa Ligi kuu ni Wazanzibar wakiongozwa na Ali Salehe na Alberto. Pili, OMO haelewi kwamba sheria za kimataifa zinaangali bendera! na iliyopo ni ya JMT.

Ili kuondoa mzozo ondoa yote 22 kama Mzee Warioba alivyoshauri ! Ondoa hata kesho tuone nani ataumia!
Mkandara waelezieni Wazanzibar kwamba Tanganyika has nothing to lose! absolutely nothing!
Muungano ni pride tu ya Pan Africanism na legacy ya Nyerere, short of that hatuihitaji Zanzibar

Kuhusu mawaziri, hili umesema vema lakini wanaohusika na ujinga ni Wazanzibar. Hivi Katiba yao inawezaje kuwa na ukuu kuliko ya JMT? Ikiwa sheria za Bunge Dodoma lazima zipitishwe BLW tena licha ya Wazanzibar kuwepo Dodoma hawa watu wanawezaje kumheshimu Waziri wa Muungano!

Nadhani ulimuona TL na T-shirt ya Tanganyika kabla ya kwenda mahabusu. Nilimwelewa baada ya kutomwelewa siku nyingi sana. Nikupe mfano wa kutafakari. Kabla ya vita ya Iran vs Marekani/Israel kulikuwa na maandamano Tehran tunayojua yaliratibiwa na CIA/MOSAD, Unadhani Trump anayeita Iran terrorists anawapenda Wairan! kama utanielewa

Piga kwenye mshono, huyu Mkandara ni Mnafiki na Muongo.
🔥🔥🔥🔥
 
Hilo sio tatizo hata kidogo kuna visiwa kibao Uchumi wake wanategemea Utalii na Zanzibar inaweza kabisa tena kwa mafanikio makubwa. Leo hii Zanzibar inapokea ndege nyingi za Kimataifa Kuliko Uwanja wa Nyerere. Bado kuna Uvuvi wa Bahari.

Tatizo likitokana na uchangiaji wa mfuko wa Taifa, kesho tutaanza kuisema Mikoa ambayo haichangii, Kanda ya Ziwa na dhahabu zao watadai NCHI yao. Kule Mtwara na gas nao watadai NCHI yao. Hujagusia Kilimanjaro na Arusha. Kumbuka kabla ya Uhuru hizi zilikuwa himaya za Machief na hawakupendana kabisa. Ukabila utarudi kwa vizazi vijavyo. Mnataka tuwaachie wajukuu zetu zahma hizo?

Tukianza Upuuzi huu wa kuigawa nchi elewa hata amani itatoweka. Tazama Sudan, Ethiopia, Somalia, Libya yaani nchi zilotengana kwa sababu za Kisiasa, vita baina yao haitakoma. Mipaka ni ujanja wa Ukoloni Mambo leo na mwanzo wa UADUI.
Wewe Mkandara mbona unapigania sana Muungano? Watanganyika tumechoka unafiki na uongo, tunaitaka Tanganyika yetu. Kwani shida iko wapiii?
 
..kosa kubwa alilofanya Mwalimu Nyerere ni kuifuta Tanganyika, huku akiiacha Zanzibar.

..sasa tumefika mahali ambapo huwezi tena kuwashawishi Wazanzibari wafute utaifa wao, kama walivyofanya Watanganyika, ili wawe WATANZANIA.

..Uendeshaji wa nchi yetu ni mgumu sana kuuelezea ukaeleweka kwa mwananchi wa kawaida. Muungano wetu hauna mantiki.

..Kwa Watanganyika muungano ni sawa ni sawa na mwanaume aliyeoa lakini unyumba hapewi. Na zaidi analazimishwa kutoa hela ya matumizi.
Uko sahihi haswaaa, Huu ni Muungano au UTAPELI.
 
Kwanza, kwa miaka 62 Watanganyika walipoteza nchi yao kwa ajili ya Muungano, hawakuwahi kuisema Zanzibar. Hoja ya Tanganyika imeletwa mezani na Wazanzibar kwa kisingizio kwamba Bara wamejificha katika koti la Muungano. Hivyo Utanganyika umeombwa na Wazanzibar. Mkandara hakuona hiyo kama chuki za kipumbavu.

Hapa JF kuna mjadala mkandara ukitetea hoja za Wazanzibar kwamba wasikilizwe. Leo unaita upuuzi na upumbavu kwa hoja zile zile ulizotetea wakati upuuzi na upumbavu ukiwa ''in the making'

Pili, Wakati Maalim Seifa na akina Jussa wakitukana Muungano na kumwita Nyerere LAANATULLAH, wakidai mamlaka kamili Mkandara alikuwa kimya hakuona upuuzi na upumbavu, leo anauona

Tatu, wakati Zanzibar inataka mgao wa kila inachotaka Mkandara ulisema '' ni wadogo'' wanastahili kusaidiwa. Mkandara hakuona upuuzi na upumbavu kwamba zilikuwa nyufa za Muungano, hatimaye amefunguka macho

Nne, wakati Wazanzibar wakiusema Muungano ilikuwa ni halali, Mtanganyika akisema muungano ni haramu.

Prof Kabudi akiwa bado 'mzima' alisema '' Watanganyika wana yao moyoni wakiyatoa na kuidai Tanganyika yao itakuwa tatizo'' . Mkandara alikuwa akimya kwasababu Zanzibar ina haki ya kusikilizwa, si Tanganyika

Tano, hoja ya Mkandara ya changu ni changu na chako ni changu haiwahusu Watanganyika. Tanganyika imebeba muungano 100% . Waeleze Z'bar si kuwalaumu waliobeba zigo la misumari mgongoni

Sita, wakati Zanzibar inaanzisha Taasisi mbadala wa zile za JMT Mkandara alikuwa kimya. Leo akilulizwa kwanini kuna Taasisi mbadala hana jibu anawalaumu Watanganyika wanaohoji.

Hizi taasisi zinazoitwa za Muungano kama TCRA ni za Tanganyika, Zanzibar wana zao. Wazanzibar wanazitumia wanapohitaji mafao. Ni kama kuwa na kitambulisho cha NIDA kwa ajili ya kufanya shughuli Tanganyika

Mfano, Makusanyo ya TCRA yatokanyo na mawasiliano, Zanzibar inapewa sehemu yake. Yaani Mkandara akimpigia simu ndugu yake Ukerewe kuna aslilimia inapelekwa Zanzibar.

Halafu Mkandara huyo huyo anasema sisi ni nchi moja Tanzania kwanini kuwe na double taxation! Hajiulizi kwanini simu ya Mtwara-Musoma iwe na asilimia inaypelekwa Zanzibar

Saba, Mkandara anasema hoja ya kudai kuona mchango wa Zanzibar katika Muungano ni ya kipuuzi.
Mkandara huyo huyo anatetea hoja za Wazanzibar kudai wapewe lakini hataki kusikia wakiambiwa wachangie.

Tumefika hapa kwasababu tlifumbia macho upuuzi wakati unajijenga! Hatukuambina ukweli kwa kisingizio cha Muungano ni tunu yetu. Tuliwapa Wazanzibar kama Raia ''special'' wanaopaswa kuhudumiwa na kuamua hatma ya Tanganyika. Ule muda aliosema Prof Kabudi nadhani umewadia.

Mnyonge mnyngeni haki yake mpeni, Prof Kabudi alikuwa mbele ya muda miaka 12 iliyopita
Tunataka Tanganyika yetu. Na wakati ni sasa.
 
