Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.


Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)


Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

Umeongea kweli tupu mkuu, viongozi wa Jiji la Mbeya hawana ubunifu kabisa. Nakumbuka mara ya kwanza kufika Mbeya nilikua nashangaa kuona watembea kwa miguu wakifika barabara ya lami lazima wakung'ute miguu, nilikua kuelewa kumbe wanakung'uta vumbi. Kingine kicho udhi Mbeya traffic, barabara yenyewe moja TANZAM highway traffic wamejaa barabara nzima. Ubunifuwa kupunguza ajali kwenye mitermko ya mbalizi na mlima nyoka ni ziro kabisa.
Na hata mbunge wetu sijawahi kusikia akiongelea maendeleo ya Jiji la Mbeya.
 
Usipangie watu Maisha,wewe ongea unayotamani yawe vinginevyo pita kushoto..

Mbeya ya Leo is way better than it used to be in 2010 wakati ikitangazwa kuwa Jiji..

Njoo 2025 pia kuandika utopolo wako maana by that time Barabara Kuu njia 4 itakuwa imeisha,Barabara za mitaa km 27 zitakuwa zimeisha na ujenzi wa Stand kubwa za Kisasa utakuwa unaendelea..View attachment 2656232

Njia 6 Kwa Sasa haipo sana sana Kuna mradi wa BRT mbeleni na njia ya Sasa ndio itakuwa reserved Kwa Ajili ya BRT..

Mbeya ipi ambayo watu hawajengi Makazi ya Kisasa? Wewe sema Serikali iongeze Kasi ya kupima Mji..

Kitu pekee nachokuunga mguu ni Chuo Cha Kilimo na JKT hapa Uyole wapishe waende Wilayani hayo maeneo yapimwe na yagawiwe viwanja kama ilivyo Kwa Forest au Iwambi Mpya,hakuna Cha NHC,hao NHC wakajenge Dodoma huko.View attachment 2658463
Dah kumbe Mbeya kijijini bora Singida
 
Umeongea kweli tupu mkuu, viongozi wa Jiji la Mbeya hawana ubunifu kabisa. Nakumbuka mara ya kwanza kufika Mbeya nilikua nashangaa kuona watembea kwa miguu wakifika barabara ya lami lazima wakung'ute miguu, nilikua kuelewa kumbe wanakung'uta vumbi. Kingine kicho udhi Mbeya traffic, barabara yenyewe moja TANZAM highway traffic wamejaa barabara nzima. Ubunifuwa kupunguza ajali kwenye mitermko ya mbalizi na mlima nyoka ni ziro kabisa.
Na hata mbunge wetu sijawahi kusikia akiongelea maendeleo ya Jiji la Mbeya.

Yupo busy na mambo ya serikali kuu. Mambo ya jimboni yana maana kidogo sana kwake. Mambo ya bandari na agenda za serikali kuu ndio kipaumbele, nyie watu wa isanga tukutane miezi kadhaa kabla ya uchaguzi.
 
Umetumwa kutuchafua ushindwe [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Muache kufananisha Majiji makubwa kama Mwanza na Vibwengo kijiji kama Mbeya, ohooo , shauri yenu.
Mbeya mtu hawezi kuishi sehemu kama hii. Vibanda kama hivi ni vya mifugo.

1686870711153.png
 
Mwanza nalo ni Jiji au mnaishi kwenye mamilima ,mawe,mapango na vijumba kama mabanda ya nguruwe 70% mnakaa huko hakuna hata usafiri, pumbavu
Nguruwe mnafuga nyie watu msiokuwa na mifugo. Usicheze na Jiji la pili hapa TZ. we endelea kujifunza uchawi huko Nkasi. Huna sifa ya kuishi kwenye majiji pendwa.
 
Back
Top Bottom