Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Mahakama Mbeya yatupilia mbali kesi ya Bandari walalamikaji kukata rufaa​

d2dcd05a-5648-4a28-a656-735d5d587e67.jpg

Humphery Mgonja
BBC Field Producer
View attachment 2713452
BBCCopyright: BBC
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.
Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.
Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.
Kumbe unaweza kuvunja sheria za nchi alafu Mahamaka ikasema sio issue?
 
𝑆𝑖𝑠𝑖 𝑊𝑎𝑡𝑎𝑛𝑔𝑎𝑛𝑦𝑖𝑘𝑎 𝑏𝑎𝑛𝑎....𝑘𝑤𝑎 ℎ𝑖𝑦𝑜 𝑘𝑢𝑛𝑎 𝑎𝑙𝑜𝑡𝑒𝑔𝑒𝑚𝑒𝑎 ℎ𝑖𝑖 𝑘𝑒𝑠𝑖 𝑡𝑢𝑡𝑎𝑠ℎ𝑖𝑛𝑑𝑎????

𝑀𝑎𝑝𝑎𝑚𝑏𝑎𝑛𝑜 𝑤𝑎𝑛𝑎𝑦𝑜𝑓𝑎𝑛𝑦𝑎 𝐶ℎ𝑎𝑑𝑒𝑚𝑎 𝑛𝑎 𝑊𝑎𝑧𝑎𝑙𝑒𝑛𝑑𝑜 𝑤𝑒𝑛𝑔𝑖𝑛𝑒 𝑘𝑖𝑛𝑎 𝐷𝑟 𝑆𝑙𝑎𝑎 𝑛𝑑𝑜 𝑦𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑝𝑒𝑤𝑎 𝑘𝑖𝑝𝑎𝑢𝑚𝑏𝑒𝑙𝑒...𝑀𝑎ℎ𝑎𝑘𝑎𝑚𝑎 𝑧𝑒𝑡𝑢 𝑠𝑖𝑜 ℎ𝑢𝑟𝑢 𝑘𝑎𝑚𝑎 𝑍𝑎 𝐾𝑒𝑛𝑦𝑎!
 
Tunakumbushana tu leo ndio tarehe 10/08/2023

---- UPDATE----
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.

Misingi minne ilianishwa kwenye malalamiko hayo ni:

- Mkataba kuridhiwa bila kuutoa kwa uma na muda wakushiriki kwa wananchi.

- Mkataba wa IGA uliosainiwa unakiuka sheria.

- Mkataba ni kinyume na maslahi ya umma na rasilimali za umma.

- Mkataba unahatarisha usalama wa nchi kwa baadhi ya vifungu.

Akiongea na waandishi wahabari Wakili wa walalamikaji Bonifasi Mwabukusi amesema wanajipanga kwenda kukata rufaa kwani hawajakubaliana na uamuzi wa mahakama.

===

Sasa ni 09:00 Asubuhi ukumbi wa kwanza umejaa na ukumbi wa pili umejaa na bado kuna idadi kubwa ya watu nje waliendelea kuingia.

Leo majaji wa kesi hii wataandika historia ya maamuzi yao kwa vyovyote watakavyoamua.

Majaji wote watatu wameingia muda huu saa 3:42.

MAJAJI WA KESI HII
  • Mhe. Ndunguru
  • Mhe. Ismail
  • Mhe. Kagomba
Wakili wa serikali anatambulisha mawakili wa pande zote mbili. Na wote wako tayari kupokea hukumu.

Mahakama imetulia kwa ukimya mkuu. Majaji wanazungumza kidogo, Mhe. Ismail na Ndunguru. Kisha, Jaji Kagomba na Ndunguru pia wanazungumza kidogo. Wanaendelea kuandika.Karani wa Mahakama leo ni MAPUNDA.

Majaji wanasema wako tayari kusoma hukumu na kwamba itasomwa kwa kiswahili.

Jaji Ndunguru anaanza kusoma hukumu.

HUKUMU YA MAHAKAMA
Katika lalamiko hili waleta maombi wanne ni raia wa Tanzania wameleta maombi haya dhidi ya Mkataba wa TZ na Emirati ya Dubai.