Wewe Mkandara mbona unapigania sana Muungano? Watanganyika tumechoka unafiki na uongo, tunaitaka Tanganyika yetu. Kwani shida iko wapiii?
Ebu nambie faida ya kuwa na Tanganyika halafu tutajadili maana nimeandika mengi kujibu hoja zenu lakini bado kuna watu wamefikia kuniita MNAFIKI sijui Unafiki wangu unatokana na nini?

Mimi najua shida yenu ni Urais wa Samia kwa sababu Mzanzibar na kaupata kupitia njia zisokubalika! Semeni Ukweli kwani shida iko wapi? Lakini najua pia kwa ayofanya yeye angekuwa Mbara msingelalamikia Muungano. Na Zanzibar wao walipinga Muungano wakaitaka Zanzibar Huru wakati rais ni Mkapa. Tena walimtukana mpaka Nyerere wakimruka Mwinyi. Even a fools can tell what's behind all that!

Kila anapotokea Rais Mbara au Mkristu, Mzanzibar, au Muislaam tunapigana kwa sababu ya Asili yake sio SERA zake. Who is wrong here! Ama hamuyaoni?

Na hata kama Samia anakosea yeye Uzanzibar wake ndio unatangulia hoja zenu. Kweli, watu wqzima mnaitaka Tangabyika kwa sababu ya Samia - Mzanzibar? Then what? Kesho akiongoza Muislaaam mtaacha kumchana kwa Uislaam wake? Nadhani mmeshaonja nyama.ya Mtu nyie..

Tatizo ni mind set zenu zinaongozwa na Ukabila, Udini na Ukanda, I don't see anything else. Hata mnaposema sijui rais apunguziwe madaraka wakati Katiba ya nchi zote duniani zinampa rais madaraka ya kuunda Serikali (Government) kwa maana ya DOLA.

Rais, Atachagua baraza lake la Mawaziri, Spika na Jaji Mkuu kuendana na Ahadi alizowapa wananchi akashinda Uchaguzi mkuu. Laa sivyo atatekelezaje SERA zake ikiwa mtamwekea watu.wenu wasiokubaliana na Sera na mrengo wake? Ushindi wa nini basi!

Ukweli ni kwamba rais anashinda Uchaguzi Mkuu kutokana na ahadi alizowaahidi wananchi kupitia Sera na Ilani na hawezi tekeleza hayo ikiwa hana mamlaka ya kuunda Serikali yake. Infact, Hakuna Chama cha Siasa kinachounda Serikali bali mamlaka hayo ni ya rais popote utakapo kwenda. Tqnzania unaambiwa ati Chama ndio kinachounda Serikali. Uongo na Ukiukaji wa Katiba dhahiri.

Ndio maana mnapopiga kura mmeweka roho zenu rehani wazungu wanasema sign your life away kumchagua rais!. Kitu pekee kinachoweza fanyika ni chaguzi zake zote zipitiwe na Bunge, pengine tuongeze sehemu nyingine ya Bunge tukiita Baraza la Wazee ama Senate. Kila aloteuliwa na rais atapitishwa na vyombo hivyo lakini haiwesekani kumuondolea rais Mamlaka ya kuunda Serikali. Nje ya hapo kwa nini tumchague rais ambaye hana Mamlaka?

Shida ya Muungano inatokana na WATU kama ilivyo katika Utawala. Kama Samia sio rais mzuri anaondoka yeye sio Muungano. Je, akitokea kiongozi Mchagga akawa na uongozi kama huu mtaitaka Arusha yenu? Ama akitokea rais Mkristu, Waislaam hawamtaki mtagawana kuti? Haya yq Utanganyika na Uzanzibar ni Upumbavu mkubwa mnajaribu kutuhadaa sote ilihali tunajua mkosa nani..

We are the one who have the problem, infact sisi ndio WENYE NCHI (Wananchi) rais kapata Urais kwa ridhaa yetu na kama Samia hakupata baraka za Wananchi then tunajua tatizo ni NANI sio Muungano. Same goes to Constitution, kuna mambo ndani ya Katiba yanakiukwa na Viongozi tunaihukumu Katiba kuwa ndiyo Mbovu!

Chukulia hili Biblia imekataza Ushoga lakini kuna Mashoga na wanazidi kuongezeka. Je, utasema Biblia ndio mbovu kwa kushindwa kuzuia watu wasipende Ushoga? Kwa hiyo, Ibadilishwe Biblia ili iweje yaani? Huu ni mfano tu nakupa..

So UNAFIKI sina ila nazungumza Ukweli ambao hamtaki kuusikia. Na miaka yote nilokuwa hapa Jamiiforums hamkunielewa mpaka yanapowakuta ndio mnabaki kutafuta Mchawi. My all life hapa JF nimekuwa nikitafuta Solution badala ya Kilalamika kutafuta Mchawi. Siasa na Historia ndio elimu nilozipenda kuliko kila kitu. Naijua Historia yetu na nazijua Siasa zetu.

Maasalaam
 
...mjadala ulikuwa mzuri sijui kwanini umeamua kutoa mashambulizi.

..Na wewe ndio mtoa mada. Sasa unataka na sisi tukushambulie?

..Mtoa mada hutakiwi kushambulia wachangiaji ktk mada yako.
 
Ebu nambie faida ya kuwa na Tanganyika halafu tutajadili maana nimeandika mengi kujibu hoja zenu lakini bado kuna watu wamefikia kuniita MNAFIKI sijui Unafiki wangu unatokana na nini?
Mkuu Mkandara hoja hii usiwaulize Watanganyika!Waulize Wazanzibar ndio wenye agenda ya Tanganyika irudi.

Rasimu ya Warioba: Wazanzibar walitaka Serikali 3(S3) au Muungano wa Mkataba. Hawakuta S2 su S1

Ushahidi ni Kitabu cha Aboud Jumbe na kilichomwondoa madarakani ni serikali 3 akisisitiza Tanganyika irudi.

Maalim Seif akaibeba agenda akisema ili Muungano uwe wa haki na sawa Tanganyika irudi ''HAKI SAWA''.

OMO na kina Jussa wanataka serikali ya Tanganyika irud kimya chao ni kuvmbiwa na vibuyu vya asali na ving'ora . Nyerere alitukanwa LANAATULLAH, unajua hili Mkandara, ndio msingi wa watu kukuambia una UNAFIKI.

Unajuwa wazi wanaoitaka Tanganyika ni Wazanzibar wakilaani 'Tanganyika kuvaa koti la Muungano'
Wazanzibar wanadai Tanganyika irudi, wanamtukana Nyerere na Jussa ni shahidi, Mkandara ulikuwa kimya

Leo unaingiza hoja za Udini kana kwamba yameanza jana. Hukumbuki Jumbe aliondolewa na kitu gani, Wariba alisema nini, Maalim alitaka nini, OMO anataka nini! Mamlaka kamili ni uwepo wa S3

Kwamba Wazanzibar wakisema sawa, akisema Mtanganyika ni kosa, unamshaiwishi vipi aliyekuita mnafiki kwamba hakuwa sahihi. Katika '' with all due respect you've double face''

Tanganyika ikirudi itafadika na nini!
Kwa miaka 62 Tanganyika imetoa kila ilicho nacho kulinda Muungano, kelele hazijakoma
Wazanzibar wanachukua uvumilivu wa Tanganyika kama advantage na kuita KERO ambazo nyingi ni upuuzi.

