Mbeya: Deogratius Ndejembi hamuwezi Mkandarasi CHICO. Hata Magufuli alimshindwa. Injinia Bishanga anaonewa bure

Mbeya: Deogratius Ndejembi hamuwezi Mkandarasi CHICO. Hata Magufuli alimshindwa. Injinia Bishanga anaonewa bure

Acha kumfananisha Magufuli na viongoxi wengine. Chico asingepewa tenda kipindi cha Magufuli akiwa Rais wa nchi.
Nawapenda watu kama nyie mnaokurupuka kukomenti bila kusoma. Sababu inakua rahisi kuwaumbua. Na mkiumbuka thread mnaipita kama hamuioni.

Nakuwekea hapa ushahidi. Naamini utaacha kuwa unatetea ujinga

 
Wakuu Salaam,


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Deogratius Ndejembi, amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa dhidi ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, sababu ikiwa ni kuchelewa kwa ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Nsalaga (Uyole) hadi Ifisi jijini Mbeya yenye urefu wa kilomita 29 kwa Bilioni 184. Amelipwa hela zote na akakopeshwa bilioni 20 lakini hayupo site.

Mimi nahisi Ndejembi anaingia kwenye vita ambayo haiwezi matokeo yake anaishia kuumiza Dagaa(Mameneja wa Mikoa) ya Songwe na Mbeya.

Kwanini nasema hana uwezo wa kugusa hii Kampuni?
View attachment 3692885
Kwa utaratibu wa kiongozi bora, Makamu wa Rais anatakiwa amhoji Waziri, Waziri amhoji Mkurugenzi wa TANROADS, Mkurugenzi amhoji Meneja kuhusu barabara kuchelewa.

Hapa chini nitaelezea kwa urefu kwanini huyu Makamu wa Rais Mgeni Ofisini asipokuwa makini atajikuta anaumiza watu wasio husika.

Hii barabara ya njia nne ya Nsalaga (Uyole) hadi Ifisi, Mbeya inajengwa na China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO)

Mkataba wa ujenzi wa hizi kilomita 29 ulisainiwa tarehe 14 Februari 2023 na ilitakiwa kukamilika tarehe 13 Machi 2025. Kumbuka Mkandarasi kashalipwa gharama zote za mradi Bilioni 184, hadai kitu.. Na kutomaliza kazi kwa wakati hakuna hatua zilichukuliwa.

Hadi kupindi cha Mkataba kuisha 13 Machi 2025, alikuwa kajenga 24% tu ya Mradi.

Kutokana kusuasua kwa ujenzi wa Barabara hii, TANROADS ilimuondoa aliyekuwa Meneja wa TANROADS Mbeya na Machi 2026 wakamleta Mkandisi Suleiman Bishanga aliyekuwa akisimamia Mradi ya Barabara Mkoani Songwe iliwemo barabara ya TAZAM (Tanzania Zambia, Malawi) njia sita. Uchapakazi wa Bishanga ndo ulisababisha aletwe Mbeya kusimamia hii barabara iishe.

Mhandisi Suleiman Bishanga aliweza kumsimamia Mkandarasi kwa miezi sita akajenga 20% ya barabara ambayo hivi sasa ipo 46% ya Ujenzi.


Cha kushangaza tarehe 17 Oktoba 2026 Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Deogratius Ndejembi akamuagiza Waziri wa Ujenzi Kadogosa amchukulie hatua Meneja wa TANROADS Mhandisi Bishanga ambaye kasimamia huo mradi kwa miezi 7 tu kati ya miezi 39 ya ujenzi wa hii Barabara.

MASWALI KWA MAKAMU WA RAIS DK. NDEJEMBI

1. Kwanini hajamchukulia hatua yoyote Mkandarasi ambaye alitakiwa akabidhi mradi mwezi Machi 2025 hadi leo Oktoba 2026 bado mradi upo 45% tu?

2. Kwaninii Ndejembi hajamchukulia hatua Mkandarasi ambaye kalipwa hela zote na akashindwa kukabidhi mradi? Pia mkandarasi hata alipo ambiwa Makamu anaenda site, wala hakufika eneo la tukio

3. Kwanini Ndejembi hajamchukulia hatua Mkurugenzi wa TANROADS anayesimamia barabara zote Nchini akakimbilia kwa Meneja wa Mkoa amabye kituo chake cha Kazi ni Songwe na Mbeya kaletwa kusimamia huu mradi?