Jaji Ndunguru: Mkataba huo uliingiwa mwaka 2022 na sehemu ya utangulizi wa Mkataba huo unarejea M.O.U iliyosaiwa tarehe 25/2/2022 wakati wa Maonyesho ya Dubai yaliyosainiwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania.

Jaji Ndunguru; Baada ya kusainiwa Mkataba huo hatua za kuridhia mkataba huo hapa Tanzania ulianza kwa mujibu wa Ibara ya 25 ya Mkataba huo.Bunge lilitoa taarifa kwa umma tarehe 5 Juni, 2023 na kuelekeza maoni yangepokelewa tarehe 6 Juni, 2023.

Jaji Ndunguru: Kusainiwa kwa Mkataba huo kumezua mgawanyiko mkubwa kimtazamo, na watu wengi wakisema mkataba huo una dosari na kwamba haukustahili kuwepo.

Jaji Ndunguru; Wanaolalamikiwa ni Waziri wa Ujenzi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Katibu wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kuunganishwa katika mashtaka yanayohusu Serikali.

Jaji Ndunguru: Malalamiko hayo yameletwa katika misingi minne.Misingi hiyo ni pamoja na kwamba IGA ibara zake kadhaa kama zilivyotajwa katika Hati ya Mashtaka, kwamba zinakiuka sheria na Katiba ya Tanzania.

Jaji Ndunguru: Kiapo cha pamoja cha Waleta Maombi kiliunga mkono maombi yaliyowekwa katika Hati ya Malalamiko.Kwa ujumla Kiapo hicho kimelalamikia Mchakato mzima wa Upatikanaji wa Mkataba huo na mwenendo wa Bunge juu ya uvunjifu wa Sheria za nchi.

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi walijibu mashtaka hayo kwa kiapo cha watu wawili, MOHAMED SALUM na MARIAM ambaye ni Mwanasheria kutoka Bungeni.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wamejibu kwamba mambo yanayolalamikiwa hayana msingi, na kwamba sheria na Katiba zimezingatiwa na masuala ya Usalama yametazamwa kikamilifu katika mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wameeleza kwamba Bunge lilitoa taarifa kwa umma ili kupata maoni, na wamesema kwamba watu 72 walijitokeza kutoa maombi. Shauri hilo lilisikilizwa kwa njia ya mdomo, mawakili wa pande zote mbili wakiwakilisha wadaawa.

Jaji Ndunguru: Kabla ya kuanza usililizwaji huo, Mawakili wa pande zote mbili waliunda kwanza viini vya kuamuliwa (Issues) pamoja na kiini kimoja ambacho kiliongezwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Viini hivyo ni pamoja na kuhoji iwapo Ibara kadhaa ya IGA zinakiuka Ubara ya 1, 8, 28(1)(3) za Katiba ya Tanzania.Pia, kiini kingine kilihoji iwapo IGA ni mkataba.

Jaji Ndunguru: Kiini cha kingine kilihoji iwapo Mkataba wa IGA ulifuata taratibu za uteuzi wa Mzabuni katika kuzingatia sheria ya Manunuzi ya Umma.Hoja zote muhimu zilizingatiwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hata hivyo, kabla ya kutoa umauzi Mahakama inapenda kuwashukuru Mawakili wa pande zote mbili kwa kufanya kazi yao nzuri na kusaidia kutupatia Mahakama maarifa na uelekeo mzuri katika kutoa uamuzi.

Jaji Ndunguru: Ukiachia kiini cha tatu, viini vingine vyote havijajielekeza katika uvunjifu wa Katiba.Hata hivyo, kiu ya Watanzania inajikita kupata majibu kwa viini vyote vilivyoletwa mbele ya Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hata hivyo, kiu ya Watanzania inajikita kupata majibu kwa viini vyote vilivyoletwa mbele ya Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hii ni kwa sababu kila shauri linapaswa kuamuliwa kwa kuzingatia mazingira yake, na pia kwa kuzingatia ibara ya 107A (2)(e) kwamba Mahakama inapotoa uamuzi na haki isifungwe na mambo ya kiufundi.

Jaji Ndunguru: Kwa kuanzia na Kiini cha tano, Walalamikaji wanasema IGA haijakidhi vigezo vya kuwa mkataba kwani hakuna consideration na mambo mengine chini ya Sheria za Mikataba hapa nchini.