Hivi kuagiza maziwa na kuyaingiza Tanganyika bila kulipia kodi ni Kero!
Kelele za Muungano zinadumaza mijadala yenye maana kwa ujenzi wa Tanganyika.

Raia wanasema Muungano uwepo lakini uwe na mipaka kwa faida ya pande zote na si mbeleko.
Mimi najua shida yenu ni Urais wa Samia kwa sababu Mzanzibar na kaupata kupitia njia zisokubalika! Semeni Ukweli kwani shida iko wapi? Lakini najua pia kwa ayofanya yeye angekuwa Mbara msingelalamikia Muungano. Na Zanzibar wao walipinga Muungano wakaitaka Zanzibar Huru wakati rais ni Mkapa. Tena walimtukana mpaka Nyerere wakimruka Mwinyi. Even a fools can tell what's behind all that!

Kila anapotokea Rais Mbara au Mkristu, Mzanzibar, au Muislaam tunapigana kwa sababu ya Asili yake sio SERA zake. Who is wrong here! Ama hamuyaoni?
Mkuu hapa hakuna ukweli.
Nimekutembeza katika Historia kuanzia Jumbe hadi OMO , wote wanadai Tanganyika.
Tupo hapa Jamvini, rudi miaka 20 nyuma utaona tatizo la Muungano halikuanza na Samia.

Nyerere alikutana na akina Jumbe , Ramadhani Faki na Maalimu.
Mwinyi alikutana na G55, Mkapa akakutana na Mauaji Pemba, JK akakutana na Katiba
Magufuli akapiga marufuku kuzungumzia kwa mkono wa chuma lakini watu walizungumza

Mkuu unapoletewa hoja zikakuzidi unatumbukiza hii karata hatari ya Udini, too low

Mbona hujiulizi kwanini Wazanzibar wapo kimya licha ya miaka mingi ya kuitaka Tanganyika

Udini should never be a line of defence. Unapaswa kujibu hoja as a veteran in this forum.

Hoja ni hizi na ndizo unatakiwa kujikita na kuzifafanua , ni katika mjadala;

1. Je si kweli kwamba waliotaka Tanganyika irudi ni Wazanzibar na ndio waanzilishi wa hoja
2. Je, si kweli kwamba OMO alipoteza cheo cha AG Zanzibar kwa hoja ya Serikali tatu Bunge la Katiba
3. Je, si kweli kwamba matatizo ya Muungano yalianza wakati wa Nyerere?
3b. Je, si kweli Wazanzibar walimtukana Mwalim na kumlaani kwa LAANATULLAH kwasababu ya Muungano
4. Je si kweli kwamba Samia akiwa Bunge la Katiba aliyakuta matatizo hayo!
5. Je, si kweli kwamba kauli za kibaguzi kama za akina Sada Mkuya na H. Mwinyi zinachochea mgawanyiko!
6Je, si kweli kwamba kila Taasisi ya JMT ina mbadala wake Zanzibar na kuzua maswali kuhusu Muungano
7. Je si kweli kwamba ndani ya Tanzania Zanzibar inapewa ''special treatment' kuliko eneo jingine!
8. Je, si kweli kwamba Zanzibar haina mchango katika kuendesha Muungano lakini inadai zaidi kila siku
9. Je, si kweli kwamba uwepo wa ZanID umelenga kuwatenga Watanganyika na fursa za Zanzibar
10. Je, si kweli kwamba Zanzibar inapewa 9% kutoka 4.5% ya pato la Tanganyika !
11. Je, si kweli kwamba kuna nafasi za upendeleo kwasababu ya Uzanzibar ndani ya JMT
12. Je, si kweli kwamba mjadala wa G55 ulianza wakati wa Mwinyi (mzanzibar) na aliyeuzima ni Nyerere (Mtanganyika ) na kwamba hakuna udini wala Utaifa bali hoja

Orodha inaendelea

Nawaalika Wakongwe watuthibitishie kama mijadala ya Muungano haikuanza 2006 hapa JF

JokaKuu Pascal Mayalla Mzee Mwanakijiji Mwalimu Gagnija Rev.Kishoka Maxence Melo Nyani Ngabu Kiranga

Mkuu Mkandara hoja hii usiwaulize Watanganyika!Waulize Wazanzibar ndio wenye agenda ya Tanganyika irudi.

Ushahidi ni Kitabu cha Aboud Jumbe na kilichomwondoa madarakani ni serikali 3 akisisitiza Tanganyika irudi.

Maalim Seif akaibeba agenda akisema ili Muungano uwe wa haki na sawa Tanganyika irudi ''HAKI SAWA''.

OMO na kina Jussa wanataka serikali ya Tanganyika irud kimya ni kuvmbiwa na vibuyu vya asali na ving'ora .
Nyerere alitukanwa LANAATULLAH, unajua hili Mkandara, ndio msingi wa watu kukuambia una UNAFIKI.

Unajuwa wazi wanaoitaka Tanganyika ni Wazanzibar kwa jina la 'Tanganyika katika koti la Muungano'
Msemo wa Tanganyika inafaidika katika koti la Muungano umeletwa na Wazanzibar

Wazanzibar wanadai Tanganyika irudi, wanamtukana Nyerere na Jussa ni shahidi, Mkandara ulikuwa kimya leo unaingiza hoja za Udini kana kwamba yameanza jana. Hukumbuki Jumbe aliondolewa na kitu gani

Kwamba Wazanzibar wakisema sawa, akisema Mtanganyika ni kosa, unamshaiwishi vipi aliyekuita mnafiki kwamba hakuwa sahihi. Katika hili nina wasi wasi kwamba una double face

Tanganyika ikirudi itafadika na nini! Kwa miaka 62 Tanganyika imetoa kila ilicho nacho kulinda Muungano, kinyume chake Wazanzibar wanabeba KERO kama kisingizio cha muungano kuwaumiza, ambazo nyingi ni upuuzi.

Hivi kuagiza maziwa na kuyaingiza Tanganyika bila kulipia kodi ni Kero! Kelele za Muungano zinasababisha mambo mengi ikiwemo Katiba kukwama. Kuondokana na hayo watu wanasema Muungano uwepo lakini sasa kuwe na mipaka na si mipaka tu bali Muungano uwepo kwa faida ya pande zote na si mbeleko.

Mkuu hapa hakuna ukweli. Nimekutembeza katika Historia kuanzia Jumbe hadi OMO , wote wanadai Tanganyika.

Mkuu tupo hapa Jamvini, rudi miaka 20 nyuma utaona tatizo la Muungano lipo pale pale pale halikuanza na Samia. Nyerere alikutana na akina Jumbe , Ramadhani Faki na Maalimu.
Mwinyi alikutana na G55, Mkapa akakutana na Mauaji Pemba, JK akakutana na Katiba
Magufuli akapiga marufuku kuzungumzia kwa mkono wa chuma lakini watu walizungumza

Tatizo lako mkuu unapoletewa hoja zikakuzidi unatumbukiza hii karata hatari sana ya Udini.
Hivi Mbona hujiulizi kwanini Wazanzibar wapo kimya licha ya miaka mingi ya kuitaka Tanganyika

Mkuu, unapo 'interject' hoja za udini ni hatari, this should never be a line of defence.

Unapaswa kujibu hoja kwa hoja bearing in mind that you're a veteran in this forum.

