Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu

Umewasomaji majaji? Wamesema wapi hakuna vifungu vilivyokuwa?

Jitahidi kuwasoma vyema; kwa kukusaidia wamesema wamefungwa mikono kuhoji bunge na mapungufu ya sheria
Inaonekana kwa hukumu hii mahakama iko chini ya Bunge. Bunge lipo chini ya Rais.

Wananchi milioni sitini hawana mtetezi,mtu wa kuwasimamia, kuwakilisha matakwa yao. Ingetakiwa kuwa mahakama na Bunge.

Tanzania kuna mhimili mmoja, Urais, Ufalme, Mungu mtu, unaotumiwa na CCM kufanya uhuni wao.
 
Nakwakua tumevunja hiyo Sheria tumepeleka mswada wa kurekebisha Ili wambea wasirudie kuwakwaza ma judge wetu, what a country, cry my people!
 
Hii kauli inaonesha namna mioyo ya majaji wetu ilivyohangaika na hili jambo. Wakafika kiwango cha kuchoka, kushindwa kufanya lolote.
Mapunziko mema Majaji. Mmefanya mlichoweza katika ubinadamu wenu.
Hapa ndipo imuhimu wa katiba mpya unapo onekana.
Mahakama imekuwa ikitumika mara nyingi kuibeba serekali..
Mambo ya aibu sana.
 
Namnukuu Magufuli, "ukiona wapinzani wako wana kushangilia sana gruka nyuma uolangalie ulipokosea"

Sasa huyu mama zile kelele za anaupiga mwingi zilizokuwa zinapigwa na kila mtu hapa nchini hadi wapinzani kumbe nyuma ya pazia anauza nchi?
 
Kufuatia maamuzi ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mjini Mbeya, Tanzania

Sasa mpira umerudishwa bungeni kuona kama vifungu vilivyokiukwa vya sovereignty ya Tanzania zitatetewa visibadilishwe au vitabadilishwa ili uwekezaji wa Dubai kupitia DP World ufanikiwe.


Bunge la Marekani walipinga uwekezaji wa DP World nchini Marekani mbali ya kutetewa sana na viongozi wa utawala waliokuwa White House wakati huo.

Tukumbuke bunge la Muungano wa Tanzania kizalendo lilijadili muswada wa sheria mpya 30 Juni, 2017

Bunge laongeza Siku ili kuchambua Miswada mitatu ya Sheria za Ulinzi wa Rasilimali za Taifa​

Bunge limeongeza siku za Mkutano wa Saba hadi tarehe 05 Julai 2017, ili kupitia Miswada mitatu ya sheria inayohusu marekebisho ya Sheria za Madini na ulinzi wa rasilimali za Taifa.
Akitoa maelezo Bungeni, Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alisema kuwa Kamati ya Uongozi ilikutana tarehe 28 Juni, 2017 Jioni, ili kufanya marekebisho ya Ratiba ya Mkutano wa saba Bunge ambao ulitarajiwa kuisha tarehe 30 Juni, 2017 na kukubaliana kuongeza siku tatu za kazi hadi tarehe 5 Julai, 2017 ili kuliwezesha Bunge kupitia Miswada hiyo.
Kufuatia uamuzi huo Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa ameunda Kamati ya pamoja itakayopitia Miswada miwili ambayo tayari imeshasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni. Miswada hiyo ni; Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms)] Bill, 2017];(iii)Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permmanent Sovereignty)] Bill, 2017].
Mhe Spika alisema kuwa Kamati hiyo ya pamoja itakayochambua miswada hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe Dotto Biteko na itajumuisha Wajumbe wa Kamati nne za Bunge ambazo ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya Sheria Ndogo.

Aidha kwa upande mwingine Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati ya Katiba na Sheria chini ya Uenyekiti wa Mhe Mohamed Omary Mchengerwa itauchambua Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017]


Na sasa miaka mitano baadaye yaani 2023 bunge hili linaona sheria hiyo ya mwaka 2017 inahitaji mabadiliko hivyo kualika wadau wakitazamia mwezi Agosti 2023 wataifanyia mabadiliko ili kuwezesha uwekezaji.
 
Kumbe ndio mana mlitaka mtangaze kituko chenu leo. Wangetangaza juzi tu, walikimbiza upepo. Kwenye kutafuta haki mara nyingi wanaetoa vitisho ndio woga na wovu
 
Back
Top Bottom