Mbarawa: Daraja la Tanzanite halilipiwi kwa sababu limejengwa kwa fedha za Serikali

Mbarawa: Daraja la Tanzanite halilipiwi kwa sababu limejengwa kwa fedha za Serikali

Acheni kujitoa akili. Daraja la Kigamboni limejengwa kwa michango ya wafanayakazi tu (nssf) lazima hela zao zirudi. Tanzanite limejengwa kwa kodi za wananchi kwanini lilipiwe?!
Halafu kuwa na adabu sio wote wakaao Kigamboni ni walalahoi!
Okay
 
Kumbukeni hii habari ni ya February mwaka huu.
 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote. Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.

Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.

Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.

MWANANCHI
Kwanini wasitafute mkopo nafuu wailipe NSSF halafu serikali iendelee Kulipia Pasi kuhusisha wananchi
 
Back
Top Bottom