Mbeya: Majambazi wapora fedha na kumuua wakala

Mbeya: Majambazi wapora fedha na kumuua wakala

Ila hii Mbeya nayo uwakala ni hatari sana
Mshikaji wangu ametapeliwa laki 5 mwezi wa 6 mwaka huu na wiki hiyohiyo aliyotapeliwa kuna wakala mwingine nae ameibiwa hela zote kwenye kibanda chake na watu wasiojulikana
Leo tena wakala mwingine kauawa. Wameona kuwatapeli haitoshi wameanza kuwaua sasa
Ushamba sasa huu, unatepeliwaje?
 
tamaa za utajiri wa haraka
Na miziki ya kila siku inawashawishi vijana kufanya Starehe

Bora ni enjoy, maisha ni simple, nataka kulewa, DJ ongeza sauti nilewe na mademu.

Yaani miziki ule wa kwetu wa

Kazi Ipo, Binadamu kazi, Majukumu yananiandama umri unakwenda, Cheza pesa usicheze kazi haipo tena
 
Mfanyabiashara wa miamala ya fedha Bi. Vaileth Libaba mwenye umri wa miaka 34, mkazi wa Shewa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya, ameuawa na kuporwa fedha taslimu shilingi 300,000/= na simu zake mbili za mkononi za Biashara yake ya miamala na majambazi watano na kati yao watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, na wawili wameuawa kwa risasi wakijaribu kuwakimbia polisi
View attachment 3663511

Hao watatu kwanini Polisi hamkuwafuta???

Enzi za Kamanda Siri hao angekuwa ameshawagonga kwa mujibu wa Sheria
 
Ameuawa na kuporwa laki 3. Marehemu kaporwa !

Na wawili wameuliwa wakijaribu kuwakimbia polisi. Ukiwakimbia polisi wanaku shuti mgongoni !

Taarifa ni utopolo mtupu na ni uongo mtupu!

Kukosa logic ndio chanzo cha u third world wa Waafrika.

Polisi anaongea utopolo na mwandishi anaripoti mashudu. Lijamii linabaki deaf dumb and blind.
 
Ameuawa na kuporwa laki 3. Marehemu kaporwa !

Na wawili wameuliwa wakijaribu kuwakimbia polisi. Ukiwakimbia polisi wanaku shuti mgongoni !

Taarifa ni utopolo mtupu na ni uongo mtupu!

Kukosa logic ndio chanzo cha u third world wa Waafrika.

Polisi anaongea utopolo na mwandishi anaripoti mashudu. Lijamii linabaki deaf dumb and blind.
Hujaelezea kwa nini ni uongo
Lakini siku ambayo marehemu aliporwa laki 3 na kuuawa na siku ambayo hao majambazi wamekamatwa ni siku mbili tofauti
Mtiririko wa tukio upo hivi

1. Majambazi wamemvamia wakala, wakamchoma visu na kumuua, na kumuibia simu na shilingi laki 3 kisha kutoweka

2. Uchunguzi ukaanza kuwabaini wahusika

3. Washukiwa walipatikana mtaa wa Ituha Relini wakiwa wanavuta bhangi, na polisi ikabidi wawavamie ili kuwakamata, na ndio vurugu ilipotokea na kusababisha polisi kuua watu wawili kati ya hao watano

4. Watu watatu waliobaki bado wanashikiliwa na polisi. Bado hakuna ufumbuzi wa kina juu ya tukio zima, hao ni suspects, lazima uchunguzi uendelee ili kujiridhisha kama wamehusika au la

5. Kesi bado haijaisha, haijapata ufumbuzi wa kina, inaendelea na mpaka sasa ilipofikia tayari imeshaondoka na watu watatu
 
Back
Top Bottom