Mbaroni kwa kumkamata, kumshambulia na kusambaza picha za utupu za waliyemfumania

Mkuu una uhakika walipeana talaka......au waliachana kimasihara.
Walifunga ndoa ya kimila, , walishatengana, mwanaume alienda kumnyang'anya mwanamke watoto , wakawa wanaishi kwa dada yake ambaye ni mmoja wa watuhumiwa.
Baada ya hapo mwanaume alitaka mwanamke arudi kijijini alikomtoa ndio chanzo Cha ugomvi na kumtumia msg za vitisho Kama ataendelea kuishi maeneo hayo atamfanyia kitu kibaya.
 
Hawakuwafumania hao wote waliokamatwa ni mwanaume na ndugu zake ndio walifanya kitendo hicho, huyo dada namfahamu vizuri waliaashaachana na huyo mwanaume zaidi ya miezi mitatu, na kila mmoja kuwa na maisha yake, kinachowauma ndugu ni huyo dada alitolewa kijijini walitegemea baada ya kuachwa angeyumba, matokeo yake amezidi kupendeza.

Na akapata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, hao ndugu baaa ya kupajua alipokuwa anaishi wakapanga mpango huo wa kumvamia kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na mume mpya lengo kumzalilisha na kumkomoa tu .

Waliwavua na nguo na kuwapiga wenyewe acha wakenyee ndoo kwanza akili ziwakae sawa
Asante mkuu, hao wafumaniaji akina Buchadi ni Wahaya? naomba tu kujua mkuu maana kuna viashiria.
 
Walifunga ndoa ya kimila, , walishatengana, mwanaume alienda kumnyang'anya mwanamke watoto , wakawa wanaishi kwa dada yake ambaye ni mmoja wa watuhumiwa.
Baada ya hapo mwanaume alitaka mwanamke arudi kijijini alikomtoa ndio chanzo Cha ugomvi na kumtumia msg za vitisho Kama ataendelea kuishi maeneo hayo atamfanyia kitu kibaya.
Mimi nashangaa watu wanaotetea kuwa ni adhabu sahihi kwa kutembea na mke wa mtu. Hivi mimi nikute mwanamme mwingine na mke wangu eti nifanye ujinga wa kupambana naye? Sijui labda katika mazingira adimu sana eg labda mwanaume ni rafiki yangu sana na nimemfumania akiwa nyumbani kwangu. Vinginevyo kama ni mazingira mengine, sijui guest house whatever, nitakachofanya ni kuachana na mke wangu tu basi. Hakuna mwanamme atakayekwenda kumlazimisha mke wa mtu atembee naye kwa nguvu. Kosa ni la mwanamke.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu watu wawili wanaodaiwa kufumaniwa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Singiba Buchadi (42) ambaye ni fundi umeme na mfanyabiashara Dephina Buchadi (42).

Kamanda Muliro amewataja wengine kuwa ni Doratea Mathayo (39), Wilbard Teobard (55), Albert Buchadi (30), Valenzi Silvester (40).

Amesema kuwa watuhumiwa hao wote ni wakazi wa Kongowe Wilaya ya Mkuranga.

“Vitendo vya kikatili walivyovifanya watuhumiwa hawa ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao si mahakimu wala majaji, vitendo hivi havikubaliki kisheria katika nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo,”alisema Muliro.

Hii story hainogi bila picha za utupu za hao waliofumaniwa, kwa kifupi siamini story yako.
 
Hawakuwafumania hao wote waliokamatwa ni mwanaume na ndugu zake ndio walifanya kitendo hicho, huyo dada namfahamu vizuri waliaashaachana na huyo mwanaume zaidi ya miezi mitatu, na kila mmoja kuwa na maisha yake, kinachowauma ndugu ni huyo dada alitolewa kijijini walitegemea baada ya kuachwa angeyumba, matokeo yake amezidi kupendeza.

Na akapata mwanaume mwingine akawa anaishi nae, hao ndugu baaa ya kupajua alipokuwa anaishi wakapanga mpango huo wa kumvamia kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na mume mpya lengo kumzalilisha na kumkomoa tu .

Waliwavua na nguo na kuwapiga wenyewe acha wakenyee ndoo kwanza akili ziwakae sawa
Nilisikiliza maelezo ya yao. Kusema ukweli yule mama hana kosa lolote. Huyo mwanaume ndiye anaonekana alimwacha akidhani anamkomoa kumbe sivyo. Alipogundua ndipo alipopanga kufanya huu unyama. Na kuonyesha kuwa alikuwa na lengo baya ni jinsi walivyowapiga, kuwatembeza nusu uchi, na kuwapiga picha. Wanatakiwa wapewe adhabu kali kabisa kwani walichofanya unyama.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu watu wawili wanaodaiwa kufumaniwa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Singiba Buchadi (42) ambaye ni fundi umeme na mfanyabiashara Dephina Buchadi (42).

Kamanda Muliro amewataja wengine kuwa ni Doratea Mathayo (39), Wilbard Teobard (55), Albert Buchadi (30), Valenzi Silvester (40).

Amesema kuwa watuhumiwa hao wote ni wakazi wa Kongowe Wilaya ya Mkuranga.

“Vitendo vya kikatili walivyovifanya watuhumiwa hawa ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao si mahakimu wala majaji, vitendo hivi havikubaliki kisheria katika nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo,”alisema Muliro.

Nani asubiri jaji
 
Lkn sio poa.
Jamaa wamempiga sana.
Hakukuwa na haja kwa sabb wao wanajua nn wanafanya.
Lkn mwanamke ni mzuri.
 
Wanabody wameacha mada wanalilia video,wakina Abdala kichwa wazi wameshasimama wanangoja waone tukio kwenye video live.
 
Kabisa unamwaacha anaenda zake salama. Wanawake ni wengi kuliko wanaume kwa nini kumgombania huyo mmoja? Hebu ona shida ambayo mwanamke huyo aliyoisababishia hiyo familia. Ndugu watatu wako ndani kisa mwanamke mmoja tu. Angemuacha haya yote yasingaliwakuta.
Yaani kaka yangu anakwenda kufumania, ananialika, na mimi huyo nyagu nyagu patata patata shoto kulia shoto kulia... Hapana kwa kweli. Angekodi tu makomandoo mimi nooooo...
 
Acha wakanyee ndoo familia nzima
kwa ufupi walitembezewa kichapo na kuzungushwa mtaa mzima,ila huyu mwanamke walikwisha achana toka mwezi wa nne kwa mujibu wa millardi ayo tv,ila wamezaa watoto2,si real fumanizi.
 
Hizi story za kufumania zimenipita nasikia sikia tu sielewi kitu....
 
Back
Top Bottom