Mbatia ni silaha ya mwisho ya CCM katika Uchaguzi wa Oktoba 2020

Kwa vile CCM ni chama HADAA, hakiwezi kutatua shida za watanzania hata kwa 10%. Si kilimo, si ardhi, si elimu just name it, hawawezi. Wanachokiweza ni propaganda tu!! Mwisho hata uchaguzi wa haki hawawezi kutoa hiyo dukuduku kwa wananchi. Angalia matakwa ya wananchi ya katiba mpya - wameshindwa kutatua tatizo hilo.

Hivyo sahau juu ya CCM ya jana, leo wala kesho kuweza kutatua matatizo ya wananchi, badala yake ni kupambana na viongozi wa upinzani na vitisho kwa wanachama wake.

Vipaumbele vyao ni kupambana na upinzani kuliko kupambana na shida zetu sababu wao wanasaza Kodi zetu, wengine tu au kusafiri tu ni shida.Utafikiri tuliwachagua wakapambane na upinzani.
Kupambana na ufisadi, upigaji,ajira,njaa, kilimo,wameshindwa wamewekeza kupambana na upinzani utadhani na propaganda tu
 
Kipindi kile cha JK chadema walikuwa wanajimwambafy huku wakiidhihaki serikali eti ni dhaifu na kwamba Mkulu alikuwa na chekacheka

Wakiitwa kwenye lile jumba jeupe wanaenda wakitoka full kupotosha..Utawasikia tuna haki ya hiki au kile Mara oh sisi ndo tunafanya siasa kuliko vyama vyote lakini huwasikii wakisema wajibu wao kwa Taifa zaidi ya kusema ..hawa lazima tuwang'oe Mara safari hii patachimbika.......

Leo serikali iko imara inachapa kazi wanalialia tena halafu kila anayehama kutoka kwao eti amenunuliwa ila akihamia kwao kama yule mwenyekiti wa kanda fulani et ni shujaa

Sikilizeni fanyeni tathimini na mbadilike
 
Uliwahi kujiuliza ni kwanini kila anaehama chama pinzani kwa sasa hivi anajiunga na NCCR- Mageuzi? Hiyo sio bahati mbaya bali ni mbinu mathubuti ya CCM kununua viongozi wa upinzani na na kuwasukumia NCCR- Mageuzi (upinzani).

Malengo makuu ya mbinu hizi ni:
  • Kuhakikisha NCCR- Mageuzi haiungani na vyama pinzani katika uchaguzi 2020
  • Kuhakikisha NCCR- Mageuzi inasaidiwa kila hali kuweka wagombea yale maeneo ambayo CCM ni hoi kwa wapinzani
  • Kuuvunja nguvu upinzani kwa kuvuruga mipango yao ya awali ya kuunganisha wapinzani wote kuitoa CCM
  • Kuwapata viongozi wa upinzani wakihamia NCCR na kueleza kwa wananchi mabaya ya upinzani hasa ACT.
Katika juhudi hizo, CCM wanaonekana kufanikiwa angalau kwa kuwapata viongozi muhimu wa ACT- Wazalendo na CHADEMA kuhamia NCCR. Sijui mafanikio haya yataathiri vipi wapiga kura wa upinzani.

Ikumbukwe kuwa baada ya ACT- Wazalendo kuimarika kwa kusomba wanachama wengi, imekuwa mwiba kwa CCM kama ilivyo CHADEMA. Hivyo CCM imelazimika kuviangukia baadhi ya vyama vya upinzani ili visiungane. Mpaka leo vyama vilivyokubali ombi hilo na kuunda umoja na CCM ni:
  • NCCR- Mageuzi
  • Chama cha Mrema (Katangaza hadharani kutoweka mgombea Urais na kumuunga mkono Magufuli)
  • CUF
  • Chama cha CHEYO
Madhara atayoyapata Mbatia baada ya uchaguzi 2020 ni mabaya sana. Kimsingi chama kitakufa baada ya uchaguzi kwa kupoteza imani kwa wanachama na wapenzi wake.

