PreGE2025 Mbele ya Dr. Biteko, TEC wasema vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe

PreGE2025 Mbele ya Dr. Biteko, TEC wasema vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
“Inavyoonekana ni kuwa wanaonufaika na mapungufu yaliyomo katika sheria za sasa, hawana haraka kufanya maboresho hayo.Wito wetu Maaskofu kwa mamlaka zinazohusika ni kuwa sauti na vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe"

Biteko nae hana cha kufanya zaidi ya kushauri tu.
Ushauri waweza pokelewa au puuzwa
 
“Inavyoonekana ni kuwa wanaonufaika na mapungufu yaliyomo katika sheria za sasa, hawana haraka kufanya maboresho hayo.Wito wetu Maaskofu kwa mamlaka zinazohusika ni kuwa sauti na vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe"

Wakiwa na Nia ovu hawatabadili Katiba lakini wakiwa na Nia njema na Mama Tanzania watafanya hayo marekebisho
 
Wewe ni mjinga usiyeelewa chochote, jihurumie kwa kukosa uelewa.

Huelewa maana ya Taifa. Taifa ni mkusanyiko wa jamii zote zilizomo ndani ya nchi. Ukiwaondoa wakatoliki wote, waislam wote, waprotestant wote, hakuna taifa. Hivyo kundi lolote, kwa kutegemea uwingi wake, likipaza sauti, hakuna mwenye akili anayeweza kupuuza, kwa sababu ni entity muhimu katika Taifa.
Hakuna Mabadiliko yatakayofanyika ku suit maslahi ya vikundi vichache vya watu kidini na Mabeberu.

Nchi hii sio Mali ya TEC wanaoteea muuminini wao kwenye kesi ya uhaini.
 
“Inavyoonekana ni kuwa wanaonufaika na mapungufu yaliyomo katika sheria za sasa, hawana haraka kufanya maboresho hayo.Wito wetu Maaskofu kwa mamlaka zinazohusika ni kuwa sauti na vilio vya watu wanaotaka kufanyika kwa maboresho ya katiba na sheria visikilizwe na visipuuzwe"

Ni kuwapiga tu za uso mpaka akina Malaria 2 na Bakwata yao, wajilipue kwa mabomu.
 
Wakiitwa ikulu hao maaskofu kesho wataimba ccm mbele kwa mbele
Kumbuka tu Maaskofu wa Katoliki kila siku kwenye milo yao wanakula ubwabwa na nyama! Ni tofauti kabisa na wale Masheikh wako wa Bakwata! Wakipigwa tu mnuso, sifa zote na utukufu ni kwa ccm na Mama.
 
Wakati wa uwekwaji wa Wakfu kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Iringa Askofu Romanus Mihali, Kanisa Katoliki nchini katika salamu zake kwaniaba ya Maaskofu wa Kanisa hilo Makamu wa Rais wa TEC, Eusebius Nzigilwa amesisitiza umuhimu wa kusikilizwa kwa sauti na vilio vya watu wanaotaka mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

“Tunaomba kauli hizi nzuri za kututia moyo za viongozi wetu zionekane kwa vitendo katika hatua zote za uchaguzi, kwani baadhi ya matukio tuliyoyashuhudia kwenye jamii yetu hayaoneshi watendaji au wasimamizi wa sheria wanatekeleza kile kinachoahidiwa na viongozi wetu,” amesema.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Huku waamini wakimsikiliza kwa utulivu, Askofu Nzigilwa amesema: “Kinachoahidiwa hakiendani na kile kinachotendeka. Ndugu mgeni rasmi (Dk Biteko, Naibu Waziri Mkuu) kwa muda mrefu kumekuwa na sauti zinazotaka Katiba na sheria zinazosimamia uchaguzi wetu zifanyiwe marekebisho ama maboresho ili ziendane na hali ya demokrasia ya vyama vingi.”

“Inavyoonekana ni kuwa wanaonufaika na upungufu wa sheria za sasa hawana haraka ya kufanya maboresho hayo, na wale wanaojiona wanaathirika na upungufu huo ndio wanapaza sauti kutaka mabadiliko ya Katiba na sheria.”

“Wito wetu sisi maaskofu kwa mamlaka zinazohusika ni kuwa sauti na vilio vya watu wanaotaka mabadiliko hayo zisikilizwe na zisipuuzwe,” amesema Nzingilwa ambaye ni Askofu wa Jimbo la Mpanda.

Akihitimisha salamu za Maaskofu amesema:“Tunaomba maboresho stahiki kwenye mifumo ya uchaguzi yafanyike ili kuruhusu ufanyike kwa uhuru na wa haki katika nchi yetu, vinginevyo chaguzi zetu zitaendelea kugubikwa na dosari nyingi kama zilivyoshuhudia kwenye chaguzi za hivi karibuni.”

Akigusia suala la uchaguzi kama lilivyozungumzwa na maaskofu, Dk Biteko amesema: “Kama mlivyoahidi na mimi nitakwenda kumwambia Rais ahadi ya kanisa kuendelea kuliombea Taifa ili uchaguzi umalizike kwa amani.”

Dk Biteko amesema: “Ujumbe alioutoa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu, jamani Askofu akisema jambo hajibiwi.” Kauli hiyo iliibua shangwe kisha Dk Biteko akasema: “Hapana ni amina, baba nimepokea. Lakini jambo moja ambalo nina amini ni Rais wetu anatamani Watanzania tuwe kitu kimoja.”

View attachment 3318342
Ccm ni janga la taifa
 
Nchi ni yawanachi, dhamana siyo umiliki. Dhamana inaweza chukuliwa muda wowote na mmiliki na kumkabidhi mwingine Kwa muda atakaye kidhi matakwa ya dhamana hiyo.
Wananchi hawajaamua ila tunasikia vikundi vya kihuni vya TEC na Chadomo
 
Back
Top Bottom