Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hiyo picha ni mali yake ana haki ya kuifanya atakavyo

Bendera za Israel na Marekani kila mara zinachomwa moto ndio sembuse chura kiziwi.

Yupo mwamba mpaka nakala za Qurani kapiga moto ni mali yake huwezi kumpangia.

Wanajitahidi kwa kila jinsi ... lakini huweza kuwalazimisha watu wampende Mtu.

Yaani, unaweza kumlazimisha punda kwenye mtoni, lakini huwezi kumlazimisha anywe maji.
 
Hiyo picha ni mali yake ana haki ya kuifanya atakavyo

Bendera za Israel na Marekani kila mara zinachomwa moto ndio sembuse chura kiziwi.

Yupo mwamba mpaka nakala za Qurani kapiga moto ni mali yake huwezi kumpangia.
Mkuu Matola,

Kuchoma picha ya mtu maana yake nini?

Viongozi ni watu kama sisi tu.
Tuwakosoa na kuwapinga kwa hoja, siyo matendo yasiyo na staha.

Mwananchi yeyote ana haki ya kumkosoa ama kumpinga Raisi Samia, lakini bado huyo ni Mkuu wa nchi na ni mama.

Kumuita majina kama chura kiziwi ni utovu wa nidhamu usiokuwa na tija yeyote kwa taifa hili.

Matola wewe ni msomi wa Phd, pamoja na uhuru unaoletwa na mfumo wa vyama vingi, tunatarajia busara zaidi kutoka kwa watu kama nyie.
 
Yeye si ndo alijiita ye Chura Kiziwi
 
Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.
Adhabu hiyo, isiishie hapo....iende moja kwa moja kwa viongozi wote wa Mikoa na wilaya ambao wameweka picha za Mama kwenye mabango Hata stika lakini picha hizo zimeishachakaa...na nyingine zimechanika ama kutobolewa...! Yaani Mkuu huyo, wa Mkoa apambane kweli kweli kuhakikisha hili linafanyika maana kero nyingine za wananchi watashughulikia viongozi wengine.
 
Hio picha Samia ndio alinunua ? Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali muda na Kodi zetu..., Na huyu dogo amepoteza hata hio njiti ya kiberiti angeifanyia jambo la maana
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.

My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.

Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.

Tanzania haiwezimkiwa Taifa lawahuni.

====

Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.

RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.

Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.

View attachment 3031314
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
Jana tulikuwa tunaongea na Wakili Peter Madeleka kuwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa hawana haki ya kuamrisha hizi kamatakamata za Polisi.

Na hizi habari za Lese Majeste (sheria za kuadhibu watu wanaomvunjia heshima mtawala) zimepitwa na wakati. Ukimkataza mtu asiichome picha ya Samia kama sehemu ya freedom of speech, unamualika amchome moto Samia mwenyewe.
 
Alijiita yeye kumbe?

Kama ni hivyo, sawa.
Unaona madhara ya kudandia kitu bila kuelewa?

Fuatilia mabandiko yangu kuhusu huyu mama aliporithi Urais kutoka kwa Magufuli tulimpa full support matokeo yake amechange gia angani ameungana na wahuni kuwafukarisha Watanzania.

Ni big dissapontment and betray.
 
Yeah, tumpinge kwa hoja. Kuchoma picha ni vitendo vya kihuni, na ninaamini mkuu huwa hauungi mkono uhuni.
 
Back
Top Bottom