Jaji Ndunguru: Mawakili wa Wajibu Maombi wao walijibu kwamba, IGA sio mkataba wa kawaida bali ni makubaliano ya upeo tu, sisi Mahakama tunakubaliana na hoja hiyo.

Jaji Ndunguru: Kuhusu hoja kwamba Emirati ya Dubai sio dola, tumepitia Montevideo Convention, tumeona Emirati ya Dubai inakidhi vigezo vingine lakini tunapata mashaka kuhusu uwezo wa Emirati hiyo kuingia kwenye mikataba ya kimataifa.

Jaji Ndunguru: Mawakili wa Waleta Maombi hawakutuelezea kama Emirati ya Dubai imezuiwa kuingia katika mkataba wa kimataifa.Ni maoni yetu kwamba, katika IGA kila upande ulikuwa na uwezo wa kuingia katika mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Hivyo ni maoni yetu kuwa IGA ni mkataba wa Kimataifa hausimamiwi na Sheria za Mikataba za Tanzania.Kuhusu kiini kwamba Mchakato wa IGA ulikiuka sheria za Manunuzi.

Jaji Ndunguru; Ni mtazamo wetu kwamba, Waleta maombi hawakujielekeza vyema katika sheria za kimataifa ambazo zinakataza kutumiwa kwa sheria za ndani katika mikataba ya kimataifa.

Jaji Ndunguru: Mahakama haijaridhishwa na hoja ya Waleta maombi kwamba Sheria ya Manunuzi ya Umma haikuzingatiwa katika kupima uhalali wa IGA.Kuhusu kiini cha kupima iwapo Umma ulipata muda wa kutosha kupata maoni kwa umma.

Jaji Ndunguru: Kukosekana kwa Viambatanisho muhimu kama Mkataba wa IGA katika Tangazo hilo, na kutokea kwa watu 72 tu, ndiyo hoja ya Waleta Maombi.

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi wamejenga hoja kwamba suala hilo ni la ndani ya Bunge.Mahakama inatambua kuwa Ibara ya 63(3)(e) na Kanuni ya 108(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Jaji Ndunguru: Baada ya kupitia hoja za pande zote, tunakubaliana na hoja za wajibu maombi kwamba Bunge halitakiwi kuingiliwa katika majukumu yake.

Jaji Ndunguru: Msimamo huu umeelekezwa pia na Wasomi mbalimbali kuhusu masuala ya Bunge, akiwemo Pius Msekwa.Licha ya dosari inayoonekana katika ushirikishwaji wa umma kutoa maoni, hata hivyo tunajizuia kufanya uamuzi wa kiasi cha kubatilisha mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Malalamiko makubwa katika Kiini cha mwisho, ni juu ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha mahakama za nje katika migogoro ya rasilimali.

Jaji Ndunguru: Tunakubaliana na hoja ya Waleta Maombi, kwamba ibara za IGA imevunja sheria za ulinzi wa Rasilimali, kwa kupeleka migogoro nje ya nchi. Hata hivyo, dosari hiyo haitatumika kuutangaza IGA kuwa ni batili.

Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.

Jaji Ndunguru: Kwa hoja tajwa hapo juu mahakama hii inatupilia mbali hoja za waleta maombi. Anamaliza kusoma hukumu hiyo .Watu wanasimama majaji wanatoka.
Hakuna cha kushangaa, hakuna jaji wa kukataa maelekezo ya samia/CJ na wengine. Hizi ni takataka kama takataka zingine!
 
Kazi kweli kweli.

Hakuna haja ya kuwa na mahakama. Uwepo wa mahakama Tanzania ni upotevu wa rasilimali. Mahakama zifutwe nchini pamoja na bunge ili tuongozwe na Rais pekee.
 
Watanzania bhana watu wa ajabu sana! Watu wameenda mahakamani wakiamini huko ndiko kuna haki, lakini hukumu ikitoka wasivyotaka wao wanasema majaji hawafai. sasa ulitaka Jaji atoe hukumu kwa kufata hisia au kwa kufata sheria?

