Kibingu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2022
- 1,078
- 1,445
Tudadavulie basi sisi tusiopenda kusumbua vichwa vyetu.Wazazi kuuwa na watoto wao imeshika kasi sana
Tutafakari kwa utulivu tutagundua kuna ujumbe tunatumiwa hapa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tudadavulie basi sisi tusiopenda kusumbua vichwa vyetu.Wazazi kuuwa na watoto wao imeshika kasi sana
Tutafakari kwa utulivu tutagundua kuna ujumbe tunatumiwa hapa
Malezi siku hizi ni balaa kabisa, mabinti wanachinja mama zao, vijana wanachinja baba zao wa kuwazaa kabisa, Kuna kitu hakiko sawa kabisa kwenye jamii. Unawezaje kuchinja mama au baba yako aliyekulea mpaka hapo ulipo.
Wekeza kwa watoto ili wasije wakajikuta wana maisha ya stress wakakuona wewe mzazi ndiye chanzo cha kufeli kwao.inaonekana bond kati ya mzazi na mtoto siku hizi inapungua sana,na sababu ni harakati za maisha,mzazi kukutana na mtoto ni usiku tena story zinazotawala ni za umesoma nini shule,sio story za mtu na rafiki yake.
enzi zetu japo wazazi walikuwa mbogo,ila ilikuwa nadra sana kusikia kitu kama hiki.
Wekeza kwa watoto ili wasije wakajikuta wana maisha ya stress wakakuona wewe mzazi ndiye chanzo cha kufeli kwao.
Ukubwa wa kuishi milimani? Ni sawaJiji la pili kwa ukubwa ni mwanza alafu unajisifu kaskazini mnajua kutafuta hela!!!
Kweli kabisa ccm na uchawi ni pete na kidoleBaba Kama alikuwa mwana ccm kweli alikuwa mchawi Wala hajasingiziwa
Atakuwa ni mchaga huyu akazamia huko mbeya sio bure. Fuatilia chimbuko lake Mana huyu aliyesema kuku.Juzi ilitokea kaskazini ikatafsiriwa kama tabia ya kabila fulani, Leo imetokea kwingine haya mambo hayafai kutafsiriwa kwa picha ya ukabila maana hasira,chuki,tamaa,ugomvi na wivu havina ukabila vinaweza kuwa katika moyo wa yeyote na ikasababisha madhara kama haya ya mauaji.
Kuna chuki gani.kwa iyo hata ukiwa mwizi ukichukiwa ni mafanikio. Mti wenye matunda ndo hupondwa usikariri unaweza kuta una tatizo ama nyoka amekaa juu ya mti.Kanda ya ziwa huko hamna madhara, nyie furaha pekee mliyochagua kuwa nayo duniani ni kusonga ugali mkubwa, mkipata ugali mkubwa tu hayo ni mafanikio makubwa sana kwenu Sasa kwenye vita ya ktafuta mafanikio/mali nani atawazungumzia vibaya?
Kaskazini inatafutwa pesa asee had nchi nzima Hadi mihimili ya nchi inashiriki kuweka chuki, maana ukiona huna adui ujue hauna mafanikio.
Ndio kwanza leo ni siku ya 12 tu.Huu mwaka uishe kwakweli sio kwa matukio haya ya mauwaji kila uchwao
ila yanashamir sana aisee Mungu atusaidieMatukio yapo tu tokea enzi
Alas! Another Mwana Versus Mzazi tragedy. Kuna kitu kilifanyika kwenye malezi ya watoto hapa nchini kuanzia miongo miwili iliyopita ambacho matokeo yake tunayashuhudia kwa sasa. Utafiti wa kina unahitajika.Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea mauaji ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Edward Ndonde anayedaiwa kuuawa kikatili kwa kuchomwa visu na mtoto wake, Mussa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT.
Mussa anadaiwa kufanya mauaji hayo leo Jumatano Januari 12, 2022 nyumbani kwa baba yake mtaa wa Lumbira Kata ya Iwambi jijini Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Christina Musyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa chanzo ni kutuhumiana kwa mambo ya kishirikina.
Amesema mtuhumiwa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT amekamatwa baada ya kufanya mauaji hayo na kwamba uchunguzi unaendelea ili hatua za kisheria ziweze kushika mkondo wake.
"Ni kweli tukio lipo na limetokea leo, ambapo pia marehemu alikuwa mwalimu msitaafu, chanzo kinadaiwa kuwa mambo ya kishirikina, ambapo mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu baba yake kuwa ni mchawi na Jeshi la Polisi limemshikiria kwa uchunguzi zaidi" amesema Christina.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Alhaji Saad Kusilawe amesema marehemu aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa ambapo alikitumikia kwa muda wote kwa uadirifu na kwamba wanasubiri maelekezo kwa ajili ya taratibu za mazishi.
"Tumepoteza hazina ya kiongozi, kwani katika utumishi wake aliweza kumaliza vyema hadi anastaafu, ni pigo kubwa na ni masikitiko makubwa" amesema Kusilawe.
Naye Balozi wa mtaa huo, Hezron Thobias amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alianza kutamka maneno kuwa amemaliza kazi yake aliyoitiwa na baba yake ya kuchinja kuku, jambo lililowashtua na kwenda kuangalia waliposikia kelele zikitoka ndani.
"Alionekana kama ana ugoro na amelewa, akawa anatamka maneno kuwa amemaliza kuchinja kuku, tukamuona mama yake analia anasema njooni muone mtoto alichofanya akiwa anatokwa machozi, ile tunaingia ndani tukakuta amemuua, damu zimemwagika" amesema Thobias.
Mwananchi imefika nyumbani kwa marehemu huyo na kukuta vilio na simanzi vikitawala huku majirani na waombolezaji wakiendelea na taratibu msiba.
Chanzo: Mwananchi, 12 January 2022
haya Mambo Niya wachagaga,mbeya mnatuaibisha jmn ,hata nyny mmeanza hii tabia !!Juzi ilitokea kaskazini ikatafsiriwa kama tabia ya kabila fulani, Leo imetokea kwingine haya mambo hayafai kutafsiriwa kwa picha ya ukabila maana hasira,chuki,tamaa,ugomvi na wivu havina ukabila vinaweza kuwa katika moyo wa yeyote na ikasababisha madhara kama haya ya mauaji.
Imani ya kijinga sana.Ukweli nikwamba uchawi upo na unaoperate katika angle ya juu (spiritual world). How, kitu ambacho hakionekani kwa macho ya nyama kikudrive kutoa nafsi ya mtu mwingine.
Those who do not believe in magic will never find it.