Mbarawa: Daraja la Tanzanite halilipiwi kwa sababu limejengwa kwa fedha za Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1643968909162.png

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote. Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.

Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.

Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.

MWANANCHI
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote.
Kweli kabisa ila tuwe wakweli zaidi, ni fedha ya msaada za wafadhili toka serikali ya South Korea, yaani Grant Aid.

Lile daraja la Nyerere Kigamboni mi mkopo wa NSSF kwa serikali.
Mkopo inabidi ulipwe.
 
Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.[emoji848][emoji848][emoji848]

NSSF wakisharushisha gharama zao na faida(naamini wamesharudisha) je watakoma kutoza tozo ya kivuko!? Jibu ni rahisi sana HAPANA!

Sasa watafanya nini!? Itachezwa movie ya kiini macho ya kuondoa hiyo tozo kishapo italetwa tozo nyingine kwa jina lingine watu waendelee kupiga hela.. Ile ni biashara yenye faida tupu haiwezi kuachwa
 
Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.

Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.

Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.

MWANANCHI
Hio mikopo yote iwe nafuu au sio nafuu inalipwa na fedha za walipa kodi watanzania na wageni.sijamuelewa kabisa Waziri nadhani kakurupuka toka usingizini.
 
Kweli kabisa ila tuwe wakweli zaidi, ni fedha ya msaada za wafadhili toka serikali ya South Korea, yaani Grant Aid.

Lile daraja la Nyerere Kigamboni mi mkopo wa NSSF kwa serikali.
Mkopo inabidi ulipwe.
Kigamboni sio mkopo ni mradi wao nssf,
 
Hata hilo tanzanite Bridge wangewalipisha mashuwa huko...
Dunia ya leo hakuna cha bure

Ova
Unamaanisha wanaopita Daraja la ruvu, wami, na kwingine nao walipie?
Kuna muda akili zako huwa zinaenda likizo, watu wanalipa Kodi. Kodi inakusanywa na serikali ili kuleta huduma Kama hizo. Sasa hapo bure ipo wapi?
Hata serikali ikichukua mikopo, bado serikali italipa hivyo mikopo kupitia Kodi wanayokusanya.
 
Madaraja mengi tu yana toll roads
Kwa hiyo mzoeee,dunia ya leo hakuna bure
Hutaki lipa piga mbizi

Ova
 
Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.[emoji848][emoji848][emoji848]
NSSF wakisharushisha gharama zao na faida(naamini wamesharudisha) je watakoma kutoza tozo ya kivuko!? Jibu ni rahisi sana HAPANA!
Sasa watafanya nini!? Itachezwa movie ya kiini macho ya kuondoa hiyo tozo kishapo italetwa tozo nyingine kwa jina lingine watu waendelee kupiga hela.. Ile ni biashara yenye faida tupu haiwezi kuachwa
Jibu ni ndio. Hesabu zao zilikuwa miaka 30 lakini mpaka sasa linaingiza hela kuliko matarajio Yao haitafika miaka 15 litarudi serikali I na kuwa bure.
 
Unamaanisha wanaopita Daraja la ruvu, wami, na kwingine nao walipie?
Kuna muda akili zako huwa zinaenda likizo, watu wanalipa Kodi. Kodi inakusanywa na serikali ili kuleta huduma Kama hizo. Sasa hapo bure ipo wapi?
Hata serikali ikichukua mikopo, bado serikali italipa hivyo mikopo kupitia Kodi wanayokusanya.
Hiyo kawaida hata huko kwa wenzetu kulipia kawaida tu kwa madaraja yaliyoko kwenye miji
Achana na mfano wa madaraja kama ruvu

Ova
 
Back
Top Bottom