Mbarawa: Daraja la Tanzanite halilipiwi kwa sababu limejengwa kwa fedha za Serikali

Mbarawa: Daraja la Tanzanite halilipiwi kwa sababu limejengwa kwa fedha za Serikali

Hahaha

Hawajazoea wanataka bwerere

Hata kwa wenzetu huko...mfano daraja la sanfransico miakaa nenda rudi watu wanalipia
Madaraja mengi yaliyopo kwenye miji inalipiwa
Hata hili tanzanite wanavutiwa pumzi tu
Watawekew toll

Ova
Tanzanite haliwezi kuwekwa tozo kwasababu alizosema waziri. Tanzanite ni kama old selander au Jangwani bridge tu.
 
Tanzanite limejengwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka korea kusini au msaada kutoka korea kusini, mbona hatuelewi
 
Ah, mama anaiachia nini mibilioni yote ile?!!! Ah, anataka kunidhi sasa.

MAMA KUSANYA MAPESA UKAJENGE MBOONGE WA DARAJA JANGWANI PALE WA KUTATUA, MILELE, KERO YA PALE WAKATI WA MVUA. AH!!
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote.

Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.

Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.

Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.

MWANANCHI
ujinga mtupu
kwahiyo hela ya nsssf siyo ya tanzania, si ni serikali imekopa nssf na serikali hiyo imekopa nje ikajenga tanzanite, yote ni mikopo
 
kiukweli kama mwenye nacho hata zidi kuwa nacho kwa sababu huduma kwake kwa nchi hii zimekuwa nzuri kuliko huku kwa kajamba nani.

Daraja la kigamboni kwa nini watu wa kipato cha chini tuna lipa ila ili la kwenda kwa matajiri ni bure.

ina maana wanakatwa kwenye kodi za biashara zao na sisi kodi zote tutalipa kama mnavo tukamua
 
Acheni kujitoa akili. Daraja la Kigamboni limejengwa kwa michango ya wafanayakazi tu (nssf) lazima hela zao zirudi. Tanzanite limejengwa kwa kodi za wananchi kwanini lilipiwe?!
Halafu kuwa na adabu sio wote wakaao Kigamboni ni walalahoi!
 
Waambie haooo

Ova
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote. Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.

Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.

Amesema daraja la Kigambo lilijengwa kutokana na uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo ni lazima zirudishwe.

MWANANCHI
Si walisema Mzee anakopa hela kimyakimya kuendeleza miradi?
 
Kwa akili zenu mlidhani mkisema tulipe tungekubali? Wakati pale kuna salenda bridge watu wangeenda kujazana pale.
 
Hahaha

Hawajazoea wanataka bwerere

Hata kwa wenzetu huko...mfano daraja la sanfransico miakaa nenda rudi watu wanalipia
Madaraja mengi yaliyopo kwenye miji inalipiwa
Hata hili tanzanite wanavutiwa pumzi tu
Watawekew toll

Ova
Hatimaye yametimia.
 
MImi nasubiria watangaze kuingia Kariakoo kwa Malipo! Hutaki nenda soko la Tandale ama Tandika!
 
Back
Top Bottom