Waliotoa hukumu wameusoma mkataba vema na sheria pia wamezisoma. Sisi tunaopinga hatujasoma hata kifungu kimoja cha huo mkataba na sheria zenyewe hatuzijui zaidi ya kufata mkumbo tu!
Watu humu huwa wajuaji sana mpaka wanapitiliza ! 😅
Waswahili husema ujanja mwingi huondoa maarifa !😅🙏
Katiba ya Nchi hii imewapa madaraka makubwa sana wakubwa wa Nchi kiasi kwamba hakuna mahali popote inaweza kuonekana eti Mkuu amevunja Katiba !
Hata JPM hakuna mahali aliivunja Katiba !😅😅🙏🙏
 
Hakuna cha kushangaa, hakuna jaji wa kukataa maelekezo ya samia/CJ na wengine. Hizi ni takataka kama takataka zingine!
JWTZ mko wapi kufanya ya Niger? Hawa ma judged na watawala fofofo watupiliwe mbali.. ndicho tunachotaka toka kwenu au mpaka mbinafsishwe?
 
Unaona hata uzi /thread hauendi sna maana watu walishajua hukumu itakuwaje.
Mwenye picha za hawa wahuni watatu atuwekee
1691657727695.png

ndiye huyu?
 
Mahakama imesema kwamba inatambua baadhi ya KASORO & MAKOSA yaliyopo kwenye mkataba wa banadari na kwamba ni Kinyume cha sheria namba 5 ya ulinzi wa rasilimali ya mwaka 2017.
Hata hivyo imesema haiwezi kutoa AMRI/ORDER yoyote juu ya hilo
 
Tunakumbushana tu leo ndio tarehe 10/08/2023

---- UPDATE----
Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.

Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.

Misingi minne ilianishwa kwenye malalamiko hayo ni:

- Mkataba kuridhiwa bila kuutoa kwa uma na muda wakushiriki kwa wananchi.

- Mkataba wa IGA uliosainiwa unakiuka sheria.

- Mkataba ni kinyume na maslahi ya umma na rasilimali za umma.

- Mkataba unahatarisha usalama wa nchi kwa baadhi ya vifungu.

Akiongea na waandishi wahabari Wakili wa walalamikaji Bonifasi Mwabukusi amesema wanajipanga kwenda kukata rufaa kwani hawajakubaliana na uamuzi wa mahakama.

===

Sasa ni 09:00 Asubuhi ukumbi wa kwanza umejaa na ukumbi wa pili umejaa na bado kuna idadi kubwa ya watu nje waliendelea kuingia.

Leo majaji wa kesi hii wataandika historia ya maamuzi yao kwa vyovyote watakavyoamua.

Majaji wote watatu wameingia muda huu saa 3:42.

MAJAJI WA KESI HII
  • Mhe. Ndunguru
  • Mhe. Ismail
  • Mhe. Kagomba
Wakili wa serikali anatambulisha mawakili wa pande zote mbili. Na wote wako tayari kupokea hukumu.

Mahakama imetulia kwa ukimya mkuu. Majaji wanazungumza kidogo, Mhe. Ismail na Ndunguru. Kisha, Jaji Kagomba na Ndunguru pia wanazungumza kidogo. Wanaendelea kuandika.Karani wa Mahakama leo ni MAPUNDA.

Majaji wanasema wako tayari kusoma hukumu na kwamba itasomwa kwa kiswahili.

Jaji Ndunguru anaanza kusoma hukumu.

HUKUMU YA MAHAKAMA
Katika lalamiko hili waleta maombi wanne ni raia wa Tanzania wameleta maombi haya dhidi ya Mkataba wa TZ na Emirati ya Dubai.

Jaji Ndunguru: Mkataba huo uliingiwa mwaka 2022 na sehemu ya utangulizi wa Mkataba huo unarejea M.O.U iliyosaiwa tarehe 25/2/2022 wakati wa Maonyesho ya Dubai yaliyosainiwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania.

Jaji Ndunguru; Baada ya kusainiwa Mkataba huo hatua za kuridhia mkataba huo hapa Tanzania ulianza kwa mujibu wa Ibara ya 25 ya Mkataba huo.Bunge lilitoa taarifa kwa umma tarehe 5 Juni, 2023 na kuelekeza maoni yangepokelewa tarehe 6 Juni, 2023.

Jaji Ndunguru: Kusainiwa kwa Mkataba huo kumezua mgawanyiko mkubwa kimtazamo, na watu wengi wakisema mkataba huo una dosari na kwamba haukustahili kuwepo.

