Si kweli! Nyerere alianza na Rais, Makamu wa kwanza wa Rais, na Makamu wa pili wa Rais.
Walikuwa Nyerere, Karume na Kawawa. Kazi za Makamu wa pili ilikuwa kusimamia shughuli za Tanganyika.
Maana yake ni kwamba kulikuwa na JMT, SMZ na Tanganyika a.k.a mambo yasiyo ya Muungano
Mkuu Mkandara ''mwiba hutoka ulipoingilia'' haya yameanzishwa na wenyewe. Kuna kiongozi alipoingia madarakani alisimama na kumwambia waziri wake wa mambo ya nje '' Jambo likifanyika huku na kule pia''
Unaweza kuona hata teuzi za nafasi. Narudia tena, mwiba hutoka ulipoingilia
Waliomsaliti Mwalimu si hawa wa mamlaka kamili! kutoka Zanzibar. Hadi leo akina OMO wanauzungumzia Muungano kwa indhara na kashfa na hapo ndipo wametibua nyongo za Watanganyika. When you live in a glass house don't throw stones
Kama ni sehemu ya Tanzania, 21% ya ajira ni za nini? 10% ya Mapato ya Tanganyika ni ya nini? Kwanini kuna fungu maalumu la HESLB kwa Wazanzibar? Nitajie mkoa mmoja tu wa Tanganyika unaopewa upendeleo kama huo
Kuchangia muungano ni gharama za kuuendesha. Muungano si gugu maji la kujiendesha lenyewe
Kodi za TRA Zanzibar hazivuki bahari, lakini za Tanganyika zinakwenda kwa mabilioni
Gharama za Taasisi zote na Wizara za Muungano Zanzibar haichangii kwa mujibu wa Gavana Ben Ndulu
Akina OMO hao na tunawaunga mkono. Wajitoe tu tutakutana EAC na SADC. Hatuna sababu za kutumia mudamwingi kuhangaika na eneo lisilo na tija kwa ustawi wa Tanganyika. Kama muungano ukiwepo ni lazima Wazanzibar watambue nafasi yao. Kwamba ni ka eno kadogo kenye watu wachache na uchumi mdogo
Hata sisi Tanzania tuna ji behave mbele ya Wababe wa Dunia. Tunajua nafasi yetu hatuwezi kutunishiana misuli na Russi, China au USA. Hakuna usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar, waambieni ukweli
Of course Muungano ni moja ya blunder za Mwalimu Nyerere. Mwl hakuangalia mbele katika mfumo na matatizo yatakayojitokeza . Mwl alikumbana na misuko suko ya akina Jumbe , Ramadhani Faki, Maalim n.k. hakuchukua hatua akiamini mambo yatakuwa salama. Mwl hakujua akina OMO watakuja kubomoa Muungano na si kuimarisha. Mtu anaulizwa mamlaka kamili ni vipi, hana jibu. Kesho anarudia yale yale asiyokuwa na majibu!
Hapa unamlaumu nani? Zanzibar wana ZRB hawataki TRA na wanailaani. Waambie ukweli huu
Yes ni kwasababu ya ''abuse''. Mfano SMZ ina shirika lake la viwango (ZBS) umewahi kujiuliza ni kwanini! Jibu ni kwamba hawataki TBS ili kuweka viwango vyao vya chini bidhaa ziingie Zanzibar kisha kuletwa Bara.
Kule Bandari Zanzibar wanalipa kodi kidogo sana. Kontena moja la milioni 5 Tanganyika ni Milioni 20.
Arguably utasema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, je, kwa mwendo huo Tanganyika itapata wapi mapato?
Kumbuka mapato ya Zanzibar yanabaki huko
Ni wewe unayepaswa kujiuliza kwanini kila Taasisi ina mbadla Zanzibar. Tanganyika wlaikubali kuwa ni JMT, unapokuwa na TBS na kisha ZBS , hii TBS ni ya nani? Unapokuwa na HESLB na kisha ZHESL hii HESLB ni ya nani?
Ulipouliza Zanzibar ina mchango gani ikiwa ni sehemu ya Tanzania, Mkandara hujiulizi kwanini kuna TBS na ZBS. Kuna HELSB na ZHESLB. Kuna TAAA na ZAAA. Kuna TDA na ZFDA, kuna NECTA na Baraza Zanzibar.
Kila Taasisi ina mbadala Zanzibar hadi Uhamiaji na Jeshi Katika nchi moja.
Watanganyika wanasema hivi, Tanganyika yao iirudi ili wajue wanahangaika na nini. Huu muungano wa kutafuta NIDA ili kupata soko la bidhaa, ajira na ardhi sioni udhati wake