Mbeya CHADEMA waandamana kwenda ofisi ya RPC kumsaka Mdude

03 May 2025
Mbeya, Tanzania

CHADEMA WAANDAMANA MPAKA OFISI ZA RPC MBEYA, KUMTAKA AWAONESHE ALIKO MDUDE


View: https://m.youtube.com/watch?v=KghIYmtSu18
Wananchi washangazwa na majibu ya RCO wasema wananchi wa Mbeya pia viongozi wa CHADEMA, CUF na DEMOKRASIA MAKINI mkoani Mbeya washindwa kumuelewa RCO wa Mbeya..
 
Hata mimba ilianza na manii
 

Kutokana na kushamirii kwa Udhalimu mbaya kabisa wa uvunjifu wa HAKI za binadamu (Grave Human Rights Violations), endapo kwa bahati mbaya yataibuka Makundi kama vile ya Boko Haram au Al Shabaab, basi naamini kwa dhati kabisa kwamba yatapata Uungwaji mkono mkubwa sana katika nchi hii.
Mungu aepushie mbali mabalaa haya yanayolikumba Taifa hili kwa Sasa.
Jeshi la Polisi na TISS wanawachezesha Kamali ya Kifo Wananchi wa Nchi hii. Tuwakatae ili tuepukane na Mabalaa!
 
Baadae tusiambiwe watu wameumizwa, polisi hawana huruma
Lisiwe swala la "polisi hawana huruma",..., ni kama unawahimiza mkuu 'gallow bird'.
Polisi hawafanyi kazi ya huruma; polisi wanafanya kazi kwa sheria zinazowalinda wananchi na kuwaruhusu wao polisi kufanya kazi yao.
Sijui kwa nini leo nahangaika sana na wewe hivi, maanake sikumbuki hata siku moja kusoma michango yako humu.
Hata hivyo, ninayo matumaini makubwa juu yako mkuu 'gallow bird', kwamba hatimae sisi sote (wewe na mimi) tutakuwa pamoja kuilinda nchi yetu Tanzania tunayo ipenda sana juu ya jambo lingine lolote.
 
Kubeza dhana hii ni sawa na kuficha kichwa ndani ya mchanga kwa kudhani kiwiliwili chote hakiwezi kuonekana.
Tupo kwenye 'link' dhaifu sana kwenye mshikamano wetu kama taifa.
Mshikamano hauwezi kuimarishwa kwa nguvu za kipolisi.
 
Huwezi andamana ghafla tu kwenda kituo cha polisi,huo ni uvamizi
 
Uhuru wa nchi hii utaaanzia mbeya na mwanza.....hawa watu DAR kazi Yao kubwa ni uchawa Tu na mdomo mwingi
Mbeya wana msimamo sana, wazee wa huko walishakuwa tayari kujitenga baada ya Mwakyembe na Mwandosya kutendewa isivyo kipindi cha JK
 
Sijamuonaaa mtu frani hivi kwenye maandamo hapo! Anyway tujitahid kutumia maombi zaidi
Nilitaka kuuliza swali hili kwa rafiki yangu 'Erythro', lakini nikaogopa nisiharibu siku yake nzuri, kama tulivyoona alama nzuri ya hapo Mbeya. Hii ni zawadi nzuri ya kuanzia.
 
Baadae tusiambiwe watu wameumizwa, polisi hawana huruma
Mimi natamani RPC awaruhusu. Wakifika awaulize mnadhani mdude yumo humu ndani?
Wente mashaka wajiorodheshe nitawaruhu waingie ndani wamtafute kila Kona ya jengo.
Mkimpata ondokeni nae mkimkosa kila alieorodhesha jina lake kwaleo makaazi yake yatakua selo.
Mbaweza masharti anzeni kunisajili, asieweza masharti natoa 5 minutes awe ameshao doka eneo hili.
 
Huwezi andamana ghafla tu kwenda kituo cha polisi,huo ni uvamizi
Bado sijakuelewa una maana ipi. Kwani kupotea kwa Mdude ilikuwa ni ghafla; au unatafuta sababu ya hao watu sasa washambuliwe na polisi? Mbona hatujaona kuwepo kwa vurugu yoyote? Polisi sheria inawaambia ukiona tu watu wanakuja kwako, washambulie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…