Jaji Ndunguru; Wanaolalamikiwa ni Waziri wa Ujenzi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Katibu wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anapaswa kuunganishwa katika mashtaka yanayohusu Serikali.

Jaji Ndunguru: Malalamiko hayo yameletwa katika misingi minne.Misingi hiyo ni pamoja na kwamba IGA ibara zake kadhaa kama zilivyotajwa katika Hati ya Mashtaka, kwamba zinakiuka sheria na Katiba ya Tanzania.

Jaji Ndunguru: Kiapo cha pamoja cha Waleta Maombi kiliunga mkono maombi yaliyowekwa katika Hati ya Malalamiko.Kwa ujumla Kiapo hicho kimelalamikia Mchakato mzima wa Upatikanaji wa Mkataba huo na mwenendo wa Bunge juu ya uvunjifu wa Sheria za nchi.

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi walijibu mashtaka hayo kwa kiapo cha watu wawili, MOHAMED SALUM na MARIAM ambaye ni Mwanasheria kutoka Bungeni.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wamejibu kwamba mambo yanayolalamikiwa hayana msingi, na kwamba sheria na Katiba zimezingatiwa na masuala ya Usalama yametazamwa kikamilifu katika mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wameeleza kwamba Bunge lilitoa taarifa kwa umma ili kupata maoni, na wamesema kwamba watu 72 walijitokeza kutoa maombi. Shauri hilo lilisikilizwa kwa njia ya mdomo, mawakili wa pande zote mbili wakiwakilisha wadaawa.

Jaji Ndunguru: Kabla ya kuanza usililizwaji huo, Mawakili wa pande zote mbili waliunda kwanza viini vya kuamuliwa (Issues) pamoja na kiini kimoja ambacho kiliongezwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Viini hivyo ni pamoja na kuhoji iwapo Ibara kadhaa ya IGA zinakiuka Ubara ya 1, 8, 28(1)(3) za Katiba ya Tanzania.Pia, kiini kingine kilihoji iwapo IGA ni mkataba.

Jaji Ndunguru: Kiini cha kingine kilihoji iwapo Mkataba wa IGA ulifuata taratibu za uteuzi wa Mzabuni katika kuzingatia sheria ya Manunuzi ya Umma.Hoja zote muhimu zilizingatiwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hata hivyo, kabla ya kutoa umauzi Mahakama inapenda kuwashukuru Mawakili wa pande zote mbili kwa kufanya kazi yao nzuri na kusaidia kutupatia Mahakama maarifa na uelekeo mzuri katika kutoa uamuzi.

Jaji Ndunguru: Ukiachia kiini cha tatu, viini vingine vyote havijajielekeza katika uvunjifu wa Katiba.Hata hivyo, kiu ya Watanzania inajikita kupata majibu kwa viini vyote vilivyoletwa mbele ya Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hata hivyo, kiu ya Watanzania inajikita kupata majibu kwa viini vyote vilivyoletwa mbele ya Mahakama.

Jaji Ndunguru: Hii ni kwa sababu kila shauri linapaswa kuamuliwa kwa kuzingatia mazingira yake, na pia kwa kuzingatia ibara ya 107A (2)(e) kwamba Mahakama inapotoa uamuzi na haki isifungwe na mambo ya kiufundi.

Jaji Ndunguru: Kwa kuanzia na Kiini cha tano, Walalamikaji wanasema IGA haijakidhi vigezo vya kuwa mkataba kwani hakuna consideration na mambo mengine chini ya Sheria za Mikataba hapa nchini.

Jaji Ndunguru: Mawakili wa Wajibu Maombi wao walijibu kwamba, IGA sio mkataba wa kawaida bali ni makubaliano ya upeo tu, sisi Mahakama tunakubaliana na hoja hiyo.

Jaji Ndunguru: Kuhusu hoja kwamba Emirati ya Dubai sio dola, tumepitia Montevideo Convention, tumeona Emirati ya Dubai inakidhi vigezo vingine lakini tunapata mashaka kuhusu uwezo wa Emirati hiyo kuingia kwenye mikataba ya kimataifa.

