Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwamba katika changamoto zoooote zilizopo mkoani mbeya ameona hii ndio ya kuipa uzito kiasi cha kuita mpaka chombo cha habari??

Vipi kuhusu biashara ya mazao ya chakula inayonyika kinyemela baina ya Tanzania na Zambia kupitia Mkoani Mbeya bila utaratibu maalumu na hatimae serikali kukosa kodi, hilo hajaliona???
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.

My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.

Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.

Tanzania haiwezimkiwa Taifa lawahuni.

====

Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.

RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.

Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.

View attachment 3031314
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
Chura hawezi kukubalika hata kdg atafute pa kwenda tu. 2025 tunapiga teke chura
 
Hiyo picha ni mali yake ana haki ya kuifanya atakavyo

Bendera za Israel na Marekani kila mara zinachomwa moto ndio sembuse chura kiziwi.

Yupo mwamba mpaka nakala za Qurani kapiga moto ni mali yake huwezi kumpangia.
Utafikiwa Mkuu .
 
Vitu vingine ni vya kukalia kimya. Huyu Mkuu wa mkoa hili tukio yeye ndo kalipublish sasa . Wala tulikua hatujui..
 
Ushahidi nnao, huku ni tanganyika binti sio zanzibar kwa hiyo kaa kwa kutulia huku hapakuhusu bibie

Uzuri huwa sina matusi, ongea vyote unavyojisikia, kwanza mimi sio mzanzibari kijana.

So, tunaomba huo ushahidi!
 
Back
Top Bottom