Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Sio surprise ilikua inatarajiwa kabisa.
Tuendelee kungojea yanayo fuata !
 
Nimeipitia hukumu ya High Court iliyotolewa Mbeya, niwazi mawakili walio wakilisha wananchi wameshinda kesi lakini Mahakama imeshindwa kutoa hukumu yake kuwapa ushindi Adv. Mwambakuzi na wenzake kwani mahakama imeeleza wazi kuwa Bunge nalo ni mhimili unaojitegemea hivyo hawawezi kutengua maamuzi yake.
AJABU SANA, mbona serikali nayo ni mhimili lakini maamuzi yake ya hovyo yanaweza kupingwa na mahakama?
Hapa inaonyesha wazi na majaji wametamka hivyo makusudi kama kufahamisha umma kuwa kuna shinikizo lililo waamuru kuamua hivyo.
 
Kwani kesi yao si ilikuwa kutaka tafsiri na sio kubatilisha maamuzi ya Bunge?!
 


Breaking News:​

Mahakama Mbeya yatupilia mbali kesi ya Bandari walalamikaji kukata rufaa​


Humphery Mgonja
BBC Field Producer
View attachment 2713456
BBCCopyright: BBC
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.
Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.
Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.
 
JWTZ mko wapi kufanya ya Niger? Hawa ma judged na watawala fofofo watupiliwe mbali.. ndicho tunachotaka toka kwenu au mpaka mbinafsishwe?
Kwanini usakizie jeshi? Hicho kinachokushinda wewe kufanya hilo na wao ndio vile vile kinawashinda
 
Uzi huu utakosa wachangiaji.Wakati hukumu ya haki ndio hii.
 
Safi sana.
 
Wananchi wengi wamefurahi uamuzi huu.
 
Majaji wanashangaa halafu wanaishia kusema dosari hizo hazitaondoa uhalali wa mkataba!
 
mwambukusi na genge lake hawana jipya wameangukia puaaaaaaaaaa waende wakacheze wanakochezaga haya mambo ya kikubwa hawayawezi
 
Kuna rufaa mwendo ni uleule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania hakuna mahakama bali kuna vikundi vya wahuni wanaojiita majudge
 
Safi sana,wananchi wazalendo wa nchi hii,tumefurahi.Mama Samia,Mungu akupe umri mrefu wenye afya na mafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…