TANZIA Mbeya: Mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi, Michael Kalinga akutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa

TANZIA Mbeya: Mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi, Michael Kalinga akutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Tawi la Machinjioni, Kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya, Michael Kalinga amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne, Desemba 3, 2024 na mwili wake kukutwa Kata ya Mkola.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa amesema wamepata taarifa za mauaji ya Kalinga na wanaendelea kuzifanyia kazi.

Katibu wa CCM Wilaya Chunga, Charles Jockel akizungumza na Mwananchi amesema amepokea taarifa hizo leo Jumanne asubuhi kutoka kwa uongozi wa CCM Kata ya Makongorosi.

"Haijulikani alikuwa anakwenda au kurudi Makongorosi maana mwili wake umekutwa eneo la kuelekea Kata ya Mkola," amesema Jockel.
Hii sumu ya "kifo ni kifo tu" aliyoipanda Sa100 hadi kufikia 2025 atavuna alichokipanda
 
Kwa ninavyowafahamu vijana wa uvccm, si ajabu huyo marehemu alikuwa mastermind wa kupanga mipango ya kuwaua/kuwadhuru wapinzani huku naye akiwindwa na wabaya wake humo ccm!

Watu wa CCM siku mkijua kuwa maisha ni ubatili mtupu na hakuna aliye na haki ya kuamua hatima za watu wengine hapa chini ya jua ndipo mtakuwa na amani mioyoni mwenu. Kifo cha Magufuli nilitegemea kiwe somo zito sana kwenu, ila kwakuwa hamjitambui hamkuambulia chochote!
Hao wana vichwa vigumu kweli kweli hawaambiliki,hawajifunzi hata kutubu hawataki.
 
Mtume Muhammad (S.A.W.) alihimiza sana haki na suluhu za migogoro kwa njia ya amani na usawa. Hadithi mbalimbali zinaelezea jinsi Mtume alivyoshughulikia mizozo kwa hekima na uadilifu, akionyesha kuwa haki ni msingi wa amani na mshikamano wa kijamii. Hapa kuna hadithi mbili mashuhuri zinazohusiana na haki:

1. Hadithi ya Wanawake Wawili na Mtoto

Imepokelewa kuwa wakati wa Mtume Suleiman (A.S.), wanawake wawili walikuja mbele ya Mtume Muhammad (S.A.W.) wakigombania mtoto mmoja, kila mmoja akidai kuwa yeye ndiye mama wa mtoto huyo. Mtume alisikiliza hoja zao kisha akaamua kutumia hekima ya kipekee.

Aliamuru mtoto akatwe vipande viwili ili kila mmoja apate nusu. Mwanamke mmoja alikubali, lakini mwingine alilia kwa uchungu na kusema:
"Mtume wa Mwenyezi Mungu, mpeni yeye mtoto mzima; sitaki afe!"

Mtume alitambua kuwa mwanamke aliyekataa kukatwa kwa mtoto ndiye mama wa kweli, kwa sababu hakutaka kuona mtoto akiangamia. Hivyo, alihitimisha mgogoro huo kwa kumkabidhi mtoto mama wa kweli, akihimiza huruma na haki.

Fundisho: Haki inahitaji hekima na uelewa wa kina wa hisia na dhamira za watu ili kufikia suluhisho la amani.
 
Ustaadh mandaz..kila upenyo dini
 
Hao wana vichwa vigumu kweli kweli hawaambiliki,hawajifunzi hata kutubu hawataki.
Wameshalaanika.

Kuna kata moja huku 2020 ilikuwa na wagombea udiwani watatu, katibu wao wa kata akamuahidi kila mmoja kuwa atampambania na kumpitisha akawapiga hela wote, alivyoshinda mmoja mabalaa yakaanza, alivimba tumbo likawa la kubebelea watu wawili kumuinua, kumkalisha na kumlaza hadi alipokufa, baada yake wameshawekwa makatibu watatu wanazimishwa, sasa hakuna anayeitaka hiyo nafasi ipo wazi
 
Back
Top Bottom