Mbeya: Mlima Kawetele wameguka, nyumba zaidi ya 20 zadaiwa kufunikwa

Mbeya: Mlima Kawetele wameguka, nyumba zaidi ya 20 zadaiwa kufunikwa

Uzunguni watu wako chini ya mlima miaka na miaka haijawahi tokea landslide. Mlima wote umejaa miti. Kwa hali inavyoenda Mbeya kutakuwa kitovu cha haya majanga. Watu wanajenga sana milimani ambako juu yake wanalima sana. Huo mlima Kawetere na wa Nsongwi watu wanajenga tu kupandisha mlimani.
SHida ya jiji la mbeya ni mipango miji hili limepelekea jiji kujaa na watu kuanza kuvamia milima
 
Salaam, shalom!!

View attachment 2963343

Mlima kawetele ulioko ITEZI, Uyole, jijini Mbeya umeripotiwa kumeguka na kuziangukia nyumba zaidi ya 20.

Chanzo Cha janga Hilo inasemekana ni mvua nyingi zinaonyesha Nchi nzima, zilizoloanisha udongo Kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni, iliaminika walioko milimani wako katika USALAMA zaidi, kumbe Si Kweli, Mvua za ernino ndio kwanza zimeanza, tuendelee kuwa na Tahadhari na kudumu katika maombi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen.

Source: ITV


Itezi Mbeya

----
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Abdi Isango

Ni kweli sehemu ya mlima imeporomoka na tope kusambaa na kuharibu nyumba 17 pamoja na Shule ya Msingi ya binafsi.

Nyumba zimebomoka kabisa hazionekani, ni kama vile hakukuwa na nyumba, tope limesabaa hakuna kipande cha bati au ubao.

Hakuna madhara kwa binadamu isipokuwa wenyeji wanasema kuna ng’ombe wanne wamesombwa na tope hilo.

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni mvua kubwa zinzoendelea kunyesha, mvua zilinyesha jana na usiku wa kuakia leo, ambapo Alfajiri ndipo tope likaasambaa.

Wenyeji wanasema kwa kuwa kuna shughuli za kilimo, inawezekana kilimo kimesababisha udongo ukose mshikamano na hivyo mvua inaponyesha inakuwa rahisi kukatika.

Chini ya huo Mlima kuna Mto, mbapo umesomba tope hilo Kwenda mbele zaidi, tope lilikuwa kubwa, limesambaa na kusababisha madhara pia katika nyumab nyingine kadhaa.

Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi wamefika eneo la tukio na kutoa maelekezo ya tahadhari, Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha, pia wanaojenga karibu na mito nao wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha.
View attachment 2963359

View attachment 2963656View attachment 2963657View attachment 2963658
Athari za kutofanya tathmini ya bwawa la mwl Nyerere
 
🤣🤣 Hiyo ni sera ya wapinzani kwa sasa
Uwezo huu mkubwa wa wapinzani kufikiri, uwezo huu wa kuja na hizi sera nzuri za kimkakati zitasaidia kutatua matatizo ya wananchi! Akili zao zinatawaliwa na chuki, bila hata commonsense, bila shaka zitawafanya Watanzania wawape nchi.

CCM ya sasa na upinzani hakuna tofauti. Wote wanataka madaraka na asali kwa maslahi binafsi. SSH, Kinana, Mwigulu, January, Nape, Mbowe, Lema, Lissu, Zitto adui wao mkubwa ni mmoja Magufuli na maskini.
 
Ni kweli kabisa hata yale ya Hanang ni haya haya tu
Wanakata miti bila akili na wakijua fika madhara ila wanajitoa ufahamu

Sasa madhara yake ndio haya
Viongozi wao wanajua kuhamisha watu tu ila akili ya kuwahimiza wapande miti kwa lazima hawana
Tuna viongozi hopeless kabisa
Yaani kiongozi akulazimishe wewe upande miti kwa lazima???
Wewe ungekubali???
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Nipo Salamaaa na nitaendelea kuwa salama kwa uweza wa Mwenyezi Mungu mpaka nitakapotimiza ahadi zangu kwako ephen.
Lucas hebu tuambie serikali ina mkakati gani wa kumdhibiti baradhuli mange Kimambi anaye mkashifu rais wetu kipenzi
 
Yaani kiongozi akulazimishe wewe upande miti kwa lazima???
Wewe ungekubali???
Tabora Aggrey Mwanri aliwalizimisha mkoa mzima wa Tabora na walifanya kwa lazima na akawaambia mti ukifa utaona
Walimwagilia mpaka ikakua yote
Leo ukoenda kila wilaya ya tabora na tabora mjini utaona mandhari na wananchi wanafurahia upepo

Unajua kuna nchi ukigonga mti unafungwa
Na kuna nchi ukitaka kukata mti mkubwq nyumbani kwako unaomba ruhusa
Uko Dunia nyingine eti
Kupanda miti ni wajibu wetu sote
 
Back
Top Bottom