Mbeya: Deogratius Ndejembi hamuwezi Mkandarasi CHICO. Hata Magufuli alimshindwa. Injinia Bishanga anaonewa bure

Mbeya: Deogratius Ndejembi hamuwezi Mkandarasi CHICO. Hata Magufuli alimshindwa. Injinia Bishanga anaonewa bure

Naona Mh kaona aje ajitetee kinamna lakini ukweli uko wazi kama ambavo tukifanya mazuri tunapenda tunavosifiwa, tukikosea pia tukubali kukosolewa.
Sio mimi nilikufanya usiende shule. Hivyo punguza wivu.. Kwamba maovu yatendeke watu wasiseme? Kama imekuuma chomoa

Umejaa roho mbaya.. Roho ya kufurahi kuona mtu akiteseka, roho mbaya ya kufurahia anguko labinadamu. Unatamani awe masikini kama wewe. Utaishi kuuza ukwaju.. Acha watu walosoma wafanye kazi.. Elimu yake ndo umemfikisha hapo. Unamtaka utamtaka na humtaki utamtaka na roho iitazidi kukuuma kwani utazidi kumuona kwenye miradi ya Serikali akichapa kazi. Dua lako la kuku.
 
Naelewa kipindi unachopitia ni hali ya kawaida kwa binadamu kupitia milima na mabonde pole Mh.
 
Sio mimi nilikufanya usiende shule. Hivyo punguza wivu.. Kwamba maovu yatendeke watu wasiseme? Kama imekuuma chomoa

Umejaa roho mbaya.. Roho ya kufurahi kuona mtu akiteseka, roho mbaya ya kufurahia anguko labinadamu. Unatamani awe masikini kama wewe. Utaishi kuuza ukwaju.. Acha watu walosoma wafanye kazi.. Elimu yake ndo umemfikisha hapo. Unamtaka utamtaka na humtaki utamtaka na roho iitazidi kukuuma kwani utazidi kumuona kwenye miradi ya Serikali akichapa kazi. Dua lako la kuku.
Usi mind mkuu.
Kila mtu anaelewa Makamu wa Rais kalishwa matango pori.

Haiwezekani miaka mitatu ipite baada ya mradi kuanza, leo tunaongelea kazi ya Advance Payment imefanya kazi gani.
Na je mkanfdarasi haja raise malipo ya Certificate kwa kazi ambazo amefanya?
Hili hatuelezwi.

Mbaya zaid tunaelezwa kuwa mkandarasi kimkataba ana Credit facility ya kupata 20biillion.
Mkandarasi hawezi kuomba Credit Facility kutoka mabenki(mkopo), kwa kazi ambayo anajua hawezi kulipwa kwa wakati.
Hilo ni kumzamisha mkandarasi na kutaka auziwe dhamana zake huku serikali haimlipi mkandarasi kwa wakati.

Serikali ijioshe tu hadharani na kukubali kuwa HAINA FRDHA za kumlipa mkandarasi.
 
Wakuu Salaam,

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Deogratius Ndejembi, amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa dhidi ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, sababu ikiwa ni kuchelewa kwa ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Nsalaga (Uyole) hadi Ifisi jijini Mbeya yenye urefu wa kilomita 29 kwa Bilioni 184. Amelipwa hela zote na akakopeshwa bilioni 20 lakini hayupo site.

Mimi nahisi Ndejembi anaingia kwenye vita ambayo haiwezi matokeo yake anaishia kuumiza Dagaa(Mameneja wa Mikoa) ya Songwe na Mbeya.

Kwanini nasema hana uwezo wa kugusa hii Kampuni?
View attachment 3692885
Kwa utaratibu wa kiongozi bora, Makamu wa Rais anatakiwa amhoji Waziri, Waziri amhoji Mkurugenzi wa TANROADS, Mkurugenzi amhoji Meneja kuhusu barabara kuchelewa.

Hapa chini nitaelezea kwa urefu kwanini huyu Makamu wa Rais Mgeni Ofisini asipokuwa makini atajikuta anaumiza watu wasio husika.

