Mbeya: Mlima Kawetele wameguka, nyumba zaidi ya 20 zadaiwa kufunikwa

Mbeya: Mlima Kawetele wameguka, nyumba zaidi ya 20 zadaiwa kufunikwa

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!!



Mlima kawetele ulioko ITEZI, Uyole, jijini Mbeya umeripotiwa kumeguka na kuziangukia nyumba zaidi ya 20.

Chanzo Cha janga Hilo inasemekana ni mvua nyingi zinaonyesha Nchi nzima, zilizoloanisha udongo Kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni, iliaminika walioko milimani wako katika USALAMA zaidi, kumbe Si Kweli, Mvua za ernino ndio kwanza zimeanza, tuendelee kuwa na Tahadhari na kudumu katika maombi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen.

Source: ITV


Itezi Mbeya

----
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Abdi Isango

Ni kweli sehemu ya mlima imeporomoka na tope kusambaa na kuharibu nyumba 17 pamoja na Shule ya Msingi ya binafsi.

Nyumba zimebomoka kabisa hazionekani, ni kama vile hakukuwa na nyumba, tope limesabaa hakuna kipande cha bati au ubao.

Hakuna madhara kwa binadamu isipokuwa wenyeji wanasema kuna ng’ombe wanne wamesombwa na tope hilo.

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni mvua kubwa zinzoendelea kunyesha, mvua zilinyesha jana na usiku wa kuakia leo, ambapo Alfajiri ndipo tope likaasambaa.

Wenyeji wanasema kwa kuwa kuna shughuli za kilimo, inawezekana kilimo kimesababisha udongo ukose mshikamano na hivyo mvua inaponyesha inakuwa rahisi kukatika.

Chini ya huo Mlima kuna Mto, mbapo umesomba tope hilo Kwenda mbele zaidi, tope lilikuwa kubwa, limesambaa na kusababisha madhara pia katika nyumab nyingine kadhaa.

Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi wamefika eneo la tukio na kutoa maelekezo ya tahadhari, Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha, pia wanaojenga karibu na mito nao wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha.


IMG_20240414_181411_997.jpg
IMG_20240414_181402_736.jpg
IMG_20240414_181345_700.jpg
 
Salaam, shalom!!

Mlima kawetele ulioko jijini Mbeya umeipotiwa kumeguka na kuziangukia nyumba zaidi ya 20.

Chanzo Cha janga Hilo inasemeka a ni mvua nyingi zinaonyesha Nchi nzima zilizoloanisha udongo Kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni, iliaminika walioko milimani, wako katika USALAMA zaidi, kumbe Si Kweli, Mvua za ernino ndio kwanza zimeanza, tuendelee kuwa na Tahadhari na kudumu katika maombi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Source: ITV

Amen
Hali ni tete
 

Attachments

  • VID-20240414-WA0035.mp4
    11.9 MB
Back
Top Bottom