Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Z. Homera ametoa Muda wa Saa 24 kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga, kumsaka na kumkamata Kijana ambaye jina lake halijafahamika mkazi Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Kwa Kosa la Kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maneno Makali na Kisha kuichoma moto Picha inayomuonyesha Rais Samia Suluhu Hassan.

Homera amesema Kitendo hicho kuwa si Cha kimaadili Wala Uungwana na Kiko tofauti na Utamaduni halisi wa Wananchi wa Mkoani Mbeya.Hata hivyo ametoa Masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga Kumkamata Kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na Mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza Moja kwa Moja kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine Homera amewasihi Wananchi Mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye Vitendo viovu kwa Kukashifu Viongozi Makusudi badala yake wajikite katika Utafutaji na Uchapa Kazi kwa Manufaa ya Familia zao na Tanzania kwa Ujumla.
hivi wanataka tuwapende hawa viongozi kwa lazima? kwani ni ndugu zetu
hatutaki hizi heshima za lazima
dogo alindwe na wanasheria
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.

My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.

Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.

Tanzania haiwezimkiwa Taifa lawahuni.

====

Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.

RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.

Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.

View attachment 3031314
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
sifa zingine za kijinga wacha akapate haki yake sero
 
Hongera sana kijana kwa kuonesha hisia zako waziwazi. Ni vile tu umezaliwa kwenye nchi ya ulimwengu wa tatu, na ambayo mpaka leo bado inavikumbatia vyeo vya kikoloni; ndiyo maana unatafutiwa zengwe.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.

My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.

Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.

Tanzania haiwezimkiwa Taifa lawahuni.

====

Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.

RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.

Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.

View attachment 3031314
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
Hiyo picha mnajua ameipataje?
Je mnaweza kuthibitisha kuwa kilichoungua pale ni picja?
 
Safi sana watanganyika hawamtaki kwa upumbavu wa kuuza rasilimali za tanganyika kwa wajomba wa oman

Ukiombwa ushahidi wa hilo utatoa? Kila siku kuwasema waarabu tu, hamuna kazi za kufanya! Mbona wazungu na wachina hamsemi kitu!
 
Back
Top Bottom