Mbatia ni silaha ya mwisho ya CCM katika Uchaguzi wa Oktoba 2020

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
4,175
Reaction score
2,294
Uliwahi kujiuliza ni kwanini kila anaehama chama pinzani kwa sasa hivi anajiunga na NCCR- Mageuzi? Hiyo sio bahati mbaya bali ni mbinu mathubuti ya CCM kununua viongozi wa upinzani na na kuwasukumia NCCR- Mageuzi (upinzani).

Malengo makuu ya mbinu hizi ni:
  • Kuhakikisha NCCR- Mageuzi haiungani na vyama pinzani katika uchaguzi 2020
  • Kuhakikisha NCCR- Mageuzi inasaidiwa kila hali kuweka wagombea yale maeneo ambayo CCM ni hoi kwa wapinzani
  • Kuuvunja nguvu upinzani kwa kuvuruga mipango yao ya awali ya kuunganisha wapinzani wote kuitoa CCM
  • Kuwapata viongozi wa upinzani wakihamia NCCR na kueleza kwa wananchi mabaya ya upinzani hasa ACT.
Katika juhudi hizo, CCM wanaonekana kufanikiwa angalau kwa kuwapata viongozi muhimu wa ACT- Wazalendo na CHADEMA kuhamia NCCR. Sijui mafanikio haya yataathiri vipi wapiga kura wa upinzani.

Ikumbukwe kuwa baada ya ACT- Wazalendo kuimarika kwa kusomba wanachama wengi, imekuwa mwiba kwa CCM kama ilivyo CHADEMA. Hivyo CCM imelazimika kuviangukia baadhi ya vyama vya upinzani ili visiungane. Mpaka leo vyama vilivyokubali ombi hilo na kuunda umoja na CCM ni:
  • NCCR- Mageuzi
  • Chama cha Mrema (Katangaza hadharani kutoweka mgombea Urais na kumuunga mkono Magufuli)
  • CUF
  • Chama cha CHEYO
Madhara atayoyapata Mbatia baada ya uchaguzi 2020 ni mabaya sana. Kimsingi chama kitakufa baada ya uchaguzi kwa kupoteza imani kwa wanachama na wapenzi wake.

Huu ni wakati muafaka kwa Mbatia kujiuliza, italipa kweli njia anayoichukua kwa long term? Yupo tayari kukiua chama baada ya uchaguzi?
 
Kwani Mbowe, Seif shariff hamad na Zitto Kabwe ni Wapinzani?

Upinzani unakuwa upinzani ukiwa na watu. Mrema mwaka 1995 alikuwa mpinzani namba 1. Leo kasalimu amri na kukubali kuwa kashughulikiwa na kuuwawa kisiasa. Hivyo si mpinzani tena.

Mbowe, Seif Shariff Hamad na Zitto wana mvuto na wana watu nyuma yao hivyo kukamilisha kigezo cha kuwa wapinzani tupende tusipende.
 
Ondoa shaka Mkuu kwani njia ya mwongo siku zote huwa ni fupi. Mh Mbatia ataambulia aibu. Watz Siyo Wajinga. Ajifunze kwa waliounga mkono juhudi hali yao kisiasa wakoje??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu mwenye kadi No. 1 wa NCCR Mageuzi(hii alisema Mbatia mwenyewe) ni Mabere Marando ambae kila mtu anajua kazi yake aliyokua anafanya huko serikalini,kwa wasiomjua ndiye alifanya kazi iliyotukuka kwa mmoja wa wale vijana waliotaka kumpindua Nyerere(wakina Maganga,Tamimu etc).

Ni mabere huyo huyo akiwa Chadema wkt Lowassa amepokelewa akaahidi kumtangaza Lowassa ni mshindi mapemaaa tu huku akiwaambia wananchi watulie tuli wasiwe na shaka ushindi ni uhakika,lkn kuelekea kupiga Kura akaumwa ghafla huyo mpk leo hajasikika tena.

Makongoro nyerere alishawahi kua Mbunge wa Arusha mjini kupitia NCCR wkt huo dingi ake akiwa hai,labda nae alikua akitekeleza majukumu yake

Mrema akaja kua mwenyekiti wa Chama hicho,huyu nae si haba.

Sasa ni Mbatia.

So NCCR hua imekaa kidizaini flani,ukiiangalia kwa jicho la pili.
 
Shida ya wanasiasa wa bongo njaa nyingi hawajali hata long term effects zitakazotokana na maamuzi yao Leo they are after money only.
 
Hiii nccr iliyopo vunjo pekee yake ndio ifanye upinzani ulio mioyoyoni mwa WaTz usishinde uchaguzi? Polisi pekee ndio silaha ya ccm.
 