Hoja ni hizi na ndizo unatakiwa kujikita na kuzifafanua , ni katika mjadala. Mijadala ni jambo la kheri

1. Je si kweli kwamba waliotaka Tanganyika irudi ni Wazanzibar na ndio waanzilishi wa hoja
2. Je, si kweli kwamba OMO alipoteza cheo cha AG Zanzibar kwa hoja ya Serikali tatu Bunge la Katiba
3. Je, si kweli kwamba matatizo ya Muungano yalianza wakati wa Nyerere?
3b. Je, si kweli Wazanzibar walimtukana Mwalim na kumlaani kwa LAANATULLAH kwasababu ya Muungano
4. Je si kweli kwamba Samia akiwa Bunge la Katiba aliyakuta matatizo hayo!
5. Je, si kweli kwamba kauli za kibaguzi kama za akina Sada Mkuya na H. Mwinyi zinachochea mgawanyiko!
6Je, si kweli kwamba kila Taasisi ya JMT ina mbadala wake Zanzibar na kuzua maswali kuhusu Muungano
7. Je si kweli kwamba ndani ya Tanzania Zanzibar inapewa ''special treatment' kuliko eneo jingine!
8. Je, si kweli kwamba Zanzibar haina mchango katika kuendesha Muungano lakini inadai zaidi kila siku
9. Je, si kweli kwamba uwepo wa ZanID umelenga kuwatenga Watanganyika na fursa za Zanzibar
10. Je, si kweli kwamba Zanzibar inapewa 9% kutoka 4.5% ya pato la Tanganyika !
11. Je, si kweli kwamba kuna nafasi za upendeleo kwasababu ya Uzanzibar ndani ya JMT
12. Je, si kweli kwamba mjadala wa G55 ulianza wakati wa Mwinyi (mzanzibar) na aliyeuzima ni Nyerere (Mtanganyika ) na kwamba hakuna udini wala Utaifa bali hoja

Orodha inaendelea

Nawaalika Wakongwe watuthibitishie kama mijadala ya Muungano haikuanza 2006 hapa JF

JokaKuu Pascal Mayalla Mzee Mwanakijiji Mwalimu Gagnija Rev.Kishoka Maxence Melo Nyani Ngabu
Kwanza nianze kusema ya kwamba Abdul Jumbe alikuwa Makamu wa rais na rais wa Zanzibar akiwa hana madaraka kamili ya Urais. Na nadhani Abdul Jumbe asili yake ni Mbara kwa hiyo simtofautishi na marais wengine walokataa Muungano wa nchi zetu EA kwa kuzingatia heshima na madaraka makubwa walopewa katika.nchi zao. Kwa Waafrika status yao na mamlaka ni kitu cha kwanza kabisa they don't care about Nationalism.

Swala la Serikali 3 limenadiwa na watu wengi walotaka nafasi zaidi za Uongozi ngazi tofauti kwa sababu tukiwa na Serikali 3 nafasi za Utawala zitaongezeka. Wale G55 na kina Malecela, Kolimba nao walitaka Serikali 3 kwa sababu akili zao wali prefer zaidi muundo wa Marekani wa Federation. Ushauri sii mbaya lakini usilazimishe kitu bila kupambanua hasara za Serikali 3 kwa jamii.

Labda nirudie kusema hivi, Leo hii Bara tuna Wabunge 222 wa majimbo, tukiwa na Serikali 3 tutaongeza tena Wabunge 222 wa Tanganyika. Kumbuka muundo wa Federation kila Jimbo hutoa wabunge wawili, mmoja wa Federation na mwingine kwa Tanganyika. Tanganyika itakuwa na Baraza lake la Mawaziri ukiacha wale wa Federation na mwisho itakuwa na Mahakama zake. Unaongeza na Watumishi wa Serikali yake bado hujaweka hesabu ya Mashangingi, mafuta, nyumba, n.k. Haya yote watakao faidika ni ViongoI sio wewe Mwananchi.

Gharama zote za kugharamia yote hayo zitafanywa na wewe MTanganyika. Halafu kwa sababu tumesha anza na mguu wa kushoto ilitakiwa Mamlaka ya kukusanya kodi iwe moja tu TRA kwa pande sote karika muundo wa Federation, lakini leo hii tuna TRA na ZRA kila upande na chake, tukiwa na Serikali 3 sidhani kama Zanzibar watakubali kurudi katika muundo waloukiuka toka mwanzo.

Na kitakacho fuata ni Mambo ya Muungano walokwisha yakiuka! Watataka yaendelee kuwa kama yalivyo sasa hivi i doubt watakubali turudi katika mambo 11 au 22 ya Muungano kwa sababu kwanza wamesha yavunja na pili wanataka zaidi Muungano wa Mkataba (Jumuiya) sio Serikali 3. Jiulize kwa nini walifanya mabadiliko ya mwaka 2010 ambayo yanakiuka Katiba hii na wala sii ya Muundo wa Serikali 3?

So they started to ignite cheche hizi za Serikali 3 makusudi while behind the scene wanataka Zanzibar HURU (Hizbu Ideology) back to Sultanate! Amini suiamini mtakuja siku nikumbuka Mkandara aliwahi kusema hivyo.

Ni laghai isokuwa na maana kusema ati Zanzibar wanatujali sana Tanganyika ndio maana wanataka Serikali 3. Viongozi wa Zanzibar wanataka Mamlaka kamili ya kuongoza nchi yao na sii ati Serikali 3 would change anything on their side, maana tayari wanayo Serikali yao. Tukiwa na Serikali 3 haitaongeza wala kupunguza chochote walichonacho leo isipokuwa Bara itabeba mzigo wote wa Federation ambao tunalipia about 96% ya gharama zote na kisha tutalipia tena gharama zote za Serikali ya Tanganyika. Huu ndio uliopo Marekani, Canada na nchi nyingi zilochukua muundo wa Federation zao.

Kwa hiyo siongei kitu nisichokijua na Mwalimu alijua na akasema wazi kwamba alikataa Serikali 3 kwa sababu alifahamu gharama zake kwa bara. Na ukiisoma Rasimu ya Warioba imependekeza rais mambo machache muhimu ya Muungano kama Usalama, Immigration sijui na nini lakini Ukweli ni kwamba Wewe mwananchi utamchahua rais wa Jamhuri kwa sifa zipi? Ahadi zipi ambazo Mwananchi atampigia kura rais ambaye hana Mamlaka? And that will be the end of Union. Rais asokuwa na faida wa nini? Ceremonial President wa nini? Sii ndio tunarudi kwenye Usultan au Uchief.

Serikali 2, imetuwezesha kulipa Wabunge 222 kwa hharama kubwa lakini wameshughulikia Mambo ya Muunhano na yasokuwa ya Muungano kwa Bara (Tanganyika) badala ya Wabunge 444 bado hujaongeza viti maalum na wengineo. Marais watatu yaani kila position Serikalini tuna wawili wawili..

Mwisho, niulize kama Kiongozi wa Federariona.kiitwa rais hao wa nchi hizo 2 nao wataitwa Marais? Yaani nchi imetoka katika marais Wawili wanapigiwa kelele tunaenda kwenye Marais Watatu, wakati huo huo Mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar! Yaani wee acha tu..
 
..Mbona huulizi Wazanzibari kwa miaka yote hii wanampigia kura Raisi wa muungano kwa ahadi zipi?

..Kama Zanzibari wenye serikali yao wameweza kumpigia kura Rais wa muungano basi hata Watanganyika wakiwa na serikali yao wataweza.

..Suala la gharama linaweza kushughulikiwa kwa namna zaidi ya moja, ikiwemo kupunguza idadi ya wabunge walioko sasa hivi, pamoja na kudhibiti uundwaji wa wizara.

