Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mwimbaji huyo Sifa Boniventure Bujune (25) ni Mkazi wa Isyesye anatuhumiwa kuimba wimbo unaojulikana kwa jina la “Tanzania Inaelekea Wapi?” wenye maudhui ya uchochezi na kisha kuurusha katika Mitandao ya Kijamii pamoja na YouTube.
Kamanda wa Polisi Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 13, 2023 huko Isyesye Jijini Mbeya baada ya kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuusambaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kurusha maudhui wa YouTube.
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Huu ndo wimbo anatuhumiwa nao
Pia, soma:
- Mbeya: Mwimbaji wa Wimbo wa "Mnatuona Nyani" afikishwa Mahakamani, asomewa mashtaka
Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara