Nyerere ameondoka madakani 1985 zaidi ya miaka 37 iliyopita. Siamini kama bado ana mchango wa kuwa na maendeleo duni. Kumepita awamu zaidi ya nne za utawala baada yake. Haya madini tunayohangaika nayo Sasa alijiweka mbali nayo, tena kwa sababu nzuri tu. Sina wataalam wa kufanya hii biashara. Sasa mmekuja wataalam mliosubiriwa ndo imekuwa shida tupu. Yako maeneo hakufanya vizuri kweli,naye alikiri. Lakini tawala zilizofuata baada yake wameharibu zaidi. Mfano kama hiyo chuki dhidi ya mkoa imechangiwa na misimamo ya kisiasa ya wakazi wa mkoa huo. Na ilipamba moto sana kuanzia 1995, uchaguzi wa kwanza kwa mfumo wa vyama vingi, mbeya walianza na mbunge wa nccr. Nakumbuka walionywa sana na huo uamuzi na kwa tabia yao hawakimsikia mtu. Tumesikia wenyewe hata uchaguzi wa 2020, ulitolewa mfano wa gunzi na betri. Na wapinzani walifananishwa na gunzi. Mkoa wa mbeya unavyo vyanzo vingi vya maji mwaka mzima, lakini kuna kubwa ya maji ya makusudi tu, eti kukomoana.