Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

hukumu tayari, habari mbaya wa watanganyika wote, Jaji atupilia mbali madai ya Mwabukusi na timu yake
 
#Jaji Ndunguru: Tunakubaliana na hoja ya Waleta Maombi, kwamba ibara za IGA imevunja sheria za ulinzi wa Rasilimali, kwa kupeleka migogoro nje ya nchi.

Hata hivyo, dosari hiyo haitatumika kuutangaza IGA kuwa ni batili.

#Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu
vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.

Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.

Attachments

Sasa vifungu kama vilikiuka sheria si ndiyo ubatili wenyewe? Hii si ni kama ku "sugar coat" sheria
Utabadilishaje vifungu wakati mkataba umesainiwa?
 
Waneamua kunawa mikono. Kazi ya kutafsiri sheria ni yao lakini mambo yakiwa magumu wanairuka kwa kutotoa maamuzi.

Mambo ya aibu kabisa. Bunge linaongozwa na mtaalamu wa sheria lakini wanafanya mambo kama kundi la wapumbavu.

Acha iuzwe tu. Tutajifunza na kurekebisha huko mbele.
 
Hii kazi ya kudai haki ya mtanganyika iliyoporwa na wasaliti toka Zanzibar lazima iendelee, bila kujali outcome ya hiyo kesi, kwasababu watanganyika bandari zetu tulipewa na muumba, hatukupewa na majaji mahakamani.

Haina maana yoyote tuwaulize maswali waliozitoa bandari zetu kwa waarabu milele, washindwe kutujibu, kisha twende mahakamani kutafuta majibu, nao waje na nusu majibu, jopo la majaji linapotamka IGA imeingilia sheria za nchi, lakini sio batili, wanatakiwa wakapimwe akili kama zipo timamu.

Mihimili yote ya hili taifa imeamua kutusaliti, imeamua kufumbia macho ushetani wa Samia, sasa kinachofuata ni watanganyika wenyewe tuwaoneshe bandari zetu ni mali yetu, urithi toka kwa muumba wetu, wao ni wasimamizi wasio na huruma na vizazi vya hili taifa.
 
Hivi kuna mtu alijua watashinda hii kesi?Mimi nilijua hawatashinda maana Serikali ndo mhimili wenye mzizi mrefu na imekula mihimili mingine yote. Hawa majaji,wanahofia vyeo vyao. Tumeshajua,sema wanamuogopa Boss wao.Hili Jeshi la Tanzania si lichukue tu hii nchi.Mabeyo ulikosea sana.Ulitakiwa ubebe hii nchi walau CCM wapoteane na tuanze upyaaaa.
 
Waneamua kunawa mikono. Kazi ya kutafsiri sheria ni yao lakini mambo yakiwa magumu wanairuka kwa kutotoa maamuzi.

Acha iuzwe tu. Tutajifunza na kurekebisha huku mbele.
Tukishajifunza 2017 katika issue za Madini mpaka Acacia Mining akaondoka! Tukatunga hizo sheria ambazo leo wanakubali zilivunjwa ila hawawezi kutangaza hiyo IGA ni batili! Na bado Bungen mwezi ujao wanaenda kurudi tulikotoka wanaenda kufuta vifungu hivyo leo vinavyowapa wakati mgumu ili warudi warekebishe viwape uwepesi
 
Mara IGA ,mara transhipment, mara umiliki wa ardhi ,mara ukomo wa mkataba .semeni kama IGA mzima haufai sio mnagawana hoja .

Mbana ujinga mtupu.
 
Tukishajifunza 2017 katika issue za Madini mpaka Acacia Mining akaondoka! Tukatunga hizo sheria ambazo leo wanakubali zilivunjwa ila hawawezi kutangaza hiyo IGA ni batili! Na bado Bungen mwezi ujao wanaenda kurudi tulikotoka wanaenda kufuta vifungu hivyo leo vinavyowapa wakati mgumu ili warudi warekebishe viwape uwepesi
Tutajifunza kwenye kuchagua makamu wa rais, tutajifunza kuwa rais anaweza kufa na makamu wake akawa rais.

Hicho kifungu kwenye katiba lazima kitaondoka within 10 years.
 
Back
Top Bottom