PreGE2025 Mbele ya Dr. Biteko, TEC wasema vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe

PreGE2025 Mbele ya Dr. Biteko, TEC wasema vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,212
Reaction score
4,676
Wakati wa uwekwaji wa Wakfu kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Iringa Askofu Romanus Mihali, Kanisa Katoliki nchini katika salamu zake kwaniaba ya Maaskofu wa Kanisa hilo Makamu wa Rais wa TEC, Eusebius Nzigilwa amesisitiza umuhimu wa kusikilizwa kwa sauti na vilio vya watu wanaotaka mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

“Tunaomba kauli hizi nzuri za kututia moyo za viongozi wetu zionekane kwa vitendo katika hatua zote za uchaguzi, kwani baadhi ya matukio tuliyoyashuhudia kwenye jamii yetu hayaoneshi watendaji au wasimamizi wa sheria wanatekeleza kile kinachoahidiwa na viongozi wetu,” amesema.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Huku waamini wakimsikiliza kwa utulivu, Askofu Nzigilwa amesema: “Kinachoahidiwa hakiendani na kile kinachotendeka. Ndugu mgeni rasmi (Dk Biteko, Naibu Waziri Mkuu) kwa muda mrefu kumekuwa na sauti zinazotaka Katiba na sheria zinazosimamia uchaguzi wetu zifanyiwe marekebisho ama maboresho ili ziendane na hali ya demokrasia ya vyama vingi.”

“Inavyoonekana ni kuwa wanaonufaika na upungufu wa sheria za sasa hawana haraka ya kufanya maboresho hayo, na wale wanaojiona wanaathirika na upungufu huo ndio wanapaza sauti kutaka mabadiliko ya Katiba na sheria.”

“Wito wetu sisi maaskofu kwa mamlaka zinazohusika ni kuwa sauti na vilio vya watu wanaotaka mabadiliko hayo zisikilizwe na zisipuuzwe,” amesema Nzingilwa ambaye ni Askofu wa Jimbo la Mpanda.

Akihitimisha salamu za Maaskofu amesema:“Tunaomba maboresho stahiki kwenye mifumo ya uchaguzi yafanyike ili kuruhusu ufanyike kwa uhuru na wa haki katika nchi yetu, vinginevyo chaguzi zetu zitaendelea kugubikwa na dosari nyingi kama zilivyoshuhudia kwenye chaguzi za hivi karibuni.”

Akigusia suala la uchaguzi kama lilivyozungumzwa na maaskofu, Dk Biteko amesema: “Kama mlivyoahidi na mimi nitakwenda kumwambia Rais ahadi ya kanisa kuendelea kuliombea Taifa ili uchaguzi umalizike kwa amani.”

Dk Biteko amesema: “Ujumbe alioutoa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu, jamani Askofu akisema jambo hajibiwi.” Kauli hiyo iliibua shangwe kisha Dk Biteko akasema: “Hapana ni amina, baba nimepokea. Lakini jambo moja ambalo nina amini ni Rais wetu anatamani Watanzania tuwe kitu kimoja.”

 
“Inavyoonekana ni kuwa wanaonufaika na mapungufu yaliyomo katika sheria za sasa, hawana haraka kufanya maboresho hayo.Wito wetu Maaskofu kwa mamlaka zinazohusika ni kuwa sauti na vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe"

No reforms no election ni lazima....hakuna namna nyingine. ChoiceVariable na wenzako mpo?
 
TEC ndio kina nani? Hakuna kitakachobadilika.

Nchi sio kanisa

Wewe ni mjinga usiyeelewa chochote, jihurumie kwa kukosa uelewa.

Huelewa maana ya Taifa. Taifa ni mkusanyiko wa jamii zote zilizomo ndani ya nchi. Ukiwaondoa wakatoliki wote, waislam wote, waprotestant wote, hakuna taifa. Hivyo kundi lolote, kwa kutegemea uwingi wake, likipaza sauti, hakuna mwenye akili anayeweza kupuuza, kwa sababu ni entity muhimu katika Taifa.
 
Hapa natakiwa kujibu kwa hoja, au nikiandika tu "wadini hao" inatosha?

Cc Mataga
 
Back
Top Bottom