Hii barabara ya njia nne ya Nsalaga (Uyole) hadi Ifisi, Mbeya inajengwa na China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO)

Mkataba wa ujenzi wa hizi kilomita 29 ulisainiwa tarehe 14 Februari 2023 na ilitakiwa kukamilika tarehe 13 Machi 2025. Kumbuka Mkandarasi kashalipwa gharama zote za mradi za eneo hilo, hadai kitu bali Serikali ndo inamdai. Kwanza alitakiwa aje na mtaji wake.

Na kutomaliza kazi kwa wakati hakuna hatua zilichukuliwa.

Hadi kipindi cha Mkataba kuisha 13 Machi 2025, alikuwa kajenga 24% tu ya Mradi wakati alitakiwa kukabidhi Mradi.🤣🤣

Kutokana kusuasua kwa ujenzi wa Barabara hii, TANROADS ilimuondoa aliyekuwa Meneja wa TANROADS Mbeya na Machi 2026 wakamleta Mkandisi Suleiman Bishangabashaija aliyekuwa akisimamia Mradi ya Barabara Mkoani Songwe iliwemo barabara ya TAZAM (Tanzania Zambia, Malawi) njia sita. Uchapakazi na kufanya kazi kwa kujituma usiku na mchana ndo kulisababisha Bishangabashaija aletwe Mbeya kusimamia hii barabara iishe(Kuokoa jahazi). Leo anaambiwa kala hela za Mkandarasi ndo maana barabara haiishi🤣🤣

Mhandisi Suleiman Bishanga aliweza kumsimamia Mkandarasi kwa miezi sita akajenga 20% ya barabara ambayo hivi sasa ipo 46% ya Ujenzi.

Cha kushangaza tarehe 17 Oktoba 2026 Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Deogratius Ndejembi akamuagiza Waziri wa Ujenzi Kadogosa amchukulie hatua Meneja wa TANROADS Mhandisi Bishanga ambaye kasimamia huo mradi kwa miezi 7 tu kati ya miezi 39 ya ujenzi wa hii Barabara.

MASWALI KWA MAKAMU WA RAIS DK. NDEJEMBI

1. Kwanini hajamchukulia hatua yoyote Mkandarasi ambaye alitakiwa akabidhi mradi mwezi Machi 2025 hadi leo Oktoba 2026 bado mradi upo 45% tu?

2. Kwaninii Ndejembi hajamchukulia hatua Mkandarasi ambaye kalipwa hela zote na akashindwa kukabidhi mradi? Pia mkandarasi hata alipo ambiwa Makamu anaenda site, wala hakufika eneo la tukio na hajsonesha kuguswa?

3. Kwanini Ndejembi hajamchukulia hatua Mkurugenzi wa TANROADS anayesimamia barabara zote Nchini akakimbilia kwa Meneja wa Mkoa ambaye kituo chake cha Kazi ni Songwe na Mbeya kaletwa kusimamia huu mradi?

4. Kwanini Ndejembi hajahoji sababu za Waziri kufanya Kikao Usiku na Meneja akapewa majukumu ya kumobilise Wakandarasi wawe Site katika maeneo 32 korofi kisa Makamu anakuja asikose sehemu ya kupita. Angekuwa yeye angeweza kuwa kila sehemu?

Na Wakandarasi waliahidi watakuwa Site, Asubuhi kaamkia kumpokea Makamu, kwenye msafara anaulizwa kama mkandarasi yupo Site akajibu ndio. Kwani walisema watakuwa site Mbele ya Waziri. Kumbe hawajaenda. Kwanini Mkandarasi hajagombezwa?

View attachment 3692901
JE MAKAMU WA RAIS DR. DEOGRATIAS NDEJEMBI ANAWEZA KUMFOKEA MKANDARASI CHICO?

Jibu ni hapana.

Hii Kampuni Mawaziri Kibao na Viongozi Mbalimbali akiwemo Hayati Pombe Magufuli, walishashindwa kuiadhibu wala kuichukulia hatua. Hadi Baadhi ya Viongozi wakampiga marufuku CHICO kufanya kazi Tanzania lakini bado inapewa Kandarasi na kulipwa fedha zote kila mradi. Hapa chini nitaweka miradi kadhaa.

Je, nani yupo Nyuma ya hii Kampuni ya Kichina?

