Mimi nimefuatilia tangu huyo dogo anadhalilishwa kwenye MAKAMERA. Ni uonevu mtupu.
Huwezi kummulika mtu na makamera unamuhoji huku unamrekodi mitandaoni na kumpiga na mawe. KWA HAKI IPI AMA UTAKATIFU UPI?
Nchi ya ajabu sana ambapo wahuni wanafanya tukio la kuumiza mtu na wanapongezwa kisha muhanga anafungwa jela.
Kwa saikolojia ya yule dogo, kwa kudhalilishwa na kuumizwa kihisia na kiakili tangu alipokamatwa, ni wazi alikiri kosa kwa sababu ya kutokuwa sawa. Alishachakazwa kiakili.
Ameonewa sana sana sana, na akimlilia mungu wake, mliohusika mtapata karmic pay back yenye maumivu makali sana.
Ni bora mtengue mlichokifanya.