..Pia sio lazima serikali ya Tanganyika na Zanzibar ziongozwe na Maraisi. Tunaweza kuwa na Mawaziri Wakuu, na tukabaki na Rais mmoja wa muungano.
 
Kwanza nianze kusema ya kwamba Abdul Jumbe alikuwa Makamu wa rais na rais wa Zanzibar akiwa hana madaraka kamili ya Urais. Na nadhani Abdul Jumbe asili yake ni Mbara....
Hapa huoni kuingiza Ubara na Uzanzibar ni makosa, lakini unatushawishi kwamba hoja za leo ni kutokana na Samia kuwa Mzanzibar. Una ji contradict vibya sana. Hoja ya Ubara wa Jumbe ni 'anachronism''

Jumbe ni Mwanamapinduzi heshimu kazi aliyoifanya 1964. Ukianza hayo hutamwacha Natepe , Hassan Nasoro Moyo, Mohamed Khatib n.k. Nakuelewa, Mzanzibar kwako lazima awe shombe!
Leo hii Bara tuna Wabunge 222 wa majimbo, tukiwa na Serikali 3 tutaongeza tena Wabunge 222 wa Tanganyika.
Rudi kasome Rasimu ya Warioba. Totally misinformed or deceiving

Kuna mambo 7 katika Rasimu:
Ulinzi na Usalama, Mambo ya Ndani, Mambo ya Nje, Fedha, Katiba, Msajili wa vyama na Ofisi ya Rais

Bunge la Dodoma halitakuwa na Wabunge 222 kama unavyosema.

Ni wajibu wa Serikali ya Tanganyika kuamua idadi ya Wabunge. Hakuna Formula inayo govern kama ambavyo Zanzibar waliamua kuwa na Wabunge 50. Ndio maana kulikuwa na transition period ili Tanganyika iweze ku settle

Pili, hakuna Formula kwamba katika federation kuwe na Wabunge wawili, hiyo ni fabrications

Rais wa Serikali ya Muungano atakuwa na mamlaka kwasababu;
Ana udhibiti wa Jeshi na Vyombo vya Usalama
na udhibiti wa Katiba na Mambo ya Fedha
Ana udhibiti wa Siasa za nje na Mambo ya Ndani

Tuangalie hali itakayokuwa katika mambo 7
1. Fedha - Tayari tunao muundo sijui gharama zitaongezeka wapi
2. Msajili wa vyama- Tayari ana Ofisi na inafanya kazi sijui gharama zitaongezeka wapi
3. Katiba- Labda kutakuwa na idara lakini sijui gharama zitaongezeka wapi
4. Mambo ya Nje, hata sasa hivi Tanganyika inabeba huo mzigo sijui gharama zitaongezeka wapi
5. Mambo ya Ndani, Tanganyika inabeba huo mzigo sijui gharama zitaongezeka wapi
6. Ulinzi na Usalama- Structure ipo tayari sijui gharama zitaongezeka wapi
7. Ofisi ya Rais- Tunayo sasa gharama zinaongezeka wapi. Kumbuka PM itakuwa Ofisi ya Rais wa Tanganyika

Mambo ya Tanganyika kama Elimu, Afya, Utalii, Viwanda , Mifugona Maji, Biashara , Ujenzi, etc ambayo leo si ya Muungano lakini yanaitwa ya JMT yatakuwa ya Tanganyika.
Mfano Elimu gharama zitaongezeka wapi? Shule na vyuo ni hivi hivi vya leo

Zanzibar Tayari wana structure yao, tena sasa kuna chuo cha Polisi, Uhamiaji vinajengwa ili kuongeza Taasisi za Zanzibar nje ya Muungano. Tayari wana Jeshi lao. Hakuna tatizo

Usijaribu ku quote kauli za Nyerere just to suit your narrative that's disingenuous. Nyerere aliposema gharama alimalizia hivi '' Kama unadhani gharama za Serikali 3 ni rahisi waulize Wazanzibar''

Nyerere alimaanisha uwepo wa Serikali 3 utaipa Zanzibar gharama kwasababu Zanzibar inategemea Taasisi kama Ulinzi kutoka Bara, Mambo ya Nje kutoka Bara, Mambo ya ndani kutoka Bara.

Bajeti ya Ulinzi ya JMT ni Trilion 8 sawa na Bajeti ya SMZ. Ukiwaambia Zanzibar wachangie 10% ni shida kwa makusanyo ya Bilioni 400 sijui, kwa mwezi.

Kuhusu Bunge la Muungano, litakuwa na Wajumbe 75 kwa mujibu wa Rasimu ya Warioba.

40 kutoka Bara kama siksoei na 35 Zanzibar. Hili halina gharama kwasababu wale wa Zanzibar watalipiwa na SMZ. Tanganyika kwasasa inalipia Wabunge 86 wa Zanzibar kuja Dodoma kulala.
Maana yake Tanganyika inaokoa pesa kwakuwa na Wabunge 40 kutoka pool ya wasinziaji 86 kutoka Zanzibar

Kuhusu Tanganyika kuwa na baraza lake la mawaziri, hiki nacho ni kichekesho, kwani lililopo sasa hivi ukiondoa mambo 4 ni la nani! Ni Tanganyika, gharama zinaongezeka wapi!

Hoja ni kwamba Tanganyika haitaingia gharama kwasababu hadi sasa inaibeba Zanzibar, lakini katika Serikali 3 Zanzibar itawajibika kuchangia na hilo ndilo linalosemwa ''Gharama zitaongezeka''

Kwasasa Mkandara haoni kwamba Tanganyika imebeba mzigo wa JMT na Zanzibar kwa Pamoja

Mkandara kama hakuna Formula inayowezekana! kwasababu S2 hazikubaliki sasa hivi, S1 ni kichekesho na S3 unasema ni gharama, suluhu yako ni ipi? Mimi ninayo, tunaweza kuwa majirani wema !

JokaKuu
 
Ebu nambie faida ya kuwa na Tanganyika halafu tutajadili maana nimeandika mengi kujibu hoja zenu lakini bado kuna watu wamefikia kuniita MNAFIKI sijui Unafiki wangu unatokana na nini?

Maasalaam
Mkandara, unafiki wako haukuanza juzi, jana wala leo kwa sababu wewe siku zote ni mmoja kati ya wafaidika wakubwa wa Muungano kama ulivyo...kwa msemo wako "mbanaga chake hana kondo"

Kati ya wasiokuwa na uzalendo kwa taifa lao kwa kutanguliza mjaslahi binafsi, wewe Mkandara uko miongoni mwa vinara ambao kwa nyakati tofauti fursa ya kulamba mema ya nchi hii huwagongea hodi.

Asanteni sana Nguruvi3, JokaKuu na wote ambao mmejitahidi kumpa ukweli huyu mtoa hoja na nawaomba misimamo ya watu kama Mkandara isiwatoe relini. Kwa sasa nitaishia hapo, sina zaidi.

​

Tulikua nchi 2 zilizo ungana ila sasahivi tuna nchi mbili zilizo ungana lakini moja (zanzibar) ina mamlaka kamili na haitakiwi kabisa kuingiliwa kwy mambo yako ilhali hii nchi nyingine (Tanganyika) haitakiwi kabisa ijulikane kama ipo bali ilikufa baada ya muungano na ukiitaja hata kwa kuiulizia tu unaonekana mbaguzi isipokuwa zanzibar ni haki kuizungumzia. Documents zinaonyesha zanzibar kumezwa ila kiutendaji Tanganyika sio tu imemezwa bali imekufa na haitakiwi kufufuka ni Uhaini.
Inaumiza sana
 
Ebu nambie faida ya kuwa na Tanganyika halafu tutajadili maana nimeandika mengi kujibu hoja zenu lakini bado kuna watu wamefikia kuniita MNAFIKI sijui Unafiki wangu unatokana na nini?