Huu ni wakati muafaka kwa Mbatia kujiuliza, italipa kweli njia anayoichukua kwa long term? Yupo tayari kukiua chama baada ya uchaguzi?

Kwa Mbatia ccm wamekula hasara ya kujitakia.
 
Nadhani Mbatia anataka kustaafu siasa na kiinua mgongo cha uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi kile cha JK chadema walikuwa wanajimwambafy huku wakiidhihaki serikali eti ni dhaifu na kwamba Mkulu alikuwa na chekacheka

Wakiitwa kwenye lile jumba jeupe wanaenda wakitoka full kupotosha..Utawasikia tuna haki ya hiki au kile Mara oh sisi ndo tunafanya siasa kuliko vyama vyote lakini huwasikii wakisema wajibu wao kwa Taifa zaidi ya kusema ..hawa lazima tuwang'oe Mara safari hii patachimbika.......

Leo serikali iko imara inachapa kazi wanalialia tena halafu kila anayehama kutoka kwao eti amenunuliwa ila akihamia kwao kama yule mwenyekiti wa kanda fulani et ni shujaa

Sikilizeni fanyeni tathimini na mbadilike

Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Kwanini unasema hivyo, sijakupata hapo!!!!!

Mbatia hana ushawishi wowote kwa umma, ccm wanadhani au wanatamani Mbatia awe na ushawishi ili wamtumie kupunguza makali ya cdm. Lakini kiukweli Mbatia hana uwezo wowote wa kuwaokoa ccm zaidi ya kuwalia hela zao.
 
Shida ya wanasiasa wa bongo njaa nyingi hawajali hata long term effects zitakazotokana na maamuzi yao Leo they are after money only.
CHADEMA NA ACT kuna wanasiasa kadhaa ambao ni Wanaelewa maana ya upinzani katika maendeleo. Wanaelewa kuwa hakuna Nchi inaweza kuendelea kwa mfumo wa mawazo na hoja za chama kimoja. Dunia nzima hakuna, labda zitumike nguvu kama za China na Urusi. Hawa wanaoamini katika itikadi ya ushindani ndio ambao hawana Bei yoyoye kutoma chama tawala, au chama Nunuliwa kama NCCR, TLP, UDP, na CUF. CHADEMA ina kundi la wanamageuzi ambao ushindani katika siasa na demokrasia siyo tu itikadi bali ni imani. Hawawezi kuuza imani hii, maana pesa haziwezi kuzika Fikra za Mtu. Atateseka sana. Mandela alikuwa na imani. Walijaribu kumnunua, kumwua, wakamfunga; lakini imani yake ilibaki palepale. CHADEMA na ACT inao watu hao. Hata wakikosa Ubunge, watabaki wakipambana kama wanaharakati ili kuleta maendeleo na demokrasia yenye ushindani. Si lazima ndani ya miaka hii mitano. Bali Daima Milele. Tanzania Upinzani Halali Hautakufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia mbatia kahaidiwa kupewa majimbo 20 Na ccm.Haahaa duh.Chadema Na ACT komaeni nyie ndo tunawatambua kama wapinzani wakweli
 
Vipaumbele vyao ni kupambana na upinzani kuliko kupambana na shida zetu sababu wao wanasaza Kodi zetu, wengine tu au kusafiri tu ni shida.Utafikiri tuliwachagua wakapambane na upinzani.
Kupambana na ufisadi, upigaji,ajira,njaa, kilimo,wameshindwa wamewekeza kupambana na upinzani utadhani na propaganda tu

..pia miaka inavyozidi kwenda ccm wanaishiwa vijana wenye akili na mvuto.

..vijana walioko ccm sasa hivi hawana mvuto, na wanaamini ktk kutumia mabavu kuliko ushawishi.

..unyama na uhayawani wanaowafanyia wapinzani muda si mrefu wataanza kufanyiana wenyewe kwa wenyewe ndani ya ccm.
 
Back
Top Bottom