Mbeya: Mtoto mwenye umri wa miaka sita akutwa amefariki kwenye korongo la maji, wazazi tukumbuke usalama wa watoto kipindi hiki cha mvua

Mbeya: Mtoto mwenye umri wa miaka sita akutwa amefariki kwenye korongo la maji, wazazi tukumbuke usalama wa watoto kipindi hiki cha mvua

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakuu kipindi hiki cha mvua nyingi kwa baadhi ya mikoa ni hatari kwa usalama wa watoto wadogo, wazazi tuwe makini na watoto wetu hasa maeneo wanayocheza na kuwadhibiti kutoka nyumbani pindi mvua zinaponyesha ili tuwaepushe na hatari hizi.
=====

Mtoto Aliyefahamika Kwa Jina La Vicent Konga Mwenye Umri Wa Miaka 6 Aliyekuwa Akisoma Darasa La Kwanza Katika Shule Ya Msingi Lyoto Iliyopo Jijini Mbeya Amefariki Dunia Baada Ya Kutumbukia Kwenye Korongo La Maji Lililopo Mtaa Wa Mwafute Kata Ya Ilemi Jijini Humo.

Wakizungumza Na dream media Baadhi Ya Majirani Wamesema Wamepokea Kwa Masikitiko Makubwa Taarifa Za Tukio Hilo, Huku Wakisema Limekuwa Funzo Kuwa Karibu Na Watoto Wao Ili Kuwaepusha Na Majanga Kama Hayo.

Kwa Mujibu Wa Balozi Wa Mtaa Huo Lusekelo Mwaigabule, Alipata Taarifa Za Kupotea Kwa Mtoto Huyo Siku Ya Juma Tatu Jioni Wiki Hii Ndipo Wakaungana Na Wananchi Wake Kwaajili Ya Kumtafuta, Ambapo siku ya jumanne Walifanikiwa Kumpata Akiwa Tayari Amefariki Katika Korongo Hilo Lenye Maji.

Constable Alpha Isaya Afisa Habari Msaidizi Wa Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji Mkoa Wa Mbeya Amewataka Wazazi Na Walezi Mkoani Humo Kuwa Walinzi Wa Watoto Wao, Kwani Kwa Kufanya Hivyo Kutasaidia Kuwaepusha Na Majanga Malimbali Ikiwemo Ya Vifo Vitokanavyo Na Maji.

 
Back
Top Bottom