Mimi najua shida yenu ni Urais wa Samia kwa sababu Mzanzibar na kaupata kupitia njia zisokubalika! Semeni Ukweli kwani shida iko wapi? Lakini najua pia kwa ayofanya yeye angekuwa Mbara msingelalamikia Muungano. Na Zanzibar wao walipinga Muungano wakaitaka Zanzibar Huru wakati rais ni Mkapa. Tena walimtukana mpaka Nyerere wakimruka Mwinyi. Even a fools can tell what's behind all that!

Kila anapotokea Rais Mbara au Mkristu, Mzanzibar, au Muislaam tunapigana kwa sababu ya Asili yake sio SERA zake. Who is wrong here! Ama hamuyaoni?

Na hata kama Samia anakosea yeye Uzanzibar wake ndio unatangulia hoja zenu. Kweli, watu wqzima mnaitaka Tangabyika kwa sababu ya Samia - Mzanzibar? Then what? Kesho akiongoza Muislaaam mtaacha kumchana kwa Uislaam wake? Nadhani mmeshaonja nyama.ya Mtu nyie..

Tatizo ni mind set zenu zinaongozwa na Ukabila, Udini na Ukanda, I don't see anything else. Hata mnaposema sijui rais apunguziwe madaraka wakati Katiba ya nchi zote duniani zinampa rais madaraka ya kuunda Serikali (Government) kwa maana ya DOLA.

Rais, Atachagua baraza lake la Mawaziri, Spika na Jaji Mkuu kuendana na Ahadi alizowapa wananchi akashinda Uchaguzi mkuu. Laa sivyo atatekelezaje SERA zake ikiwa mtamwekea watu.wenu wasiokubaliana na Sera na mrengo wake? Ushindi wa nini basi!

Ukweli ni kwamba rais anashinda Uchaguzi Mkuu kutokana na ahadi alizowaahidi wananchi kupitia Sera na Ilani na hawezi tekeleza hayo ikiwa hana mamlaka ya kuunda Serikali yake. Infact, Hakuna Chama cha Siasa kinachounda Serikali bali mamlaka hayo ni ya rais popote utakapo kwenda. Tqnzania unaambiwa ati Chama ndio kinachounda Serikali. Uongo na Ukiukaji wa Katiba dhahiri.

Ndio maana mnapopiga kura mmeweka roho zenu rehani wazungu wanasema sign your life away kumchagua rais!. Kitu pekee kinachoweza fanyika ni chaguzi zake zote zipitiwe na Bunge, pengine tuongeze sehemu nyingine ya Bunge tukiita Baraza la Wazee ama Senate. Kila aloteuliwa na rais atapitishwa na vyombo hivyo lakini haiwesekani kumuondolea rais Mamlaka ya kuunda Serikali. Nje ya hapo kwa nini tumchague rais ambaye hana Mamlaka?

Shida ya Muungano inatokana na WATU kama ilivyo katika Utawala. Kama Samia sio rais mzuri anaondoka yeye sio Muungano. Je, akitokea kiongozi Mchagga akawa na uongozi kama huu mtaitaka Arusha yenu? Ama akitokea rais Mkristu, Waislaam hawamtaki mtagawana kuti? Haya yq Utanganyika na Uzanzibar ni Upumbavu mkubwa mnajaribu kutuhadaa sote ilihali tunajua mkosa nani..

We are the one who have the problem, infact sisi ndio WENYE NCHI (Wananchi) rais kapata Urais kwa ridhaa yetu na kama Samia hakupata baraka za Wananchi then tunajua tatizo ni NANI sio Muungano. Same goes to Constitution, kuna mambo ndani ya Katiba yanakiukwa na Viongozi tunaihukumu Katiba kuwa ndiyo Mbovu!

Chukulia hili Biblia imekataza Ushoga lakini kuna Mashoga na wanazidi kuongezeka. Je, utasema Biblia ndio mbovu kwa kushindwa kuzuia watu wasipende Ushoga? Kwa hiyo, Ibadilishwe Biblia ili iweje yaani? Huu ni mfano tu nakupa..

So UNAFIKI sina ila nazungumza Ukweli ambao hamtaki kuusikia. Na miaka yote nilokuwa hapa Jamiiforums hamkunielewa mpaka yanapowakuta ndio mnabaki kutafuta Mchawi. My all life hapa JF nimekuwa nikitafuta Solution badala ya Kilalamika kutafuta Mchawi. Siasa na Historia ndio elimu nilozipenda kuliko kila kitu. Naijua Historia yetu na nazijua Siasa zetu.

Maasalaam
Mkandara
Mbona unaonekana mkongwe sana humu lakini unashindwa kusimama kwenye hoja na consistency. Yaani tumetoka kwenye mjadala wa Muungano mpaka Udini!!

Halafu unakuwa kama haupo well informed. Uliisoma rasimu ya Jaji warioba na mependekezo ya Serikali tatu?
Unafahamu kuwa Zanzibar wana taasisi zao zisizoingiliwa na Muungano ikiwemo vikosi vya usalama?
Unafahamu hoja za Serikali tatu zilianza na nani kati ya Watanganyika au Wazanzibari?

Zanzibar kukiuka katiba ni kwa sababu ya Udini, Ubinafsi au Uzalendo?
 
Msingi mkuu wa mauzauza tuliyo nayo sasa kwenye huu muungano ni hoja dhaifu iliyotumika kuhalalisha muundo wa serikali mbili eti kwa sababu muundo wa serikali moja utasababishwa Zanzibar imezwe na Tanganyika. Huwezi kusema unataka muungano wa nchi 2 huru zenye haki na hadhi sawa halafu wakati huo huo unatumia mbeleko kuibeba nchi moja ili isimezwe na kupoteza identity yake huku unaifuta kabisa nchi nyingine! You cant eat your cake and still have it!

Huwezi ukasema nchi 2 huru zimeungana wakati upande mmoja umefutika kabisa wakati upande wa pili una katiba yake unayoitambua kama ni NCHI KAMILI... mnakumbuka mwanasiasa mmoja aliyejaribu kusema ZNZ sio nchi alivyoshambuliwa?? Mauzauza tu!
 
..Mbona huulizi Wazanzibari kwa miaka yote hii wanampigia kura Raisi wa muungano kwa ahadi zipi?

..Kama Zanzibari wenye serikali yao wameweza kumpigia kura Rais wa muungano basi hata Watanganyika wakiwa na serikali yao wataweza.

..Suala la gharama linaweza kushughulikiwa kwa namna zaidi ya moja, ikiwemo kupunguza idadi ya wabunge walioko sasa hivi, pamoja na kudhibiti uundwaji wa wizara.

..Pia sio lazima serikali ya Tanganyika na Zanzibar ziongozwe na Maraisi. Tunaweza kuwa na Mawaziri Wakuu, na tukabaki na Rais mmoja wa muungano.
Ok, naona hoja zimekuwa nyingi na zote muhimu kuzitolea maelezo kwa Uelewa wangu japo nafahamu hapa tumefika mahala Hojanzote zinazojadiliwa zinanihusu MIMI sasa na sio MUUNGANO. Nitarudi kwa Nguruvi3 na wengineo fanyeni subira. Maswali ama hoja ni nyingi.

