Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Kuna yule popoma sugu aliyeishia la saba ni kufanya uhuni tu

Huyu tulia naye nilimwona mtu wa maana naye ameungana na mafisadi ya kiarabu kuuza nchi

Watu wa mbeya waache kuchagua clowns , sugu is a typical clown [emoji1782],
huyu spika ni chawa wa namba moja. Huwezi kuwa na mwakilishi chawa ukategemea maajabu. Mambo ya mbeya ni ya hovyo mno ,
Kuna shida nyingi sana . Kuna barabara inabidi msubiliane yapite malori then zipite gari zenu ndogo ,
Juzi kati nlikuwa tunduma tulikaa mbalizi karibu lisaa tukisubiri malori yamalizike kisha twende sisi,
Ajabu hizi shida na kero zote mwakilishi chawa wala hana habari na hajui, kazi yake ni kuhamasisha na ku support mikataba ya hovyo.
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city , hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.

View attachment 2656210

Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)

View attachment 2656212

Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

View attachment 2656217
Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

View attachment 2656219
Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

View attachment 2656211
View attachment 2656213
View attachment 2656214
View attachment 2656215
View attachment 2656218
Umepiga kwenye mshono[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Fremu kujengwa Zina shida gani? Kwamba Leo hii NHC inavunja makazi yake ya zamani huko Dar ,kwani pindi ikojitajika kujenga vinginevyo hizo fremu zitashindwa kuvunjwa?

CBD Wala Haina Uhitaji kama ilivyo Eneo la Kando ya Barabara Kuu ndio maana unaona Kuna shift ya majengo ya biashara.
Ni ujinfa, frame za nini?
 
Tuanze kwanza we ni kwenu wapi bukoba maeneo gani? Afu why mbeya ilihari kwenu ni masikin huko kagera?
 
Usipangie watu Maisha,wewe ongea unayotamani yawe vinginevyo pita kushoto..

Mbeya ya Leo is way better than it used to be in 2010 wakati ikitangazwa kuwa Jiji..

Njoo 2025 pia kuandika utopolo wako maana by that time Barabara Kuu njia 4 itakuwa imeisha,Barabara za mitaa km 27 zitakuwa zimeisha na ujenzi wa Stand kubwa za Kisasa utakuwa unaendelea..View attachment 2656232

Njia 6 Kwa Sasa haipo sana sana Kuna mradi wa BRT mbeleni na njia ya Sasa ndio itakuwa reserved Kwa Ajili ya BRT..

Mbeya ipi ambayo watu hawajengi Makazi ya Kisasa? Wewe sema Serikali iongeze Kasi ya kupima Mji..

Kitu pekee nachokuunga mguu ni Chuo Cha Kilimo na JKT hapa Uyole wapishe waende Wilayani hayo maeneo yapimwe na yagawiwe viwanja kama ilivyo Kwa Forest au Iwambi Mpya,hakuna Cha NHC,hao NHC wakajenge Dodoma huko.
Kwahiyo Mkuu umeamua kumbishia tu mleta uzi? Sisi watu wa Mbeya tukubali tu ukweli hata kama unauma. Asilimia 95 ya aliyosema mleta uzi ni sahihi.
 
Tuanze kwanza we ni kwenu wapi bukoba maeneo gani? Afu why mbeya ilihari kwenu ni masikin huko kagera?
Bukoba imetoka wap we mtu....mtu akiiponda Mbeya ni wa Bukoba?

But anyway hata hio bukoba iko more organized kuliko hiyo Mbeya japo nayo miundombinu yake ni duni hasa stendi....naona wameanza ujenzi wa stendi mpya juzi tu hapa


Kuhusu Umaskin kagera inachangia pato dogo kwa taifa kuliko population yake...ndo maana inaonekana maskini...




Lakin Averagely hakuna mkoa wenye vijiji vyenye makazi Bora kama kama kagera labda Kilimanjaro...
Screenshot_20230613-192321.jpg
 
Back
Top Bottom