Mbeya: Majambazi wapora fedha na kumuua wakala

Mbeya: Majambazi wapora fedha na kumuua wakala

Mfanyabiashara wa miamala ya fedha Bi. Vaileth Libaba mwenye umri wa miaka 34, mkazi wa Shewa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya, ameuawa na kuporwa fedha taslimu shilingi 300,000/= na simu zake mbili za mkononi za Biashara yake ya miamala na majambazi watano na kati yao watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, na wawili wameuawa kwa risasi wakijaribu kuwakimbia polisi
View attachment 3663511
Wamerudi tena ,wamerudi tena wateule wamerudi.

Hao waliobaki wapigwe PINCHI wataje mtandao wao wanaofanya kazi ,wakusanye mtandao wao nao WALE VYUMA.

Tusiwachekee ,tulishasahau ,wasiturudishe enzi za JK ambapo ilikuwa kutoka hata na "Mlio" unaogopa utakula Chuma....Hao wawataje wenzoa kisha wale vyuma.
 
Kuna genge la uhalifu limeuvamia huo ukanda hadi basi. Wanatembeza mapanga kwa mawakala na kuwapora fedha na simu za biashara.
 
Mfanyabiashara wa miamala ya fedha Bi. Vaileth Libaba mwenye umri wa miaka 34, mkazi wa Shewa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya, ameuawa na kuporwa fedha taslimu shilingi 300,000/= na simu zake mbili za mkononi za Biashara yake ya miamala na majambazi watano na kati yao watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, na wawili wameuawa kwa risasi wakijaribu kuwakimbia polisi
View attachment 3663511
Jambazi anaua kwa laki 3?
Hao ni vibaka sio majambazi.
 
Majambazi wengi hawana akili unaua mtu laki 3! Kwanza siku hizi kupatikana ni rahisi sana. Mijitu inaenda kwenye uhalifu na simu. Halafu tena inaiba simu!! Ujambazi haulipi kabisa siku hizi, ni wa kuacha kabisa.
 
binadamu hawana utu hawaangalii wanaemua anaachaje familia yake kisa laki 3 ambapo hiyo laki tatu unaweza ipata kihalali kabisa shughuli zipo nyingi ,Mungu awape nguvu familia iliyompoteza ndugu yao
 
Back
Top Bottom