Nd. JokaKuu, Tunajadili uhalisia hapa na sii dhana dhaifu ya hoja. Umenambia kwa nini nisiwaulize Wazanzibar kwa nini humchagua rais wa JMT? Sielewi unataka kudhihirisha nini maana Uchaguzi Mkuu ni haki ya kila Mtanzania Kikatiba hakuna tofauti ya Serikali 1, 2 wala 3. Hivyo wanapiga kura kwa mgombea Urais wa JMT kwa sababu Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri.

Na miaka yote Upande wa Zanzibar wamekuwa wakimpigia Kura mgombea wa JMT ambaye kwanza SIFA kubwa kwao lazima awe Mzanzibar mwenzao (Ukanda), tena wa Upinzani kutoka CUF hadi sasa ACT. Umeuliza kwa Ahadi zipi? Bila shaka ni Sera za CUF na ACT kutaka Muungano wa Mkataba.

Na kama nilivyosema awali wanatumia Serikali 3 kama kiingilio tena katika hotuba hizi baada ya Uchaguzi. Kabla na wakati wa kampeni hutasikia Serikali 3 isipokuea Muungano wa Mkataba, wakidai Zanzibar HURU kama kwamba leo hawapo Huru pamoja na kwamba wana Serikali yao.

Kwa hiyo mnanishangaza sana mnapodhani mimi nawatetea Zanzibar lakini ni mimi nilosema Kinacho haribu Muungano wetu ni kuruhusu Siasa za HIZBU kurudi Zanzjbar na hizi zitatugawa kwa sababu ni maadui wa ASP toka zamani hata kabla ya Mapinduzi.

Maelezo kama haya nilisha yazungumza mara nyingi sana humu JF toka zamani na sijabadilisha maneno na kwa bahati mbaya sana Wazanzibar wengi hawaelewi Historia yao nje ya Usultan chini ya Muingereza. Wasijue hata Marais wao toka Uhuru Walowahi kuongoza Zanzibar karibu wote wana Asili ya Bara.

Swala la Gharama za Serikali 3. Mkuu wangu yaani watu tunalalamika kwa matumizi makubwa ya muundo huu wa Serikali 2 unawezaje sema zinaweza shughulikiwa kwa njia tofauti ikiwa leo hii na Seeikali 2 pekee inatushinda? Kwa nini hizo njia tusianze kubadilisha LEO tukiwa na Serikali 2 kurahisisha mfumo wa Utawala? Unawezaje fikiria hata hilo wakati unaongozwa na watu wenye tamaa na Uchu wa mali ukadhani kesho ati watageuka kuwa Malaika?

Mkuu wangu mathlan wee Mke mmoja anakupa shida unawezaje ongeza mke wa pili ili kumkomoa jeuri ya mke wa kwanza, ukasema nitapunguza matumizi kwa kupunguza kitu gani? Watoto ulowazaa au michepuko yako?😂😂😂

Maasalaam
 
Mkandara, unafiki wako haukuanza juzi, jana wala leo kwa sababu wewe siku zote ni mmoja kati ya wafaidika wakubwa wa Muungano kama ulivyo...kwa msemo wako "mbanaga chake kondo"

Kati ya wasiokuwa na uzalendo kwa taifa lao kwa kutanguliza mjaslahi binafsi, wewe Mkandara kwa hakika ni miongoni mwa vinara kwani unakula mema ya nchi hii.

Asanteni sana Nguruvi3, JokaKuu na wote ambao mmejitahidi kumpa ukweli huyu mtoa hoja na nawaomba misimamo ya watu kama Mkandara isiwatoe relini. Sina zaidi.

​

Kila pahala naposoma nanyooshewa kidole mimi hadi kuitwa MNAFIKI kwa sababu sijui ni mfaidika wa hali iliyopo. Inabidi nicheke tu, maana kwa wale wanaonijua personally wanajua maisha yangu na familia yangu. Yote namwachia Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma. Ahsante sana Mag3 pengine waniombea mema katika uzee huu..
 
Msingi mkuu wa mauzauza tuliyo nayo sasa kwenye huu muungano ni hoja dhaifu iliyotumika kuhalalisha muundo wa serikali mbili eti kwa sababu muundo wa serikali moja utasababishwa Zanzibar imezwe na Tanganyika. Huwezi kusema unataka muungano wa nchi 2 huru zenye haki na hadhi sawa halafu wakati huo huo unatumia mbeleko kuibeba nchi moja ili isimezwe na kupoteza identity yake huku unaifuta kabisa nchi nyingine! You cant eat your cake and still have it!

Huwezi ukasema nchi 2 huru zimeungana wakati upande mmoja umefutika kabisa wakati upande wa pili una katiba yake unayoitambua kama ni NCHI KAMILI... mnakumbuka mwanasiasa mmoja aliyejaribu kusema ZNZ sio nchi alivyoshambuliwa?? Mauzauza tu!
Nitakujibu kwa maelezo mafupi sana. Zanzibar wanayo Serikali yao na Serikali ya JMT ni Serikali ya Bara kwa mambo yote ya Muungano na yasokuwa ya Muungano. Tumeua ndege wawili kwa jiwe moja. Kinachokosekana ni JINA tu la Tanganyika. Ni sawa leo badala ya kukuita Mwalimu tukupe jina la Mhadhili.. yaani tumekupandisha hadhi 😂😂😂
 
Mkandara
Mbona unaonekana mkongwe sana humu lakini unashindwa kusimama kwenye hoja na consistency. Yaani tumetoka kwenye mjadala wa Muungano mpaka Udini!!

Halafu unakuwa kama haupo well informed. Uliisoma rasimu ya Jaji warioba na mependekezo ya Serikali tatu?
Unafahamu kuwa Zanzibar wana taasisi zao zisizoingiliwa na Muungano ikiwemo vikosi vya usalama?
Unafahamu hoja za Serikali tatu zilianza na nani kati ya Watanganyika au Wazanzibari?

Zanzibar kukiuka katiba ni kwa sababu ya Udini, Ubinafsi au Uzalendo?
Nimeisoma Rasimu ya Warioba, ni nzuri lakini vipo vifungu sikubaliani navyo. Kama raia nina haki ya Maoni yangu kama ulivyokuwa na haki wewe.

Najua vizuri sana Muundo wa Serikali 3 na ndio kiini cha hoja zangu. Isitoshe hunsikia Mzee Warioba akihutubia kuhusu Ukiukaji wa Katiba wa Wazanzibar na nadhani kule nyuma nimeweka kipande kimoja cha hotuba yake.

Nisichokubaliana naye nu kuunda Serikali 3 Ukaifanya ya JMT kuwa dhaifu kuliko zile za States. Na kibaya zaidi kuifanya Serikali ya JMT haina mapato maana sehemu zote zilowekwa hazina mapato yake, Je watapata hela kutoka wapi? Wachangiwe na hizo States wanapojisikia kutoa? Utaendeshaje Serikali Kuu anbayo inategemea Ufadhili?

Laa mkinambia Serikali Kuu itakuwa ya Kifalme (Ceremonial President) then kwa nini tunahitaji Serikali hiyo, nipe sababu! Mwanachi atampigia kura rais asokuwa na Mamlaka kwa sifa zipi yaani? Aliwahi kuwa Chief Mtemi fulani au! Halafu ndiye awe Amiri Jeshi Mkuu?