TUJIKUMBUSHE MAWAZIRI WALIOWAHI KUKUTANANA MFUPA WA CHICO

1. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 9 Oktoba 2012, wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikagua barabara ya Sekenke–Shelui, mkoani Singida, iliyokuwa imejengwa upya na CHICO.
Alisema Serikali ilikuwa imetumia zaidi ya shilingi bilioni 35, lakini barabara hiyo ilikuwa imejengwa chini ya kiwango kiasi kwamba ng'ombe akkikannyaga lami inabonyea. Hata hivyo alilipwa hela ypte.

2. Abdallah Ulega akiwa Waziri wa Ujenzi Tarehe: 22 Aprili 2025. Alikosoa kasi ya ujenzi wa Nsalaga–Ifisi, Mbeya, na kumpa CHICO siku 30 kuongeza kasi ya kazi. Lakini hadi leo 17 Oktoba 2026 bado ipo 45%

3. Innocent Bashungwa akiwa Waziri wa Ujenzi Tarehe 22 Machi 2024 alikosoa ubora wa barabara ya Kilindoni–Utende, Mafia, iliyojengwa na CHICO, na kuagiza mkandarasi arudie sehemu yenye mapungufu kwa gharama zake. Hakurudia na hajafanywa chochote

4. Seleman Kakoso akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu
Tarehe: 12 Machi 2024 aliitaka Wizara ya Ujenzi kuhakikisha CHICO inakamilisha barabara za Noranga–Itigi na Doroto–Noranga kwa wakati kulingana na mkataba lakini hakufanya hivyo.

5. Godfrey Kasekenya akiwa Naibu Waziri wa ujenzi, Tarehe Desemba 2021 lionyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Tanga–Pangani iliyokuwa ikijengwa na CHICO, na kueleza wasiwasi kuhusu ubora wa baadhi ya barabara nyingine zilizojengwa na kampuni hiyo. Hata hivyo alikuwa kashalipwa hela zote.

OFF TOPIC: Hii siku nilikuwepo sababu nilijiunga kwenye msafara, nilikuwa nafuatilia Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tanga na Ujenzi wa Gati ya Bandari ya Tanga. Nilienda kufuatilia kuhusu Malalamiko ya Wananchi kuhusu kulipwa fidia watu wasio na Viwanja. Baada ya kutoka hapo ndo tukapita ile barabara ya kwenda kwa Aweso kutokeezea Saadani. Pia Hii barabara ilitakiwa itokezee saadani bagamoyo ila wanadai wanataka itokee Mkata. Kuna Mvutano wa Watawala)

Nikipata nafasi nitaandika kuhusu upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tanga na Hujuma ya Reli Tanga kwenda Kilimanjaro.

Alionya kwamba wakandarasi wa kimataifa wanaofanya vibaya wanaweza kukosa kazi sehemu nyingine ikiwemo CHIKO. Hata hivyo, taarifa hiyo haithibitishi kuwa CHICO iliwekewa marufuku rasmi.

Mjadala upo wazi. Ni kipi kinafanya Viongozi wa CCM waiogope hii Kampuni ya China?
View attachment 3692863View attachment 3692864
Kumbukizi 2012: Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu.
View attachment 3692933
Suleiman Bishanga ni Mhandisi wa barabara na ujenzi (Civil Engineering) ambaye kaajiriwa na TANROADS.

Rekodi ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) inaonesha Suleiman Bishanga ni Civil Engineer, mwenye Leseni namba ya usajili 3525.