4. Kwanini Ndejembi hajahoji sababu za Waziri kufanya Kikao Usiku na Meneja akampa majukumu ya kumobilise Wakandarasi wawe Site katika maeneo 32 korofi kisa Makamu anakuja asikose sehemu ya kupita. Angekuwa yeye angeweza kuuwa kila sehemu? Na Wakandarasi waliahidi watakuwa Site, Asubuhi kaamkia kumpokea Makamu, kwenye msafara anaulizwa kama mkandarasi yupo Site akajibu ndio. Kwani walisema watakuwa site Mbele ya Waziri. Kumbe hawajaenda. Kwanini Mkandarasi hajagombezwa?
View attachment 3692898
JE MAKAMU WA RAIS DR. DEOGRATIAS NDEJEMBI ANAWEZA KUMFOKEA MKANDARASI CHICO?

Jibu ni hapana.

Hii Kampuni Mawaziri Kibao ni Viongozi Mbalimbali akiwemo Hayati Pombe Magufuli, walishashindwa kuiadhibu wala kuichukulia hatua. Hadi Baadhi ya Viongozi wakampiga marufuku CHICCO kufanya kazi Tanzania lakini bado inapewa Kandarasi na kulipwa fedha zote kila mradi. Hapa chini nitaweka miradi kadhaa.

Je, nani yupo Nyuma ya hii Kampuni ya Kichina?

TUJIKUMBUSHE MAWAZIRI WALIOWAHI KUKUTANANA MFUPA WA CHICO


1. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 9 Oktoba 2012, wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikagua barabara ya Sekenke–Shelui, mkoani Singida, iliyokuwa imejengwa upya na CHICO.
Alisema Serikali ilikuwa imetumia zaidi ya shilingi bilioni 35, lakini barabara hiyo ilikuwa imejengwa chini ya kiwango kiasi kwamba ng'ombe akkikannyaga lami inabonyea. Hata hivyo alilipwa hela ypte.


2. Abdallah Ulega akiwa Waziri wa Ujenzi Tarehe: 22 Aprili 2025. Alikosoa kasi ya ujenzi wa Nsalaga–Ifisi, Mbeya, na kumpa CHICO siku 30 kuongeza kasi ya kazi. Lakini hadi leo 17 Oktoba 2026 bado ipo 45%

3. Innocent Bashungwa akiwa Waziri wa Ujenzi Tarehe 22 Machi 2024 alikosoa ubora wa barabara ya Kilindoni–Utende, Mafia, iliyojengwa na CHICO, na kuagiza mkandarasi arudie sehemu yenye mapungufu kwa gharama zake. Hakurudia na hajafanywa chochote

4. Seleman Kakoso akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu
Tarehe: 12 Machi 2024 aliitaka Wizara ya Ujenzi kuhakikisha CHICO inakamilisha barabara za Noranga–Itigi na Doroto–Noranga kwa wakati kulingana na mkataba lakini hakufanya hivyo.

5. Godfrey Kasekenya akiwa Naibu Waziri wa ujenzi, Tarehe Desemba 2021 lionyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Tanga–Pangani iliyokuwa ikijengwa na CHICO, na kueleza wasiwasi kuhusu ubora wa baadhi ya barabara nyingine zilizojengwa na kampuni hiyo. Hata hivyo alikuwa kashalipwa hela zote.

Alionya kwamba wakandarasi wa kimataifa wanaofanya vibaya wanaweza kukosa kazi sehemu nyingine ikiwemo CHIKO. Hata hivyo, taarifa hiyo haithibitishi kuwa CHICO iliwekewa marufuku rasmi.

Mjadala upo wazi. Ni kipi kinafanya Viongozi wa CCM waiogope hii Kampuni ya China?
View attachment 3692863View attachment 3692864
Kumbukizi 3012: Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu.
OMG, siasa inaweza kumpandisha mtu na kumshusha mtu. Yani huyu Tulia, Dr. Former speaker, aliekuwa analindwa ndo huyu yupo huku mavumbini juani anadai barabara za tarura?
 