Mtu mwenye kadi No. 1 wa NCCR Mageuzi(hii alisema Mbatia mwenyewe) ni Mabere Marando ambae kila mtu anajua kazi yake aliyokua anafanya huko serikalini,kwa wasiomjua ndiye alifanya kazi iliyotukuka kwa mmoja wa wale vijana waliotaka kumpindua Nyerere(wakina Maganga,Tamimu etc).

Ni mabere huyo huyo akiwa Chadema wkt Lowassa amepokelewa akaahidi kumtangaza Lowassa ni mshindi mapemaaa tu huku akiwaambia wananchi watulie tuli wasiwe na shaka ushindi ni uhakika,lkn kuelekea kupiga Kura akaumwa ghafla huyo mpk leo hajasikika tena.

Makongoro nyerere alishawahi kua Mbunge wa Arusha mjini kupitia NCCR wkt huo dingi ake akiwa hai,labda nae alikua akitekeleza majukumu yake

Mrema akaja kua mwenyekiti wa Chama hicho,huyu nae si haba.

Sasa ni Mbatia.

So NCCR hua imekaa kidizaini flani,ukiiangalia kwa jicho la pili.
Hata katika interview na Mwananchi, nilimuona akipanic kwa maswali mengi sana na kila wakati akijihisi kuwa hata waandishi wamemstukia.

Nafikiri huu ni uamuzi anaoujutia sana, lakini amajikuta kama kalazimishwa hivi. Wakati huu kakosea!!!
 
Uliwahi kujiuliza ni kwanini kila anaehama chama pinzani kwa sasa hivi anajiunga na NCCR- Mageuzi? Hiyo sio bahati mbaya bali ni mbinu mathubuti ya CCM kununua viongozi wa upinzani na na kuwasukumia NCCR- Mageuzi (upinzani).

Malengo makuu ya mbinu hizi ni:
  • Kuhakikisha NCCR- Mageuzi haiungani na vyama pinzani katika uchaguzi 2020
  • Kuhakikisha NCCR- Mageuzi inasaidiwa kila hali kuweka wagombea yale maeneo ambayo CCM ni hoi kwa wapinzani
  • Kuuvunja nguvu upinzani kwa kuvuruga mipango yao ya awali ya kuunganisha wapinzani wote kuitoa CCM
  • Kuwapata viongozi wa upinzani wakihamia NCCR na kueleza kwa wananchi mabaya ya upinzani hasa ACT.
Katika juhudi hizo, CCM wanaonekana kufanikiwa angalau kwa kuwapata viongozi muhimu wa ACT- Wazalendo na CHADEMA kuhamia NCCR. Sijui mafanikio haya yataathiri vipi wapiga kura wa upinzani.

Ikumbukwe kuwa baada ya ACT- Wazalendo kuimarika kwa kusomba wanachama wengi, imekuwa mwiba kwa CCM kama ilivyo CHADEMA. Hivyo CCM imelazimika kuviangukia baadhi ya vyama vya upinzani ili visiungane. Mpaka leo vyama vilivyokubali ombi hilo na kuunda umoja na CCM ni:
  • NCCR- Mageuzi
  • Chama cha Mrema (Katangaza hadharani kutoweka mgombea Urais na kumuunga mkono Magufuli)
  • CUF
  • Chama cha CHEYO
Madhara atayoyapata Mbatia baada ya uchaguzi 2020 ni mabaya sana. Kimsingi chama kitakufa baada ya uchaguzi kwa kupoteza imani kwa wanachama na wapenzi wake.

Huu ni wakati muafaka kwa Mbatia kujiuliza, italipa kweli njia anayoichukua kwa long term? Yupo tayari kukiua chama baada ya uchaguzi?
Uzuri nccr na tlp vinafahamika Moshi pekee,hii nayo imeshabuma Kama ile ya kuuwa upinzani kwa kutumia wasiojulikana,polisi, DPP,wakurugenzi, manunuzi na teuzi,msajili.Ccm,cuf,nccr,tlp watachezea kipigo kitakatifu toka kwa ACT na CDM uzuri Zitto na Mbowe ni miamba iliyogomea manunuzi ili kulinda heshima zao.
Njia rahisi na nyepesi ya kuuwa upinzani ni kutatua shida za watz mfano ajira,afya,elimu,njaa,nk sijui kwann awataki kuelewa,hizo zingine wataikausha hazina na awatofaulu.Tuombe tu mabeberu yazidi kukaza nati ya kushinikiza uchaguzi huru.
 
Kwani Mbowe, Seif shariff hamad na Zitto Kabwe ni Wapinzani?
We L7 umerudi au umeruhusika toka carantini maana mlituaga rasmi jf tena kwa herufu kubwa kumbe mpo bado mnatuchungulia karibuni.
 
Mbatia kwa kubali kuwa karantini ya ccm keshajimaliza labda apewe ubunge wa fadhila ya kuteuliwa.
 
Back
Top Bottom