Kabla ya kupelekwa Mbeya 2026, alikuwa anakaimu kama Meneja wa TANROADS Mkoa wa Songwe mwaka 2024 na Mwaka 2025 akapandishwa kuwa Meneja Mkoa wa Songwe wa TANROADS
Umeandika andiko refu lakini limejaa UPOTOSHAJI ULIOTUKUKA.....Iko hivi:
Hakuna sehemu serikali ya Tanzania inaweza kumlipa Mkandarasi kwa kazi ambayo hajafanya eti Mlandarasi abaki anadaiwa kazi........ukitoa Advance Payment ambayo ina masharti yake na taratibu zake kimkataba
Huu mradi ulishasemwa tatizo ni malipo ndo mana umekua ukienda kwa kusua sua na sio kwamba Mkandarasi ana ujeuri....
Kimkataba hata rais hatakiwi kutoa maagizo yoyote kwa Mkandarasi mana kwenye kila jambo linapaswa kushughulikiwa kimkataba na sio kwa kauli za wanasiasa...na ikitokea Mkandarasi akachukuliwa hatua kwa influence ya kisasa basi akienda kwenye Arbtration serikali inaangukia pua na kuishia kumlipa pesa nyingi hata zaidi ya Contract Sum
Serikali inaposhindwa kumlipa Mkandarasi malipo yake kwa wakati uliowekwa kimkataba, huyo Mkandarasi anapaswa kupongezwa...na sio kuwa harrassed na wanasiasa...mana Mkandarasi hana jukumu kimkataba la kutafuta fedha kwenye mradi...
Ukimkuta mkandarasi smart kama huyo huwezi kumpelekesha kijinga kama ambavyo wakandarasi wazawa wanapelekeshwa kisa hawana pa kukimbilia.....
Kwa hiyo sio kwamba Mkandarasi ni mjeuri bali ni mtu anayezijua haki zake vizuri na anajua kuzisimamia vizuri....kwenye miradi kuna maujinga mengi sana yanafanywa na Government officials kwa ujinga au maslahi yao binafsi...
 
Kwanza na wewe umedanganya hakuna mahala kwenye ripoti za Serikali ambako mkandarasi kaliowpesa zote ,hayo ni Yako hela alizolioqa ni Bilioni 40 tuu kati ya 188 za mradi.

Shida hapa ni Serikali haitoi pesa Kwa wakati Wala sio swala la mkandarasi au meneja.

Leo hii Barabara za Afcon Arusha na Dar zinaisha Kwa sababu pesa inatoka,waache upuuzi
True.....
 
Usi mind mkuu.
Kila mtu anaelewa Makamu wa Rais kalishwa matango pori.

Haiwezekani miaka mitatu ipite baada ya mradi kuanza, leo tunaongelea kazi ya Advance Payment imefanya kazi gani.
Na je mkanfdarasi haja raise malipo ya Certificate kwa kazi ambazo amefanya?
Hili hatuelezwi.

Mbaya zaid tunaelezwa kuwa mkandarasi kimkataba ana Credit facility ya kupata 20biillion.
Mkandarasi hawezi kuomba Credit Facility kutoka mabenki(mkopo), kwa kazi ambayo anajua hawezi kulipwa kwa wakati.
Hilo ni kumzamisha mkandarasi na kutaka auziwe dhamana zake huku serikali haimlipi mkandarasi kwa wakati.

Serikali ijioshe tu hadharani na kukubali kuwa HAINA FRDHA za kumlipa mkandarasi.
NIliposikia hiyo credit facility inahesabiwa kama pesa aliyonayo Mkandarasi hapo ndo nikajua kiongozi kalishwa bonge la tango pori naye kashindwa hata kutafakali karopoka tu.....Responsibility ya Employer ni kulipa kazi zilizofanywa na Mkandarasi. .....umeshindwa kumlipa afu unamwambia akakope Bank kwa niaba yako...kama ni rahisi si serikali ikakope yenyewe iweke dhamana zake
 
Ni ukweli usiopingika, mkandarasi hawezi kukopa, huku akijua huwezi kumlipa ili akajikwamue na huo mkopo.
Credit facility si mali ya serikali.
Kiukweli, serikali imeonyesha kuwa haina fedha za kumlipa mkandarasi, na pili, haijaonyesha mkandarasi anadai certificates ngapi.
Makamu wa Rais kayameza matango pori mazima mazima.
 
Mbona kuna miradi mingi kwa sasa imesimama kulikoni?
Mbona kuna miradi mingi kwa sasa imesimama kulikoni?
TANROADS HAINA FEDHA ZA MIRADI, hilo siyo siri.
FEDHA zilikuwa zinatoka ROAD FUND, serikali ya Awamu ya sita ikachota fedha hizo kupeleka miradi ya Pwagu na Pwaguzi AFCON, bila ridhaa ya Bunge.
Hapa aliyeruhusu hili kufanyika(Waziri wa Fedha wakati huo) Mwigulu Nchemba inabidi ashitakiwe.
 
Halafu Hasira wanataka wazimalizie kwa Bishangabashaija😂😂😂
 
Back
Top Bottom