Mbeya: Hakimu wa Mahakama ya Wilaya auawa kwa kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira kali

Jambo lingine, serikali iangalie hawa watu waliopewa Mamlaka ya uamuzi. Hakimu mzima umeshindwa kwenye kesi badala ukate rufaa unalazimishia mabavu, yawezekana hata hukumu zake ni za kijanjajanja.
Sasa hapo serikali inahusikaje na ingejuaje hakimu atagombana na raia kwenye mapori Rungwe?
 
Hakimu na mtoa hukumu ya mwisho kwa viongozi wote ni wananchi. Wananchi ndio hakimu wa mwisho.
 
Afrika ujinga ni tatizo kuu. Hakimu amekufa Kwa ujinga wake
Tatizo kubwa mnoooo
sasa hvi ni kuyaacha na ujinga wao, yatajijua, hapa africa watu wengi tena hawa wanaojikuta wana videgree ni wajinga wakubwa sana,
mpaka wanakera.
 
Hakimu hakuheshimu hukumu iliyotolewa na mahakama ikiwa yeye ni expert katika masuala ya kesi na sheria....alale anapostahili
Hapo Sasa Double Standard Hata Ccm Wanafanya Hayo Hayo
 
Eneo ambalo limesababisha auawe ni kubwa kuna karibia ekari 1000, ni msitu na ni hifadhi ambayo imekuwa ikisadia mvua, alinunua kinyemela, wananchi wakamshtaki Mahakamani.[emoji818]
 
Kuna vijiji hawana macheko na hawatak madharau,sijui hata waliwezaje kujikusanya fasta hvyo na kufanya jambo.

Ila hicho kijiji watateseka mpaka wajute kuna nyumba zitabaki na wanawake tu
Hatari kweli kweli...
 
Yani unashindwa kesi unachimbia dawa kwenye ardhi, duh! hivi sisi binadamu tukoje? ardhi hii hii tunayozikiwa tunahangaika nayo kiasi kwamba uhai unapotea, alifikiri uhakimu wake ni katika kila kitu, kimsingi kwa stori hii inaitwa KOSA la Marehemu, awekwe anapostahili na aacha ushirikina na kutumia uhakimu vibaya, kiburi ni kitu kibaya sana kwa binadamu. Tuache kibri na majigambo.
 
Ardhi imemmeza ,ardhi inaweza kuwa baraka,ardhi inaweza kuwa laana.Mauti ilikuwa ikimuita
 
Inasikitisha sana.Bila kujali taaluma yake
 
Sio ajabu Kuna mgosi alikua amepania kumfunga kule Handeni. Mgosi akaenda kwa wataalam (Kama kawaida Yao) mtaalam akasakizia kifo mbaya wa mgosi na kumuambia ' huyu harudi Handeni Tena.
Handeni isikie kwenye redio tu.
Daah ushatengeneza movie tayari
 
NAWAPONGEZA SANA WANANCHI
 
Nia hatuifahamu ila nadhani ilikuwa kuchimbia vitu ambavyo mhusika katika rufaa angetumia kama vielelezo vya umiliki na uhusika katika eneo husika.
 
uchu na tamaa ya kujilimbikizia mali matokeo yake ni kifo.

Punguzeni taamaa, tamaa mbele mauti nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…