Jaji Ndunguru: Mawakili wa Waleta Maombi hawakutuelezea kama Emirati ya Dubai imezuiwa kuingia katika mkataba wa kimataifa.Ni maoni yetu kwamba, katika IGA kila upande ulikuwa na uwezo wa kuingia katika mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Hivyo ni maoni yetu kuwa IGA ni mkataba wa Kimataifa hausimamiwi na Sheria za Mikataba za Tanzania.Kuhusu kiini kwamba Mchakato wa IGA ulikiuka sheria za Manunuzi.

Jaji Ndunguru; Ni mtazamo wetu kwamba, Waleta maombi hawakujielekeza vyema katika sheria za kimataifa ambazo zinakataza kutumiwa kwa sheria za ndani katika mikataba ya kimataifa.

Jaji Ndunguru: Mahakama haijaridhishwa na hoja ya Waleta maombi kwamba Sheria ya Manunuzi ya Umma haikuzingatiwa katika kupima uhalali wa IGA.Kuhusu kiini cha kupima iwapo Umma ulipata muda wa kutosha kupata maoni kwa umma.

Jaji Ndunguru: Kukosekana kwa Viambatanisho muhimu kama Mkataba wa IGA katika Tangazo hilo, na kutokea kwa watu 72 tu, ndiyo hoja ya Waleta Maombi.

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi wamejenga hoja kwamba suala hilo ni la ndani ya Bunge.Mahakama inatambua kuwa Ibara ya 63(3)(e) na Kanuni ya 108(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Jaji Ndunguru: Baada ya kupitia hoja za pande zote, tunakubaliana na hoja za wajibu maombi kwamba Bunge halitakiwi kuingiliwa katika majukumu yake.

Jaji Ndunguru: Msimamo huu umeelekezwa pia na Wasomi mbalimbali kuhusu masuala ya Bunge, akiwemo Pius Msekwa.Licha ya dosari inayoonekana katika ushirikishwaji wa umma kutoa maoni, hata hivyo tunajizuia kufanya uamuzi wa kiasi cha kubatilisha mkataba huo.

Jaji Ndunguru: Malalamiko makubwa katika Kiini cha mwisho, ni juu ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha mahakama za nje katika migogoro ya rasilimali.

Jaji Ndunguru: Tunakubaliana na hoja ya Waleta Maombi, kwamba ibara za IGA imevunja sheria za ulinzi wa Rasilimali, kwa kupeleka migogoro nje ya nchi. Hata hivyo, dosari hiyo haitatumika kuutangaza IGA kuwa ni batili.

Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.

Jaji Ndunguru: Kwa hoja tajwa hapo juu mahakama hii inatupilia mbali hoja za waleta maombi. Anamaliza kusoma hukumu hiyo .Watu wanasimama majaji wanatoka.
Tulijua tuuuu hata walioshitaki nao walijua tuuuu hiyo kesi watagaragazwa asubuhiii. Yaaani serikali ikiruhusu kila inachofanya halawanaibuka makundi ya watu na kuwekea pingamiziii, itakwamaaa.

Uwekezaji hauna shida kiasi kwa jinsi wanavyovumisha na kuhofisha watu. Serikali imetoa mda raia watoe maoni na mapendekezoo kwa maboreshoo, sasa badala ya watu kutoa maoni walikimbilia mahakamaniiii. Duuuuuuh ni shida kwelikweliii
 
Kwa kilichopelepelekwa Mahakamani basi mi nafikiri Mahakama ilipaswa kwenda mbali zaidi kwa Maslah ya Taifa.
Mahakama.zio shule ya kufundisha sheria,mahakama iliombwa itafsiri sheria kuhusu uhalali wa mkataba ule.

Kaka hauhitaji kuwa mwanasheria kwamba IGA hauwezi kuichallange kwa sheria za Tanzania bali mikataba ya kioperesheni ndio unaweza kufanya hivyo.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Mahakama imesema kwamba inatambua baadhi ya KASORO & MAKOSA yaliyopo kwenye mkataba wa banadari na kwamba ni Kinyume cha sheria namba 5 ya ulinzi wa rasilimali ya mwaka 2017.
Hata hivyo imesema haiwezi kutoa AMRI/ORDER yoyote juu ya hilo
Unaleta habari nusu nusu una haraka gani?
 
Back
Top Bottom