Zanzibar wamekiuka Katiba ya Jamhuri kwa.mageuzi mengi, vile vile Bara tumekiuka Katiba sehemu nyingi haswa katika HAKI, USAWA, UWAKILISHI na UTEKELEZAJI.

Ikiwa tunataka Mabadiliko ya Katiba ni muhimu kwanza tudhibiti huu Ukiukaji wa KATIBA. Hatuwezi andika Katiba Mpya kwa watu ambao kwanza wanaudharau Katiba, wanakiuka na hata kutoa matamshi yanayokinzana na Katiba.

Mtazamo wangu ni huu, Ukitaka kukomesha USHOGA pambana kwanza na MABASHA.. kuwahukumu ******* ukaacha Mabasha mtaani ni sawa na kupanda mbegu juu ya Kichuguu..

Maasalaam.

Mh Nguruvi3 nitakuja kwako baadae kidogo nipate riziki maana mmeniweka kati utadhani tuna Ugonvi..😂😂😂
 
Ok, naona hoja zimekuwa nyingi na zote muhimu kuzitolea maelezo kwa Uelewa wangu japo nafahamu hapa tumefika mahala Hojanzote zinazojadiliwa zinanihusu MIMI sasa na sio MUUNGANO. Nitarudi kwa Nguruvi3 na wengineo fanyeni subira. Maswali ama hoja ni nyingi.

Nd. JokaKuu, Tunajadili uhalisia hapa na sii dhana dhaifu ya hoja. Umenambia kwa nini nisiwaulize Wazanzibar kwa nini humchagua rais wa JMT? Sielewi unataka kudhihirisha nini maana Uchaguzi Mkuu ni haki ya kila Mtanzania Kikatiba hakuna tofauti ya Serikali 1, 2 wala 3. Hivyo wanapiga kura kwa mgombea Urais wa JMT kwa sababu Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri.

Na miaka yote Upande wa Zanzibar wamekuwa wakimpigia Kura mgombea wa JMT ambaye kwanza SIFA kubwa kwao lazima awe Mzanzibar mwenzao (Ukanda), tena wa Upinzani kutoka CUF hadi sasa ACT. Umeuliza kwa Ahadi zipi? Bila shaka ni Sera za CUF na ACT kutaka Muungano wa Mkataba.

Na kama nilivyosema awali wanatumia Serikali 3 kama kiingilio tena katika hotuba hizi baada ya Uchaguzi. Kabla na wakati wa kampeni hutasikia Serikali 3 isipokuea Muungano wa Mkataba, wakidai Zanzibar HURU kama kwamba leo hawapo Huru pamoja na kwamba wana Serikali yao.

Kwa hiyo mnanishangaza sana mnapodhani mimi nawatetea Zanzibar lakini ni mimi nilosema Kinacho haribu Muungano wetu ni kuruhusu Siasa za HIZBU kurudi Zanzjbar na hizi zitatugawa kwa sababu ni maadui wa ASP toka zamani hata kabla ya Mapinduzi.

Maelezo kama haya nilisha yazungumza mara nyingi sana humu JF toka zamani na sijabadilisha maneno na kwa bahati mbaya sana Wazanzibar wengi hawaelewi Historia yao nje ya Usultan chini ya Muingereza. Wasijue hata Marais wao toka Uhuru Walowahi kuongoza Zanzibar karibu wote wana Asili ya Bara.

Swala la Gharama za Serikali 3. Mkuu wangu yaani watu tunalalamika kwa matumizi makubwa ya muundo huu wa Serikali 2 unawezaje sema zinaweza shughulikiwa kwa njia tofauti ikiwa leo hii na Seeikali 2 pekee inatushinda? Kwa nini hizo njia tusianze kubadilisha LEO tukiwa na Serikali 2 kurahisisha mfumo wa Utawala? Unawezaje fikiria hata hilo wakati unaongozwa na watu wenye tamaa na Uchu wa mali ukadhani kesho ati watageuka kuwa Malaika?

Mkuu wangu mathlan wee Mke mmoja anakupa shida unawezaje ongeza mke wa pili ili kumkomoa jeuri ya mke wa kwanza, ukasema nitapunguza matumizi kwa kupunguza kitu gani? Watoto ulowazaa au michepuko yako?😂😂😂

Maasalaam

..hivi tunavyozungumza Tanganyika imebeba gharama za kuendesha mambo ya muungano, na mambo ya Tanganyika.

..kwani wanaposema Tanganyika imevaa koti la muungano wewe unadhani wanamaanisha nini?

..Kwa hiyo kuigatua serikali ya Tanganyika kutoka ktk serikali ya muungano siamini kama kutaleta ongezeko la gharama kwa kiasi kikubwa.

..Kwa hiyo hoja yangu, iko palepale kwamba serikali ya Tanganyika iundwe, na hatua za kudhibiti ukubwa wake, na gharama zake, zizingatiwe.
 
Nimeisoma Rasimu ya Warioba, ni nzuri lakini vipo vifungu sikubaliani navyo. Kama raia nina haki ya Maoni yangu kama ulivyokuwa na haki wewe.

Najua vizuri sana Muundo wa Serikali 3 na ndio kiini cha hoja zangu. Isitoshe hunsikia Mzee Warioba akihutubia kuhusu Ukiukaji wa Katiba wa Wazanzibar na nadhani kule nyuma nimeweka kipande kimoja cha hotuba yake.

Nisichokubaliana naye nu kuunda Serikali 3 Ukaifanya ya JMT kuwa dhaifu kuliko zile za States. Na kibaya zaidi kuifanya Serikali ya JMT haina mapato maana sehemu zote zilowekwa hazina mapato yake, Je watapata hela kutoka wapi? Wachangiwe na hizo States wanapojisikia kutoa? Utaendeshaje Serikali Kuu anbayo inategemea Ufadhili?

Laa mkinambia Serikali Kuu itakuwa ya Kifalme (Ceremonial President) then kwa nini tunahitaji Serikali hiyo, nipe sababu! Mwanachi atampigia kura rais asokuwa na Mamlaka kwa sifa zipi yaani? Aliwahi kuwa Chief Mtemi fulani au! Halafu ndiye awe Amiri Jeshi Mkuu?

Zanzibar wamekiuka Katiba ya Jamhuri kwa.mageuzi mengi, vile vile Bara tumekiuka Katiba sehemu nyingi haswa katika HAKI, USAWA, UWAKILISHI na UTEKELEZAJI.

Ikiwa tunataka Mabadiliko ya Katiba ni muhimu kwanza tudhibiti huu Ukiukaji wa KATIBA. Hatuwezi andika Katiba Mpya kwa watu ambao kwanza wanaudharau Katiba, wanakiuka na hata kutoa matamshi yanayokinzana na Katiba.

Mtazamo wangu ni huu, Ukitaka kukomesha USHOGA pambana kwanza na MABASHA.. kuwahukumu ******* ukaacha Mabasha mtaani ni sawa na kupanda mbegu juu ya Kichuguu..

Maasalaam.

Mh Nguruvi3 nitakuja kwako baadae kidogo nipate riziki maana mmeniweka kati utadhani tuna Ugonvi..😂😂😂
Unapozungumzia Bara unamaanisha Tanganyika?
Hiyo 'bara' unaweza kueleza ni kwa namna gani imekiuka vipi katiba kwenye HAKI, USAWA, UWAKILISHI na UTEKELEZAJI.

Na hiyo Zanzibar imekikuka katiba katika mambo yapi?
 
Back
Top Bottom