Acha kumfananisha Magufuli na viongoxi wengine. Chico asingepewa tenda kipindi cha Magufuli akiwa Rais wa nchi.
Ujenzi rasmi wa barabara ya Tanga – Pangani (km 50) ulianza mnamo Desemba 7, 2022, baada ya mkataba wake kusainiwa mapema tarehe Agosti 31, 2019. [1, 2]
Mambo muhimu kuhusu mradi huu:
  • Urefu: Sehemu ya kwanza ya barabara ya Tanga hadi Pangani ina urefu wa kilometa 50.
  • Mkandarasi: Unatekelezwa na kampuni ya CHICO kutoka China.
  • Daraja la Pangani: Mradi huu pia unahusisha ujenzi wa Daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara unganishi, ambazo ujenzi wake ulianza rasmi tarehe hiyo ya Desemba 7, 2022. [1, 2, 3]
"Godfrey Kasekenya akiwa Naibu Waziri wa ujenzi, Tarehe Desemba 2021 lionyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Tanga–Pangani iliyokuwa ikijengwa na CHICO, na kueleza wasiwasi kuhusu ubora wa baadhi ya barabara nyingine zilizojengwa na kampuni hiyo. Hata hivyo alikuwa kashalipwa hela zote."

Tuwe na kumbukumbu tunavyo msifia Magufuli,mwaka 2019 alikuwa ofisini akiwa na miaka minne tu ya utawala wake,alimpa mkataba wa kilomita 50 CHICO.
 
Chicco alpewa barabara ya mtwara kwenda tandahimba magufuli akiwa raisi
Hahahaaa... Umenikumbusha mbali. Halafu Magufuli akawa anasema tunajenga hii barabara kwa fedha za ndani. Kwamba tumewabana mafisadi kwani walituchelewesha, eti ndugu zangu kupanga ninkuchagua🤣 . Kumbe hela kakopa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kujenga kilometa 160.

Hadi leo barabara ya Mnivata–Mitesa, Mitesa–Masasi na na Daraja la Mwiti TANROADS bado wanapambana na CHICO awakabidhi mradi.. Msimamizi yupo zake China anakagua miradi kwa Video Call🤣🤣🤣
 
Kesi ya Meneja wa mkoa ni kumdanganya mkuu wake kuwa kuna njia zimefunguliwa wakati sivyo.
Nani azifungue? Kazi kapewa usiku. Na sio njia moja tu. Alipewa maeneo 32 usiku ahakikishe yanapitika.. Yaani wamwage udongo kufukia mashimo. Asubuhi kaamkia kumpokea Makamu wa Rais, wanazunguka sehemu za mradi Mingine Mkoani. Mategemeo yake ni Mkandarasi atakuwa amefanyia kazi tangu asubuhi sababu ndivyo alimuahidi Waziri. Na yeye alijua mkandarasi kaenda hadi alipoambiwa na msaidizi kwamba hajakanyaga site. Ndo maana akaongea ukweli hapajatengenezwa. Yeye alijua pametengenezwa.

Watu wadhani hizo sehemu 32 za kufanyia kazi kapewa siku nyingi. Hapana, kapewa jana usiku leo Makamu anakuja na yeye anatakiwa awe kwenye msafara. Kwa matumaini Wakandarasi watakuwa site kwani ni kazi ndogo ya kufungua njia tu. Angejigawaje sehemu 32?
 
Kwanza na wewe umedanganya hakuna mahala kwenye ripoti za Serikali ambako mkandarasi kaliowpesa zote ,hayo ni Yako hela alizolioqa ni Bilioni 40 tuu kati ya 188 za mradi.

Shida hapa ni Serikali haitoi pesa Kwa wakati Wala sio swala la mkandarasi au meneja.

Leo hii Barabara za Afcon Arusha na Dar zinaisha Kwa sababu pesa inatoka,waache upuuzi

Huwa unapofanya uchawa wako kusema Samuya amemwaga mipesa kujenga miradi mara Samuya katoa pesa kufanya nini huwa ndio akili hizi unatumia kuandika kama hapa?
 
Back
Top Bottom